Hellow mdau na mfuatailiaji
wa blogu yako hii ya jifunzeujasiriamali, katika makala hii naenda
kukushirikisha majibu niliyompatia mdau wetu mmoja aishiye nchini Irani
aliyeuliza kama ifuatavyo;
Mimi
ni ndugu yako mtanzania
Niko
nchini Iran
Nimesoma
articles mbalimbali ulizoandika na kuziweka mtandaoni kuhusu ujasiriamali wa
ufugaji wa kuku wa mayai
Na
kuku wa nyama
Naomba
nikuulize swali la Kitaalamu ndugu yangu
Ninachotaka
kujua ni bei tu ya banda la kuku kwa kukisia..
Yaani:
Mfano:
Kuku
1000 chotara au kienyeji
Banda
lao zuri na la kisasa linaweza kutengenezwa kwa *Shilingi ngapi (kwa bei ya
kukisia kwa haraka haraka)?*
Asante kaka.......
Kwa kuku 1000, tuchukulie ni
kuku wa kienyeji wakubwa au wa kisasa ambapo kuku 6 mpaka 10 wanapaswa kukaa
ndani ya eneo la mita 1 ya mraba yaani upana mita 1 na urefu wa mita 1. Kumbuka
ujenzi wa banda la kuku wa kienyeji ni tofauti na ule wa banda la kuku wa
`kisasa katika ukubwa tu, kuku wa kisasa banda lao hukaa kwenye eneo dogo
zaidi.
Tutatumia idadi ya kuku 6
kwenye eneo la mita moja ya mraba ambapo kwa kuku 1000 watahitaji; (1000/6)
eneo la miata za mraba 166 sawa na makisio ya mita 160 au Urefu wa mita 16 na
upana wa mita 10
SOMA: Muongozo kamili wa jinsi ya kufuga kuku wa nyama (Broilers) kitaalamu
Tukichukulia ukubwa wa
chumba kimoja cha kawaida cha mita 3 kwa
upana wa mita 3 sawa na mita za mraba 9 eneo hilo linatakiwa kuwa na wastani wa
vyumba vipatavyo(160/9) = 18
Ikiwa chumba kimoja kinaweza
kugharimu shilingi mpaka milioni 2 kwakuwa ni banda tu la kuku hakuna finishing
wala nini, basi mabanda yote jumla yatagharimu wastani wa shilingi milioni 36.
Picha za banda la kuku la mfano unaweza ukaziona katika makala yangu nyingine
niliyoiandika hapa isemayo, Banda la kuku 100 wa kienyeji, vipimo, ramani, picha na jinsi ya kulijenga kwa ubora
Nimetumia milioni 2 kwa
makadirio tu, unaweza mwenyewe ukauliza mafundi gharama, mahitaji ya 'let say' bati zinazotosheleza chumba
kimoja ni ngapi, tofali, wavu wa kuku, gharama za fundi, mchanga, misumari, sementi
nk. kisha ukajumlisha zote na kupata gharama za chumba kimoja cha mita za mraba
9 kisha gharama hiyo ukazidisha kwa vyumba vyote 18 kupata gharama kuu. Hivyo
bei ya mabanda ya kuku hutofautiana kulingana na materials zilizotumika kujengea
SOMA: Shilingi milioni 5 itatosha kufuga kuku wangapi wa mayai? naomba mchanganuo
Ikiwa ni mabanda ya mbao
tupu utafuata njia hiyohiyo niliyotumia. Hivyo unaweza kuona siwezi kuwa na
jibu kamili moja kwa swali lako kwakuwa sijui utaamua kutumia material gani
kujengea mabanda yako, hata hivyo mafundi wana utaalamu mzuri zaidi wa
kukadiria gharama za ujenzi wa nyumba yeyote ile hata ikiwa ni ya kuku
utakapokuwa tayari na kuita fundi ataweza kukusaidia zaidi. Mabanda ya kuku yapo
ya aina nyingi sana mfano kuna mpaka banda la kuku la ghorofa nk. Hivyo gharama
zake zitakuwa tofauti
Ni mimi,
PETER
AUGUSTINO
Mtaalamu wa kuandika
michanganuo ya Biashara za aina mbalimbali zikiwemo za ufugaji wa kuku aina
zote, blogger na mjasiriamali
Karibu kwenye Group langu la
MICHANGANUO-ONLINE kwa masomo zaidi na mijadala ya kila siku. 0712202244 au
0765553030
0 Response to "GHARAMA ZA UJENZI WA BANDA LA KUKU 100 CHOTARA AU KIENYEJI NI SHILINGI NGAPI?"
Post a Comment