Nimewahi kuandika mara nyingi sana juu ya Mifereji ya
pesa au kipato mpaka nikaandika na kitabu nilichokiita, MIFEREJI 7 YA PESA NA
SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA. Bila shaka yeyote ile mtu kuwa na mifereji ya
kipato ndiyo njia inayotambulika duniani kote kuwa yenye tija zaidi ya
kutengeneza utajiri haraka au kuwa milionea ba hatimaye bilionea (Uhuru kamili wa
kifedha)
Kwani Mifereji ya pesa au Mifereji ya Kipato ni kitu gani? Ni njia za kujiingizia kipato cha ziada nje ya kile mtu unachokipata kutokana na shughuli yako ya msingi unayoifanya, kwa mfano ikiwa umeajiriwa basi ukianzisha mradi wako pembeni, huo ni mfereji wa kipato na ukiwa na biashara moja ukianzisha ya pili basi ile ya pili ni mfereji wa kipato. Kwa ujumla shuguli yako ya msingi nayo ni moja kati ya mifereji inayokutiririshia pesa.
Kulingana na tafiti mbalimbali zilizokwisha fanywa na
wachumi au wakereketwa wa masuala ya pesa sehemu nyingi Duniani imegundulika kwamba
Mamilionea wengi na watu matajiri sana kwa wastani wanamiliki idadi fulani ya
mifereji ya kipato. Idadi (namba) hiyo kama vile ni ya kimuujiza vile unaweza
kushangaa ni kwanini iwe hiyo na wala siyo nyingine.
Zipo sababu kadhaa ambazo nitazizungumzia hapa hapa
kwenye hili somo na wala sitasubiri mpaka somo jingine ingawa kwa kweli
kulistahili niwe na somo zima kuzijadili sababu hizo nyeti kikamilifu.
Nilipokuwa natafiti Mifereji hiyo ya kipato nikiwa kama
mwanafikra yakinifu (Critical thinker)
maswali machache nitakayoorodhesha hapo chini yalinijia katika fikra zangu;
(1) Ni
idadi hiyo ya Mifereji ya kipato iliyo na uwezo wa kimaajabu wa kumfanya mtu
aweze kuwa Milionea ama imetokea tu kwa Mamilionea wengi kujikuta utajiri wao
ukianzia katika hiyo namba/idadi ya mifereji ya kipato?
(2) Hivi
inawezekana idadi yote ya Mifereji hiyo ya kipato ikawa katika kundi moja
(sekta moja) kwa mfano katika sekta ya ardhi na majengo, sekta ya usafirishaji
nk. au inapaswa kuwa katika makundi/sekta tofauti?
(3) La
tatu na la mwisho, Hivi kweli waajiriwa katika zile fani zinazolipa fedha
nyingi sana (wanaopokea mishahara minono) kuna umuhimu wowote ule kwa wao
kumiliki idadi hiyo ya mifereji ya kipato au ni bora tu wakaendelea na ajira
zao hizo zinazowalipa mamilioni ya shilingi?
Kwa bahati mbaya sana katika utafiti wangu huo mtandaoni
na nje ya mtandao sikufanikiwa kupata kwa urahisi majibu ya maswali hayo ingawa
mwishoni kabisa nilikuja kufanikiwa kuyapata majibu yote kwa usahihi kabisa.
Hivyo basi hebu turudi kwenye swali letu la mwanzo kabisa
na la msingi katika somo hili lisemalo; Ni mifereji mingapi ya Kipato kwa
wastani mtu yeyote yule anapaswa kuimiliki kabla hajatoboa na kuwa tajiri?
...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Mpenzi
mfuatiliaji wa masomo haya ya fedha kila siku, Somo hili ni moja kati ya masomo
tunayojifunza kwenye Mastermind group letu la MICHANGANUO-ONLINE na hapa tumeweka
sehemu fupi tu ya somo lenyewe. Somo kamili ni leo usiku saa 3 tarehe 23/1/2023
Ili
kupata somo zima lililokamilika pamoja na masomo mengine yaliyopita zaidi ya
80, jiunge na Darasa letu kwa kiingilio cha shilingi elfu 10 tu kwa mwaka
mzima.
Ukiwahi
kujiunga kabla ya OFFA yetu kumalizika (OFFA
ISIYOWAHI KUTOKEA) utatumiwa papo hapo vitabu na michanganuo ifuatayo hapo
chini mwishoni. Kifupi ni kwamba unapata E-book zangu zote kwa bei karibu na
bure! Offa hii itadumu muda mfupi.
...............................
VITU VYA OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA NI HIVI VIFUATAVYO;-
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali
KITABU: Siri ya Mafanikio ya Biashara Duka la Rejareja
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa
KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30
MCHANGANUO: Kuku wa mayai
MCHANGANUO: Kuku wa nyama - kwa kiswahili
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
MCHANGANUO: Kuku wa kienyeji
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa Kiswahili
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa kiingereza
MCHANGANUO: Kiwanda cha Dona (Usado milling)
SEMINA: Jinsi ya kuandika mchanganuo wa kiwanda cha unga
SEMINA: Kuandika mchanganuo wa kuku wa nyama
MCHANGANUO: Kuandika mchanganuo wa Cafe
SOMA PIA NA HIZI HAPA;
1. Njia za kuingiza kipato cha ziada nje ya kazi yako
2. Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
3. Kwanini kila mwanamke anastahili kumiliki vyanzo vingi vya mapato?
4. Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio & utajiri wa haraka
5. Ujanja matajiri wanaoutumia kupata pesa kutoka vyanzo vingi vya mapato
0 Response to "KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA KIFEDHA UNAHITAJI MIFEREJI MINGAPI YA KIPATO/PESA?"
Post a Comment