KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA
CHAKULA HATUA KWA HATUA (UPENDO CAFE)
RATIBA YA MAFUNZO
SIKU
YA KWANZA TAR. 25/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO;
UTANGULIZI
1.
Maana
halisi ya Mpango wa Biashara
2.
Kitu
cha kwanza kufanya kabla hujaanza kuandika mpango wako wa biashara
3.
Jinsi
ya kufanya Utafiti wa biashara ya Cafe
4.
Njia
kuu 3 unazoweza kuzitumia kuandika mpango wako
5.
Vipengele
muhimu 8 vya mpango wa biashara
6.
Jalada
la nje linatakiwa liwe na vitu gani juu yake?
SIKU
YA PILI TAREHE 26/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO;
1.
Muhtasari
wa mpango wako
2.
Maelezo
ya Biashara
3.
Maelezo
ya Bidhaa/Huduma
SIKU
YA TATU TAREHE 27/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO
1.
Tathmini
ya soko
2.
Mikakati
na Utekelezaji
SIKU
YA NNE TAREHE 28/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO
1.
Mpango
wa Uendeshaji
2.
Uongozi
na Nguvukazi
SIKU
YA TANO TAREHE 29/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO
1.
Mpango
wa Fedha
· Mauzo ya kurudisha gharama(Break even
Analysis)
· Makisio ya Faida na hasara miezi yote 12
· Makisio ya Faida na Hasara miaka 3
· Makisio ya Mtiririko wa fedha miaka 3
· Makisio ya Mali na madeni miaka 3
UTANGULIZI:
Mpango wa biashara maana
yake ni nini?
Kabla hatujaenda kuanza
rasmi kuandika hatua kwa hatua mpango wa biashara hii ya UPENDO CAFE, kwanza ni
vizuri kujikumbusha maana hasa ya Mpango/Mchanganuo wa biashara ni kitu gani.
Mpango wa biashara unaweza
ukaulezea kwa namna nyingi tofauti lakini kwa mujibu wa Kitabu cha MICHANGANUO
YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI mpango wa biashara maana yake ni hii;
Maandishi yanayoelezea kila jambo kuhusu
biashara unayotaka kuiendesha, mambo hayo ni, malengo, mikakati, bidhaa/hudumu
utakayouza, soko (wateja), shughuli mbalimbali za masoko na uongozi, gharama,
mahitaji, na masuala yote yanayohusiana na fedha.
Au
pia unaweza ukasema hivi;
Mpango wa Biashara ni jumla ya maelezo
yote yanayoihusu biashara, kuanzia malengo ya biashara mpaka mbinu mbalimbali
zitakazotumika kufanikisha biashara husika.
Au unaweza ukasema tu kwa
kifupi hivi;
Ni dira au ramani inayokuongoza katika
biashara yako kujua unatoka wapi na unaelekea wapi.
NUKUU
MUHIMU
“Mpango
wa biashara ni andiko linaloishi, unachokiandika leo siyo lazima kiwe kile
kitakachotokea kesho na ndiyo maana unaitwa utabiri/makisio. Cha msingi ni
kufanya marejeo mara kwa mara wakati wa utekelezaji ukilinganisha hali halisi
na makisio yako, uongeze nini au upunguze kitu gani kusudi biashara yako iweze
kufanikiwa zaidi. Na hii haimaanishi kwamba mpango wa biashara hauna maana
hapana, kwani hakuna mtu yeyote yule duniani anayeweza kudai ameanzisha
biashara bila kwanza ya kupanga kichwani mwake au kwenye makaratasi
ataifanyafanyaje biashara hiyo” – Peter Augustino Tarimo
KITU
CHA KWANZA KABISA KUFANYA KABLA HUJAANZA KUANDIKA MPANGO WAKO WA BIASHARA YA
CAFE
Kuandika mpango wa biashara
maana yake ni kwamba utahitaji taarifa mbalimbali wakati unaandika na taarifa
hizo ili kuzipata ni lazima uzitafute kwanza. Kwahiyo kitu cha kwanza kabisa
kufanya ni kuanza kuzitafuta taarifa mbalimbali zinazohusiana na biashara yako
ya Cafe na kitendo hiki kinaitwa Utafiti wa biashara, wengine huita utafiti wa
soko au feasibility study kwa
kimombo.
JINSI
YA KUFANYA UTAFITI WA BIASHARA YA CAFE
Kimsingi katika Utafiti wa
biashara mtu unapaswa kuchunguza mazingira yote yanayoihusu biashara husika,
kwa maana nyingine ni kwamba unatakiwa kuifahamu hiyo biashara nje ndani. Hivyo
ukishindwa kufuata njia za kitaalamu kufanya utafiti usihofu, wala siyo jambo
baya, kwani watu wengi hufanya utafiti wa biashara zao bila hata ya wao wenyewe
kujua kama wanachokifanya ni utafiti
Siyo kila kitu kwenye mpango
wako utahitaji taarifa za utafiti, sehemu nyingine unahitaji tu maelezo ambayo
tayari utakuwa unayo kichwani. Hivyo katika utafiti tutazingatia zaidi maeneo
makuu yafuatayo
1. Ufafiti wa soko na bidhaa utakazouza.
2. Utafiti wa maswala ya
kiufundi na Utawala.
3. Utafiti wa maswala ya fedha.
Katika vipengele hivyo 3
hapo juu unaweza kuona vinafanana na baadhi ya vile tutakavyokwenda kuona
kwenye mpango wa biashara kwa kuwa kimsingi mambo yanayotakiwa uyachunguze
katika utafiti ndiyo yaleyale tutakayokuja kutumia majibu yake wakati tukiandika
mpango wa biashara.
Kwenye utafiti wa soko na
bidhaa wamiliki wa biashara hii, UPENDO CAFE waliongozwa na maswali
yafuatayo;
1.
SOKO.
· Soko
la bidhaa zao ni lipi?
· Walengwa
wao ni akina nani?
· Tabia
za wateja wao zikoje.
· Wapo
wateja wangapi kwenye hilo soko?
· Kuna
changamoto zipi zinazolikabili soko hilo?
· Ni
gharama kiasi gani itakayotumika kulifikia soko?
· Ni
nani washindani wao wa moja kwa moja na wsiokuwa wa moja kwa moja?
· Bidhaa
zao zinafanana au kutofautiana vipi na za washindani wao?
· Ni nini
siri yao kuu ya mauzo?
· Je
washindani wao wanaweza kuwaiga kirahisi?
· Washindani
wao wanachukuliaje ujio wao katika soko?
2.
Bidhaa /Huduma.
Katika kipengele hiki
walitafiti maswali haya yafuatayo kuhusiana na bidhaa na huduma watakazozitoa;
· Sifa
za bidhaa(chapatti, mandazi supu nk.) watakazouza
· Jinsi
mauzo yatakavyofanyia je ni ndani ya cafe, take away au njia gani nyingine?
· Chanzo
cha malighafi za kutengenezea vyakula mbalimbali ni wapi, na je zinapatikana
kwa urahisi?
· Mahitaji
ya wateja kwa vyakula mbalimbali ni kiasi gani?
· Kiwango
cha uzalishaji kwa siku/mwezi
· Upekee
wa bidhaa zao ni kitu gani?.
· Ni teknolojia
ipi au ufundi utakaotumika?
· Ukubwa
na aina ya mashine na vifaa vitakavyotumika ukoje?
· Kukadiria
mahitaji ya vifaa na malighafi zitakazohitajika.
· Ni
kina nani, watakaowapatia
teknolojia itakayotumika
· Je,
teknolojia watakayotumia ni ya kisasa au imepitwa na wakati?
· Je,
ni teknolojia inayoweza ikaigwa kirahisi?
· Je,
soko linafikika kirahisi?
· Tathimini upatikananji wa vitendea kazi kama vile
umeme, gesi maji n./k
· Tathimini
ya uchafuzi wa mazingira.
· Ni
faida gani jamii itakayopata kutokana na huu mradi?
· Kuangalia
sheria na taratibu mbalimbali za nchi zinazohitajika kufuatwa.
· Kutathimini
mwitikio wa jamii inayouzunguka mradi juu ya kuanzisha biashara husika katika
mazingira yao.
· Kutafiti
upatikanaji wa malighafi sasa na wakati ujao.
· Kutathmini
ubora na bei za malighafi na njia mbadala za kupata malighafi.
4.
Uongozi/Organisation;
· Jinsi
muundo wa uongozi wa biashara utakavyokuwa?
· Ni
kina nani watakaounda menejiment?
· Uwezo
wao ni upi?
· Uwezo
wao utasaidiaje biashara?
· Wana
uaminifu gani?
· Udhaifu
wao utarekebishwaje?
· Idadi
ya watu watakaoajiriwa ni wangapi?
· Je
upo mpango wa kuwapeleka mafunzoni (course)?
Fedha/Financials
· Mahitaji
yote ya biashara ni shilingi ngapi?
· Ni
kiasi gani cha fedha zitakazotumika kuiendesha?
· Fedha
hizo zitapatikana toka wapi?
· Matarajio
ya mauzo kwa mwezi, mwaka, yatakuwa kiasi gani?
· Faida
itaanza kupatikana baada ya muda gani kupita?
· Kuna
uhitaji wowote wa kukopa mahali ili kuweza kutimiza malengo waliyojipangia?
· Kuna
haja ya kutafuta wabia zaidi?
· Biashara
itarudisha mtaji baada ya muda gani kupita?
NJIA KUU 2 ZA KUFANYA UTAFITI WA
BIASHARA
Jinsi wamiliki wa Upendo
Cafe Bibi Gladius na Mariam walivyofanya
utafiti wao kupata majibu kwa maswali mbalimbali yaliyotajwa hapo juu kuhusiana
na biashara yao hii, iliwabidi kutumia
njia hizi mbili zifuatazo;
1.
Utafiti wa Msingi (Kuzungumza na watu ana kwa ana)
Waliwafuata moja kwa moja
wadau mbalimbali wa biashara za vyakula kama vile wamiliki wa mikahawa, cafe na
hoteli, wateja wa vyakula, wauzaji wa malighafi za vyakula taasisi mbalimbali
zinazojihusisha au kusimamia biashara za vyakula zikiwemo zile za serikali na
za watu binafsi. nk. kisha kuwauliza
maswali mbalimbali kama tulivyoona kwenye orodha pale juu, lengo likiwa ni
kupata majibu yake kwa usahihi.
2.
Utafiti wa Dawati (Kusoma machapisho na vyombo vingine vya habari)
Walisoma pia machapisho nje
na ndani ya mitandao pamoja na kufuatilia vyombo mbalimbali vya habari
kuhusiana na biashara hii ya chakula.
Katika vipengele vyote
vikubwa 3 walivyochunguza, soko ndiyo kitu muhimu zaidi na kilichohitaji majibu
yenye uhakika mkubwa kwani kuanguka au kushamiri kwa biashara yeyote ile
kunategemea sana kitu hiki, soko. Ilikuwa ni lazima kulijua soko lao vizuri na
kwa kina sana ili kujiridhisha ikiwa kama kweli biashara hii inao uwezo wa
kuwaletea faida. Ijapokuwa biashara ya cafe ni moja ya biashara yenye faida kubwa na ya haraka wakati mwingine hata mara 2 ya mtaji uliowekezwa lakini ukikosea kwenye soko hasa eneo basi utaishia kulia na kusaga meno
Majibu ya maswali hayo yote
yatawawezesha hapo baadae katika kuandika mpango wa biashara hii kuweka
mikakati mbalimbali ya kufanikisha biashara yao.
NJIA
KUU 3 UNAZOWEZA KUZITUMIA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA YAKO
Baada ya kufanya utafiti wa biashara yako na kufahamu
mambo mengi kuihusu sasa unaweza kuandika mpango wa biashara yako ya Cafe au
nyingine yeyote kwa kutumia moja kati ya njia 3 zifuatazo;
1. kufuata
mfululizo wa vipengele vinavyounda mpango wa biashara
2. .......................................................
3. .......................................................
Ili kupata somo lililokamilika, tafadhali Jiunge na darasa letu la Michanganuo-online
Hapa kwenye somo hili nitatumia njia ya 1 ya kufuata
mfululizo wa vipengele vinavyounda mpango wa biashara. Mlolongo wa vipengele
hivyo muhimu ni huu ufuatao;
1.0
MUHTASARI TENDAJI
2.0
MAELEZO YA KAMPUNI / BIASHARA
2.1
Malengo
2.2
Dhamira kuu
2.3
Siri za mafanikio
2.4
Umiliki wa Biashara
2.5
Kianzio(kwa biashara mpya au historia kwa kampuni
iliyokwishaanza)
2.6
Eneo la biashara na vitu vilivyopo
3.0
BIDHAA au HUDUMA
3.1
Maelezo ya bidhaa/huduma
3.2
Utofauti wa bidhaa/huduma na za washindani
3.3
Vyanzo vya malighafi/bidhaa
3.4
Kopi za matangazo
3.5
Teknolojia
3.6
Bidhaa au Huduma za baadae
4.0
TATHMINI YA SOKO
4.1
Mgawanyo wa soko
4.2
Soko lengwa
4.2.1
Mahitaji ya soko
4.2.2
Mwelekeo wa soko
4.2.3
Ukuaji wa soko
4.3
Tathmini ya sekta
4.3.1
Washiriki katika sekta
4.3.2
Usambazaji 4.3.3 Ushindani
4.3.4
Washindani wako wakubwa
5.0
MIKAKATI NA UTEKELEZAJI
5.1
Nguvu za kiushindani
5.2
Mkakati wa soko
5.2.1Kauli
ya kujipanga katika soko
5.2.2
Mkakati wa bei
5.2.3
Mkakati wa matangazo/promosheni
5.2.4
Programu za masoko
5.3
Mkakati wa mauzo
5.3.1
Makisio ya mauzo
5.3.2
Programu za mauzo
5.4
Mkakati wa ushirikiano
5.5
Vitendo na utekelezaji
5.5.1
Uendeshaji
6.0
MAELEZO YA UONGOZI NA WAFANYAKAZI
6.1
Mfumo wa uongozi
6.2
Timu ya uongozi na wafanyakazi
6.3
Mpango wa mishahara
7.0
MPANGO WA FEDHA
7.1
Dhana/makisio muhimu
7.2
Tathmini ya mauzo ya kurudisha gharama (Break Even
Analysis)
7.3
Makisio ya faida na hasara
7.4
Makisio ya mtiririko wa fedha
7.5
Makisio ya mali na madeni (mizania ya biashara)
7.6
Sehemu muhimu za biashara
8.0
VIELELEZO/VIAMBATANISHO
•
Taarifa za mahesabu ya fedha kwa undani
•
Mahesabu yako ya nyuma
•
Leseni, vibali ripoti za kodi, hatimiliki na alama za biashara
•
Mikataba mbalimbali
•
Orodha ya mali na vifaa mbalimbali (Dhamana)
• CV
za viongozi na wafanyakazi muhimu
•
Kopi za matangazo ya biashara.
JALADA
LA NJE LA MPANGO WA BIASHARA
Jalada la nje au (Cover page), hiki siyo moja kati ya vipengele vya mpango wa biashara lakini ni sehemu muhimu sana na ambayo ndiyo msomaji wa mpango wako huanza kukutana nayo mbele kabisa kabla hajafungua ndani kuona kuna nini.
Juu ya jalada au ‘cover page’ panawekwa vitu
vifuatavyo;
1. Jina
la biashara/kampuni
2. Mwaka
na tarehe ya kuandikwa
3. Anuani
ya biashara
4. Unaweza
pia ukaweka namba ya toleo, majina ya walioandaa, logo ya biashara/kampuni
pamoja na hadhira (kwa wale mpango unakolengwa kwenda).
Hata ikiwa hutaweka kila
kitu kilichoorodheshwa hapo juu lakini angalau jina la biashara, mwaka na
anuani ya mwandishi au biashara visikosekane. Jalada la mchanganuo wa biashara
ya Upendo Cafe unaweza kuliona hapa chini;
Mpaka
kufikia hapo, kwa siku ya leo tumefika mwisho wa somo letu la kuandika
mchanganuo wa biashara ya chakula ya UPENDO CAFE hatua kwa hatua. Tukutane tena
kesho tarehe 26/12/2022 na tutajifunza vitu vifuatavyo;
1.
Muhtasari
Tendaji (Executive Summary)
2.
Maelezo
ya Biashara/Kampuni (Business Description)
3.
Maelezo
ya Bidhaa/Huduma (Products/Service Description)
Kumbuka
pia mwisho wa somo hili tutaunganisha vipengele vyote 8 na kupata mchanganuo
kamili wa biashara hii ya UPENDO CAFE.
Kupata
mfululizo kamili wa mafunzo haya, jiunge na Familia yetu ya MICHANGANUO-ONLINE
mahali ambapo tunajifunza michanganuo ya biashara kwa kina kabisa pamoja na
masomo adimu ya fedha usiyoweza kuyapata mwingine kokote.
Kujiunga
lipia ada yako ya mwaka sh. Elfu 10 kwa namba 0712202244 au 0765553030 jina
Peter Augustino Tarimo na nitakuunganisha papo hapo pamoja na kukutumia vitabu
na michanganuo ya bure. Ndani ya channel yetu ya Telegram pia utakutana na
Masomo mengine yote ya fedha tuliyojifunza siku za nyuma.
Njoo
na swali lolote kuhusu michanganuo na ikiwa una Biashara yeyote ile ambayo
ungependa tuiandikie mchanganuo wake hatua kwa hatua ndani ya group njoo nayo pia. Usikose kesho muendelezo wa somo hili.
Somo limeandaliwa na
Peter Augustino Tarimo
Business Plan expert
3. Unajua bishara ya chipsi kuku, soda inavyolipa Dar?
4. Chakula cha kuku wa kienyeji kina tofauti gani na cha kuku wa kisasa?
0 Response to "KUANDIKA MPANGO KAMILI WA BIASHARA YA CAFE, MTAJI MILIONI 3 (3,000,000/=)"
Post a Comment