Siri ya
kufanikiwa kimaisha ni vitu vidogovidogo sana kama ulikuwa hujui, mathalani
utunzaji mzuri wa pesa zako, jinsi ya kuwekeza vizuri pesa zako zizae, jinsi ya
kuweka na kutunza akiba yako nk.
Na wala usije
ukafikiri eti suala kama la la utunzaji mzuri wa fedha ama kuwa na nidhamu ya
pesa limeanza juzijuzi tu hapana, tokea enzi na enzi mababu na mabibi zetu
walikuwa na njia zao bora kabisa za wakati huo walizokuwa wakizitumia na
walijifunza jinsi ya kuishi kwa bajeti maishani katika kuhakikisha mambo yao
kiuchumi yanakwenda barabara na hawaingii katika mikwamo ya kuishiwa fedha ovyo
ovyo. Walikuwa pia na mbinu zao za kujifunza jinsi ya kuwa tajiri.
SOMA: Elimu
ya fedha na umuhimu wake, njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima!
Licha ya siku
hizi teknolojia kwenye nyanja ya fedha kuwa imekua sana,
tukishuhudia kwa mfano mpaka ujio wa ma ‘apps’ yenye uwezo wa
kumfundisha mtu jinsi ya kuishi kwa bajeti kulingana na kipato cha biashara au
hata jinsi ya kupangilia mshahara utokanao na kazi/ajira yako.
Kuna apps nyingine pia zinazomwezesha mtu kufanya manunuzi mtandaoni (online)
kwa urahisi, lakini bado njia hii ya kizamani sana (OLD SCHOOL…Technick)
imethibitishwa na wataalamu wengi wa uchumi kote duniani kuwa inao uwezo wa
kumfanya mtu atengeneze nidhamu ya hali ya juu ya pesa na ni bora zaidi
kushinda hata zile za kisasa, na isitoshe ni ya kutegemewa.
Usidhani kwamba
siri ya kufanikiwa kibiashara ni lazima tu mtu utumie teknolojia za kisasa kama
applications za kwenye simu janja au mifumo ya kiuhasibu iliyobobea hapana,
kwani unafikiri waliokuwa mabilionea miaka hiyo ya arobaini na saba walitumia
compyuta na simu janja kutunza fedha zao?
SOMA: The
sky is very wide, every star can shine( Mbingu ni kubwa mno, kila nyota inaweza
kung'ara)
Njia hii ya
kitambo unayoweza pia ukaiita mfumo ama siri ya kutunza pesa siyo ngumu kutumia
hata kidogo mpenzi msomaji wangu na hata wewe mwenyewe unaweza leo ukaamua kwenda
kuijaribu, ni rahisi sana na itakayokwenda kuufanya mzunguko wako wa fedha kuwa
chanya muda wote na hivyo pia kukufanya wewe mwenyewe kutabasamu muda wote
kwani ni sheria ya asili kwamba,
MZUNGUKO CHANYA
WA FEDHA = FURAHA (POSITIVE CASH FLOW = HAPPINESS)
Njia hii ni nzuri sana hasa
kwa watu wa vipato vya kawaida na wasioweza kuilinda vyema mizunguko yao ya
fedha au kwa wale wanaosumbuliwa na madeni ya mara kwa mara. Huweza kukomesha
kabisa matumizi ya hovyo kwenye vitu kama chakula na starehe kwa kifupi hufundisha
jinsi ya kutunza akiba ama hata ukipenda jinsi ya kuwa tajiri haraka
SOMA:
Niweke akiba kiasi gani cha mapato yasiku katika faida ya duka la mahitaji ya nyumbani?
Watu wengi huwa hawaoni kabisa umuhimu wa kupanga kabla matumizi ya vitu kama umeme na maji lakini kwa kweli kufahamu utatumia kiasi gani cha umeme au maji kabla hata ya mwezi wenyewe haujaanza ni jambo la msingi sana na litakalokujengea nidhamu nzuri ya matumizi yako ya pesa kwa vitu hivyo.
Kwa njia hii utaweza kufahamu kwa uhakika zaidi ni wapi fedha zako zinakokwenda lakini pia ni wapi zinakotokea. Siri kubwa ya kufanikiwa kwenye suala la pesa iwe ni biashara au matuumizi yako binafsi ni kuwa na mfumo thabiti unaohakikisha unafahamu bayana kile unachoingiza na kile unachotoa.
SOMA: Kwanini mikopo ya riba mitaani, michezo ya upatu na baadhi ya vocoba si salama kujiunga?
Si mganga, si mchawi wala
wataalamu wa mambo ya pesa watakaokufundisha wewe jinsi ya kutajirika kwa
haraka ikiwa utashindwa zoezi hili muhimu la kuzitunza pesa zako vizuri. Mfumo
huu wa kizamani uliovuma sana miaka ya 50, 60, 70, na 80 ni kama vile
ilivyokuwa dhahabu, hauchuji wala haupitwi na wakati na unatumiwa bado na watu
mpaka huko Marekani, Uchina na hata Bara la Ulaya.
......................................................
Mpenzi
msomji wangu, somo hili au mbinu hii ya utunzaji pesa tutakwenda kujifunza
kikamilifu leo tarehe 14/07/2023 katika Group la Masomo ya kila siku WHATSAPP
la MICHANGANUO ONLINE. Ili kujiunga katika group hili mwanachama anapaswa
kulipa kiingilio cha shilingi elfu 10 tu kwa mwaka mzima
Unapata
papo hapo vitu mbalimbali vikiwemo vitabu, masomo yaliyopita na michanganuo
mbalimbali ya biashara zinazolipa. Jumla ni items 12. Package ama kifurushi
hiki kitakuwezesha kujifunza ujasiriamali na biashara kwa kina na ikiwa kama
ulikua hujui ni nini maana ya Business plan (Mpango wa biashara) basi hapa
ndiyo mahala pake.
Si hivyo
tu unapata pia fursa ya kujiunga na group letu la masomo ya fedha kila siku,
kumbuka hili ndiyo group pekee Tanzania unaloweza kupata somo jipya lenye
maudhui ya fedha kila siku. Siyo dondoo, narudia tena, ni masomo kamili ya
fedha usiyoweza kuyapata mahali pengine popote nje na ndani ya mtandao.
Malipo ni
kupitia namba; 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo. Ukishatuma,
tuma pia ujumbe usemao, "NIUNGE NA
GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA YA VITU 12" au wasiliana na sisi moja kwa
moja kupitia hizo namba.
0 Response to "SIRI ZA PESA: NI MBINU YA KIZAMANI SANA YA KUTUNZA PESA LAKINI WATAALAMU WANASEMA NI NZURI KUSHINDA ZILE ZA KISASA"
Post a Comment