Katika nyingi ya nukuu za waliofanikiwa kuna moja
inayosema hivi; njia rahisi na bora zaidi ya kufanikiwa katika jambo lolote lile ni
kuiga na kujifunza kutoka kwa wale waliofanikiwa kwenye jambo hilo.
Kwa mjasiriamali yeyote anayetaka kufanikiwa ama
kutajirika, mtu wake mkubwa wa mfano ni yile mtu ambaye tayari ni tajiri
aliyefanikiwa. Ingawa kauli hii inaweza kuwa kweli lakini inaweza ikawa na
matatizo makubwa.
SOMA: Jinsi ya kupata mafaniko maishani; usipande mlima bila kiongozi
Unapotazama tabia za mtu mwenye mafanikio tayari, usije
ukafikiria kwamba anafanya mambo yaleyale aliyokuwa akiyafanya wakati kabla
hajafanikiwa. Tabia za matajiri ni kwamba wanafanya vitu tofauti kabisa
ukilinganisha na kipindi kile walipokuwa hawajapata pesa/hawana kitu. Ukiwa
mdadisi wa historia za mafanikio ya watu wengi matajiri, utakubaliana nami juu
ya hilo.
Mfano mmoja mkubwa unaweza kuuona kwa matajiri na tabia yao ya kuwa au kumiliki mifereji mingi ya kipato, utasikia watu wengi wa kipato cha chini nao wakijaribu kuiga tabia hii lakini huishia kukata tamaa na kuona ni jambo gumu lisilowezekana kirahisi. Kumbe wanafanya kosa kubwa bila kujua! Unajua ni kwanini hii haiwasaidii? Nitaelezea baadae kidogo....
SOMA: Ukaribu na wajasiriamali mashuhuri waliofanikiwa kunavyoweza kukuinua kimtaji ( Networking)
Binafsi mimi mwenyewe kuna nyakati niliwahi kujihusisha
na biashara nyingi nikidhania kwamba kufanya biashara moja ni hatari inaweza
ikafa muda wowote.... Chakushangaza biashara zote hamna hata moja iliyoweza
kufanikiwa kama nilivyotamani ziwe. Mpaka nakuja kugundua siri ilikuwa ni nini,
nilijuta sana kwani nilishapoteza muda wangu mwingi wa thamani.
SABABU
KUBWA 2 KWANINI WATU WANAOIGA KWA WALIOFANIKIWA HUFELI KIRAHISI
1.
Wanataka utajiri wa haraka:
Hakuna kitu kama utajiri wa haraka chini ya jua, huu ni
ukweli mchungu kila mtu anatakiwa kuujua. Zinahitajika juhudi na umakini (Focus) kwanza ili mtu aweze kufanikiwa
katika jambo lolote lile. Utajiri wa haraka unaweza kutokea mara chache sana,
mmoja katika watu maelfu, ni kwa waliokuwa na bahati ya mtende kama vile
washindi wachache wa bingo na michezo ya kubahatisha. Sifa za utajiri hautaki
haraka.
Kinachoonekana mara zote kuwa ni utajiri au mafanikio ya
haraka mara nyingi ni watu waliofanya kazi usiku na mchana kwa miaka mingi kabla
hawajafanikiwa. Watu waliofanikiwa kupitia kilimo kwa mfano unaweza kudhania
ndio waliofanya kazi ngumu zaidi lakini hata shughuli zingingine kama muziki
msanii ataonekana kama kafanikiwa haraka lakini watu hawawezi kufikiria kipindi
msanii alipokuwa akikariri mashairi ya nyimbo za wasanii wakubwa wenye majina
alivyosota.
SOMA: Wanaofanikiwa maishani wengi husema no (hapana) kwa vitu hivi 3
Sisemi haiwezekani kabisa mtu kutajirika haraka hapana,
bali ninachosisitiza hapa ni kuwa ili ufanikiwe ni lazima uonyeshe hali fulani ya
uvumilivu, bidii, nidhamu ya fedha na msimamo, na haya ndiyo miongoni mwa mambo
yaliyosisitizwa sana ndani ya kitabu cha Think
& Grow Rich ambacho sasa hivi kinapatikana pia kwa lugha adhimu ya Kiswahili
katika kiungo hiki, FIKIRI & UTAJIRIKE
2. KIU
YA KUTAKA KUWA NA MIFEREJI MINGI YA KIPATO MAPEMA MNO
Tunarudi katika mada yetu tuliyoanza nayo pale mwanzo.
Nimewahi hata kutunga kitabu kiitwacho, MIFEREJI 7 YA PESA NASIRI MATAJIRI
WASIYOPENDA KUITOA kusisitiza dhana hiyo lakini ndani ya kitabu kuna mahali nilisema
Mifereji 7 ya kipato siyo kwa masikini bali kwa watu ambao tayari
wameshafanikiwa kwa kiasi fulani.
Ukweli ni kwamba ukiwa masikini na ukatawanya nguvu na
rasilimali zako kwenye miradi zaidi ya mmoja kabla haijafanikiwa kusimama
yenyewe kwa miguu yake ni lazima tu utaanguka/utafeli. Ikiwa hautatumia
asilimia 100% ya nguvu zako kuanzisha biashara fulani mpaka isimame kwanza ndipo
uanzishe nyingine, utakuwa ukicheza patapotea. Hauwezi kutajiruka kwa kuanza na
utitiri wa biashara bali ni kwa kuwa kwanza na msimamo na biashara moja mpaka
pale itakaposimama imara ndipo uanzishe nyingine hivyo hivyo na ukitaka hata
kuwa na biashara 10.
Natumaini hautafanya makosa niliyowahi kuyafanya kwa
kuingia mtego wa kuanzisha biashara nyingi wakati hazijasimama imara. Natamani
haya nikwambiayo ningeambiwa mika 10 au 15 iliyopita, ndiyo maana nikaamua
kuanzisha darasa langu kwenye Group la Telegtam na Wasap liitwalo
MICHANGANUO-ONLINE kwa ajili ya kufundisha watu mbinu mbalimbali za biashara na
ujasiriamali.
Kujiunga na Group letu ambalo kwa sasa tuna somo la SIRI ZA BIASHARA YA SUPU TAMU NA CHAPATI
LAINI linaloendelea, lipia tu kiingilio cha mwaka mzima shilingi elfu 10
kwa namba 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha nitumie
kwa meseji namba yako ya TELEGRAMU na anuani ya Email kisha ujumbe usemao;
NIUNGE NA MASTERMING GROUP NA OFFA YA VITU 21 YA KUFUNGA MWAKA. Utatumiwa muda huohuo kila kitu na kuunganishwa na group.
Kama utahitaji na kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE
nijulishe ili nikupe link na kuponi ya kukinunua kutoka mtandao wa GETVALUE kwa
sh. Elfu 5 tu badala ya elfu 10
ZAWADI hii itadumu kwa muda mfupi sana kabla
hatujaiondoa.
ZAWADI
YENYEWE YA KUFUNGA MWAKA (VITU 22) NI HII HAPA CHINI;
1.
KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI –cha kiswahili
2.
KITABU: Jinsi ya kuandika
mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA
SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha
kiswahili
4.
KITABU mashuhuri zaidi duniani,
HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ndio
hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha
kiingereza
5.
KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO
WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza
6.
Mchanganuo wa biashara: Kiwanda
kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili
7.
Mchanganuo wa Kikundi cha
Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili
8.
Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili
9.
Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili
10. Mchanganuo Biashara ya
ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza
11. Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili
12. Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa
kiswahili
13. Mchanganuo kamili wa
kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili
14. Mchanganuo wa biashara ya
mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili
15. Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza
16. Mchanganuo kamili wa
Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi
(KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
17. Mchanganuo wa Biashara ya
Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
18. Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika
michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili
19. Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza
20. Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili
21. KITABU CHA SEMINA: Masomo 11 ya
michanganuo ya Biashara
22. Kujiunga GROUP LA WHATSAP & TELEGRAM LA MICHANGANUO-ONLINE
0 Response to "JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA LAKINI USIIGE KILA KITU KAMA KILIVYO UTAFELI"
Post a Comment