Kwa karne nyingi binadamu wamekuwa ni viumbe walio na kiu
ya kutaka kujua ni kwa jinsi gani wanaweza kupata utajiri kwa haraka na
kuufikia uhuru wa kifedha katika muda mfupi kwa kadiri inavyowezekana. Lakini
zoezi hilo kila mara kwa watu wengi limeonekana kuwa ni gumu.
SOMA: Kuwa
bilionea naweza kutumia njia zipi?
Katika somo letu la leo tutakwenda kuona kwanza kabisa,
hatua za kuchukua pale mtu anapotaka kuianza safari ya kuusaka uhuru kipesa
halafu pia tutakwenda kuona ipi ni biashara nzuri ya kuanzia unapotaka kuwa
tajiri na kufikia uhuru kamili kifedha.
Hatua za kufuata
Hatua ya 1:
Anzisha na kumiliki Biashara
Hakuna
vyanzo vya utajiri endelevu na wa uhakika nje ya biashara. Dalili ya utajiri
huanzia tu pale mtu anapochukua hatua ya kufungua biashara ama kufanya
uwekezaji wenye faida wa namna yeyote ile iwe ni kwenye ardhi, nyumba, shamba,
ufugaji nk.
SOMA: Biashara
7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.
Biashara
zenye faida Tanzania unazoweza kuanza nazo zipo nyingi lakini unatakiwa uwe
makini kidogo, kuna kitu muhimu sana cha kuzingatia kama makala hii inavyoenda
kukujuza.
Hapa
unatakiwa kufanya kazi kwa bidii sana kabla biashara haijatengemaa na kuweza
kujiendesha yenyewe bila ya wewe kulazimika kuwepo pale. Biashara kujiendesha
maana yake inatumia nyenzo mbalimbali kama vile wafanyakazi, fedha za watu
wengine, mifumo mbalimbali ya kimasoko kama vile tovuti na mitandao ya kijamii.
Lengo
hapa ni ili baadae uweze kumiliki rasilimali zilizo na uwezo wa kukuletea kiasi
kikubwa cha fedha hata ikiwa hautafanya kazi moja kwa moja. Katika steji hii ya
mwanzo elimu ya pesa ni muhimu sana hasa kuzijua siri mbalimbali za pesa,. Saikolojia
ya pesa na jinsi ya kujiwekea akiba.
kujua
siri ya pesa hapa simaanishi eti uende kwa wale jamaa wanaojitangaza kwenye
mabango njiani kuwa wanatoa ujajiri bila masharti au dawa ya mafanikio wakati
ukishafika kwao sharti la kwanza tu unaambiwa ukalete kondoo mweusi.
Njia
sahihi ya kuzijua siri za pesa na utajiri ni kusoma vitabu, mitandao ya kijamii
kama hivi unavyosoma hapa, kuhudhuria semina mbalimbali za makocha na waalimu
wa ujasiriamali nk.
Hatua ya 2:
Weka vitegauchumi
Chukua mapato yatokanayo na biashara yako uliyoanzisha
hapo juu na uwekeze katika vitegauchumi vyenye uwezo wa kuzalisha faida kwa
mfano, uwekezaji katika ardhi na majengo, hisa katika makampuni mengine,
biashara za kuazimisha vifaa na mitambo, miradi hii itakuletea mapato ya ziada
kila mwezi.
Hatua
ya 3:
Jenga
msimamo:
Endelea kuwekeza gawio na
faida itakayotokana na miradi tuliyoiona namba 2 hapo juu katika vitegauchumi
zaidi ili kunufaika na ongezeko kubwa la mapato mara dufu, kwanza kutokana na
biashara yako ya awali lakini pia kutokana na vitegauchumi vilivyotokana na
faida ya biashara hiyo.
SOMA: Biashara ndogo rahisi kwa wajasiriamali zinazoenda na wakati
tulio nao
Baada ya muda fulani mapato
ya ziada yaliyotokana na biashara yako ya awali pamoja na vitegauchumi
ulivyoanzisha yatakuwa yameshazidi gharama zako za maisha (matumizi) na hivyo
kuwa tayari umeshaufikia uhuru wako kifedha.
Badala ya biashara ya
kawaida mwanzoni kwenye ile hatua ya 1, unaweza hata ukaanza na kazi ya ajira
yenye uwezo wa kukupatia mapato kila mwezi.
Baada ya kufikia uhuru
kifedha sasa unaweza kuachana na biashara yako ya awali au ajira na kuamua
kufanya chochote utakacho kama vile kusafiri, kwenda kutalii maeneo mbalimbali
duniani yenye vivutio, kutumia muda wako mwingi na familia yako au hata ukaamua
kutulia tu huku ukiendelea kuwekeza katika vitegauchumi.
Kujianzishia makampuni
mengine kwa ubia na watu hata kutoka nje ya Bara la Afrika kama alivyokuwa
akifanya Marehemu Mzee
Reginald Abraham Mengi (Mungu amlaze pema peponi). Mzee Mengi alikuwa
ameshaanza mazungumzo na makampuni toka nje kuja kuwekeza viwanda vya simu na
magari hapa Tanzania. Lakini kumbuka wakati huo mapato yako ya ziada (namba 2)
bado yanaendelea kuingia.
Katika safari yako yote hiyo
ni lazima uwe ni mtu wa kutengeneza mtandao
na watu mbalimbali, kujifunza kupitia vitabu na vyombo vingine
mbalimbali vya habari hasa kuhusiana na taaluma yako au sekta ya biashara
ulizowekeza, wajasiriamali na wawekezaji ni sawa tu kama walivyokuwa
wanasheria, madaktari na wahasibu, ni watu wa kujifunza kabla na ni lazima
ubobee katika kile unachokifanya ikiwa utataka mafanikio na utajiri, na
haiwezekani ukatumia njia ya mkato ndio maana watu wengi huona kama ni jambo
gumu kupata utajiri.
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi
bado-1
Habari njema ni kwamba, kwa
makadirio ikiwa mtu anaweza akafuata hatua zote vizuri inaweza ikamchukua
takribani miaka 5 hivi kutajirika na kuwa huru kabisa kifedha, na hiki ni
kipindi kifupi kabisa.
Jinsi
ya kuwa na uhuru wa kifedha
Kabla hatujaenda kuona aina
za biashara za kuanza nazo unapotaka kuufikia utajiri na hatimaye uhuru kifedha
hebu kwanza tuone nini maana ya uhuru wa kifedha hasa. Uhuru wa kifedha ni hali ambayo mapato yako
ya ziada kutoka kwenye vile vitegauchumi usivyohusika moja kwa moja katika
mchakato wa uzalishaji yanapokuwa makubwa kuliko gharama zako zote za maisha (matumizi).
SOMA: Mbinu
za kufanikiwa kufikia malengo katika uwekezaji wowote utakaofanya.
Kwa mfano kama una biashara
inayoingiza faida shilingi laki 5 kwa mwezi kama mapato ya ziada na matumizi
yako kwa mwezi ni shiligi laki 3, tayari
wewe unakuwa umeshaufikia uhuru kifedha na unaweza hata ukaachana na kazi yako
ya awali.
Aina
ya biashara nzuri ya kuanzia unapotaka kuwa tajiri na kufikia uhuru kamili
kifedha
Kumiliki biashara bila shaka
kunatajwa kuwa ndiyo njia bora zaidi ya kuwa tajiri haraka au kuanza safari ya
kuufikia utajiri na hatimaye uhuru kamili wa kifedha, lakini siyo biashara zote
zenye uwezo huo, baadhi yake mtu unaweza kutajirika haraka na kwa gharama
kidogo lakini nyingine huchukua muda mrefu na uwekezaji wa pesa nyingi.
Biashara hizo ni hizi
zifuatazo;....................................................
...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Mpenzi
mdau wa masomo haya ya fedha hii ni sehemu ndogo tu ya somo letu hili. Masomo
kamili unaweza ukayapata yote ndani ya MASTERMIND
GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE ambapo yanatolewa mfululizo kila siku.
Kujiunga
na Kundi hilo lipia ada ya mwaka sh. 10,000/= tu kupitia namba 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo kisha SMS au ujumbe wasap
usemao “NATAKA OFFA YA VITU 14 NA GROUP LA MASOMO”
Ukishalipia
tunakutumia pia OFFA ya vitabu na
Michanganuo ya biashara mbalimbali kwenye simu au kompyuta muda huohuo, jumla
ni vitu 14, tazama orodha hapo chini.
Ndani
ya group pia tunakuwa na semina za jinsi ya kuandika Michanganuo ya biashara
bunifu zinazolipa haraka.
CHINI NI ORODHA YA VITU 14
VYA HIYO OFFA;
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa Kiswahili
2.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 tu - kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani, hutumika
vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
5.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
6.
COMPILLATION: Masomo 30 ya fedha
usiyoweza kuyapata popote, mengine 70 utayapata kwenye group kila siku - kwa Kiswahili
7.
MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji
Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
8.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa
kiingereza
9.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa Kiswahili
10. MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili
11. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiswahili
13. MCHANGANUO: Kiwanda cha mvinyo na juisi ya Rosella –Choya Investment – kwa kiswahili
14. MCHANGANUO: Kilimo cha Tikiti maji:- Kibada Watermelon Fruits – kwa kiswahili
0 Response to "BIASHARA NZURI YA KUANZIA UNAPOTAKA KUWA TAJIRI NA KUFIKIA UHURU KAMILI KIFEDHA"
Post a Comment