Kuna
vitabu vingi, makala na maandiko mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii
yanayohusiana na mada ya pesa au hali za watu kifedha. Katika somo letu hili la
leo tutakwenda kuona ni aina gani za fikra na tabia zinazompeleka mtu kwenye
umasikini na wala siyo kumpeleka kwenye kumiliki utajiri ambako ndio kila mtu
hapa duniani anatamani kuelekea.
Siku
hizi kwa kila mtu siyo siri tena kwamba fedha ni sawa na kama ilivyo nishati ya
umeme iendeshayo karibu kila kitu. Nguvu ya umeme inapokatika nadhani sote
tunafahamu ni taharuki kiasi gani watu huwa tunaipata, hali kadhalika na pesa
nayo ndiyo hivyo hivyo ilivyo. Watu wanapoikosa au kuwa nayo kidogo sana huibua
taharuki sawa na ilivyokuwa kukatika kwa nguvu ya umeme.
Ikiwa
mtu hana pesa kuna uwezekano mkubwa kwamba ni mawazo na vitendo vyake vinavyochangia
yeye kukimbiwa na nguvu hii muhimu, PESA. Hebu sasa pasipo kupoteza muda wako
mwingi, tukaone ni kwa jinsi gani vitendo na fikra za mtu(saikolojia) inavyoweza kumnyima hela hata akadhania labda
ameshalogwa tayari.
1. Pesa siyo furaha, haiwezi kununua kila kitu bwana!
Wakati
upande mmoja wa nafsi yako akilini ukiwa umejijengea mtazamo kwamba pesa
haiwezi ikanunua furaha, upande mwingine wa pili wa nafsi unatamani ule vizuri
na familia yako, ununue simu nzuri ya gharama, ujenge nyumba, ununue kiwanja,
uende matembezini na wale uwapendao kustarehe nk. Hivyo unapokuwa na pande
mbili zinazokinzana juu ya jambo moja, ni dhahiri kabisa jambo hilo
umeshaliwekea vizingiti na kamwe hautaweza kufaulu au kusonga mbele, na hivi
ndivyo tunavyokosa pesa pasipo wenyewe kujua.
2. Sihitaji Pesa!
Ni
kauli nyingine ya kimasikini iliyo rahisi kutamka mdomoni lakini inayoweza
kugeuka na kuwa chanzo kizuri cha mtu kutokupata pesa inavyotakiwa. Kuridhika
na kile kidogo unachokipata huku akilini ukiwaza tu juu ya kupunguziwa bei na
kuweka akiba ya kile kidogo unachokipata wakati mwingine siyo sahihi na ni
hatari pia kwani kunaweza kupunguza au kukatisha kabisa mzunguko wako wa fedha
taslimu.
Fikra
hii inamfanya mtu aishie tu kulenga katika kumiliki fedha kidogo(uhaba/ukata)
badala ya kulenga katika kumiliki fedha nyingi(Ukwasi/Utajiri) hali ambayo
hatimaye humlazimisha kutawanya rasilimali chache alizokuwa nazo badala ya
kulenga katika kuzikuza na kuzizalisha zaidi.
3. Kushindwa kutumia Pesa
Pesa
kama zilivyo nguvu za aina nyingine huwa haina tabia ya kustahimili udumavu,
pesa haipendi kukaa tu bure bila ya kufanya kazi yeyote, na hii ndiyo sababu
utawasikia watu wengi wakisema wanapata pesa zaidi na kwa urahisi pale
wanapoamua kutumia pesa lakini wanapozibanabana zinapotea hawazioni (*Angalizo: lakini siyo matumizi holela,
hapa namaanisha matumizi yale ya busara tu na yenye kuleta faida siyo
utapanyaji)
Tafiti
zimebainisha pia kwamba majanga mbalimbali kama vile magonjwa, wezi na majanga
mengine ya asili huwa na kawaida ya kuwanyemelea zaidi watu walio na tabia ya
kubana sana pesa zao wakihofia zitaisha au kupotea ilihali walizipata kwa
jasho.
Cha
ajabu sasa inakuwa ni kinyume chake kwani pesa hizohizo wanazochelea kuzitumia hatimaye
zinakuja kutoka kirahisi kupitia kukabiliana na majanga hayo au nguvu za asili
ambazo wanakuwa hawana uwezo mwingine wa kuzizuia zaidi ya kutumia kile walichokuwa
nacho.
Sasa
unaweza kujiuliza ni kwanini tu wasingeamua mapema kufanya matumizi ya pesa zao
kupitia njia nzuri ya kuzizalisha kama vile uwekezaji katika miradi na biashara
mbalimbali kuliko kuziweka kabatini wakisubiria majanga?
4. Peponi (Mbinguni) Hakuna Pesa !
Mawazo
ya masikini wengi ni kwamba, hata ukitafuta pesa vipi lakini mwisho wa siku
utaziacha hapahapa Duniani, hutaenda nazo peponi. Dhana hii inakufanya usione
umuhimu wa ‘kufight’ kufa na kupona
na mwishowe ni umasikini hadi unaingia kaburini kweli kama mawazo yako hayo
yanavyokudanganya. Midhali unaishi na kupumua, tafuta pesa uishi maisha mazuri
hapa Duniani, achana na dhana hizo za kiboya zisizofaa
5. Haujipi thamani wewe mwenyewe kama mtu, mtaalamu au
raia unayestahili malipo makubwa
Hili
mara nyingi limekuwa chanzo cha watu wengi kuishia kupata vipato vidogo. Mpaka
pale wewe mwenyewe utakapoamini kwamba ni wa gharama(aghali) ndipo na nguvu ya pesa nayo itakapokuamini. Ili watu nao
waweze kukupa pesa zao kwa ajili ya huduma ama bidhaa unazowauzia, ni muhimu
kujifunza jinsi ya kutenganisha mahusiano ya fedha na watu kutoka yale
mahusiano binafsi ya kawaida.
6. Kutokuiheshimu fedha !
Ikiwa
utatamka kwa kinywa chako kwamba “pesa ni makaratasi tu”, “Pesa haina mwenyewe”
sijui “ pesa ni takataka”nk. fedha nayo utashangaa inakukwepa kama ukoma. Pesa
haitaki hata kubebwa kwenye fuko kuu kuu lililochakaa. Kuwachukia na kuwadharau
wenye pesa huku ukiwaita majina mbalimbali kama vile, freemasons, wachuma pesa za majoka, chuma ulete, misukule nk.
Yote
hayo yanathihirisha jinsi mtazamo wako kwenye fedha ulivyokuwa potofu na namna
amabvyo huamini kabisa katika kufanya kazi na kutajirika kihalali. Kwa vyovyote
vile ni lazima utaishia kufa masikini kwani hakuna namna utakayoweza kujituma
upate pesa zaidi ya kudhani wenye pesa wote ni madhalimu waliopora, kuua na
kuiba.
Kuna
kisa kimoja nilichoshuhudia kipindi uchumi ulivyokuwa bora sana watu wakipata
pesa nyingi, jamaa mmoja aliamua kufanya kufuru na kuona pesa haina maana kwa
kuajiri vibarua wamuoshee gari yake kwa kinywaji aina ya bia, alinunua kreti za
bia nyingi vijana wakazimimina kwenye pipa na kuanza kuosha pajero lake huku
wengine waliokuwa waroho wakijinyea kinywaji hicho chini kwa chini kutoka
pipani. Yule jamaa ninavyoandika hapa hana hata mia na anatamani hata kikombe
cha mbege hakipati ....................................... ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………...............................................
Mpenzi msomaji, Saikolojia ya Umasikini ina mambo mengi watu wala
hatuyadhanii hata kidogo kama ndiyo chanzo cha sisi kuwa masikini.
Somo hili halijamalizika na litaendelea leo hii
tarehe 31/5/2023 usiku saa 3 ndani ya Mastermind group la Fedha & Michanganuo-online
ü Mtu yeyote yule anakaribishwa
kujiunga kwa kutoa ada ya mwaka mzima sh. 10,000/=
kupitia namba zetu 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino
Tarimo.
ü Baada ya
malipo tuma ujumbe wa, “NATAKA OFFA YA
VITU 12 NA KUUNGANISHWA GROUP LA MASOMO”.
ü Masomo ya
fedha ni kila siku, na unapojiunga unatumiwa masomo mengine yote yaliyopita
tangu darasa lianze pamoja na OFFA yetu
ya vitu 12 yenye Vitabu na Michanganuo ya biashara
ü Tunakuwa pia na semina za mara kwa mara juu ya
Michanganuo ya biashara zinazolipa Tanzania
Kupata Vitabu zaidi na
Michanganuo ya biashara kwa bei nzuri, tembelea Duka letu la vitabu &
Michanganuo hapa>> SMARTBOOKSTZ
Tunatoa
pia huduma ya kuandika Michanganuo ya biashara / Business Plans kwa biashara yeyote ile
iwe kubwa au ndogo kwa lugha ya kiingereza au Kiswahili- mteja unachagua.
Michanganuo yetu ni ya
kipekee kulingana na mahitaji ya mteja na huwa tunatumia taarifa utakazotupatia
wewe, tunafanya pia utafiti pale taarifa zako zinakuwa hazitoshelezi mahitaji
ya mchanganuo husika. Ukihitaji Tuwasiliane zaidi kwa namba 0765553030 au
0712202244
Unaweza kucheki kwa kifupi summary za baadhi ya kazi tulizowahi kuwafanyia wateja wetu hapa>>BAADHI YA KAZI ZETU
Somo
hii limeandaliwa na:
Peter
Augustino Tarimo
Mtaalamu
wa Michanganuo ya biashara aina zote
Phone/Watsap:
0765553030 au 0712202244
SOMA NA HIZI HAPA;
1. Usilaumu kukosa pesa, bali laumu njia
iliyokufikisha pale ulipo(Parti & ii)
2. Njia 6 za kuondoa woga na stress za fedha katika maisha yako
0 Response to "SAIKOLOJIA YA UMASIKINI: SABABU 9 KWANINI HUPATI PESA NYINGI HATA UKIJITAHIDI VIPI?"
Post a Comment