Utajibu vipi kama
nikikuuliza, Je, unataka mwaka 2023 ujaliwe bahati, pesa na kila fursa za
mafanikio? Ikiwa jibu lako ni ndiyo, basi somo hili ni kwa ajili yako, endelea
kusoma. Ikiwa jibu ni hapana, basi samahani naomba uishie hapohapo na muda wako
ukafanye jambo jingine chanya la kukusaidia maishani.
Duniani hakuna mtu anayeweza
akapinga kwamba bahati zipo na mtu yeyote yule anaweza akaipata, lakini pia
ninaamini kwamba mtu anaweza akajitengenezea bahati yeye mwenyewe kwa
kudhamiria.
Zifuatazo ni njia 9 za nguvu
mtu unazoweza kuzifuata mwaka huu mpya wa 2023 na ukajitengenezea chansi kubwa
ya wewe kupata mafanikio makubwa na bahati maishani.
2.
Rekebisha upya mtazamo wako juu ya pesa
Ni nini unachoamini juu ya
pesa? Je, unaamini kwamba pesa ni shetani na kamwe tajiri hatauona ufalme wa
Mbinguni? Kama unaamini hivyo na vitu vingine vinavyofanana navyo, basi kuanzia
sasa acha kabisa na uanze kuamini kwamba unastahili kumiliki utajiri, kwamba
pesa ni kitu kizuri na pia anza mara moja kufikiria mambo yote mazuri unayoweza
kuyafanya kwa kutumia pesa. Ndiyo, unastahili kuwa na pesa hivyo zidai ni haki
yako!
3.
Kuwa mvumilivu
Waswahili wana usemi usemao,
Roma haikujengwa kwa siku moja. Kiukweli Roma inayosifika leo hii ilijengwa
ukuta kwa ukuta, jiwe kwa jiwe na Watawala au Wafalme zaidi ya 70 katika
nyakati tofauti. Na wewe sasa amua ni kitu gani unachokitaka kisha uanze kwa
vitendo kufanyia kazi malengo yako hayo kwa uvumilivu mkubwa. Uvumilivu siyo
blaa blaa wala maneno matupu bali kitu cha kutia kwenye matendo.
5.
Kufikiri Chanya
Watu walio na fikra chanya
siku zote ndio walio na bahati. Wanao uwezo mkubwa na wa ajabu wa kuziona fursa
na suluhisho mahali ambapo walio na fikra hasi hawawezi kamwe kuona. Kuna usemi
mwingine mashuhuri ndani ya kitabu cha Fikiri & Utajirike usemao, Kile unachofikiri siku zote ndicho unachokuwa,
hivyo anza sasa hivi kujijengea fikra chanya akilini mwako kwani hakuna
chochote kile kizuri unachoweza kukipata kwa kuanza kufikiria karibu kila kitu
katika mlengo hasi.
6.
Kuwa na Maono
Ikiwa
kitu huwezi kwanza kukimiliki akilini basi na kamwe hutaweza kukimiliki
mkononi, Hii ni busara nyingine kubwa niliyojifunza ndani ya
kitabu cha Fikiri & Utajirike (Think & Grow rich). Matajiri wote
uwaonao leo, waliota kwanza utajiri wao akilini kabla hawajaupata. Anza sasa
kuwaza na kuona akilini mwako kila bahati na utajiri duniani vikivutwa kwako
mithili ya vile sumaku ivutapo misumari au vyumavyuma vingine.
8.
Fahamu kile unachokitaka
Ikiwa kama Pesa ndiyo kitu unachotaka
kukipata mwaka 2023, ni wakati sasa wa kuchagua, andika mahali malengo yako na
hatua za kuchukua ili kuyafikia. Kama malengo yako ni ya kiafya pia fanya
hivyohivyo, andika ungetaka pengine kupunguza uzito kilo ngapi na utaruka kamba
kila siku mara ngapi nk. Unataka kuanzisha biashara fulani au ungependa
kuiboost biashara ndogo uliyonayo ili ikuingizie pesa hata kama umelala usiku? Chukua kalamu na
karatasi andika mikakati yako hata kama siyo kwa undani sana au njoo
MICHANGANUO=ONLINE tunaandika michanganuo kila siku na malengo ya biashara
mbalimbali.
9.
Samehe na Sahau
Watu walio na bahati za
mtende huwa kamwe hawachafui ulimwengu wao kwa vitu hasi. Wanajua roho ya
Ibilisi ipo na inaishi. Kwahiyo kuwa makini sana na nguvu unazozitoa. Msamehe
kila mtu aliyekutendea ubaya na uwatakie kheri. Kuondoa vizingiti kutakufungua
mwenyewe ili bahati iweze kugeuza makazi ya Neema na Utajiri ndani yako .
........................................................
Mpendwa mdau
wa blogu hii, niwie radhi kwa kutokuweka makala hii hapa nzima, utaona nilitaja
njia 9 lakini ya 1, ya 4 na ya 7 hazipo, sababu ni kwamba tuna masomo ya aina
mbili, kwa ajili ya group la MICHANGANUO na megine kwa ajili ya blogu hii. Hili
ni la group na hapa tunaweka sehemu tu, mtu akivutiwa basi anajiunga na group
kupata masomo kamili. Zamu ya somo la blogu tunaweka somo kamili.
Tunayo masomo
zaidi ya 100 ya kipekee katika channel ya MICHANGANUO-ONLINE ambayo kila
mwanachama anuwezo wa kuyasoma yote. Unakaribihswa sana kupata na offa yetu ya
vitu 22+ leo kwani kesho ndiyo mwisho wake
Mafunzo ya
kuandika mchanganuo wa UPENDO CAFE nayo yanaendelea na leo ni siku ya pili ambapo
tutaandika maelezo ya Biashara na Bidhaa/huduma hatua kwa hatua. Bofya
hapa>>> kusoma dondoo za somo la jana
Kucheki jinsi wadau wanavyo changamkia Offa na vitabu vyetu bofya hayo maandishi.
SOMA PIA NA
HIZI HAPA;
1. Kwanini vitabu na semina za elimu ya pesa na mafanikio haviwasaidii watu wengi?
2. Je, ipo kanuni ya mafanikio ya kifedha? Mtazamo wa kisaikolojia
3. Salamu zangu mwaka mpya kukutakia heri na mfanikio ya kweli 2023
4. Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio & utajiri wa haraka
0 Response to "NJIA TISA (9) ZA KUKUSAIDIA KUVUTA PESA, BAHATI NA MAFANIKIO 2023"
Post a Comment