SIKU
YA PILI 26/12/2022, KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, UPENDO CAFE HATUA KWA HATUA
Habari za muda huu ndugu mdau wa masomo haya;
Katika mafunzo yetu leo tutakwenda kuona jinsi ya kuandika
vipengele vitatu ambavyo ni kati ya vile vipengele 8 vinavyounda mchanganuo
mzima wa biashara yetu kama tulivyoona jana. Navyo ni;
1.
MUHTASARI,
2.
MAELEZO
YA BIASHARA na
3.
MAELEZO
YA SOKO
Baada sasa waanzilishi wa cafe huu kumaliza kazi ya
kufanya utafiti wa biashara yao kwa kina
na kupata majibu ya maswali mbalimbali, kilichobakia ni wao kuketi chini na
kuanza kuandika vipengele kimoja baada ya kingine hadi mwisho.
Hawafungwi na ni kipengele gani waanze nacho ila tu
kurahisisha mambo mimi nimeonelea hapa tuanze na kipengele cha kwanza (muhtasari)
na kuendelea jinsi mfululizo wa vipengele rasmi unavyoonyesha. Tungeliweza hata
kuanza katikati au karibu na mwishoni kwa mfano kipengele cha Uongozi na
wafanyakazi ilimradi tu wakati wa
kumaliza basi tukumbuke kuja kuvipanga jinsi mlolongo unavyotaka viwe.
Samahani
kidogo kuna kitu nilisahau jana, baada ya Jalada la nje tulitakiwa kuona YALIYOMO ni nini kinakaa pale, sasa
ngoja nizungumzie hapo kidogo ingawa tulitakiwa tufanye hivyo jana.
Ukurasa
wa Yaliyomo ni muhimu na pale ndipo unatakiwa kuorodhesha yale mambo yote
muhimu katika kila sura pamoja na namba za kurasa mambo hayo yanakopatikana
kusudi wasomaji iwe rahisi kwao kujua ni vitu gani andiko lako limebeba na vipo
wapi.
Sasa hebu tuanze rasmi mada zetu za leo;
1. MUHTASARI
TENDAJI
Hii ndiyo sehemu/sura ya kwanza kabisa kwenye mchanganuo
wako. Ingawa inaanza mwanzoni lakini ndiyo huandikwa mwishoni baada ya kumaliza
kuandika sura nyingine zote. Hapa tutaelezea tu jinsi ya kuiandika lakini ya UPENDO
Cafe tutaandika mwishoni.
Wakati wa kuandika Muhtasari wako unatakiwa kuchagua zile
pointi muhimu tu za mchanganuo wako. Unaweza kuchukua ufupisho wa kila sura
ambao tutakwenda kuona wakati wa kuandika sura zingine au hata ukachagua
sentensi moja moja au chache kwenye kila sura na kuunda Muhtasari wako na hapo
unakuwa umemaliza.
2.0
MAELEZO YA BIASHARA/KAMPUNI
Sura hii ni ya pili na huwa ina vipengele vyake vidogo
kama tulivyokwishaona jana, ambavyo kila kimoja inabidi ushughulike nacho peke
yake. Vipengele vyake hivyo vidogo ni hivi vifuatavyo;
2.0
MAELEZO YA KAMPUNI / BIASHARA
2.1 Maono
2.2
Dhamira kuu
2.3 Malengo
2.4
Siri za mafanikio
2.5
Umiliki wa Biashara
2.6
Kianzio(kwa biashara mpya au historia kwa kampuni
iliyokwishaanza)
2.7 Eneo la biashara na vitu
vilivyopo
Kwanza Sura yeyote ile huanza na muhtasari wa sura nzima
ambao pia huandikwa mwishoni baada ya kumaliza sura husika. Sasa baada tu ya
neno MAELEZO YA KAMPUNI pale juu chini yake acha nafasi kwanza (kama nilivyofanya mimi) ya kuja kuandika
muhtasari wa sura yako kisha endelea na Maono...........
2.1
Maono
Maono ni picha pana ya biashara yako unayotaka uione
baada ya muda kupita, (You visualize)
mara nyingi huwa ni muda mrefu. Biashara yako inaweza ikawa ni ndogo tu lakini
maono yako ni lazima yawe makubwa (think
Big but start small), na kwenye
biashara hii ya Upendo maono yao ni haya hapa;
Kuja kumiliki msururu wa Migahawa mikubwa nchini Tanzania.
2.2
Dhamira kuu
Dhamira kuu ni ile biashara unayoifanya. Kwa mfano kwa
kuwa Upendo ni biashara ya chakula basi dhamira kuu ya waanzilishi wake ni
lazima ionyeshe ni kitu gani wanakusudia kukifanya. Lakini pia katika kuelezea
kile unachokusudia kukifanya unaweza kuongezea na ubunifu fulani katika
kujitofautisha na biashara nyingine kama yakwako, kwa mfano ukasema wewe
dhamira yako ni kutoa huduma za chakula mahali fulani lakini siyo chakula
ilimradi tu ni chakula bali ni chakula
bora kisichokuwa na mafuta mengi. Dhamira kuu ya Upendo ni hii hapa;
“Kuuza vyakula na vinywaji
baridi ikiwemo supu na chapati laini kwa madereva wa vyombo vya usafiri wa umma
na abiria katika stendi ya Goba Njia nne Ubungo Dar es salaam”
2.3
Malengo.
Tuingie kwenye Malengo. Hizo namba mwanzoni nimeweka
kuonyesha msisitizo kwamba namba ni sura ya 2 kipengele cha 3, ila unaweza
kutumia staili nyingine yeyote ile.
Malengo unataja vile vitu unavyokusudia kuvipata baada ya
kutekeleza mpango wako katika kipindi fulani, navyo vinaweza kuwa ni mauzo,
faida, idadi ya wateja, idadi ya wafanyakazi, au kitu kingine chochote kile. Malengo mazuri ni
lazima yawe halisi, yanayopimika, yenye kutekelezeka na yaliyokuwa na muda
maalumu wa utekelezaji.
Bibi Gladys na Mariam wameyataja malengo yao kwa Upendo
Cafe kuwa ni haya yafuatayo;
1.
Kukanda kilo 5 za unga wa ngano kwa ajili ya chapati na
vitafunwa vingine kama maandazi kila siku
2.
Kununua kilo 5 za nyama ya ngombe kila siku kwa ajili ya supu,
mishikaki na mchuzi wa vyakula
3.
Kupata faida kila siku ya shilingi elfu 78
4.
Kufikisha mauzo ya shilingi milioni 100 kwa mwaka
5.
Kufungua tawi la kwanza ifikapo mwaka wa 3
Kama ulivyoona hapo, hivyo vipimo kama, kilo 5, kwa siku, mwaka, na mwaka wa 3 ni muhimu sana kwani ndio vitu vinavyoonyesha
malengo yao yanapimika, kutekelezeka na yana muda maalumu.
2.4
Siri za mafanikio
Hiki ni kipengele kingine kidogo ndani ya kipengele
kikubwa cha Maelezo ya Biashara/Kampuni.
*(Kumbuka vipengele
hivi vidogo na hata vikubwa siyo lazima kwenye mchanganuo wako uviweke vyote
kama vilivyo hapana, itategemea kama kina umuhimu wa kukiweka. Kuna aina au
biashara nyingine kipengele fulani hakina umuhimu (irrelevant))
Siri za mafanikio maana yake
utaorodhesha yale mambo muhimu kwako utakayoyapa kipaumbele katika biashara
yako kusudi uweze kufanikiwa.
Upendo Cafe siri zao za
mafanikio ni hizi hapa chini;
· Uwezo wetu wa kuchagua
Eneo zuri lililo na iadi kubwa ya watu
· Kupunguza gharama
mbalimbali kwa kadiri iwezekanavyo, zile za moja kwa moja na zile za kudumu
· Kujijengea uwezo mkubwa wa
kutambulika sokoni kupitia matangazo na ujenzi wa jina zuri katika jamii
inayotuzunguka.
2.5
Umiliki wa Biashara
Hapa taja jina kamili la
biashara na mmiliki au wamiliki wake ukielezea aina ya usajili kisheria kama ni
ya mtu binafsi, ubia au kampuni. Eleza
kama ni wamiliki zaidi ya mmoja, kila
mmoja anamiliki hisa kiasi gani. Taja na sababu za kuchagua aina ya umiliki
uliochagua. Hebu tuone Upendo waliandika nini;
Biashara itakuwa chini ya umiliki wa ubia kati ya kina mama
wawili, Bibi Gladius Msaki na Bibi Mariam Salim, wote wawili wakiwa na umiliki
wa asilimia 50 kila mmoja. Sababu za kuchagua aina hii ya umiliki kisheria ni
urahisi wake katika maswala mbalimbali kama ya ulipaji wa kodi na upatikanaji
wa mtaji.
2.6
Kianzio
Kwa kuwa ni biashara mpya inayoanza tutachora jedwali la
mahitaji yote kisha jingine la vyanzo vya mahitaji hayo kama ifuatavyo;
Mahitaji yetu ni gharama zote
zitakazotumika pamoja na rasilimali zote zitakazohitajika
Mahitaji:
Gharama za
Awali |
Tsh |
Ukarabati
chumba cha biashara |
150,000 |
Usajili na
vibali |
50,000 |
Matangazo |
50,000 |
Mengineyo |
50,000 |
Jumla |
300,000 |
Rasilimali
za kudumu (Vifaa na mashine)........
0 Response to "MAFUNZO YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA UPENDO CAFE SIKU YA PILI 26/12/2022"
Post a Comment