Hakuna shaka kwamba kila binadamu angetamani siku moja aje kuufikia uhuru kamili wa kifedha, kwahiyo ikiwa lengo lako kuu kwenye safari hii ya maisha ndio hilo basi hauna budi kubadili ‘meli’ uliyopanda sasa kutoka ile ya ajira kwenda ya biashara, hili halina ubishi, inawezekana usibadili sasa lakini ni lazima utafanya hivyo hapo baadae hata baada ya kustaafu.
Katika somo letu hili leo, hiki hasa ndio kitu tutakachoenda kujifunza. Biashara peke yake tu inaweza isiweze kukupa uhuru kamili wa kifedha lakini ni moja kati ya viungo muhimu sana vinavyosaidia kuharakisha kukufikisha huko.
Uwezekano wa mtu kuufikia uhuru wa kifedha akiwa katika ajira ni mdogo ingawa hatuwezi kabisa kuuondoa uwezekano huo. Si kama mwajiriwa hawezi kabisa kupata uhuru wa kifedha ila mchakato wake ni mrefu na mgumu kuliko vile ilivyo kwa mfanyabiashara. Wafanyabiashara mara nyingi sana utakuta hujiandaa kisaikolojia katika safari hii, kivipi? - tutajua zaidi kwenye aya zinazofuata.
Katika kazi za ajira, watu wengi huishi maisha ya wasiwasi kutokana na upungufu wa fedha. Na wala haijalishi ni mshahara mkubwa kiasi gani aupatao mtu, mara nyingi utamkuta akibeba akilini fikra za upungufu wa fedha. Na hili hutokea kwasababu waajiriwa wengi wanakuwa na tabia ya kufanya matumizi mengi zaidi kushinda wenzao wafanyabiashara. Wafanyibiashara wao mara nyingi hupenda kuwa waangalifu sana kwenye matumizi yao ya fedha.
SOMA: Fedha zako zinapotea kiajabu? Njia rahisi ya kutambua fedha zako zinakoishia kila siku hii hapa.
Kwanini basi mfanyabiashara huwa mwangalifu sana kwenye matumizi ya pesa?
Mchakato wa biashara mpaka imetengeneza faida unahusisha mlolongo wa vitu vingi na hivyo kumfanya mfanyabiashara kuchukua pia hatua mapema za kujihadhari kusudi biashara isije kuanguka. Kumbuka kwenye biashara hakuna ulinzi(security) kama ilivyo kwenye ajira, hivyo mfanyabiashara anajua kabisa akiteleza kidogo tu imekula kwake.
Ufuatao ni mchakato mzima wa biashara mpaka imezalisha faida kisha FEDHA ZA ZIADA pale mwishoni kabisa;
Chati hiyo hapo juu inaonyesha jinsi biashara inavyotengeneza yenyewe fedha za ziada. Utaona ya kwamba biashara hupitia mchakato mrefu mpaka imeweza kutengeneza fedha za ziada ambazo ndizo zinazobeba jukumu kubwa katika zoezi la kufanikisha uhuru wa kifedha wa mfanyabiashara kama tutakavyoona baadae kidogo.
Wakati sasa mfanyabiashara akitekeleza shughuli mbalimbali za biashara yake ndipo anapojijengea tabia hii ya kuwa muangalifu kupita kiasi kwenye matumizi ya fedha kusudi ahakikishe mwishoni kunakuwa na fedha za ziada kwa ajili ya kuzirudisha tena kwenye biashara kama mtaji lakini pia kwa ajili ya kulipia gharama zake nyingine mbalimbali za kimaisha.
KAZI/AJIRA
Hivyo ndio kusema kwamba mwajiriwa hawezi kabisa kusimamia fedha zake vizuri mpaka na yeye akaufikia uhuru wa kifedha? Hebu tena tuangalie chati hii ifuatayo;
Kama ilivyokuwa kwa biashara, ajira nayo inaweza ikatengeneza fedha za ziada. Lakini tofauti na biashara katika ajira kunakosa muunganiko, kunakuwa na pengo kati ya ajira yenyewe(kazi) na fedha. Uthibiti wa mwajiriwa kwenye kutengeneza fedha zake za ziada umewekewa mipaka, kivipi? Kuna vitu viwili (2) vifutavyo;............
................................................................................................................................................................................................................................
..............................................................................................................
Ndugu msomaji somo hili litaendelea katia Group la Michanganuo- online leo hii tarehe 06/06/2023 usiku saa 3. Ili kuweza kulisoma kwa ukamilifu na masomo mengine yaliyopita yenye maudhui ya fedha, jiunge na group hilo kwa kiingilio cha sh. elfu 10 tu mwaka mzima.
Utapata pia na OFFA yetu ya vitu 12 yenye vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara.
Namba za kulipia ni 0712202244 au 0765553030 Jina Peter Augustino Tarimo. Baada ya malipo tuma na ujumbe usemao, "NIUNGANISHE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 12"
Utaunganishwa muda huohuo na kutumiwa kila kitu. Ikiwa hutaki group ungependelea offa peke yake nijulishe nisikuunge.
1. COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili
2. KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu. – kwa kiswahili
3. KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4. KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
5. KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili
6. KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
7. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili
8. MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
9. MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)
Somo hii limeandaliwa na:
Peter Augustino Tarimo
Mtaalamu wa Michanganuo ya biashara aina zote
Phone/Watsap: 0765553030 au 0712202244
0 Response to "KWANINI BIASHARA HUMPA MTU UHURU ZAIDI WA KIFEDHA KULIKO AJIRA?"
Post a Comment