Inawezekana, hauhitaji mtaji wowote ule wa pesa ili
kuanzisha biashara. Aidha biashara zinatofautiana kwani zipo biashara rahisi
zaidi kuanza bila mtaji kabisa mfano hizi hapa 7, na nyingine zitahitaji mtaji
angalao kidogo katika hatua fulani.
Kama mwandishi na mshauri wa biashara na ujasiriamali,
nimewahi kuulizwa swali hili mara nyingi sana na waulizaji wengi waliuliza kama
ifutavyo;
· Ni
kwa Jinsi gani naweza kuanza biashara bila mtaji wa pesa?
· Kuanza
biashara bila mtaji au kwa mtaji mdogo sana inawezekana?
· Biashara
za bila mtaji ni zipi?
· Naweza
kuanzisha biashara yangu pasipokuwa na pesa kabisa?
Katika maswali yote hayo na mengine yanayofanana nayo
huwa nawajibu; Inawezekana, huhitaji
mtaji wowote ule wa pesa ili kuanza biashara ijapokuwa unaweza kuhitaji aina
nyinginezo za mitaji mfano muda, nguvu na maarifa.
Kitu kimoja cha kustaajabisha kwenye kuanzisha biashara
ni kwamba kufeli ama kuanguka kwa biashara fulani hakuna uhusiano wowote ule na
kiasi cha mtaji wa kuanzia.
SOMA: Biashara 5 za mtaji kidogo kuanzia elfu 2, kumi mpaka laki moja unazoweza kuanza zikakutoa.
Takwimu zimethibitisha mahali pengi kuwa asilimia 90% ya
biashara zote zinazoanza (Startups)
ziwe zilianzishwa kwa mtaji wa kutosha ama bila ya mtaji wa pesa kabisa, zote
huishia kufeli muda mfupi tu baada ya kuanzishwa kwake jambo linalosababisha
maisha ya biashara kuonekana ya kuchanganya na watu wengi kuamua kukomaa na
ajira zao maisha yao yote.
Lakini faida za biashara ni nyingi ikiwa mtu ataamua
kujifunza biashara vizuri hasa mbinu mbalimbali za kuanzisha biashara isiishie
njiani.
Njia
za kuanzisha Biashara bila ya kuwa na Pesa kabisa (Biashara bila Mtaji)
Kutokana na maswali ya badhi ya wasomaji wangu pale juu
nimeona ni vyema nikaweka muongozo kidogo wa namna mtu anavyoweza akaanzisha
biashara yake angali hana hata senti tano mfukoni.
SOMA: Kupata mtaji wa biashara cha msingi ni wazo na muda wako, pesa baadae.
Hatua karibia zote nitakazozielezea hapa hazihitaji mtaji
wa pesa isipokuwa labda aina nyinginezo za mitaji kama vile muda, nguvukazi na
maarifa.
1. Kitu
cha kwanza kabisa ni lazima uwe na wazo la Biashara.
Kutafuta wazo la bishara inayokufaa hauhitaji mpaka uwe na
fedha, ni suala tu la kutumia ubongo wako. Kuna njia mbalimbali za kuweza
kupata wazo la biashara itakayokulipa zikiwemo;
· Kuchunguza
ni mahitaji gani katika jamii uliyopo watu wanayakosa
· Ujuzi,
uzoefu au fani uliyonayo na jinsi unavyoweza kuvitumia katika kujiingizia pesa.
· Mapungufu
katika biashara za watu wengine unayoweza kuyarekebisha.
· Kubuni
bidhaa/huduma mpya kabisa sokoni
· Kupeleka
au kuleta bidhaa/huduma katika soko/eneo ambalo hapo kabla zilikuwa hazijafika
nk.
2. Kufanya
utafiti wa soko
Kama nilivyoeleza kwenye kitabu changu cha MICHANGANUO
YA BIASHARA & UJASIRIAMALI, utafiti wa biashara ama feasibility
Study unaweza ukaufanya mwenyewe binafsi hata pasipo kuyahusisha makampuni ya
ushauri ama wataalamu wa biashara. Kwenye kitabu niliweka hadi majedwali ya
dodoso na sampuli mtu wa kawaida kabisa anaweza akayakopi na kuanza utafiti wa
biashara yake mara moja bila gharama zozote.
SOMA: Utafiti wa soko la biashara yako/Upembuzi yakinifu -1
Kifupi tu ni kwamba kwenye utafiti wa biashara na sekta uliyochagua
kufanya unatakiwa uhakikishe unalifahamu barabara soko lako, washindani wako na
njia unazoweza kutumia ili kuwapiku.
Fahamu wateja wako wanajishughulisha na nini, kiwango
chao cha elimu, umri, tabia zao na mahali wanapopatikana, Ongea nao uso kwa uso
ili kujua kile wanachokikosa kutoka kwa washindani waliopo sasa.
Mpaka hapo inawezekana kufanya yote niliyoorodhesha pasipo
kutumia hata shilingi moja.
3. Kulijaribu
wazo lako la biashara sokoni.
Katika hatua hii pia huhitaji bado kuweka pesa yeyote
labda kiasi kidogo sana kwa ajili tu ya bando la kwenye simu yako au kompyuta.
Unafanya majaribio bidhaa au huduma zako pasipo kutumia gharama kubwa kuona
ikiwa kama wateja wanazihitaji kweli ama la.
SOMA: Jinsi ya kuuza wazo la biashara au ubunifu kwa wawekezaji na watu wengine
Utatumia mbinu gani isiyokuwa na gharama? Siku hizi njia
bora kabisa isiyohitaji mtaji pesa mkubwa ni kupitia mitandao ya kijamii kwa
kupost wazo lako, picha au hata makala zinazohusiana nalo kisha kuona mirejesho
ya wateja wako ikoje. Hapa unaweza kuanza kupata oda, pongezi, likes na maoni mbalimbali
yanayoashiria kwamba watu wanavutiwa au wana uhitaji na kile unachotaka
kuwauzia.
Kumbuka lakini mpaka hapo hujaingiza pesa yeyoye ya maana
kwenye biashara yako zaidi ya bando tu la simu.
4. Tengeneza
mpango wa biashara na kisha uanze na kile ulichokuwa nacho kwanza.
Hapa sishauri utengeneze mpango rasmi wa biashara kama
ile ya kuombea mikopo benki hapana bali mpango kichwani mwako au ukitaka
unaandika mpango wa biashara uitwao “Ukurasa mmoja wa mchanganuo”, aina
hii fupi ya mchanganuo wa biashara mifano yake halisi inapatikana katika kitabu
changu kingine kiitwacho JINSI YA KUANDIKA MPANGO MFUPI WA BIASHARA (UKURASA MMOJA) na haichukui
zaidi ya dakika 15 mpaka 30 kuuandika.
SOMA: Pata kitabu cha bure (Free E-book) jinsi ya kuandika mchanganuo mchanganuo mfupi wa biashara yako
Ni moja kati ya njia zenye nguvu mno za kuandika mpango
wa biashara kwa mtu anayeanza sifuri pasipokuwa na mtaji wa fedha kwani unaweza
kuuboresha kuwa mpango sanifu wenye kila kitu baadaye.
5. Tengeneza
bidhaa/huduma yako ya kwanza kabisa.
Hapa sasa nisikudanganye maanake Motivational Writers na
Motivational Speakers ndipo tunapoonekana manabii wa uwongo au matapeli kwa
kuwaaminisha watu kuwa biashara inaweza ikafanyika pasipo kuwa na mtaji kabisa
mwanzo mwisho.
Kiukweli kama ulivyosoma kipengele cha 1 – 4 yapo mambo
unayoweza kuyafanya bila kutumia hata shilingi lakini kuna mahali fulani utafika
hamna ujanja lazima uweke tu angalau kiasi kidogo cha fedha biashara iweze kusonga
mbele vinginevyo itabakia kuwa wazo tu.
Naomba nieleweke vizuri hapa, nilisema kuanzisha biashara
bila mtaji wowote wa pesa inawezekana lakini ili biashara hiyo iendelee na kukua
katika mazingira ya karne ya sasa ni lazima uweke pesa na si vinginevyo. Hata
biashara ya udalali inayosifiwa zaidi kutohitaji mtaji wa pesa lakini kuna
wakati utapiga simu, kuhitaji kula muda unapozunguka, nauli nk. Hii yote maana
yake ni pesa huwezi kukataa.
SOMA: Mtaji wangu ni mdogo sana lakini nahitaji kufanya biashara na sina ajira naomba ushauri wako
Tukirudi kwenye mada yetu kwa kuwa sasa tayari umeshapata
uhalali wa wazo lako, soko umejua lipo la uhakika, umeshawafahamu washindani
wako vizuri, unaweza hata kuazima fedha kidogo kwa mtu wako wa karibu utakazogharamia bidhaa au
huduma yako ya mwanzo kabisa. Si unajua utauza?
6. Tengeneza
utaratibu rahisi wa malipo
Amua wateja wako wakulipe kupitia njia ipi, kwa fedha
taslimu mkononi au kupitia mitandao ya simu? Kumbuka wateja mara zote
wanapendelea njia nyepesi na rafiki ya kufanya malipo pindi wafanyapo manunuzi.
Itategemea aina ya biashara yako.
7. Tumia
njia za bure kujitangaza
Kwa kuwa huna pesa jitahidi sana kutumia mitandao ya
kijamii kutangaza biashara yako. Sahau kwa muda matangazo ya kulipia (sponser
ads) hadi pale mapato yako yatakapokuwa makubwa. Tumia tovuti au blogu
kupatikana ‘gugo’ na search engine nyinginezo kwa urahisi.
SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara unayoipenda
8. Tafuta
njia nyinginezo za kupata mtaji
Ukishafika hatua hii ukitaka kukua zaidi na zaidi ni
lazima utafute mtaji wa kutosha na njia maarufu zaidi ni mikopo ya benki au taasisi
nyinginezo za kifedha. Unaweza kuomba mikopo ya ndugu au jamaa lakini hakikisha
mmepeana kimaandishi/kimkataba kusudi undugu wenu usijekufa kisa pesa
..............................................................
OFFA
MPYA YA VITU 12 KUELEKEA NUSU YA PILI YA MWAKA 2023
Ni offa ya kukata na shoka !
Ukilipia
Tsh. 10,000/= Unapata vitu hivi vyote 12 papo hapo;
· Course
kamili ya uandishi wa michanganuo ya biashara
· Vitabu,
E-books vitano (5), michanganuo kamili sita (6) ya biashara, Tempates/vielezo
vya michanganuo viwili (2), kwa kiingereza na Kiswahili. Vitu vyote ni kwa kupitia njia ya email au watsap
· Kujiunga
na group letu la masomo ya kila siku ya fedha mwaka mzima ukipenda.
· Ni kwa
shilingi elfu 10 tu !
OFFA hii
ni ya muda mfupi sana na itaondolewa au kupunguzwa vitu! Aidha magroup yakijaa itasitishwa
pia.
VITU HIVYO 12 VYA OFFA NI
HIVI VIFUATAVYO;-
1.
COURSE/SEMINA: (compiled
complete course) ya Jinsi ya
kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa
kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili
2.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
5.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili
6.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani na ndio
hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
7.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers - kwa
kiswahili
8.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
9.
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za
saruji- kwa
kiswahili
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. Kuunganishwa Group la
masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka
hatukuunganishi)
Lipia offa yako kupitia
namba zangu, 0712202244 au 0765553030
jina, Peter Augustino Tarimo, kisha ujumbe watsap au sms usemao;
“NATAKA OFFA MPYA YA VITU 12”
Ukihitaji kuunganishwa na
group, kwenye ujumbe ongeza maneno; “NATAKA OFFA MPYA YA VITU 12 & GROUP”
Na utapata OFFA zako ndani ya dk. 3 tu
Thamani halisi ya offa hii
ni Tsh. 90,000/= lakini lipa Tsh. elfu 10 tu uokoe sh. 80,000/= !
Ukitaka kuthibitisha
uaminifu wetu bonyeza hapo chini kuona baadhi ya wadau wengine waliowahi
kuchangamkia offa na vitabu vyetu siku za nyuma bofya hapa>>>TESTIMONIAL
..................................................
Kwa zaidi ya miaka 4 sasa
tumewasaidia wajasiriamali na makampuni mbalimbali kuandika michanganuo ya
biashara zao kwa madhumuni mbalimbali hasa ya kuombea mikopo toka mabenki &
taasisi za kifedha, ruzuku na hata mipango mikakati kwa ajili ya kuendeshea
biashara zao kwa ufanisi.
Badhi ya biashara na
makampuni hayo tumeweka sehemu ndogo ya mihutasari ya michanganuo yao hapa bila
ya kufichua utambulisho wao, bofyahapa>>>BAADHI
YA KAZI ZETU
Ikiwa na wewe ungependa
tukuandikie Mpango kamili wa biashara yako unaolingana na maono, dhima na
malengo ya biashara au kampuni yako, tunakukaribisha kwa mikono miwili.
Tunaandika Michangauo ya Biashara yeyote, iwe kubwa au ndogo, na katika lugha
za Kiingereza au Kiswahili kulingana na matakwa ya mteja.
Michanganuo yetu tofauti na
kwingineko huwa tunatumia taarifa(Data) unazotupatia wewe mwenyewe mteja lakini
pia na sisi huwa tunafanya tafiti katika yale maeneo tunayoona hukuyatafiti vya
kutosha. Kamwe hatukopi na kupesti taarifa kwa lengo la kutengeneza michanganuo
inayoakisi maono halisi ya mteja.
Mawasiliano yetu ni;
Simu/Whatsap: 0765553030 au 0712202244
Peter Augustino Tarimo
(Get
a comprehensive, customized Business Plan that
fits your unique vision, goals and challenges)
0 Response to "KUANZISHA BIASHARA BILA MTAJI, HIVI INAWEZEKANA AU NI KUTIANA MOYO TU?"
Post a Comment