Katika maisha kuna wakati tunajikuta katika
hali ambayo tunashindwa kutimiza mambo muhimu maishani, mambo tunayotamani kwa
udi na uvumba kuyafanikisha lakini tunakosa hamasa ya kuyakamilisha. Unaweza
kuwa kwa muda mrefu labda umekuwa na ndoto ya kukamilisha kuandika kitabu
chako, umekuwa na ndoto ya kuanzisha biashara fulani, kujifunza kozi fulani nk. lakini jambo hilo
limegeuka kuwa kama jinamizi kwako kwa kutokuweza kulikamilisha. Unakosa tabia
za kufanikwa ama tabia za mafanikio ambazo ni nguzo muhimu mno katika
kufanikiwa jambo lolote maishani
Sababu ni kwanini unashindwa kutimiza ndoto zako hizo inaweza kuwa ni
woga wa kushindwa kumaliza, woga wa kuchukua muda mrefu kupita kiasi au sababu
nyingine zozote zile unazoweza kuwa nazo. Hata pale unaposema ngoja sasa
nianze, mara nyingi unajikuta ukiachia njiani kwa kukosa hamasa ya kuendelea mpaka ukamilishe jukumu lako hilo
nyeti maishani. Sasa kuna dawa au mbinu ambazo zinaweza zikatumika mtu ukaweza
kukamilisha majukumu yako muhimi kwa wakati na siyo kuchukua tena muda wako
mwingi huku hautimizi kitu.
SOMA: Kanuni: Unaijua thamani ya fedha kwa muda wako ni shilingi
ngapi?
Nakupa mfano wangu binafsi katika group hili la whatsapp la
Michanganuo-online, wakati nilipoanza nilikuwa na wasi wasi na kujiuliza
maswali mengi mfano, ‘hivi nitaweza kweli kuandika vitu kila siku?’, ‘Hawa watu
ninaowaita kujiunga na group, nitawaeleza nini nitakaposhindwa kutimiza ahadi
ya kuweka masomo humu kila siku?” Lakini wakati najiuliza hayo, nikakumbuka
mbinu moja iliyoniwezesha kutimiza majukumu yangu mengi muhimu, majukumu au
miradi hiyo huwa ninapoikumbuka hunipa hamasa kubwa kila ninapokuwa na jambo la
kukamilisha iwe ni kuandika makala, kitabu au hata jukumu lolote jingine la
kibiashara au la kijamii.
Hakuna kitu kikubwa kama kujipangia muda maalumu wa kukamilisha jukumu,
“DEAD LINE” Ninapokuwa naandika kila siku najipangia kwamba, kabla
ya kufika muda fulani ni lazima niwe nimekamilisha makala husika. Kwa kuweka
muda maalumu wa kukamilisha jukumu hilo najijengea nidhamu ambayo kila siku nalazimika
kuitimiza, na hata ninapokiuka siku moja moja dhamira yangu hunishtaki na
najisikia vibaya, si hivyo tu bado ninapokumbuka nyuma yangu kuna watu
nimewaahidi kuwaletea makala kila siku dhamira inakuwa inazidi kunisuta na
hivyo kujisukuma kukamilisha kile ninachoahidi kila siku.
SOMA: Njia 10 za kuhamasika na kuendelea kubakia na hamasa hiyo
kwa muda mrefu ujao
Mfano mwingine nakupa wa mwanafunzi, hivi unaweza kukumbuka ulivyokuwa
unasoma kama tayari ulishamaliza au kama bado unasoma unakumbuka mwalimu
anapokupangia homework na kukupa dead line? Hakupi deadline tu ila anakuahidi
pia viboko endapo utakwenda kinyume na muda huo wa mwisho. Unaweza kukumbuka
hapo ni nini kinachokusukuma mpaka kweli unahakikisha kazi ya mwalimu
inamalizika katika ule muda aliokupangia?
Katika mifano hiyo miwili niliyotoa, lengo langu nilitaka ufahamu hapo
vitu viwili tu navyo ni hivi hapa;...........................................
...........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................makala hii bado
inaendele group la Michanganuo-online................................
Kupata mtiririko mzima wa somo hili pamoja na masomo mengine yote
yaliyopita kwenye group tangu lianze jiunge na Group letu kwa kulipa ada ya
mwaka shilingi elfu 10 tu. Utapata pia na OFFA yetu ya vitu 12 yenye
mchanganyiko wa vitabu na Michanganuo kamili ya biashara zinazolipa Tanzania
kwa kiswahili na kiingereza.
Kulipia tumia namba zetu hizi; 0712202244 au 0765553030 jina
ni Peter Augustino Tarimo. Kisha baada ya malipo tuma ujumbe wasap au sms
usemao, "NATAKA OFFA YA VITU 12 NA KUUNGWA MASTERMIND GROUP".
Muda huohuo nitakutumia kila kitu na kukuunganisha kwa group. Ikiwa hupendi
group unataka offa ti peke yake nijulishe ili nisikuunge.
Ikiwa pia hutumii watsap, tunaweza kukutumia offa zako kwa njia ya
email.
VITU HIVYO 12 VYA OFFA NI
HIVI VIFUATAVYO;-
1.
COURSE/SEMINA: (compiled
complete course) ya Jinsi ya
kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa
kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili
2.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
5.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili
6.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani na ndio
hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
7.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers - kwa
kiswahili
8.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
9.
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za
saruji- kwa
kiswahili
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. Kuunganishwa Group la
masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka
hatukuunganishi)
0 Response to "TABIA ZA KUFANIKIWA: JE, UNASHINDWA KUKAMILISHA JAMBO LAKO MUHIMU ULILOANZISHA?"
Post a Comment