MPANGO WA UENDESHAJI, UONGOZI &
WAFANYAKAZI
6.0
UENDESHAJI
Mara nyingi kipengele hiki hutegemea kama biashara
inahusisha shughuli nyingi za kiuendeshaji mfano kiwanda, au hata biashara ya
uzalishaji bidhaa kama hii ya chakula. Ni kipengele wakati mwingine
kinachojitegemea na ndio maana hata kwenye mchanganuo huu wa Upendo kimepewa
sura yake chenyewe ya 6.
Ikiwa uendeshaji kwenye aina ya biashara yako hauna mambo
mengi basi unaweza kujumuisha vipengele vyake kwenye Sura ya mikakati na
utekelezaji kwani utekelezaji na uendeshaji ni kitu hichohicho kimoja.
Kwenye sura hii ya Uendeshaji kwa kawaida huwa na maelezo ya jinsi biashara
itakavyoendesha mambo mbalimbali kila siku. Hapa chini ni vipengele vidogo
mbalimbali unavyoweza kuvitumia katika sura hii;
1. Hatua mradi ulipofikia
mpaka sasa hivi
2. Mchakato mzima wa
uzalishaji utakavyokuwa
3. Teknolojia/maelezo ya
kiufundi
4. Vihatarishi vya mradi
5. Eneo
6. Vifaa na gharama
mbalimbali
7. Malighafi na vyanzo vyake
8. Masuala ya kisheria
9. Sera ya mikopo nk.
Kama nilivyotangulia kusema, unaangalia tu vile vipengele
vinavyofanya kazi kwenye biashara yako, vingine kama unaona haviendani
unaachana navyo, kwa mfano kwenye biashara hii ya Upendo waliweka vipengele
vifuatavy katika sura yao ya uendeshaji;
Kwanza kwenye Muhtasari wa Sura waliweka maelezo kidogo
ya namna mchakato mzima wa uendeshaji wa shughuli za biashara unavyofanyika
kila siku kisha chini vikaendelea vipengele vingine vidogo vya;
1) Eneo
au Chumba cha biashara
2) Mahitaji
ya Kisheria
3) Tathmini
ya Vihatarishi vya Mradi
4) Vifaa
na mashine
5) Mauzo
na Gharama mbalimbali
Hapa ndipo unapoweza kuonyesha kwa kina jinsi mauzo na
gharama zako zitakavyokuwa na namna ulivyokisia. Kwa mfano katika kukisia Mauzo
ya siku na gharama zake, Upendo walichora jedwali na kuweka safu ya Gharama na
mauzo ambapo kwa kila aina ya chakula yaliwekwa makisio ya mauzo yake kwa siku
na kisha orodha ya gharama za kila aina za vyakula hivyo na jumla yake. Kwa
njia hiyo waliweza kupata jumla ya mauzo yote ya siku na gharama za mauzo hayo
ambazo pia zimeweza kutabiri mauzo ya mwezi na mwaka.
Hapa pia unaainisha gharama zote za kudumu za uendeshaji
wa biashara yako kama Upendo walivyoainisha kwenye jedwali hili hapa chini;
..............................
Tumemaliza Sura au Sehemu yetu ya Uendeshaji sasa tuingie
Sura nyingine ya Uongozi na Wafanyakazi
7.0 UONGOZI
& WAFANYAKAZI
Maelezo haya pia unaweza ukayaita maelezo ya Utawala na
Nguvukazi. Kama kawaida Sura inaanza na muhtasari mdogo unaoandikwa mwishoni na
unaacha kwanza nafasi ya aya moja hivi. Kisha unazingatia vipengele vidogo
vinavyounda sura hii ambavyo mara nyingi huwa ni hivi hapa chini;
7.1 Mfumo/Muundo wa uongozi
7.2 Timu ya uongozi na wafanyakazi
7.3 Mpango wa mishahara
7.1
Muundo wa Utawala
Hapa unaweza ukapaelezea tu kwa maneno ikiwa ni biashara
ndogoisiyo na wafanyakazi wengi au kama watu ni wengi basi unaweza ukatumia
mchoro/chati ya utawala.
7.2
Timu ya uongozi na wafanyakazi
Taja kila kiongozi, wadhifa wake kwenye kampuni, historia
yake kitaaluma na kikazi pamoja na uzoefu aliokuwa nao kulingana na majukumu
atakayokuwa nayo kwenye kampuni. Eleza pia idadi ya wafanyakazi
watakaohitajika, eleza pia kama kuna mapungufu au pengo la utawala kama kuna
watu wanaohitajika lakini bado nafasi zao hazijapata watu na sababu za upungufu
huo.
Kwenye Upendo Cafe baada ya muhtasari wa sura nzima
walielezea mfumo wa utawala kwa maneno kwani biashara haina bado watu wengi;
Timu yetu itakuwa na Mkurugenzi mtendaji mmoja na msaidizi wake
ambao wote ni waanzilishi wenza, mmoja atashikilia nafasi ya mpishi muu na
mwenzake mtu wa manunuzi ya malighafi na vifaa mbalimbali vya biashara.
Kutakuwa pia na wafanyakazi wawili, mmoja atashughulika na kazi ya kuhudumia
wateja wakati mwingine atamsaidia mpishi mkuu jikoni
Kisha walimuelezea kila kiongozi, majukumu yake na sifa
zake.
7.3
Mpango wa Mishahara
Katika kipengele hiki kidogo unaanza na maelezo kidogo
kisha unachora jedwali linaloonyesha kiasi cha mishahara ya wafanyakazi wote
kwenye kampuni kwa kila mwaka kwa miaka yote mitatu. Unaanza kwa kujumlisha
mishahara ya mfanyakazi mmoja mmoja kila mwezi kisha kwa mwaka. Namba hizi ndio
huja kuunganishwa na gharama nyingine za kudumu kwenye ripoti ya Faida na Hasara hapo baadae
kwenye ripoti za fedha;
...............................................
Mpaka
hapo tumemaliza vipengele vyetu kwa siku ya leo tukutane tena kesho kwa sehemu
ya mwisho ya Taarifa za fedha.
Masomo haya yanatolewa ndani ya group la MICHANGANUO-ONLINE kila siku na hii ni sehemu ndogo tu ya somo la leo. Ili kupata masomo kamili pamoja na masomo yote mengine ya siku za nyuma jiunge na group hilo kwa kulipia ada kidogo ya mwaka shilingi 10,000/=. Unaweza kutumia moja kati ya namba zetu hizi, 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo.
0 Response to "SIKU 4 TAREHE 28/12/2022 KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA UPENDO CAFE HATUA KWA HATUA"
Post a Comment