Kuna baadhi ya watu wasiojua ukweli wa mambo ulivyo,
wanapotoa maoni yao juu ya kazi ya ajira utawasikia wakiilaumu na kuifanya
ajira kana kwamba haifai kabisa, inamfanya mtu kuwa mtumwa maisha yake yote na
hata wakati mwingine wanafikia hatua ya kutoa viapo kuwa hawatakaa maisha yao
yote waajiriwe.
Lakini wasichokijua watu hawa ni fursa ya ajabu
iliyojificha nyuma ya ajira au kazi ya kulipwa mshahara. Hawajui kama ajira
inaweza kuwa daraja bora kabisa linalowezesha kumvusha mtu mahali ambapo
ingelimchukua muda mrefu sana akihaha (hustling)
huku na kule akisaka mtaji kwa ajili ya kuwekeza katika vitegauchumi vingine.
Jana kwenye darasa letu ndani ya kundi la MICHANGANUO-ONLINE
nilitoa somo lililokuwa na kichwa cha habari, Ili mtu afanikiwe kifedha
anatakiwa kuwa na mifereji mingapi ya kipato? Katika somo hili pia
kulikuwa na swali jingine lililouliza ikiwa mtu mwenye ajira nzuri inayomlipa
mamilioni ya pesa kama kuna umuhimu wowote ule wa yeye kumiliki mifereji
mingineyo ya kipato. Majibu kwa swali hilo niliyatoa ndani ya somo hilohilo na
kwa kweli ikiwa na wewe ni miongoni mwa wale wanaolaani kazi za ajira basi
majibu hayo nadhani yanaweza yakakuacha midomo wazi.
Kwani
mashine ya kutengeneza pesa ni kitu cha namna gani?
Kabla ya kulijua hilo hebu kwanza tuone Mashine ni nini? Kwa
mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu, mashine ni kitu chochote chenye uwezo wa
kurahisisha kazi. Unatumia juhudi kidogo kupata matokeo makubwa zaidi.
Tuchukulie mfano wa gari, ukiambiwa utoke Dar mapaka Morogoro ukitembea kwa
miguu ni kazi ngumu kwelikweli, lakini kwa kutumia gari inakuchukua muda mfupi
sana. Gari ni aina ya mashine na juhudi kidogo unayotia pale ni nauli yako tu.
Hivyo mashine ya kutengeneza pesa haina tofauti na gari tuliloona
hapo juu, unaweka pesa kidogo kupata pesa nyingi ndani ya muda mfupi tena hata
pasipo kufanya kazi yeyote ya ziada zaidi ya nauli yako uliyotoa, hakuna
atakayekuambia njoo ukasukume gari limekwama matopeni labda tu itokee bahati
mbaya sana limeharibika.
Katika makala nzima hii wala dili siyo mashine yenyewe ya kutengeneza pesa bali kitu cha muhimu zaidi ni jinsi gani mtu unavyoweza kugeuza mshahara kuwa mashine ya pesa (mchakato mzima), watu wengi hujaribu na kuishia katika pointi hii. Sasa kaa tayari kabisa nitakwenda kukuelezea ‘exactly’ ni nini cha kufanya (Hatua 4 muhimu sana) ili kuondoa kizuizi hiki na hatimaye kumiliki mashine yako mwenyewe ya kutengeneza pesa itakayoamua mustakabali mzima wa maisha yako ya baadae.
Je ungependa kuzijua hatua (njia) hizo na kuanza
kuzifanyia kazi mara moja? Basi ungana na mimi leo hii tarehe 24/01/2023 saa 3
usiku katika somo hili zima ndani ya MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP kwa
kiingilio cha shilingi elfu 10 tu kwa mwaka mzima. Ndani ya group utakutana na
masomo mengine yaliyopita zaidi ya 80 usiyoweza kuyapata mahali kwingine kokote
nje na ndani ya mtandao.
VITU VYA OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA NI HIVI VIFUATAVYO;-
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali
KITABU: Siri ya Mafanikio ya Biashara Duka la Rejareja
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa
KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30
MCHANGANUO: Kuku wa mayai
MCHANGANUO: Kuku wa nyama - kwa kiswahili
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
MCHANGANUO: Kuku wa kienyeji
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa Kiswahili
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa kiingereza
MCHANGANUO: Kiwanda cha Dona (Usado milling)
SEMINA: Jinsi ya kuandika mchanganuo wa kiwanda cha unga
SEMINA: Kuandika mchanganuo wa kuku wa nyama
MCHANGANUO: Kuandika mchanganuo wa Cafe
1. Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?
2. Ajira siyo laana, ni mtaji wa uhakika kuliko aina nyingine zote za mitaji
3. Kwanini biashara humpa mtu uhuru zaidi wa kifedha kuliko ajira?
4. Kwanini kama huipendi ajira yako bado unaendelea kuifanya?
0 Response to "JINSI YA KUGEUZA MSHAHARA WAKO KUWA MASHINE YA KUTENGENEZA PESA"
Post a Comment