TATHMINI
YA SOKO, MIKAKATI & UTEKELEZAJI
Karibu tena ndugu msomaji
unayefuatilia masomo haya, leo tutajifunza jinsi wamiliki wa Upendo Cafe
walivyoandika Sura inayohusu Soko na Mikakati & Utekelezaji. Tutaanza na
Sehemu ya Soko.
Taarifa nyingi tutakazotumia
katika kukamilisha kuandika Sura hii ya Soko zitatokana kwa kiasi kikubwa sana
na taarifa zile za Utafiti wa soko la biashara tulizoona wakati tunazungumzia jinsi
ya kufanya utafiti pale mwanzoni.
Taarifa hizo tulisema kuwa
ni kama vile idadi ya wateja watarajiwa, sifa na tabia zao, mahitaji na kipato
chao. Taarifa nyingine ni za bidhaa zitakazouzwa au huduma, sekta ya biashara, washindani,
bei na mfumo mzima wa usambazaji huduma na bidhaa zako.
Hebu sasa tuanze moja kwa
moja kuona Upendo Cafe walielezeaje sura hii, lakini kwanza tutaweka mbele yetu
vipengele vidogo vitakavyotuongoza katika kuandika Sura nzima kama ifuatavyo;
4.0
TATHMINI YA SOKO
4.1
Mgawanyo wa soko
4.2
Soko lengwa
4.2.1
Mahitaji ya soko
4.2.2
Mwelekeo wa soko
4.2.3
Ukuaji wa soko
4.3
Tathmini ya sekta
4.3.1
Washiriki katika sekta
4.3.2
Usambazaji
4.3.3
Ushindani
4.3.4
Washindani wako wakubwa
Kama kawaida Sura inaanza na muhtasari mfupi
ambao huandikwa mwishoni baada ya kumaliza kuandika sura yote kwahiyo ni kama
panaachwa wazi kwanza.
Kisha kinaanza kipengele cha kwanza,
“Mgawanyo wa soko”
4.1
Mgawanyo wa soko
Chini yake panaandikwa makundi mbalimbali ya wateja biashara
ya Upendo cafe inayotarajia kuwauzia bidhaa/huduma zake. Makundi hayo upendo
waliyabainisha kuwa ni;
·
Abiria wa vyombo vya usafiri wa Umma stendi
ya Goba
·
Madereva wa vyombo vya usafiri wa umma stendi
ya Goba
·
Wauzaji wa maduka na biashara za jirani
·
Wakaazi jirani na eneo la stendi ya Goba njia
nne
Makundi yote manne yaliorodheshwa kisha kila moja
kuelezewa sifa na tabia zake (Kidemografia).
4.2
Soko lengwa
Hapa unatakiwa kuchagua kati ya makundi/vipande vya soko
ulivyotaja katika mgawanyo wako wa soko ni makundi au kundi lipi utakalolilenga
zaidi kimkakati kwani huwezi kuyatimizia makundi yote kwa ufanisi.
Upendo wao wamelenga zaidi makundi mawili lile la abiria
na Madereva wa vyombo vya usafiri wa umma. Wametoa pia na sababu za kuyachagua
makundi hayo 2 na namna watakavyoyahudumia kama ifuatavyo;
Katika makundi manne ya
soko kipaumbele chetu kikubwa kitakuwa ni katika makundi mawili ya, Madereva wa
vyombo vya usafiri pamoja na lile la Abiria. Sababu za kuchagua makundi haya
mawili ni kutokana na uwezekano wao wa kununua vyakula vyetu mara kwa mara
kwani hawana muda wa kusubiri vyakula vya majumbani mwao hasa kifungua kinywa
na mlo wa mchana. Juhudi zetu nyingi za masoko zitaelekezwa kwao.
4.2.1
Mahitaji ya soko
Ni lazima katika soko ulilolenga uainishe mahitaji yanayowafanya
wateja wanunue bidhaa/huduma zako. Haulengi kile unachomuuzia mteja bali yale
mahitaji yake unayoyakidhi.
Upendo wao wameainisha mahitaji makubwa ya madereva kuwa
ni muda, kwani kutokana na kukosa muda wa kwenda nyumbani kujipatia chakula
basi watahitaji mahali pa kupata kifungua kinywa asubuhi na lunch mchana, hivyo
upendo watatoa suluhisho hilo kwao na wala siyo chakula au vinywaji;
Watu hasahasa madereva wa vyombo vya usafiri kula kwenye migahawa
na kwa mama lishe imekuwa ni jambo la kawaida kwao sasa hivi kutokana na
kukosekana muda wa kwenda kula majumbani saa za kazi hasa asubuhi na mchana.
Tutatoa huduma zetu tukilenga zaidi masaa hayo ili kukidhi mahitaji yao.
4.2.2
Mwelekeo wa soko
Hapa utaelezea sababu inayoonekana kubadilisha hali ya
soko au biashara. Muelekeo unaweza kuwa, kubadilika mahitaji ya wateja,
kupungua ama kuongezeka idadi ya watu, kuingia kwa staili au fasheni mpya nk.
Kwa upande wa Upendo wao kwa mujibu wa utafiti wa soko
walioufanya walikuta kwamba wateja wao wengi watarajiwa mwelekeo wao ulikuwa ni
kupendelea zaidi kula chapati na supu asubuhi, mchana ugali na nyama choma au
rosti kushinda vyakula vingine. Huu ni mwelekeo ina maana hapo kabla hawakuwa
na tabia hii.
Kulingana na utafiti tulioufanya madereva wengi wa vyombo vya
usafiri wa umma hupendelea zaidi supu na chapati kama kifungua kinywa na mchana
wanapendelea ugali na nyama choma au rosti na ndizi za kukaanga.
4.2.3
Ukuaji wa soko
Katika kipengele hiki unatoa takwimu zinazoonyesha
uwezekano wa soko kukua kama vile, idadi ya wakaazi wa kutosha, kutokuwepo kwa
biashara kama hiyo eneo lile, idadi ya kutosha ya biashara unazotarajia
kuzihudumia. Takwimu utazipata kutoka vyanzo vya takwimu na taarifa
vilivyokwishatajwa.
Upendo kipengele hiki hawakukiweka ila wangeweza kukiweka
kwa kuonyesha jinsi idadi ya madereva na abiria inavyoongezeka na takwimu hizi
wangeliweza kuzipata kutoka ofisi za serikali wilayani au hata takwimu kutoka
mamlaka ya Takwimu ya Taifa au taarifa za sensa ya watu na makazi
4.3
Tathmini ya sekta ................................................
.............................................
Masomo haya yanatolewa ndani ya group la MICHANGANUO-ONLINE kila siku na hii ni sehemu ndogo tu ya somo la leo. Ili kupata masomo kamili pamoja na masomo yote mengine ya siku za nyuma jiunge na group hilo kwa kulipia ada kidogo ya mwaka shilingi 10,000/=. Unaweza kutumia moja kati ya namba zetu hizi, 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo.
0 Response to "SIKU 3 TAREHE 27/12/2022 KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA UPENDO CAFE HATUA KWA HATUA"
Post a Comment