Mpendwa msomaji wangu Karibu tusome
makala ya leo isemayo;
TAFUTA PESA ILIMRADI TU HUVUNJI SHERIA ZA NCHI WALA ZA
MUNGU KWANI KAMA ZILIVYO VYOTA ANGANI
HUWEZI KUZUIA WALA KUZUIWA NA WATU WENGINE KUPATA PESA. MAFANIKIO NI HAKI
YA MTU YA MSINGI
Hivi uliwahi kusikia pamoja
na nyota angani kuwa mamilioni ipo siku hata nyota moja ilimzuia mwenzake kung’ara?
Hata pamoja na kwamba Jua kuna kipindi inasemekana hupatwa na Dunia lakini hali
hiyo uliwahi kusikia imedumu hata kwa siku mbili au tatu?
Sasa kwanini uanze kuhofia
eti mwenzako akifanikiwa kama wewe mafanikio yako yatashuka? Au ili wewe
ufanikiwe ni lazima kwanza uhakikishe mwenzako aliyefanikiwa unamshusha kwanza
chini kwa kutumia mbinu zozote zile hata ikiwezekana kuutoa uhai wake?
Pamoja na kwamba waswahili
husema, Tafuta pesa uheshimike na kuna mpaka nyimbo zimewahi kuimbwa redioni
tafuta pesa uringe lakini haimaanishi kwamba ukishapata pesa basi wewe ndiyo
ujifanye Mungu mtu hapana, pata pesa heshimika, pendwa na kila mtu, ringa
lakini pia usijaribu kuzuia wengine nao kupata pesa kama wewe, wala usijaribu
kuwashusha wale waliokuzidi kifedha ili wawe kama wewe.
Ukweli mchungu ni huu hapa;
kitu kimoja binadau tunashindwa kufahamu ni kwamba ikiwa kila mtu duniani humu
angelikukuwa na mafanikio basi dunia isingelishindwa kuhimili, wala rasilimali
zilizopo zisingelimalizika kisa eti kila mmoja wetu amefanikiwa.
Lakini jambo la kustaajabisha
mno ni kwamba juhudi za watu wengi iwe masikini au hata baadhi ya matajiri mara
zote kwenye akili zao wamekuwa wakipoteza muda mwingi wakiwaza jinsi ya
kuwashusha chini wenzao, (majirani, marafiki, ndugu na jamaa) wale waliowazidi
kidogo kimafanikio ama kuwazuia walio chini yao kupanda juu. Utafutaji pesa wa
jinsi hii unavunja si sheria za nchi tu bali hata na zile alizoziweka Mwenyezi
Mungu katika vitabu vyake vitukufu.
Sikatai kwamba ushindani ule
wenye tija haukatazwi mfano unaona mwenzako kajenga nyumba kali nzuri na wewe
unajitahidi kufanya kazi kwa juhudi zote kusudi na wewe ujenge yakwako kali
zaidi, laki si ule ushindani wa kuona jirani kalima mahindi yake shambani
yamestawi vizuri na wewe eti unavizia na kagiza unakwenda kuyakatakata kwa
upanga ili umkomoe yeye ashuke na wewe upande juu.
Ukweli ni kwamba mafanikio yako
yanapaswa yapimwe na ni kwa jinsi gani umeweza kuwasaidia wenzako kwa kuwekeza
kwao, na siyo tu ni mara ngapi umewapa chakula au mahitaji ya msingi. Fikiria
umewahi kuwapa binadamu wenzako fursa au kuwawezesha na wao waweze kupata
mafanikio kama yakwako mara ngapi na siyo wamewahi kuja kwako mara ngapi kuomba
kibaba cha unga wa kupikia ugali. Ukimpa unga leo wa ugali kesho na kesho kutwa
shida zake zipo palepale, je hapo umemwezesha?
Bora kipi, kuacha ‘legacy’
duniani kwa vizazi na vizazi baada ya kufa kwako mfano kina Hayati Mzee ReginaldMengi, Mwalimu Julius Nyerere, Steve Job, Mahatma Ghandi na wengineo au kuacha
duniani majumba marefu, madebe ya pesa, magari ya kifahari na kila aina ya
utajiri? ...................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Mpenzi msomaji wangu somo hili
lijulikanalo kama; “THE SKY IS VERY WIDE,
EVERY STAR CAN”, ni
refu na bado halijamalizika. Ili kupata somo zima lililokamilika jiunge na mimi
leo tarehe 29/05/2023 usiku saa3 kwenye
darasa letu maalumu la watsap
Masomo haya maalumu ya pesa
yasiyopatikana mahali pengine popote pale nje na ndani ya mtandao (exclusive)
hutolewa kila siku saa 3 ndani ya group la Michanganuo-online. Washiriki ni mtu
yeyote mwenye kiu ya kujifunza kwa kina masomo ya fedha na Michanganuo ya
biashara
Ukijifunza kuchanganua biashara
nakuhakikishia umejifunza kila kitu kuhusiana na biashara kwani mpango wa biashara ni jumla ya kila
kipengele kinachounda biashara nzima kuanzia Mtaji, masoko, Mauzo, hesabu zote
za biashara, bidhaa/huduma, uongozi na hata changamoto na fursa ndani ya
biashara husika.
Kupata nafasi ya kujifunza
masomo haya kila siku unalipia ada ya mwaka mzima shilingi 10,000/= tu kupitia
namba zetu; 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo,
kisha tuma ujumbe watsap au SMS usemao;
“NIUNGE GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA MPYA YA VITU 12”
Nitakuunganisha mara moja kwa
group pamoja na kukutumia OFFA yako
ya vitu 12 vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali papo hapo kama
ifuatavyo;
1.
COURSE/SEMINA: (compiled
complete course) ya Jinsi ya
kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa
kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili
2.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
5.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili
6.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani na ndio
hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
7.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers - kwa
kiswahili
8.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
9.
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za
saruji- kwa
kiswahili
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. Kuunganishwa Group la
masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka
hatukuunganishi)
Makala
hii imeandikwa na:
Peter Augustino Tarimo
Mtaalamu wa Michanganuo ya biashara aina zote
(Get a comprehensive, customized Business Plan that fits
your unique vision, goals and challenges)
Phone/Watsap: 0765553030 au 0712202244
Unaweza kusoma na hizi pia:
1. Kwanini kufanikiwa kifedhasi dhambi na kila mtu anastahili afanikiwe
2. Elimu ya fedha na umuhimu wake
3. Huna mtaji wa kutosha,hukopesheki? Jaribu njia hii ya kufunga mkanda (Bootstrapping)
4. Biashara 7 nzuri za kufanyamwaka huu, chagua moja uingize kipato cha ziada kwa urahisi
0 Response to "TAFUTA PESA ILIMRADI TU HUVUNJI SHERIA KWANI HATA NYOTA ANGANI KILA MOJA HUNG’AA KWA NAFASI YAKE"
Post a Comment