Usije ukadhani labda hapa naandika nadharia tupu
nilizosoma mahali hapana, ni biashara niliyowahi kuifanya mimi na mke wangu
tulipoamua kuanzisha mgahawa mdogo. Hapo kabla hatukuwa tunafahamu kabisa kama chapati
zingeliweza kutupa changamoto tulizozipata. Kila mke wangu alipojaribu
kutengeneza chapati za wateja zilionekana laini tu pale zinapotoka jikoni
lakini baada ya muda kidogo kupita zikianza kupoa zinageuka kuwa ngumu ajabu
utafikiri ni ngozi ya mnyama.
Tulifanya majaribio ya kununua chapati kutoka kwa mtu
ambaye chapatti zake zilikuwa zikipendwa sana na wateja tukabaini zilikuwa na
uwezo wa kukaa hata siku nzima(saa 24) pasipo kugeuka kuwa ngumu. Tukajaribu
kuingia mitandaoni, Utube nk. Lakini maelezo yote tuliyopata huko hayakutusadia
sana.
SOMA: Uzuri wa mafunzo ya mapishi ya vitafunwa, chakula, lambalamba whatsap mtandaoni
Mke wangu aliamua aende kwa rafiki yake mmoja hivi kusudi
aweze kumfundisha, akamsimulia tu kwa mdomo jinsi ya kuchanganya unga na kila
kitu hadi kukaanga. Maelezo yalifanana kidogo na yale ya kwenye mitandao na
aliporudi tukajaribu kwa shauku lakini cha kushangaza hatukuweza kupata matokeo
ya kutia moyo.
Wateja waliendelea kulalamika kuwa chapati zetu ni ngumu,
wengine hata wakadiriki kuhama. Kuna waliotushauri tubadilishe vitafunwa
ikibidi tuchemshe ndizi badala ya chapati, lakini ukweli ni kwamba wateja wengi
hupendelea chapati kwa supu au chai kuliko ndizi za kuchemsha.
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado-1
Binafsi nilichukua uamuzi wa kufanya utafiti sehemu
mbalimbali ndipo nikakutana na dada mmoja Kariakoo ambaye chapatti zake
nilionja na kuona zilikuwa za kiwango kinachostahili. Bila kusita nilimuomba
anipatie darasa la vitendo nimlipe kiasi cha fedha atakacho akanikubalia lakini
kwa kuwa ilikuwa ni kipindi cha mfumgo wa Ramadhani alikuwa na ratiba ngumu
akanipangia niende baada ya siku kadhaa.
Sikuweza kuvumilia zile siku zifike nikamfuata dada
mwingine aliyekuwa akiuzia chapatti maeneo ya Mbezi Mwisho, huyu alikubali
kunifundisha siku ileile na akaniagiza nikanunue vifaa nije saa 12 jioni baada
ya kumaliza kazi zake za mama lishe. Aliniagiza Unga nusu kilo, mafuta ya kula
Robolita na mkaa kiasi kama wa mia tano hivi, mimi nilinunua wa buku kabisa
ukibaki nimwachie.
SOMA:Biashara ndogondogo zenye faida ya haraka Tanzania hizi hapa, zipo nne(4)
Tulianza darasa letu saa 12, huku nikimfuatalilia kwa
umakini mkubwa kila hatua aliyopitia. Dada alinieleza kwamba chapati zake ni
simple sana na kwanza hajisumbui hata kutumia maji ya moto au ya uvuguvugu na bado
chapatti zake zinatoka nzuri, alidai kuchemsha maji ya kusukumia chapati za
biashara ni kupoteza muda.
Kwenye ukandaji alikadiria tu maji, mafuta na chumvi na
wala hakuonyesha kipimo exactly ni kiasi gani mtu unapaswa kuweka, (hapa kama huna uzoefu imekula kwako)
Baada ya kukanda ukalainika alilifunika donge la unga kama dakika kumi kisha
akaanza kukata matonge madogomadogo saizi ya limao na kuyapanga mle kwenye
beseni alilokandia.
SOMA: Jinsi kiwanda kidogo kinavyoweza kukutoa kimaisha na kuwa tajiri wa kutupa
Alipomaliza madonge yote, yalikuwa kama 7 au 8 hivi kama
sikosei, aliweka kikaangio(frying pan)
jikoni ili kianze kupata moto kisha akaanza kusukuma lile donge la mwanzo kabisa
tayari kwa kuanza kukaanga chapati zetu. Alinisisitizia sana juu ya kuhakikisha
moto unakuwa wa kutosha lakini usizidi sana kwani chapatti zinaweza zikababuka
bila ya kuwiva sawasawa, pia moto ukiwa kidogo sana zinakuwa ngumu.
Baada ya zoezi la kukaanga kumalizika alinikabidhi chapatti
zangu tukaonja hapo moja mbili huku nyingine nikiwabebea watoto nyumbani,
nyumbani nilihakikisha nabakiza chapati mbili ili nione ingechukua muda gani
zikiwa laini. Asubuhi kweli nilizikuta bado laini ingawa kuna kitu kimoja
hakikunipendeza, chapati za huyu dada hazikuwa zimewiva sawasawa jambo ambalo
nadhani wateja pia huwa hawalipendi na mara nyingi utakuta wakikata vipande
maeneo yanayoonyesha weupe au ubichi, nilifikiria huyu dada alifanya vile
kusudi chapati zionekane laini.
SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?
Pamoja na hayo yote tulijipa moyo na kujiambia labda
mambo yatakuwa tu mazuri tutakapozidi kufanya mazoezi ya kupika chapati tena na
tena. Siku ileile iliyofuata tukapika chapati kwa mbwe mbwe zote tukitumia
utaalamu niliochukua kwa dada Mama lishe lakini chakushangaza tena matokeo
hayakuwa kama nilivyotegemea. Bado chapati ziliendelea kuwa kavu na ngumu,
labda uipue haijawiva sawasawa ndipo utaona ikiwa laini kidogo. Hili nalo
likaendelea kutusumbua vichwa.
Ilikuja kutuchukua zaidi ya miezi 3 kupata kanuni sahihi
ya kutengeneza chapati laini bila ya kubahatisha tena. Nikiamua kupika chapati
najua kabisa matokeo yake yatakuwaje kulingana na hatua nitakazopitia na vipimo
vya viambato mbalimbali.
Fuatana
na mimi kwenye somo hili la Supu na Chapati kila siku mpaka mwisho, bado
hatujafika mahali penyewe pazuri penye siri za kupika chapati laini mchambuko
na supu tamu, haya bado ni maelezo tu ya awali.
Ikiwa unapenda kujifunza somo hili kikamilifu ungana na sisi kwenye Group na Channel yetu ya Telegram, MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP kwa kuchangia kiingilio cha mwaka cha shilingi 10,000/=
Kujiunga lipia kwa namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augstino Tarimo
Ukilipia mapema kabla nafasi hazijajaa unapata
ZAWADI/OFFA ya kufunga mwaka ya vitabu na Michanganuo ya biashara/Business
Plans, jumla vitu 22 katika mfumo wa nakalatete kwenye simu yako au kompyuta.
Baada ya kulipa sh. 10,000/= nitumie anuani yako ya E-mail na namba uliyojiunga nayo TELEGRAMU kisha ujumbe ufuatao;
“NATAKA OFFA YA MWISHO WA MWAKA YA VITU 22”
ZAWADI HIYO YA KUFUNGIA MWAKA 2022, VITABU NA MICHANGANUO JUMLA VITU
22 NI HII IFUATAYO;
1.
KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI –cha kiswahili
2.
KITABU: Jinsi ya kuandika
mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA
SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha
kiswahili
4.
KITABU mashuhuri zaidi duniani,
HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ndio
hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha
kiingereza
5.
KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO
WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza
6.
Mchanganuo wa biashara: Kiwanda
kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili
7.
Mchanganuo wa Kikundi cha
Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili
8.
Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili
9.
Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili
10. Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa
wa kuku wa nyama- kwa kiingereza
11. Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili
12. Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa
kiswahili
13. Mchanganuo kamili wa
kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili
14. Mchanganuo wa biashara ya
mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili
15. Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza
16. Mchanganuo kamili wa
Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi
(KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
17. Mchanganuo wa Biashara ya
Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
18. Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika
michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili
19. Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza
20. Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili
21. KITABU CHA SEMINA: Masomo 11 ya
michanganuo ya Biashara
22. Kujiunga GROUP LA WHATSAP & TELEGRAM LA MICHANGANUO-ONLINE
Ukishajipatia zawadi hii na pia kama ungependa kupata na kitabu
cha THINK
& GROW RICH nakala ya Kiswahili, na una Smartphone unaweza
kujipatia kwa shilingi elfu 5 tu badala ya sh. elfu 10 bei ya kawaida. Maelezo
zaidi ya namna ya kukipata tuwasiliane nikupatie. Kama hujajipatia offa hiyo
hapo juu bei ya kitabu FIKIRI & UTAJIRIKE inabakia kuwa sh. Elfu 10 kama
kawaida.
Offa kama hizi huwa tunazitoa mara chache sana hivyo
nakuomba ikiwa upo makini na masomo ninayoyatoa basi ni fursa ya kipekee
kujipatia mafunzo hayo kwa kina kwa gharama hii karibu na bure
0 Response to "UZOEFU WANGU BINAFSI KWENYE BIASHARA YA SUPU NA CHAPATI LAINI ZA KUSUKUMA"
Post a Comment