Habari
mpenzi msomaji wa blogu yako hii ya jifunze ujasiriamali, sina shaka umewahi
kusikia juu ya kitabu hiki cha Think & Grow Rich, lakini pengine hujawahi
kuchunguza kwa undani ni kwanini watu wengi hivyo Duniani huwa wanakihusudu,
pengine ni shauri ya lugha ya kizungu iliyotumika, lakini uzuri sasa hivi ni
kwamba hata nakala ya kitabu hicho kwa Kiswahili ipo.
Katika
makala hii ya leo na nyingine nitakazoendelea kukuletea utapata kujua kwa
undani kile kinachofanya kitabu hiki kipendwe mno na watu kote Duniani.
Mwishoni kabisa mwa makala hii pia kuna habari njema kwa wale wote wanaopenda
kujifunza zaidi.
KARIBU....
Falsafa za kitabu mashuhuri cha fedha na mafanikio cha
THINK & GROW RICH (Fikiri & Utajirike) zimetumiwa na matajiri na watu
wengi waliofanikiwa kimaisha pasipo hata wao wenyewe kujua kama wamezitumia.
Mwishoni mwa makala hii pia nitaelezea jinsi baadhi ya
watu mashuhuri na matajiri Duniani walivyoweza kuitumia falsafa mojawapo kwenye
hiki kitabu na kufanikiwa kupata utajiri mkubwa, nitaanza na hapa hapa nyumbani
Tanzania kwa kumzungumzia Diamond Platnumz, Harmonize kisha wengine wa nje kama
kina Elon Musk tajiri namba moja duniani, Michael Jackson, Muhamad Ali, Pele,
Maradona, Neymar, Messi na Ronaldo,
Jambo la kustaajabisha ni pale tu utakapojaribu
kuwafuatilia mabilionea na mamilionea au yeyote aliyepata mafanikio makubwa
katika maisha yake na kubaini kumbe walitumia falsafa na kanuni zilezile
walizotumia wengine wote waliofanikiwa kama yeye, awe ni mtoto tajiri zaidi
Duniani kama Kylie Jenner mwenye biashara ya urembo na vipodozi kule nchini Marekani au mtu
mwingine yeyote tajiri kama alivyokuwa Vladmir Putin wa Urusi na Rais tajiri
zaidi Duniani kwa utajiri wa dola bilioni 69. Wala haijalishi ni kutoka nchi
tajiri zaidi duniani ama ni kutoka nchi masikini.
Katika kitabu hiki chenye siri za matajiri mwandishi
ameziweka falsafa (13) za mafanikio na Utajiri lakini mimi hapa leo nitajikita
zaidi kwenye ile falsafa ama kanuni ya 13 na ya mwisho katika Sura ya 14 kwenye
kitabu iitwayo; MLANGO FAHAMU WA SITA
( Mlango wa hekalu la hekima) kwa
anayesoma nakala ya kitabu ya kiingereza sura hii inaitwa; THE SIXTH SENSE (The door to the Temple of Wisdom) Kwenye
nakala ya kitabu ya Kiswahili iliyotafsiriwa na Peter Augustino Tarimo mwaka
2021, sura hii inapatikana ukurasa wa 335
Falsafa zote 13 za kitabu hiki zinatengeneza orodha ya
matajiri wengi sana duniani wasiokuwa na idadi ila mimi kama nilivyotangulia
kusema nitakwenda kukupatia tu baadhi yao kama mifano
Falsafa ya Mlango fahamu wa sita ni watu wachache sana
wanaoifahamu vizuri na sababu ya kutokueleweka vizuri ni sharti la mwandishi
kwamba ili uweze kuishika vyema ni sharti kwanza uzijue na kuzifanyia kazi falsafa
nyingine zote 12 zinazotangulia. Hata hivyo kwa wale walioweza kuitumia na bado
wakafanikiwa pasipokujua kama walichotumia ni falsafa/kanuni hii inawezekana
kabisa pia walizitumia na hizo kanuni nyingine 12 pasipo hata wao wenyewe
kubaini kama wamezitumia.
Kwani
Mlango Fahamu wa Sita ni kitu gani hasa?
Binadamu tunao ufahamu wa aina mbili, kwanza ni ule
ufahamu wa kawaida tunaoutumia kupitia milango nitano (5) ya kawaida ya fahamu
yaani pua, masikio, ulimi, macho na ngozi,
lakini tunao mlango wa fahamu mwingine wa 6 uliojificha ndani kabisa katika
ubongo wetu, na ambao ni tofauti sana na hiyo mitano. Watu wengi tumezoea
kuuita “MAONO”, ‘MACHALE’ au ‘UFUNUO’.
Je, Umewahi siku moja kutaka kupanda basi stendi lakini
ukasita kidogo kisha ukaamua kurudi nyumbani halafu baadae ukaja kupata taarifa
kwamba lile basi lilienda kupata ajali mbaya ya kutisha? Basi ikiwa ulikuwa
hujui kitu kilichokushitua mpaka ukaahirisha safari kilikuwa ni huo mlango
fahamu wa sita tunaouzungumzia leo na hufanya kazi yake kimaajabu sana kiasi
kwamba wengi huuhusisha na miujiza na siyo kila mtu mlango huu unafanya kazi,
isipokuwa tu habari njema ni kwamba unaweza kujizoesha mwenyewe kwa kutumia
kanuni zilizo ndani ya hii sura ili mlango huo uweze kukufanyia mambo makubwa
ikiwemo kupata utajiri au hata kukulinda na majanga kama ajali nk.
Katika Sura hii ya 14 ya kitabu cha Think & Grow Rich
kuna maelezo ya kutosha ya jinsi mlango fahamu wa 6 unavyofanya kazi na namna
unavyoweza kuutumia kwa manufaa yako mwenyewe.
Sipendi nikuchoshe na maelezo meengi, hebu twende moja
kwa moja kwenye orodha ya matajiri na watu walio na mafanikio kimaisha
nilioahidi pale mwanzoni kukudadavulia jinsi walivyoweza kuutumia mlango fahamu
wa sita kujipatia mafanikio ya kustaajabisha kimaisha. Tutaanzia hapahapa
nyumbani Tanzania;
DIAMOND
PLATNUMZ
Kuna mbinu za kufanya kusudi uweze kujenga uwezo mkubwa
wa kiubunifu (kimaono) kwa kutumia kanuni hii. Mbinu hizo mwandishi mwenyewe
alizitumia kwenye jaribio lake na zikafanya
kazi vizuri katika kile alichodai ni Mikutano na Washauri wake wasioonekana uk.
Wa 338 Sura ya 14
“Zamani kabla hata sijawahi kuandika mstari wa
chapisho, au kujaribu kutoa hotuba kwenye hadhara nilifuatilia tabia ya
kurekebisha tabia yangu mwenyewe kwa kujaribu kuwaiga watu tisa ambao maisha
yao na kazi vilinivutia sana. Watu hao tisa walikuwa ni, Emerson, Paine,
Edison, Darwin, Lincoln, Burbank, Napoleon, Ford na Carnegie. Kila siku kwa
kipindi kirefu cha miaka niliitisha mkutano wa kufikirika na kundi hili
niliowaita, ‘Washauri wangu wasioonekana’”
Na unapomwangalia msanii Diamond Platnum anafanya vitu
vilevile vinavyofanana na vile alivyoshauri mwandishi vifanyike kumuwezesha mtu
anayetamani kuukuza uwezo wake wa mlango fahamu wa 6. Nisichokijua ni ikiwa Diamond anafahamu kama anachokitumia ni
falsafa hii.
Mbinu
ya Kujishauri Binafsi, kwa kimombo “Autosuggestion”
Katika mbinu hii mhusika anayetaka mafanikio, iwe ni
utajiri wa pesa, mafanikio kwenye sanaa au michezo mfano kwenye mchezo wa mpira
wa miguu (soka), Kuimba (uanamuziki), mchezo wa ngumi (ndondi) nk. huwa wana
iga ama kujifananisha na magwiji waliowatangulia, unaweza ukasema wanawatazama
Role models wao na kukariri ama kujizoesha vitendo na nyendo zao zote nzuri
mpaka kufikia hatua ya akili zao za ndani kabisa au tunaweza kusema Milango
fahamu yao ya sita kuwasaidia moja kwa moja kutimiza ndoto zao tofauti na wale
wanaotamani tu kutimiza ndoto zao kwa kutumia milango fahamu mitano (5) ya
kawaida bila ya mafanikio.
“Kupitia msaada wa Mlango-fahamu wa sita utatahadharishwa juu ya hatari
zinazokunyemelea katika muda muafaka ili kuzikwepa, na kuarifiwa juu ya fursa
kwa wakati ili kuzitumia.
Unapoukuza mlango-fahamu wa sita unakupa msaada, na kufanya kile
utakacho, huja malaika mlinzi ambaye muda wote atakufungulia mlango kuelekea
hekalu la hekima” Uk. 336 Sura: 14
Hali kadhalika unapomtazama Mwanamuziki Diamond au Naseeb
Abdul, ijapokuwa watu wengi wanaweza wakawa hawajastukia lakini huu ndio ukweli
wenyewe, kuna mahali Diamond anapokuwa jukwaani hahasa kwenye uchezaji wake
utabaini fika kuna mahali anaigilizia miondoko ya Mfalme wa Pop Duniani Michael
Jackson, Diamond hakuna mahali amewahi kutamka rasmi anavutiwa na Michael
Jackson, hii ni observation yangu
binafsi tu kama mimi. Hata katika
video ya wimbo wake mmoja uitwao Baba lao na baadhi ya show zake nyingine kuna
vitu vingi unaweza ukafananaisha na filamu ya Thriller ya Michael Jackson.
Inawezekana kabisa Diamondo hukaa mahali na kutizama
magwiji kwenye tasnia yake Ulimwenguni wanaomvutia, jinsi walivyokuwa
wakifanya, wanamsisimua kiasi mpaka mlango fahamu wake wa 6 unaiga hata pasipo
mwenyewe kujua ameiga kitu kwao. Diamond aliwahi kunukuliwa na media akitamka
kwamba, ‘Hakuna jipya chini ya jua,
miziki inayoimbwa leo ilishaimbwa kitambo na kikubwa wanamuziki ni kuongezea tu
ubunifu.’
HARMONIZE
Ukiwacheki vizuri wanafunzi wa Diamond na hasahasa
Harmonize, utabaini hakuwa vile kabla hajajiunga na bosi wake huyo, Sasa hivi
Harmonize anafanya mambo yake mengi utadhani ni Diamond, ‘swaga’ zake na hata
miondoko unaweza ukaifananisha na ile ya bosi wake mpaka vaa yao. Harmonize
ameiga mpaka ile hulka ya Diamond ya kutokutulia na kina dada.
MICHAEL
JACKSON MWENYEWE
Usije ukadhani labda Michael Jackson staili na ‘swaga’
zake zoote zile alizipata tu hewani hivihivi kutokea kusikojulikana hapana,
tunaporejea ule msemo, Hakuna jipya chini ya jua, Michael Jackson kuna magwiji
hata zaidi yake nao waliokuwa wamemtangulia na ambao kwa kiasi kikubwa ndio
waliomfanya awe kama alivyokuwa.
Mwimbaji mwingine mashuhuri wa Pop na Rock duniani miaka ya 50 na 60 Elvis Presley maarufu kama Sukari ya Warembo kwa jinsi alivyopendwa mno na kina dada, uchezaji wake hata leo ukiamua kutizama video zake utakubaliana nami kwamba ulimwathiri kwa kiasi kikubwa sana Michael Jackson ingawa yeye mwenyewe Michael Jackson alikuwa akikanusha kwamba Presley hakuwa kabisa akimhamasisha. Wimbo wa Michael Jackson wa “This Place Hotel” ambao kwa kiasi kikubwa ulifanana sana na ule wa Ellvis uitwao “Heart break Hotel.” ni ushahidi tosha kwamba Elvis alimhamasisha sana Michael Jackson sema tu ni vile hulka ya watu wengi wanapopata umaarufu huwa hawapendi sana kuweka wazi watu halisi waliowahamasisha, pengine kutokana na kuhofia ushindani au watu kushusha thamani yake. Hivyo hapana shaka Michael Jackson alikuwa akivutiwa sana na Elvis Presley.
AKINA
NEYMAR, LEONEL MESSI NA RONALDO
Inasemekana hakuna kipya hata kimoja wanachokifanya wanasoka
mashuhuri wakati wa leo, mengi wanayarudia yaleyale aliyokuwa akiyafanya Mfalme
wa soka duniani Pele miaka ile ya 60, 70 na 80 pamoja na wengineo kama vile
Maradona miaka ya 80 na 90. Neymar hata pale alipofariki Pele hivi karibuni
alisikika akisema kwamba alikuwa ndiyo mtu wake wa mfano, role model, na si
yeye tu bali ni takriban karibu wanasoka wote wakubwa duniani walijaribu kuwa kama Pele.
MUHAMMAD ALI
Mfalme huyu wa Masumbwi Duniani wa wakati wote wala yeye hakuhangaika kuwatumia watu wa mifano katika kuukuza mlango fahamu wake wa 6 bali alitumia mbinu ya kujishauri binafsi yeye mwenyewe kwa kuuzoesha maono ya ushindi mlango fahamu wake wa 6 mwenyewe kiasi kwamba kufanikiwa kwake hakukuepukika kabisa. Alisifika kwa kauli zake mashuhuri za kimaono kama vile, “you’ve got to float like a butterfly and sting like a bee.” (Unapaswa kuelea kama kipepeo na kuuma kama nyuki). Nyingine ni; "I am the greatest, I said that even before I knew I was." (Mimi ni mkali, na nilisema hivyo hata kabla sijajua nilikuwa hivyo)
Miaka ya nyuma kidogo hapa nchini kulikuwa na wimbi la vijana wasanii kupenda kuwaigiza wasanii wakubwa wa muziki kutoka nje kama vile kina Michael Jackson, Kanda Bongoman na wengineo, ungesikia watu wakisema Kanda Bongoman wa Tanzania. Michael Jackson wa Bongo nk. na kweli walifanana nao kwa karibu kila kitu kuanzia uchezaji, uimbaji na hata mavazi yao. lakini nafikiri walichokuwa wakikikosa hapa ni ile kutumia milango fahamu yao ya 6 sawa na wale niliowataja pale juu na ndio sababu pengine hatukuweza kuwashuhudia wakifika mbali sana na hata kuwazidi waimbaji orijino, waliishia tu kusikojulikana na maslahi kidogo waliyojipatia.
ELON
MUSK
Tajiri wa kwanza Duniani 2022 Elon Musk, wakati alipokuwa
akianza miradi yake ya anga za juu Space X na ule wa magari ya umeme Tesla
hakuwa na mtaji wa kutosha akajaribu kuwafuata wawekezaji wakubwa lakini kila
aliyemfuata alikataa kwa madai kwamba miradi hii ilikuwa ni ndoto za alinacha
(pipe fantacy/dream) na kweli walikuwa sahihi kwani ni watu wengi walikuwa wamekwishajaribu
miradi kama hiyo ikawashinda, hata NASA wenyewe ingawa walifanikiwa miaka ya 60
na 70 lakini ilikuja kuwashinda shauri ya gharama kuwa mno kubwa.
Lakini ni kwa msaada tu wa Mlango Fahamu wa Sita wa bwana
Elon Musk uliomwambia hata kila mtu akiona haiwezekani, lakini itawezekana.
Elon akatumia mpaka senti yake ya mwisho kabisa kugharamia miradi hii kwa ugumu
ajabu! na mwishowe mwanaume akatoboa na mpaka hivi niandikapo hapa ndio Tajiri mkubwa
zaidi Duniani akimiliki Dola Bilioni
239.2
Amewezesha tena mashindano ya kwenda sayari za mbali
kuanza upya kwa kuvumbua roketi ya gharama nafuu yenye uwezo wa kwenda sayari
za mbali na kurudi Duniani ikaja kutumika tena badala ya zile za NASA na za Warusi
za miaka ya 60 zilizokuwa zikishaenda huko anga za mbali huishia hukohuko na
hivyo kufanya zoezi zima kuwa la gharama za kutisha.
HITIMISHO
Kitabu hiki cha Think
& Grow Rich kina kanuni nyingi na hatua za mafanikio za kuchukua kusudi
mtu uweze kufanikiwa katika jambo lolote lile maishani ikiwemo kifedha na leo
nimegusa tu falsafa moja ama mbinu moja kati ya zile 13. Vyanzo vya utajiri wa
matajiri wengi utakuta asili yake ni matumizi ya falsafa hizi wawe wanajua au
hawajui kama walizitumia. Huna haja ya kwenda kwa mganga kusaka dawa ya
mafanikio wakati unaweza kujifunza elimu ya pesa na jinsi ya kuwa tajiri haraka
kupitia vitabu kama hiki cha Think and Grow Rich, tena kwa lugha yako ya mama.
Ikiwa utapenda kusoma nakala yako ya Kiswahili basi
unaweza kuamua moja kati ya haya mawili;
1.
Kusoma nakala laini (softcopy) kupitia simu yako ya mkononi-smartphone.
Bonyeza link ifuatayo, >>GETVALUE, kisha kwenye mtandao huo wa GETVALUE, fanya manunuzi kwa kujaza taarifa zote utakazoelekezwa pamoja na kulipia kitabu sh. Elfu 10 kwa mitandao ya simu. Kisha nenda play store download application(APP) ya GETVALUE, Jaza tena taarifa ulizotumia wakati wa manuuzi, ambazo ni email na password na hapo APP itafunguka utasoma kitabu chako.
2.
Kusoma Nakala ngumu (Hardcopy)
Wasiliana nasi kwa namba 0712202244 na tutakuletea mpaka pale ulipo Dar es salaam
kwa sh. 25,000/= Mikoani tunatuma kwa mabasi kwa sh. 35,000/=
HABARI
NJEMA ZAIDI KWA WALIOKOSA OFFA ZETU 2022
Kutokana na maombi ya wadau wetu wengi tumeamua kusogeza
mbele kidogo muda wa zawadi yetu au OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA tuliyofunga nayo
mwaka. Sababu kubwa ni kwamba wadau wengi wanasema muda ulikuwa mfupi mno na
hawakuwa wamejiandaa vizuri.
Hata hivyo kutokana na nafasi za kujiunga na group letu
la masomo ya pesa ya kila siku kuwa chache, OFFA hii itadumu hewani mpaka tu
watakapotimia idadi ya members waliobakia group lijae na muda huo hautazidi
mwezi huu wa January 2023.
Hivyo naomba sana wadau mliotuma maoni yenu msichelewe tena safari hii kwani mimi sitaangalia ni nani aliyelalamika bali ni nani aliyechukua hatua ya kuhitaji zawadi hii. Kumbuka vitabu na michanganuo ninayoitoa kama zawadi kwa sh. Elfu 10 thamani yake halisi inazidi sh. Laki moja!
VITU VYA OFFA ISIYOWAHI
KUTOKEA NI HIVI VIFUATAVYO;-
KITABU: Michanganuo ya Biashara na
Ujasiriamali
KITABU: Siri ya Mafanikio ya Biashara
Duka la Rejareja
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30
MCHANGANUO: Kuku wa mayai
MCHANGANUO: Kuku wa nyama - kwa
kiswahili
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa
kiingereza
MCHANGANUO: Kuku wa kienyeji
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za
saruji
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa
Kiswahili
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa
kiingereza
MCHANGANUO: Kiwanda cha Dona (Usado milling)
SEMINA: Jinsi ya kuandika mchanganuo
wa kiwanda cha unga
SEMINA: Kuandika mchanganuo wa kuku
wa nyama
MCHANGANUO: Kuandika mchanganuo wa
Cafe
Lipia offa yako kupitia namba zangu, 0712202244 au 0765553030 kisha ujumbe watsap au sms
usemao;
“NATAKA
OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA”
Na utapata offa zako ndani ya dk. 3 tu
Thamani halisi ya offa hii ni sh. 180,000/= lakini lipa
sh elfu 10 tu uokoe sh 170,000/= !
Ukitaka kuthibitisha uaminifu wetu bonyeza hapa kuona
baadhi ya wadau wengine waliowahi kuchangamkia offa na vitabu vyetu.
1. Mwanasoka Eusebio Da Silva Ferreira ni kama EdsonPele, Muhammad ali na Michael jackson
2.Diamond kama Michael Jackson na wimbo wake My Number One
3. Ili ufanikiwe kuwa Tajiri mkubwa jiepushe kabisa na kauli hizi 4
4. Kanuni kuu ya mafanikio duniani iliyo kubwa kushinda zote
5. Kanuni za mafanikio (The success principles) by Jack Canfield
6. Jifunze kwa waliofanikiwa lakini usiige kila kitu kamakilivyo utafeli
0 Response to "IJUE FALSAFA YA KITABU ILIYOTENGENEZA MATAJIRI & MABILIONEA WENGI ZAIDI DUNIANI"
Post a Comment