Tukiwa tunakaribia kuingia mwaka mpya wa 2023 sisi blogu
ya jifunzeujasiriamali kama ilivyokuwa ada kwetu ni wakati wa kutoa tathmini ya
mwaka mmoja uliopita, pia kutoa Dira na mwelekeo wa mwaka unaofuata, tumekuwa
tukifanya hivi kwa miaka mingine yote ya nyuma.
Mwaka unaomalizika wa 2022 kaulimbiu yetu kuu ilikuwa ni;
“BADILISHA TABIA KUJENGA TIJA NA UFANISIZAIDI” na tumeweza kuona jinsi ambavyo tabia ya kufanya mambo kidogokidogo
bila ya kuahirishaahirisha inavyoweza kufanikisha mtu kutimiza lengo kubwa
alilojiwekea. Falsafa hii si kama niliielezea tu kinadharia hapana, ni uzoefu
wangu binafsi nilioupata wakati nafanya kazi ya kukitafsiri kitabu cha THINK & GROW RICH katika lugha ya
Kiswahili kazi niliyoikamilisha mwishoni mwa mwaka 2021 wakati naandika
kaulimbiu hiyo.
Ni matumaini yangu kwamba wote wale tuliokuwa pamoja
katika safari nzima ya mwaka 2022 hasahasa Wanamastermind Group wenzangu wa
MICHANGANUO-ONLINE wameshuhudia jinsi falsafa hii ilivyo na uwezo wa ajabu wa
kufanya kazi licha ya vikwazo kadhaa. Vikwazo hivi yalikuwa ni majanga ya asili
kama vile ukame, vita na magonjwa ya mlipuko kama corona na ebola, vitu ambavyo
kibinadamu ni vigumu sana kuvizuia.
Biashara hazikwenda vizuri kama ilivyotarajiwa jambo
lililopelekea malengo mengi kushindwa kufikiwa. Gojwa la Covid 19, Vita ya
Urusi na Ukraine, Ukame mkali na mfumuko mkubwa wa bei hasa za vyakula, nishati
na zana za ujenzi ni matatizo ambayo mpaka sasa hivi yanaisumbua siyo Tanzania
tu peke yake bali Dunia nzima kwa ujumla.
SOMA: Amua hatma yako tengeneza mwaka uliokuw bora zaidi kushinda mingine yote iliyopita
Katika kitabu cha Think & Grow Rich hali kama hii
naweza kuifananisha na kipindi cha mdororo mkubwa zaidi wa kiuchumi Duniani (The Great Depression) 1929 1939, kipindi
ambacho ndipo kitabu hiki kiliandikwa muda mfupi tu kabla ya kuanza kwa vita
kuu ya pili ya Dunia.
Licha ya maelfu ya watu wakati huo kutokuwa na kazi huku
mfumo mzima wa kibenki ukiwa umefeli na kila mtu akihaha kutafuta mlo wa siku,
lakini Napoleon Hill katika kitabu chake hiki mashuhuri aliweza kuwathihirishia
Wamarekani kwamba bado maisha yangeweza kuwa bora kwa mara nyingine tena na
ukweli ikaja kuwa hivyo. Wamarekani na hatimaye Dunia nzima ikaimarika tena
kiuchumi licha ya kuwepo kwa vita kuu ya ii ya dunia.
SOMA: Heri ya Krismasi na mwaka mpya wenye mafanikio. 2019 ishi kama Mbayuwayu
Magumu tunayopitia sasa hivi kama Tanzania na Dunia kwa
ujumla ni kama tone tu la maji kwenye bahari kubwa ukilinganisha na hayo niliyoyataja
ya Great Depression na Vita kuu ya Dunia mika ya 30. Matumaini Napoleon Hill
aliyowapa Wamarekani miaka hiyo ya 30 yanafanya kazi hata na leo hii kupitia
kitabu chake cha FIKIRI & UTAJIRIKE (think & grow rich)
Hivyo basi namimi kwa mwaka huu tunaouanza leo wa 2023
kama mfuasi wa Napoleon Hill nimeamua kujitolea kwa dhati ya moyo wangu kutumia
fikra na ubunifu kusaidia kubadilisha hali iliyokuwepo sasa hivi na kurudisha
tena matumaini yanayokaribia kupotea.
Katika madarasa yangu Group za watsap na Telegram au
makala nitakazoandika hapa katika blogu hii ya jifunzeujasiriamali, nimelenga
zaidi katika mambo makuu 3 yafuatayo;
1. Ububifu
na teknolojia katika biashara kubwa na ndogo kwa lengo la kutengeneza faida
kubwa haraka zaidi
2. Uhamasishaji
matuimizi ya nishati mbadala na rafiki kwa mazingira kupunguza ujoto duniani
3. Elimu
ya kujitambua binafsi na matumizi ya akili katika kujiletea maendeleo binafsi.
Tayari kwa kuanza leo hii kwenye MASETRMIND GROUP la
MICHANGANUO-ONLINE tunaanza masomo yetu chini ya mwavuli wa maudhui
niliyoyataja hapo juu, Tunaanza na biashara rahisi tu ya chakula, ‘SUPU NA CHAPATI’. Kwa juu juu unaweza
kuona ni biashara ndogo rahisi zisizokuwa na maana yeyote lakini tunachokitaka
hapa ni kuwajengea uwezo na matumaini wajasiriamali wadogowadogo wa kawaida
kabisa “wanaostraggle” na maisha yao ya kila siku.
SOMA: Biashara ya chakula, mchanganuo na mtaji mdogo wa kuanzia
Ingawa sehemu ya masomo haya pia tutayaweka katika blogu
yako hii pendwa lakini kwa kiasi kikubwa yatakuwa yakifanyika ndani ya MASTERMIND GROUP la MICHANGANUO-ONLINE.
Huu ni mwanzo tu, tutakuwa na masomo mengi ya thamani huku wanachama wakiwa na
uwezo wa kuyapata pia baadhi ya masomo mengine mazuri ya zamani. Tunafanya hivi
kwani si kila mtu anapenda kujifunza kwa kina, mwingine angependa kusoma kwa
kifupi tu kwenye blogu hii basi.
Ikiwa wewe ni mtu unayependa kujifunza mambo kwa kina
pamoja na kushea na wenzako kile unachokijua, nakukaribisha sana kwenye
MASTERMING GROUP LETU LA MICHANGANUO-ONLINE, kiingilio cha mwaka mzima ni
shilingi elfu 10 tu na hii tumeweka kwa
ajili tu ya kulipa group thamani, magroup ya bure mara nyingi watu huwa
hawayathamini wala kuzingatia kile wanachojifunza humo.
ZAWADI
YA KUFUNGA MWAKA (Haijawahi kutokea)
Kwa watu wachache wa mwanzo watakaolipia viingilio vyao
vya mwaka sh. 10,000/= nitawapatia
zawadi ya vitabu vyangu muhimu pamoja na michanganuo ifuatayo,( Jumla ni vitu
22); Offa hii ni ya muda mfupi na itamalizika muda wowote kuanzia sasa hivi
idadi inayohitajika ikitimia.
Thamani halisi ya vitu vyote 22 ni zaidi ya Tsh. laki
moja na nusu lakini unalipa sh. Elfu 10 tu! Na ninakutumia papo hapo kila kitu
kama nakalatete mara unapomaliza kulipia kisha kukuunganisha na magroup yetu
Whatsap & Telegram.
Ikiwa hupendi kuungwa kwenye group niambie nikutumie
zawadi zako peke yake, na pia kama hutumii Whatsap wala Telegram, email
inatosha kukutumia kila kitu.
Lipia mapema kiingilio chako sh. Elfu 10 kupitia namba
zangu, 0712202244 au 0765553030 Jina ni Peter Augustino Tarimo kisha ujumbe wa
SMS au Watsap usemao;
“NATAKA OFFA YA MWISHO WA
MWAKA YA VITU 22”
ZAWADI YENYEWE YA KUFUNGA MWAKA 2022, VITABU NA MICHANGANUO JUMLA VITU
22 NI HII HAPA CHINI;
1.
KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI –cha kiswahili
2.
KITABU: Jinsi ya kuandika
mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA
SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha
kiswahili
4.
KITABU mashuhuri zaidi duniani,
HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ndio
hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha
kiingereza
5.
KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO
WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza
6.
Mchanganuo wa biashara: Kiwanda
kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili
7.
Mchanganuo wa Kikundi cha
Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili
8.
Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili
9.
Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili
10. Mchanganuo Biashara ya
ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza
11. Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili
12. Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa
kiswahili
13. Mchanganuo kamili wa
kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili
14. Mchanganuo wa biashara ya
mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili
15. Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza
16. Mchanganuo kamili wa
Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi
(KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
17. Mchanganuo wa Biashara ya
Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
18. Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika
michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili
19. Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza
20. Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili
21. KITABU CHA SEMINA: Masomo 11 ya
michanganuo ya Biashara
22. Kujiunga GROUP LA WHATSAP & TELEGRAM LA MICHANGANUO-ONLINE
Ukishajipatia offa hii na pia kama ungependa kupata na kitabu
cha THINK
& GROW RICH nakala ya Kiswahili, na una Smartphone unaweza
kujipatia kwa shilingi elfu 5 tu badala ya sh. elfu 10 bei ya kawaida. Maelezo
zaidi ya namna ya kukipata tuwasiliane nikupatie. Kama hujajipatia offa hiyo
hapo juu bei ya kitabu FIKIRI & UTAJIRIKE inasalia kuwa sh. Elfu 10 kama
kawaida.
Zawadi kama hizi huwa tunazitoa mara chache sana hivyo
nakuomba ikiwa upo makini na masomo ninayoyatoa basi ni fursa ya kipekee
kujipatia mafunzo hayo kwa kina kwa gharama hii sawa na bure. Njoo kwa pamoja
tumsaidie Rais wetu mama Samia Hassan Suluhu kuwatua kinamama kuni vichwani
mwao pamoja na maswala mengine kibao tutakayojadiliana kwenye group letu na
channel ya telegram.
Tukutane tena jioni kwa masomo ya kila siku ndani ya
MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE
Ni mimi, mwandishi na mhamasishaji wako;
PETER TARIMO
0 Response to "2023 MWAKA WA UBUNIFU ZAIDI KWENYE BIASHARA KUKABILIANA NA MAJANGA"
Post a Comment