Ikiwa una
matazamio ya biashara yako ndogo kukua mwaka huu ujao wa 2023 ni lazima kwanza
utilie maanani ukweli huu kwamba, kuna biashara nyingi za mitaji midogo kama
yakwako ambazo hazitaweza kuuona mwaka mpya wa 2023, lakini pia baadhi ya
biashara hizo chache zikashamiri na kustawi licha ya kuwa zilianza kipindi
kimoja.
Ni kitu gani
hasa kilichosababisha biashara hizi chache kustawi ilihali nyingi zikifa?
Majibu ya swali hili bila shaka yatakusaidia sana katika kuiweka mikakati ya
kuiinua biashara yako ndogo ya mtaji mdogo ili hatimaye nayo iweze kufikia
viwango vingine itakapokwenda kufika kipindi kama hiki mwakani kuelekea 2024.
SOMA: Hatua 7 rahisi za kuanzisha biashara yako ndogo ukiwa bado kazini umeajiriwa
Takwimu
mbalimbali zilizofanyika nje na ndani ya Tanzania zinaonyesha kwamba karibu
asilimia 50% ya biashara zote ndogondogo mpya hufa kila mwaka na zile
zinazobakia ni chache sana zitatimiza umri wa miaka 5. Sababu kubwa nne (4)
zinazopelekea vifo vya kusikitisha vya biashara hizi na njia za kukabiliana navyo
ni hizi zifuatazo;-
1. Ukosefu wa Fedha/Mtaji
Sababu moja
kubwa zaidi inayozifanya biashara nyingi
za mitaji midogo zisiweze kusheherekea birthday zao za mwaka mmoja 2023 ni
ukata au kutokuwa na mtaji wa kutosha, wataalamu huita, mtaji endeshi wa
biashara (working capital).
Wakati
mwingine mjasiriamali anaweza akafahamu kabisa ni kiasi gani cha fedha
zinazohitajika kwenye uendeshaji wa biashara yake kila siku kama vile, kulipa
mishahara, kulipia gharama za kudumu na zile zisizokuwa za kudumu pamoja fedha
za kununulia malighafi au bidhaa kwa ajili ya kuuza lakini shida huja pale
mjasiriamali huyu anaposhindwa kujua apate wapi fedha hizo baada ya kupata
fedha kidogo za kuanzia.
SOMA: Biashara ndogondogo Tanzania zenye faida ya haraka ni hizi hapa, zipo nne(4)
Wajasiriamali
wengi hujipa moyo kwa kusema, “labda
mauzo ya biashara yangu yatakuwa mazuri na nitapata fedha za kuendeshea
biashara kutokana na hayo mauzo”. Hata hivyo ni bahati mbaya sana biashara
nyingi mpya na hasa zile ndogondogo za mitaji midogo huweza kuanza moja kwa
moja na mauzo ya kuridhisha, mauzo hupanda taratibu mno kiasi cha kutokumpa
mjasiriamali muda wa kuendelea na biashara yake na matokeo yake ni kufungwa kwa
biashara.
Kuna wakati
pia mjasiriamali hushindwa kupanga vizuri bei zake na kuweka bei ya chini mno
akifikiria eti ndiyo anawavutia wateja wengi zaidi waje kununua kwake kumbe
ndiyo njia nyepesi ya kujimaliza mwenyewe.
SOMA: Njia rahisi ya kupanga bei ya huduma au bidhaa unayouza
Matokeo ya
mkakati huu mbovu ni kwamba hataweza asilani kumudu gharama za uendeshaji wa
biashara na hujikuta anatumia fedha nyingi zaidi kuendesha
biashara kuliko zile anazozipata kama mauzo. Mbinu hii inaweza kufaa tu kwa
muda mfupi ila siyo endelevu.
Ingawa
mjasiriamali anaweza akakopa fedha mahali, lakini biashara nyingi ndogondogo
huwa hazina uwezo wa kuwashawishi wakopeshaji kutokana na kukosa mauzo mazuri,
kutokuwa na dhamana za mkopo wala historia ya muda mrefu.
SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini
Suluhisho kwa tatizo hili la ufinyu wa mtaji ni kwa
mjasiriamali mwenyewe kufahamu jinsi ya kubajeti fedha kidogo alizokuwa nazo
ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha za kuendeshea biashara
yake kabla hata hajaianza. Uelewa huu anaweza kuupata kwa kupitia kujua namna
ya kuandaa mpango wa biashara (Business
plan) katika karatasi au hata kichwani mwake tu inatosha.
2. Kukosekana Usimamizi mzuri wa biashara
Sababu
nyingine ya biashara nyingi ndogondogo zilizoanzishwa mwaka 2022 kushindwa kufika
mwaka 2023 ni wamiliki wa biashara hizo au timu nzima ya usimamizi kukosa mbinu
bora za usimamizi wa biashara. Ikumbukwe kuwa biashara nyingi zile ndogo
huendeshwa na kusimamiwa na wamiliki wenyewe, na mara nyingi mmiliki asipokuwa
na ujuzi katika eneo fulani tuseme labda katika masoko, fedha au kuajiri basi
anaweza akasababisha biashara kufeli kiurahisi.
SOMA: Kama una biashara ndogo ya mtaji mdogo, hizi hapa njia 11 za kuibusti
Suluhisho la tatizo hili ni mjasiriamali kutafuta mtu
anayeweza eneo fulani yeye asilolimudu badala ya kujidai kufanya kila kitu peke
yake.
3. Kutokuwa na Mpango wa Biashara
Biashara nyingi ndogondogo huwa wamiliki wake
hawaweki uzito kwenye mpango wa biashara. Kama ninavyosisitiza kila mara kuwa
mpango wa biashara siyo lazima uuandike katika karatasi ndipo ukusaidie,
ukiupangilia vizuri kichwani kwako tu inatosha ilimradi ujue jinsi ya
kuupangilia na vipengele vyake vyote ni nini. Ili mtu uweze kuielewa mipango ya
biashara ikoje na ni vipi unaweza ukaandaa wa kwako unaweza ukasoma ‘sample’
mbalimbali zilizokwishaandikwa.
Sisi tunazo sample hizo ambazo ni michanganuo
mbalimbali kamili iliyoandikwa kwa kiingereza na Kiswahili tunaweza kukupatia
usome. Tuna michanganuo ya aina za biashara ndogondogo za mtaji mdogo lakini
pia aina za biashara za mtaji mkubwa na wa kati zikiwemo pia na aina za viwanda
mbalimbali vya kusindika vyakula na vya bidhaa nyinginezo mbalimbali
Mpango mzuri wa biashara utakuwezesha kulifahamu
vizuri soko lako, sekta biashara yako ilipo pamoja na ushindani unaokuzunguka
kabla hata hujaanzisha biashara yenyewe
4. Kukosa mikakati mizuri ya Masoko
Mkakati mzuri wa masoko unahitaji bajeti ya
pesa ambazo kama tulivyokwishaona huko nyuma mmiliki wa biashara ndogo anakuwa
hana na kosa kubwa tunalolifanya wamiliki wa biashara ndogo ni kuhamishia hata
pesa kidogo za bajeti ya masoko zilizopo kwenda kuziba mapengo katika maeneo
mengine jambo ambalo ni kosa kubwa sana la kiufundi. Hakuna kitu chenye umuhimu
mkubwa kwenye biashara kushinda soko hasa ikiwa kama bado ni mpya.
SOMA: Katika vitu 3, usimamizi, soko na uendeshaji kipi ni muhimu zaidi katika mafanikio ya biashara?
Pia wamiliki wa biashara hizo wakati mwingine
hushindwa kujua ni jinsi gani wakadirie soko lao, namna ya kulifikia na tabia
za wateja wao kwa ujumla vitu ambavyo ni muhimu mno katika uhai wa biashara
yeyote ile.
Suluhisho
la matatizo yote manne 4 kwa pamoja linaweza kupatikana tu pale mjasiriamali
atakapoelewa vyema jinsi ya kuipangilia biashara yake kabla na baada ya kuianza
kwani kwa kila hatua ya biashara huwa ina kipengele chake kwenye mchanganuo wa
biashara.
SOMA: Sababu kubwa kwanini biashara inaweza kufa hata kama ina faida nzuri tu na ya kutosha
Ninayo PACKAGE/KIFURUSHI kizima cha vitu 21,
vitabu, michanganuo kamili ya biashara na masomo mbalimbali kinachomwezesha mtu
yeyote yule kuelewa nje ndani Michanganuo ya biashara, jinsi ya uandaaji wake,
uandishi na hata ikiwa unapenda tu kuisoma kama kujihamasisha “Inspiration” ili uweze kuiendesha na
kuisimamia vyema biashara yako kwa uhakika isife.
Package hii kwa bei ya Offa kabla wiki hii
haijamalizika (kwani ndiyo wiki ya mwisho) utaipata kwa kulipia shilingi elfu
10 tu ikiwa ni pamoja na kuunganishwa na group letu la masomo whatsapp na telegram
(Michanganuo-online). Kwenye group pia utapata masomo mengine yote
tuliyojifunza siku zilizopita.
Lipia sasa hivi kupitia namba zetu,
0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo kisha nitumie ujumbe wa
Wasap au SMS usemao;
“NITUMIE KIFURUSHI CHANGU NA KUNIUNGA GROUP LA
MASOMO”
Nitumie pia na anuani ya email na namba ya telegramu
kama unayo
Ikiwa hutumii watsap wala telegramu unaweza
kutumiwa offa zote na masomo kwa njia ya email.
Kumbuka hii offa inamalizika wiki hii hii muda wowote ule
kwani idadi ya wanachama wanaotakiwa karibu inatimia na hata wasipotimia offa
bado itafungwa rasmi.
Peter
Augustino Tarimo
Mtaalamu wa michanganuo ya Biashara
SIMU/WATSAPP: 0712202244 au 0765553030
0 Response to "KWANINI BIASHARA ZA MTAJI MDOGO NYINGI ZILIKUFA 2022 LAKINI CHACHE ZIKASTAWI?"
Post a Comment