Tunapozungumzia
njia ya kutengeneza kipato cha ziada (Passive income) maana yake hasa ni pesa
au kipato kile mtu anachoingiza iwe anafanya kazi au hafanyi. Mara nyingi
kipato cha ziada huhusishwa na uhuru wa kifedha ingawa siyo lazima mtu
unapoingiza kipato cha ziada basi pia uwe huru kifedha. Siri ya utajiri ipo
kwenye ujanja wa kuingiza pesa nyingi za ziada na wala mtu asikudanganye eti
ipo dawa ya kupata pesa ama utajiri nje ya hiyo.
Kwa
upande mwingine uhuru wa kifedha unaweza kuwa na maana moja kati ya hizi 2 zifuatazo
kulingana na mazingira na kipato cha mhusika.
1. Maana
ya kwanza mtu anajihesabu kuwa huru kifedha pale anapokuwa anaingiza kipato cha
ziada kinachotosha kugharamia mahitaji yake yote ya msingi.
2. Maana
ya pili ni pale mtu anapokuwa na kipato cha ziada cha kumuwezesha kulipia kitu
chochote kile akitakacho maishani ikiwa ni pamoja na vitu vyote visivyokuwa
muhimu hata vile vya anasa.
Mtu
aliyekuwa huru kifedha yeye afanye kazi asifanye pesa au kipato huingia kama
kawaida. Watu tumezoea na tunafahamu kwamba ili mtu kupata kipato cha ziada ni
lazima aanzishe au awe na moja kati ya vitegauchumi hivi vifuatavyo
vinavyohusisha uwekezaji wa mara moja tu kisha kutoa mapato endelevu kwa muda
wote unaofuata bila ya uwekezaji mwingine, tena bila ya kufanya kazi moja kwa
moja. Vitegauchumi hivyo ni kama vile;
· Kodi
itokanayo na upangishaji wa jengo/nyumba
· Riba
kutoka katika akaunti ya akiba ya benki
· Gawio
kutokana na uwekezaji kwenye hisa za kampuni/biashara
· Mirahaba
kutokana na kazi za kisanii, muziki, filamu na utunzi wa vitabu nk.
Kwa
kifupi hivyo ndiyo baadhi ya vitegauchumi watu wengi walivyozoea kuona kama ni vipato
vya ziada (passive income). Kodi ya nyumba kwa mfano mmiliki kazi pekee
atakazofanya ni kukusanya tu kodi yenyewe na labda kufanya matengenezo
madogomadogo pale yatakapojitokeza, kazi ambazo huwezi ukasema zisipofanyika
kipato kitakoma kuingia.
Tukiingia
kwa undani kujua zaidi maana ya kipato cha ziada (passive income) tunaambiwa ni
kipato kile mtu anachoweza kuingiza hata ikiwa yeye mwenyewe hayupo pale katika
eneo la tukio. Kwa lugha rahisi mtu huyu fedha zinatiririka kwake hata ikiwa
ataamua kulala mchana kutwa na usiku, siku 7 za wiki na hii ndiyo njia kuu
matajiri wanayoitumia kupata utajiri haraka.
Watu
wengi hii huifanya pasipo kutambua kama ni kipato cha ziada. Kwa mfano hata
ukiweza kununua mashine ambayo unaweza ukaiweka mahali ikahudumia wateja wakati
wewe haupo pale, nayo ni njia ya kukuingizia kipato cha ziada.
Hata
ukiweza kubuni jinsi ya kuingiza pesa kupitia simu yako kama vile kuingiza pesa
mtandaoni kwa kutumia blog na mitandao ya kijamii nayo inahesabika kama mbinu
ya kuingiza pesa za ziada.
Hata
hivyo siyo kila njia ya kuingiza pesa online unaweza ukaiita ni kipato cha
ziada hapana, kwa mfano huwezi kusema blogu au ukurasa wa mtandao wa kijamii
unaotakiwa kupost kila siku ndipo upate wateja ni passive income hapana lakini
ikiwa utapost siku moja moja huku wateja wakija hata baada ya muda mrefu kupita
basi hiyo ni njia ya kukupa kipato cha ziada.
Kabla
hatujaenda kuona njia hiyo ya kuingiza kipato cha ziada isiyojulikana na watu wengi bado, hebu kwanza tuone ni kipato cha
ziada kiasi gani mtu anahitaji ili kuwa huru kifedha.
Unahitaji kipato cha shilingi ngapi kuwa
huru kifedha?
Unaweza
ukajiuliza, upate kipato cha ziada kiasi gani kusudi ujue sasa umeshakuwa huru
kifedha?” hupaswi wala kuumiza kichwa kwani jibu lake ni rahisi sana. Tumesema
awali kwamba, kuwa huru kifedha kunaweza kutafsiriwa katika maana 2, ya kwanza
ni pale mtu utakapoweza kuyamudu mahitaji yako yote ya msingi pasipo kubabaika
na ya pili ni pale utakapoweza kuingiza kipato cha ziada kinachotosha
kugharamia mahitaji yako yote ya msingi hata yale yasiyokuwa ya msingi mfano
anasa huku ukiwa huna haja ya kuuza muda wako ndipo uweze kulipia gharama hizo.
Sasa
kanuni au hesabu rahisi ya kujua kama umeingia kwenye uhuru wa kifedha,
unaorodhesha mahitaji yako yote ya msingi mahali kisha unayajumlisha, jibu
utakalopata sasa ndiyo kipimo. Kipato chako inabidi kiwe kikubwa ama juu ya
mahitaji yako yote ya msingi.
UHURU
KIFEDHA = KIPATO CHA ZIADA > MATUMIZI
Hiyo
ni hatua ya kwanza, ukitaka sasa kuufikia ule uhuru wa kifedha namba 2, inabidi
katika matumizi yako yote ujumuishe na yale matumizi yako yote yasiyokuwa na
umuhimu sana kama vile matumizi ya anasa nk. Ikiwa kama bado hujamudu kufikia
hatua ya uhuru namba 2 wa kifedha basi usijaribu kuweka matumizi yasiyokuwa na
umuhimu kwani huo hautakuwa tena uhuru kifedha bali utakuwa ni utumwa kifedha.
Njia ya kupata kipato cha ziada watu
wengi wasiyoijua
Kichwa
cha somo hili pale juu ni “NJIA YA KUINGIZA PESA ZA ZIADA AU TUSEME KIPATO CHA
ZIADA WATU WENGI WASIYOIJUA” sasa hebu tukaone njia hiyo ni kipi;
Pale
juu niliorodhesha baadhi ya miradi iliyozoeleka kuwa ndiyo njia kuu za kuingiza
kipato cha ziada au passive income mfano biashara za uwekezaji kwenye majengo
na hisa lakini inasahaulika mara nyingi kuwa ipo njia nyingine kubwa ya
kuingiza pesa za ziada tofauti kabisa na hizo nilizozitaja. Sasa basi njia hiyo
ni ipi na inafanyajefanyaje kazi?
Ili
kujua kila kitu kuhusiana na njia hiyo, ungana namimi kwenye darasa la
Michanganuo na masomo ya pesa kila siku, MICHANGANUO-ONLINE kwa kiingilio cha
sh. Elfu 10 tu ada ya mwaka mzima.
Punde
tu ulipiapo nakutumia vitu vifuatavyo;
1.
OFFA
ya vitu 12
2.
Masomo
yote ya pesa yaliyopita
3.
Kukuunga
na group la masomo ya kila siku
Kulipa
tumia namba zetu; 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo
Na
baada ya malipo tuma ujumbe kwa sms au wasap usemao, “NATAKA OFFA YA VITU 12 NA
KUUNGANISHWA NA GROUP”
OFFA YA VITU 12 INA VITU VIFUATAVYO;
1.
COURSE/SEMINA: (compiled
complete course) ya Jinsi ya
kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa
kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili
2.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
5.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili
6.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani na ndio
hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
7.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers - kwa
kiswahili
8.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
9.
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za
saruji- kwa kiswahili
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. Kuunganishwa Group la
masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka
hatukuunganishi)
SOMA NA HIZI HAPA:
1. Njia za kuingiza kipato cha ziada nje ya kazi yako
2. Kama pesa haijawahi kuwa rahisi kupatikana kwanini uchezee pesa?
3. Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?
4. Sababu 5: Kwanini masikini wengi hawafanikiwi kirahisi (Nakosea wapi part ii)
5. Bajeti: Jinsi ya kusimamia, kutunza na kutumia vizuri fedha binafsi na za biashara yako
0 Response to "NJIA YA KUTENGENEZA PESA ZA ZIADA ISIYOJULIKANA NA WATU WENGI BADO (PASSIVE INCOME) "
Post a Comment