Hapo
zamani miaka ya nyuma kidogo jamii za Wahindi, Wachagga, Wakinga na Wapemba
zilisifika sana kwenye tasnia ya biashara za maduka hususani maduka yale ya
rejareja hata kukazuka majina na misemo kama vile; dukani kwa Mangi, dukani kwa Mpemba,
maduka ya wakinga kariakoo na maduka ya Wahindi au “Wadosi” katika kila mji
ulioenda.
Hata
hivyo siku hizi kutokana na mwamko mkubwa wa ujasiriamali nchini dhana ya
biashara hii kumilikiwa na makabila hayo machache inazidi kutoweka na kila mtu
sasa kutoka makabila mengine tofautitofauti wameanza kuzichangamkia fursa za
biashara hiyo maarufu nchini.
Leo
tunaichunguza tabia moja ya kushangaza sana ambayo miaka mingi huko nyuma
ilionekana ni tabia ya Wahindi zaidi kuliko jamii zingine, tabia ya wenye
maduka ya rejareja kukaa wenyewe dukani au na wenza wao tu. Ni mwiko kumwamini
mtu mwingine ashike pesa dukani kwao.
Mhindi
na Mwarabu hata leo hii ukifika dukani kwake anaweza kuwa na wafanyakazi hata
watano wa kuhudumia wateja lakini pale kwenye fedha(Cashier) hukaa mwenyewe
habanduki na hata ikishindikana basi labda mke wake, basi. Hata mwanaye ni mara
chache sana anaweza akamwamini labda tu iwe ni muda mwafaka umewadia na
anamfundisha kazi kwa ajili ya mpango wa kumrithisha mali. Mhindi akitaka
kwenda lunch mchana saa 7 anapiga kufuli duka na kuwaacha wahudumu wa duka nje
wakilinda geti mpaka atakaporudi ndipo kazi iendelee.
Kilichonisukuma
kuandika makala hii ni utafiti wangu nilioufanya kutaka kujua, je siku hizi
wachagga, wakinga na wapemba huajiri kina nani kwenye maduka yao? Maana zamani
hasa hasa Wachaga walipendelea sana kuajiri ndugu zao waliowatoa vijijini huko
Kilimanjaro. Mtu ‘alivizia’ ule muda wa vijana kumaliza darasa la saba
anakwenda kutafuta kijana na kuja kumpa kazi ya kuuza duka, kijana akikaa kwa
uaminifu mwishowe anamfunguliwa na yeye duka lake ili ajiendeleze kimaisha
mwenyewe kama malipo ya kufanya kazi kwake muda wote huo.
Nimegundua
kwamba siku hizi watu wengi mijini na hata vijijini wameachana na kasumba hii
kwa kiasi kikubwa na badala yake wanafanya kazi wenyewe ama na wenza wao tu
basi, ikiwa wote hawapo basi na duka hufungwa kama wafanyavyo Wahindi.
Sababu
kubwa inayofanya wenye maduka kutokuajiri watu, kwanza ni vijana wengi siku
hizi kuendelea na masomo ya sekondari, watu wengi kutokuwa na uaminifu tena
kwenye pesa, unamwajiri mtu leo dukani, lakini yeye anajiongeza baada ya miezi
michache tu anataka amiliki lakwake, watu wengi hasa vijijini kuhofia imani
potofu za kishirikina kuwa eti matajiri mijini huwachukua misukule watoto wao
pindi wanapowaajiri na kupelekea vifo vya ghafla au madhara mengine mbalimbali
kimwili na kiakili.
Utafiti
huu mpya unasadifu kile nilichokuwa nimekiandika kwenye kitabu changu cha MAFANIKIO
YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA, kwamba njia nyepesi zaidi ya usimamizi wa
duka changa linaloanza ni ile ya mmiliki mwenyewe au na mwenza wake kuuza
dukani basi. Uzoefu unaonyesha watu wengi waliofanikiwa kwa muda mfupi katika
biashara hii ya duka la rejareja ni wale wanaouza wenyewe au na wenza wao tu.
Hii
inamaanisha kwamba mtu mwingine yeyote yule anayetaka kufungua duka lakini hana
muda wa kuuza mwenyewe wala mwenza wake hana muda pia, pengine wana majukumu
mengine kikazi mahali, ni lazima wachague njia ya kumuajiri mfanyakazi, na kwa
kuwa haiwezekani kuwapata vijana wadogowadogo kutoka kijijini hawana budi
kuwaajiri watu wengine wa kawaida tu, wale hata waishio mjini hapohapo.
Kumchukua
mfanyakazi wa duka kwa mtindo huo kuna changamoto moja kubwa ya mahesabu. Ni
kwa namna gani utaweza kumdhibiti huyu mfanyakazi msiokuwa na uhusiano wowote
ule wa damu na yeye katika jukumu lenye mtihani mkubwa namna hii la pesa? Wahindi si wajinga na wana uzoefu wa biashara
hizi kwa mamia ya miaka tokea huko kwao Uhindini, wanafahamu pesa ilivyokuwa
tamu na inavyotamaniwa na kila mtu.
Kudhibiti
mahesabu ya duka la rejareja kwa staili hii ya Mhindi ni nzuri na ina tija ndio
maana katika kitabu niliandika kwamba huo ni mfumo unaofaa sana hasa pale mtu
anapokuwa anaanza biashara ya duka bado mtaji wake ukiwa haujakua sana kiasi
cha kufikiria kufungua matawi mengine. Lakini vipi kama mtu sasa umeshafikia
hatua ya kujitanua unataka umiliki maduka zaidi ya moja?
Na
mtu ukitaka kutajirika kwa duka moja inawezekana lakini itakuchukua muda mrefu
kidogo ila ukitaka kutumia muda mfupi kutajirika huna budi kuwa na maduka zaidi
ya moja. Au, ni kwa jinsi gani utajigawa ikiwa una kazi nyingine mfano ajira
lakini ungetaka kuwa na duka mahali la kukuongezea kipato cha ziada? Au
inakuwaje kama mmiliki wa duka bado hajaoa na angependa kumuweka msaidizi
dukani?
Nimekumbuka
pia Mwanafunzi mmoja hivi karibuni aliniomba ushauri afanyeje ili biashara yake
ya duka la rejareja aliyoanzisha baada ya kuhitimu kidato cha nne na sasa
amepata nafasi katika chuo fulani anachotarajia kujilipia ada mwenyewe kwa pesa
ya hilo duka, amepanga alihamishie jirani na hicho chuo, lakini changamoto
kubwa inayomkabili ni msaidizi wa kwenda kukaa pale dukani kusudi yeye awe
anafika tu pale kucheki hesabu zake na kurudi chuoni. Na hata ikiwa atampata,
je, ni mfumo upi rahisi wa udhibiti atakaotumia ili faida yake iendelee
kuonekana laivu bila chenga na mtaji kubakia vilevile bila ya kudokolewa na
msaidizi?
Majibu
ya maswali yote niliyouliza katika aya mbili zilizopita yanapatikana katika
ukurasa wa 99 – 101 wa KITABU CHA MAFANIKIO YA BIASHARA, DUKA LA REJAREJA toleo
jipya la mwaka 2023 ambapo njia iliyokuwepo kabla ya kusimamia na kudhibiti
stoku ya duka imefafanuliwa na kurahisishwa zaidi kwa mjasiriamali wa kawaida
kuweza kuielewa bila ya kuhitaji msaada wowote ule. Tumeweka hatua 7 za kufuata,
majedwali mtu anayoweza kubadilisha na kujaza tu namba zinazoendana na biashara
yake pasipo kuanza upya moja kwa moja.
Chakufurahisha
zaidi ni kwamba njia hii haihitaji mahesabu mengi na wala haijalishi ikiwa kama
wewe unatumia mifumo ya kiuhasibu ya
kuweka kumbukumbu kidigitali ama daftari la kawaida la mahesabu, vyote hufanya
kazi vizuri. Kifupi ni njia rahisi sana ya kudhibiti hesabu za duka la rejareja
kwa wajasiriamali wa kawaida mitaani wanaoteseka na udokozi na hujuma za
wasaidizi ama wafanyakazi wao.
Kitabu
hiki pia kina mbinu nyingine nyingi za uanzishaji na uendeshaji wa biashara ya
rejareja mwandishi alizoandika akitumia uzoefu wake binafsi kwenye biashara hii
kwa takribani muda wa miaka 12, mfano ni jinsi alivyoanzisha duka la rejareja
mtaa wa Msimbazi Karikoo Jijini Dar es salaam akiwa na mtaji mdogo sana, mfano
huo umewekwa katika kitabu ukurasa wa 10 kwa picha za rangi tangu akianza na
keki na soda mpaka anafungua duka kamili na msaidizi wa kazi ya mauzo.
Mjasiriamali
anayenunua kitabu hiki pia anayo fursa ya kuwasiliana na mtunzi wa kitabu moja
kwa moja kupitia namba zake, 0712202244
au 0765553030 kwa ushauri zaidi ama
jambo jingine lolote lile ndani ya kitabu ama kuhusiana na biashara ya duka la
rejareja, jambo ambalo anaona hajalielewa vizuri ili kupata ufafanuzi wa
kutosha.
Ikiwa
una duka la rejareja, biashara yeyote ile ya rejareja ama una ndoto kichwani
siku moja uje ufungue biashara hii basi kitabu hiki siyo cha kukosa, ni moja
kati ya asseti zako muhimu kabisa
katika kufanikisha biashara itakayokutiririshia pesa mithili ya mgodi wa almasi.
Kumbuka duka la rejareja ndiyo biashara rasmi nyepesi zaidi kufungua na mtaji mdogo na imewaweka watu wengi mjini na hata vijijini kuna watu wanatajirika kwa biashara hii. Usikubali kamwe duka likufanye kuwa mtumwa wa kukaa hapo masaa yote 12, siku 7 za juma, unaweza ukaweka msaidizi ‘ukaenjoy' uhuru wako huku hesabu zako zikiwa salama pasipo kudokolewa hata senti 5
UPATIKANAJI WA KITABU:
Kitabu
kinapatikana kwa njia kuu 3 zifuatazo;
1. NAKALA-NGUMU (HARDCOPY)
Ukiwa
Dar es salaam wasiliana na sisi kwa namba 0712202244 tutakufikishia ulipo na
kulipa shilingi elfu 15 (15,000/=) nauli ni juu yetu sisi wenyewe.
Kama
upo mkoa mwingine wowote ule tujulishe tutakutumia kwa njia ya basi kwa
shilingi elfu 25 (25,000)
2. NAKALA-LAINI (SOFTCOPY) KWA E-MAIL
Ukiwa
Popote pale duniani, lipia kitabu shilling elfu 5 (5,000/=) kupitia namba
0712202244 au 0765553030 jina, Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe watsap
au sms usemao, “NATAKA KITABU CHA DUKA” kisha nitakutumia kitabu chako muda
huohuo kwenye simu au kompyuta yako.
3. NAKALA-LAINI (SOFTCOPY) KUPITIA
APPLICATION YA GETVALUE
Kwa
kutumia simu yako ya smartphone unaweza kufuata kiungo kifuatacho ukakinunua
kwenye mtandao wa GETVALUE kwa shilingi elfu 10 (10,000/=)
Fungua mtandao wa GETVALUE hapa kununua kitabu cha duka la rejareja sasa hivi.
SOMA NA HIZI PIA:
1. Jinsi ya kujua faida ya duka la rejareja kila siku jioni unapofunga hesabu zako
2. Faida Duka la mahitaji ya nyumbani: niweke akiba kiasi gani cha mapato ya siku?
3. Aina za bidhaa za duka zenye faida ndogo lakini hutoka harakaharaka
4. Biashara ya duka inavyoweza kukutoa kimaisha ukiwa mjanja
5. Mtaji wa biashara ya duka la rejareja, nianze na shilingi ngapi ili nifanikiwe?
6. Hatua sita (6) za kuanzisha biashara ya rejareja (duka) sehemu ya II
0 Response to "SIRI MADUKA YA KINA MANGI, WAPEMBA NA WAKINGA SIKU HIZI KUTOKUAJIRI MTU BAKI ZAIDI YA WAKE ZAO "
Post a Comment