8.0 Mpango wa Fedha
Katika
mwaka wa kwanza mauzo yetu kwa mwezi yanakadiriwa kuwa shilingi milioni 8.8,
katika kipindi hiki tunatarajia kuuza mchanganyiko wa vyakula ikiwemo supu,
chapati, wali, ugali, chipsi nk. Kwa ujumla katika kipindi chote cha miaka 3
tunatarajia kutengeneza faida nzuri
Kama zilivyo Sura nyingine zote zilizopita hii nayo kuna
muhtasari mdogo unaogusa zile sehemu muhimu za Sura yote kama unavyoona hapo
juu. Lakini kabla hatujaendelea hebu kwanza tuone ni vipengele gani vidogo
vinavyounda sura nzima ya fedha;
8.1 Dhana/makisio muhimu
8.2 Tathmini ya mauzo ya
kurudisha gharama (Break Even Analysis)
8.3 Makisio ya faida na
hasara
8.4 Makisio ya mtiririko wa
fedha
8.5 Makisio ya mali na
madeni (mizania ya biashara)
8.6 Sehemu muhimu za
biashara
8.1 Dhana/Makisio
muhimu
Kwenye makisio muhimu unaorodhesha vile vigezo
(assumptions) utakazotumia katika kuamua hesabu zako ziwe vipi. Kwa mfano
ukuaji wa mauzo mwaka wa pili na wa tatu upendo wametumia asilimiaa 50%, haya
ni makisio (assumptions) kulingana na
tafiti walizofanya.
Pia kukisia vitu kama wafanyakazi wangapi mwaka wa
kwanza, kodi ya mapato na riba ya mkopo kama mpango huu ungehusisha mkopo pia
vyote hivyo ni makisio muhimu ambayo yangelipaswa kuandika hapa kwa kifupi
kusudi msomaji wa mpango huu atambue hesabu zimefikajefikaje hapa zilipo na
wala hazikutokea tu hewani.
Upendo assumptions zao ni hizi;
· Makisio ya
mauzo kwa siku = 294,500/=
· Wastani wa
Gharama za mauzo kwa siku = 215,750/=
· Mahitaji ya
fedha za mtaji ni shilingi Milioni 3
· Uchakavu wa
vifaa kwa mwezi = 39,400/=
· Kodi ya mauzo
kwa mwaka asilimia 30%
· Mauzo yetu
yote ni kwa fedha taslimu hakuna kukopesha
· Uchumi imara
usiokuwa na misukosuko mikubwa
8.2
Tathmini ya Mauzo yatakayorudisha Gharama zote kwa mwezi (Break Even Analysis)
“Break Even
Analysis” ni tathmini ya kiasi cha mauzo yanayohitajika ili kurudisha gharama
zote zilizotumika katika kipindi fulani, inaweza ikawa mwezi, mwaka au kipindi
kingine chochote kile ila mwezi ndiyo hutumika mara nyingi zaidi.
Namba zote zinazotumika kwenye tathmini hii zinapatikana
kutoka katika jedwali la Ripoti ya Faida na Hasara, hivyo ni vizuri kuifanya
tathmini hii baada ya kukamilisha jedwali hilo.
Ili kukokotoa Mauzo hayo tutahitaji kuwa na vitu 3 muhimu
vifuatavyo;
·
Wastani wa gharama za kudumu
kwa mwezi
·
Asilimia ya Gharama za mauzo
kwenye mauzo
·
Kanuni ya kukokotoa mauzo
hayo(Break even Formula)
Katika jedwali la Faida na Hasara mwaka wa kwanza,
wastani wa gharama za kudumu kwa mwezi ni zile gharama za uendeshaji kwa mwezi
ambazo katika jedwali la upendo ni shilingi 914,200 baada ya kugawanya za mwaka
kwa miezi 12
Asilimia ya Gharama za mauzo kwenye Mauzo, walichukua jumla
ya gharama zinazobadilika za mauzo sh. 77,670,000 kutoka
katika jedwali la makisio ya faida na hasara mwaka wa kwanza kisha wakagawa kwa
Mauzo ambayo ni sh. 106,020,000/= Hizi ukichukua za mwezi au za mwaka asilimia
utapa hiyohiyo moja ambayo walipata ni asilimia 73% au 0.73
Kanuni ya kukokotoa “Break
Even Sales” zipo nyingi kulingana na data/taarifa unazopewa, kwa mfano hapa
tayari tuna mauzo, gharama za mauzo na gharama za kudumu;
Kimsingi kabisa kanuni zote za kukokotoa Break even point
hutokana na kanuni kuu ifuatayo;
Faida
= Mauzo – Gharama za mauzo – gharama za kudumu
(Nikisema Break Even sales namaanisha Mauzo ya kurudisha
gharama zote zilizotumika yaani Mauzo yamelingana na gharama, hamna faida wala
hasara). Hivyo;
FAIDA
= 0
Kutokana na kanuni hiyo ndipo tunapata;
Break even sales = Gharama za kudumu /1-gharama za mauzo/Mauzo
au
Ukipachika namba tulizoona pale juu jibu lake utapata =
shilingi 3,385,926/=
Chati
ya mauzo ya kurudisha gharama (Break even chart)
Chati ya mauzo hayo hutengenezwa kwa kutumia data za “Mauzo vs Faida” na data hizi zinapatikana
kwa kutumia kanuni (formula) ile pale juu;
Faida
= Mauzo – Gharama za mauzo – gharama za kudumu
Lakini kumbuka kila thamani ya gharama za mauzo kulingana
na data zao pale juu ni asilimia 73% au 0.73 ya Mauzo
Hivyo Fomula yetu itakuwa kama ifuatavyo
Faida = Mauzo –
0.73Mauzo – 914,200
Baada ya hapo katika kila chumba kwenye jedwali la mauzo
vs faida walitafuta thamani ya faida na kutengeneza jedwali la Mauzo vs Faida;
Chukulia kwamba
hakuna mauzo hivyo weka 0 kwenye sehemu ya mauzo na ukokotoe faida itakuwa sh.
Ngapi,
Faida = 0 - 0.73(0) – 914,200 = – 914,200
Kisha endelea kuweka namba za mauzo chukulia sasa labda
umeuza milioni 5
Faida = 5,000,000 - 0.73(5,000,000) – 914,200 = 435,800
Kisha utaendelea kufanya hivyohivyo kwa milioni 10, 15
nk. Mwishoni utapata kiasi cha faida kwa kila mauzo utakayoweka halafu sasa
utachora chati yako na kuangalia ni wapi faida inakuwa zero(0) na hapo ndipo
mauzo ya kurudisha gharama zote yalipo. Ukicheki vizuri utaona faida ikiwa 0
mauzo ni 3,385,926/= nilipozungushia
duara, sawa na jibu la kwenye formula
yetu lilivyosema.
Jedwali:
Mauzo vs Faida
Mauzo |
Faida |
0 |
-914,200 |
5,000,000 |
435,800 |
10,000,000 |
1,785,800 |
15,000,000 |
3,135,800 |
20,000,000 |
4,485,800 |
25,000,000 |
5,335,800 |
30,000,000 |
7,185,800 |
35,000,000 |
8,535,800 |
40,000,000 |
9,885,800 |
|
|
Katika ripoti hii ya faida na hasara unatumia hesabu
ndogondogo ambazo zimeshajitokeza kwenye vipengele vingine vya mchanganuo huu
huko nyuma. Ukichunguza mchanganuo wetu huu tangu mwanzoni mpaka sasa utagundua
kuna sehemu kadhaa hesabu zimejitokeza kwa mfano kwenye
·
Sura ya ‘5.0’ kipengele
kidogo cha 5.3.1 Makisio
ya Mauzo na na gharama za mauzo halafu
·
Sura ya sita Uendeshaji kipengele kidogo ch 6.4
Vifaa na Mashine (Uchakavu) na 6.5
Makisio ya mauzo kwa undani
·
Sura ya 7 Uongozi na
Wafanyakazi (Mishahara)
Katika Makisio ya faida na
hasara kuna vitu vikubwa 5 vifuatavyo,
1) Mauzo
2) Gharama
za mauzo (zinazobadilika)
3) Gharama
za uendeshaji(za kudumu)
4) Kodi
5) Faida
halisi
Kuna majedwali ya faida na hasara mawili, moja ni la
miezi yote 12 na la pili ni la mwaka wa kwanza lakini unaweza ukakisia na miaka
miwili inayofuata. Upendo walianza na jedwali la miezi 12 kwa kuchora safu za
kusimama(columns) za miezi yote 12 pamoja na safu za kulala (rows) zenye vile
vitu 5 bilivyotaja pale juu.
Walichora jedwali la Faida na hasara kwa miaka 3 kama ifuatavyo na kuweka namba za mwaka wa kwanza ambazo zote tumeshaona zimepatikana hapo juu kisha walikadiria mauzo ya mwaka wa kwanza na wa pili kwa kutumia njia ya asilimia. Ukuaji wa mauzo ni asilimia 50% hivyo walichukua 50% na kuzidisha mara mauzo ya mwaka wa kwanza halafu jibu wakajumlisha na mauzo hayo ya mwaka wa kwanza ili kupata mauzo ya mwaka wa pili.
Mauzo ya mwaka wa tatu halikadhalika walizidisha ya mwaka
wa 1 kwa 50% kisha jibu wakajumlisha na mauzo hayo kupata ya mwaka wa 3
Gharama za mauzo kwa miaka ya 2 na 3 ni rahisi walichukua
tu asilimia 73 ya mauzo kama ilivyo mwaka wa 1
Gharama za uendeshaji kwa mwaka wa kwanza tayari zipo
kukisia za miaka ya 2 na 3 unatumia tu akili ya kuzaliwa kwa kufikiria iwapo
mauzo yatakua kwa asilimia 50 vitu kama umeme na vifaa vya usafi ni lazima vipande kidogo pengine
kwa asilimia 50% nk. Msishahara itapanda kwani wafanyakazi wataongezwa, kod ya
pango nayo itapanda mwala wa 3
Baada ya kumaliza walikokotoa faida halisi mwishoni kwa
kila mwaka miaka yote 3
Jedwali: Faida na hasara kwa miaka 3
|
|||
|
Mwaka 1 |
Mwaka 2 |
Mwaka 3 |
|
Tsh. |
Tsh. |
Tsh. |
Mauzo |
106,020,000 |
159,030,000 |
238,545,000 |
Gharama za mauzo |
77,670,000 |
116,505,000 |
174,757,500 |
Faida Ghafi |
28,350,000 |
42,525,000 |
63,787,500 |
Faida ghafi % |
27% |
27% |
27% |
Gharama za uendeshaji |
|
|
|
Mishahara |
7,200,000 |
10,800,000 |
10,800,000 |
Kodi ya Pango |
1,800,000 |
1,800,000 |
2,400,000 |
Uchakavu |
470,400 |
470,400 |
470,400 |
Matangazo na promosheni |
360,000 |
500,000 |
1,200,000 |
Umeme na maji |
240,000 |
360,000 |
360,000 |
Vifaa vya usafi |
360,000 |
720,000 |
1,200,000 |
Ushuru wa taka |
60,000 |
60,000 |
60,000 |
Dharura |
480,000 |
500,000 |
1,000,000 |
Jumla gharama za uendeshaji. |
10,970,400 |
15,210,400 |
17,490,400 |
Faida kabla ya riba na
kodi |
17,379,600 |
27,314,600 |
46,297,100 |
Riba |
0 |
0 |
0 |
Kodi ya mapato 30% |
5,213,880 |
8,194,380 |
13,889,130 |
Faida halisi |
12,165,720 |
19,120,220 |
32,407,970 |
Faida halisi/Mauzo% |
11.5% |
12% |
14% |
Baada ya hapo walianza kutengeneza jedwali la Faida na
hasara kwa miezi 12 ya mwaka wa kwanza kama ifuatavyo;
Kwanza kama unakumbuka tulipokisia mauzo ya siku, mwezi
na mwaka tulisema mauzo ya siku yalikuwa ni shilingi 294,500/= Hivyo katika
miezi 12 mauzo hayataweza kutokana na sababu mbalimbali kama vile miezi mingine
ni ya likizo watu si wengi sana mjini, kuna miezi ya mvua nk, kwa hiyo ni lazima kila mwezi uupe mauzo
yake kulingana na jinsi ulivyotafiti mauzo yako yatakuwaje.
Mfano Upendo mwezi wa kwanza kwa kuwa walikuwa wakianza
walikadiria mauzo kuwa kidogo chini ya wastani ule wa tuliopata kwa siku wa sh.
Milioni 8 kwa siku na kuweka milioni 6.8 Pia ukicheki miezi ya likizo kama
June, Julai na Novemba mauzo yatashuka kidogo wakati miezi kama ya 4, 10 na 12
yenye pilika nyingi mauzo yapo juu
Jedwali lake lina mistari iliyosimama columns (12) na
mistari iliyolala(rows) inayolingana na vitu 5 nilivyotaja pale juu,mauzo,
gharama zote na mwishoni faida halisi. Kila mwezi unapewa mauzo yake na gharama
kulingana na makisio ya mauzo na gharama kwa siku tulizopata wakati wa makisio
ya Mauzo sura ya 5 lakini pia utazingatia vigezo vingine kama likizo, miezi ya
mvua nk.
Lifuatalo ni jedwali la faida na hasara kwa la Upendo kwa
miezi 12 lakini hapa tumeweka tu miezi 5 kwanza, ukitaka kuona miezi yote 12
tazama mchanganuo wa Upendo Cafe.
Makisio ya Faida na hasara miezi 12
Mwezi1 |
Mwezi 2 |
Mwezi 3 |
Month4 |
Mwezi 5 |
|
Tsh. |
Tsh. |
Tsh. |
Tsh. |
Tsh. |
|
Mauzo. |
6,800,000 |
7,500,000 |
8,000,000 |
9,200,000 |
9,100,000 |
Gharama za mauzo |
4,964,000 |
5,475,000 |
5,840,000 |
6,716,000 |
6,643,000 |
Faida
ghafi |
1,836,000 |
2,025,000 |
2,160,000 |
2,484,000 |
2,457,000 |
Faida
ghafi %. |
27% |
27% |
27% |
27% |
27% |
Gharama
za uendeshaji. |
|||||
Mishahara |
600,000 |
600,000 |
600,000 |
600,000 |
600,000 |
Kodi
ya pango |
150,000 |
150,000 |
150,000 |
150,000 |
150,000 |
Uchakavu |
39,200 |
39,200 |
39,200 |
39,200 |
39,200 |
Matangazo
na promosheni |
30,000 |
30,000 |
30,000 |
30,000 |
30,000 |
Umeme
na maji |
20,000 |
20,000 |
20,000 |
20,000 |
20,000 |
Vifaa
vya usafi |
30,000 |
30,000 |
30,000 |
30,000 |
30,000 |
Ushuru
wa taka |
5,000 |
5,000 |
5,000 |
5,000 |
5,000 |
Dharura |
40,000 |
40,000 |
40,000 |
40,000 |
40,000 |
Jumla |
914,200 |
914,200 |
914,200 |
914,200 |
914,200 |
Faida kabla ya riba na Kodi |
921,800 |
1,110,800 |
1,245,800 |
1,569,800 |
1,542,800 |
Riba |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Kodi ya mapato 30% |
276,540 |
333,240 |
373,740 |
470,940 |
462,840 |
Faida
halisi |
645,260 |
777,560 |
872,060 |
1,098,860 |
1,079,960 |
%Faida halisi |
9.5% |
10% |
11% |
12% |
12% |
Baada ya ripoti hii ya Faida na Hasara hufuata ripoti
nyingine 2 ile ya Mtiririko wa fedha taslimu, Mizania ya biashara(Rasilimali na
Madeni) pamoja na Sehemu muhimu (Ratios),
ni rahisi kuziandaa kwani taarifa nyingi hutokana na taarifa hii.
.......................................................
Ili kupata Somo hili zima kwa ukamilifu wake, jiunge na Mastermind Group la MICHANGANUO-ONLINE au ujipatie kitabu kipya kiitwacho;
SANAA & SAYANSI YA UPISHI WA CHAPATI LAINI
Ada ya group kwa mwaka ni sh. elfu 10, unapata na offa ya vitabu na Michanganuo bure.
Kujiunga lipia kwa namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo, kisha ujumbe wa "NIUNGE NA MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITABU"
0 Response to "SIKU YA 5 TAREHE 29/12/2022 KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA UPENDO CAFE HATUA KWA HATUA (MPANGO WA FEDHA)"
Post a Comment