UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBOOST BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBOOST BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE

Roboti za 'kike' zinazotumia akili bandia

Binadamu kutokana na kujaliwa uwezo wa ubunifu na akili siku zote tokea zile zama za kale za mawe amekuwa akijitahidi kutafuta njia za kurahisisha na kuyaboresha maisha yake ikiwemo biashara kwa kutumia mbinu mbalimbali na katika kila hatua amekuwa akienda viwango vingine.

Ukisoma histroria ya maendeleo yake utaona binadamu amepitia zama tofautitofauti zikiwemo zama za kale za mawe, zama za chuma, zama za utumwa na ukabaila mpaka sasa hivi zama za mapinduzi ya viwanda ambayo nayo yamegawanyika katika hatua kuu 4

Mapinduzi ya kwanza ya viwanda yaliyoanza mwaka 1765 (karne ya 18) huko ulaya na Marekani yalihusisha mashine zilizoendeshwa kwa mvuke wa makaa ya mawe.

Mapinduzi ya pili mwaka 1870 yalishuhudia umeme na gesi vikitumika katika uzalishaji kwa wingi viwandani (mass production) huku wanasayansi na wajasiriamali wakiendelea kufanya ubunifu wa vitu mbalimbali

Na mapinduzi ya tatu yaliyotokea kuanzia mwaka 1969 ambapo elektroniki na nyuklia ndiyo vilitawala na kuwa mwanzo wa matumizi ya kompyuta za kisasa za kidigitali na teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) wakati huohuo dhana ya ubunifu ikiendelea kushika kasi

Sasa hivi tupo katika hatua ya 4 ya mapinduzi ya kiviwanda yaliyoanza tangu miaka ya 2000 ambapo akili mnemba a.k.a akili bandia (Artificial Intelligence au AI) ndiyo habari ya mjini. Compyuta na mashine za kidigitali zilizotumika katika mapinduzi ya tatu hapo juu sasa hivi vinapewa uwezo wa akili unaofanana na ule wa binadamu kutenda mambo kwa kufikiria na wakati mwingine kujifunza na kufanya maamuzi bila usaidizi wa mtu.

Kwani Akili bandia –Artificial Intelligence (AI) ni nini hasa?

Wengi huwa tunajiuliza akili mnemba ni nini?. Akili bandia/akili mnemba ni matumizi ya mashine/kompyuta kufanya vitu ambavyo kimsingi hapo zamani vilikuwa vinahitaji akili ya binadamu. Ni sayansi inayozifanya mashine zifikirie sawasawa na binadamu anavyofikiria na kutenda mambo kwa akili.

Akili bandia imeleta fursa kubwa kwa binadamu kutokana na kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu magumu ambayo yangelimgharimu muda mwingi na fedha. Hivyo wafanyabiashara na wajasiriamali wanapaswa kulijua hili na kujaribu kuzichangamkia fursa hizo pale inapowezekana wakitilia maanani ukweli kwamba ujasiriamali na ubunifu ni kama watoto mapacha hawatengani.

Akili bandia imeleta mapinduzi katika karibu kila nyanja uijuayo kuhusiana na maisha ya watu ya kawaida kuanzia afya, usafirishaji, mitandao ya kijamii, lugha & mawasiliano, biashara, benki na nyinginezo nyingi, nitatoa mifano michache hapa chini;

1.Lugha & mawasiliano:

Siku hizi kutafsiri lugha yeyote kwenda nyingine duniani imekuwa rahisi mno, ujio wa programu mpya ya ChatGPT yenye uwezo wa kuulizwa swali la aina yeyote ile na kujibu kwa usahihi kama binadamu, imefikia hata hatua ya kuanza kuzua waiwasi juu ya akili bandia kuleta maafa makubwa ya kimaadili na kibinadamu isipodhibitiwa mapema, mfano imegundulika kuwa hata programu hii inao uwezo wa kujibu mtihani wowote unaohusisha lugha kwa ufasaha kuzidi binadamu.

Unaweza kuandika taarifa yeyote zikiwemo, makala, barua, ripoti na proposal mbalimbali kwa kuitumia hii application bila kutoa jasho lolote. Tena isitoshe unaweza ukaiagiza ikushoree picha yeyote ile na ikafanya hivyo kwa usahihi mkubwa.

Auto-correct, wakati unapotype kitu kwenye kompyuta mfano barua au maandishi yeyote utaona unapokosea spelling kompyuta inakuwekea alama nyekundu na unapoweka mouse yako pale inakupa mapendekezo ya spelling sahihi za neno ulilokosea.

2.Tasnia ya uanahabari:

Waandishi wa habari akili mnemba imekuja kama muokozi wao kwani sasa hivi inaweza kutumika kuokoa muda na kuwahisha habari zao katika vyumba vya habari kwa wakati kupitia matumizi ya zana na application mbalimbali zinazoendeshwa kwa akili bandia mfano matumizi ya ChatGPT na hata google lens kwa ajili ya uhakiki wa habari na picha kabla havijafika kwa mhariri

3.Afya:

Akili bandia inatumika kwenye vifaa vya kufanya uchunguzi wa afya kama vile sampuli za tishu kwa usahihi mkubwa na kutoa majibu na aina ya matibabu yanayofaa. Akili bandia inatumiwa katika utafiti na uundaji wa dawa za kutibu magonjwa hatari mfano ebola na covid 19 kwa muda mfupi isivyo kawaida.

4.Usafiri na usafirishaji:

Magari na ndege zinazojiendesha zenyewe pasipo kuhitaji dereva ni matokeo ya AI. Gari hukwepa hatari zote barabarani wakiwemo wapita kwa miguu na magari mengine bila ya kuwagonga  au kusababisha ajali. Kwenye ramani za google mtu naweza kwenda popote pale akitumia usafiri kama wa Uber huku ikitabiri foleni au kikwazo chochote kile kinachoweza kuchelewesha safari na hivyo dereva kubadilisha njia.

5.Sekta ya Fedha

Unakumbuka ni lini umekwenda kupanga foleni benki? Kama wewe ni wa zamani kidogo vipi miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000 ulikuwa ukienda benki mara ngapi kwa juma? Shida zote hizi zimekuja kuondolewa na teknolojia ya akili bandia. Akili bandia imefanya iwe rahisi mabenki kuthibiti wizi na udanganyifu kwa mfano haiwezekani mtu kuiba password kwani watu hutumia utambulisho wa sauti, fingerprint, ama sura kama neno siri kitu ambacho mwizi kamwe hawezi kuiga, na akili bandia kutokana na kuwa na taarifa zote za mteja hushituka na kuchukua hatua mara moja inapoona dalili za kitendo kisichofanana na cha mteja husika kikiendelea kwenye akaunti yake. Hufunga mara moja au kuitisha mteja kuweka upya taarifa zake za msingi.

 6.Mitandao ya kijamii

Mitando ya kijamii kwa kutumia akili bandia inaweza kubaini ni kitu gani unachotafuta na kutoa mapendekezo kwa bidhaa, maneno au chochote kile unachotafuta mtandaoni. Wakati mwingine hata unaweza kushangaa kwani inajuaje? Kumbe ni kazi ya akili bandia inayochunguza muda wote uwapo mtandaoni kujua mienendo na tabia zako zikoje.

Taarifa hizi ndizo huzitumia katika kuonyesha matangazo watu wanayoweka. Wamiliki wa hii mitandao pia hutumia akili bandia kuisimamia kwani ingelikuwa vigumu sana kuajiri maelfu ya watu kama watoa huduma kwa mamilioni ya wateja wanaojiunga kila siku.

Mfano mzuri ni facebook, ukiona akaunti yako facebook imefungiwa ghafla kutokana na kuvunja miiko yao usidhani ni mtu wa kawaida kaifunga hapana, ni hiyohiyo akili bandia (bot) na utafanya kazi ya ziada kuweza kuwasiliana na mtu halisi/mfanyakazi wa facebook akufungulie.

Sachi injini mfano google na nyinginezo kama yahoo, Bing nk. inatumia akili bandia kuwezesha watumiaji wake kutafuta vitu mbalimbali mtandaoni.

Kwenye matangazo ya kulipia, facebook ads na hata Instagram ni akili bandia hufanya kazi kwa kutumia taarifa na tabia za watumiaji wa mitandao hiyo kuamua wanapaswa kuona tangazo lipi.

7.Kwenye Biashara za Rejareja

Lengo la makala yangu hii ya leo lilikuwa ni kipengele hiki hapa kutokana na maboresho tuliyoyafanya katika toleo jipya la kitabu chetu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA lakini pia kampeni yetu kwa ujumla ya mwaka huu isemayo, UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBUSTI BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE

Ili kwenda sambamba na kauli mbiu hii tumefanya maboresho makubwa kwenye hili kitabu na kuongeza sura moja nzima inayoelezea na kuonyesha jinsi akili bandia na ubunifu vinavyoweza kusaidia katika kuboost biashara ndogo isiyokuwa na mtaji wa uhakika hatimaye ikapata mtaji ndani ya muda mfupi ikapanda viwango vya juu. Kuiboost biashara maana yake ni kuichangamsha ama kuipa nguvu zaidi.

Kitabu hiki kwa ujumla wake kinalenga kumfanya mjasiriamali wa rejareja kukua haraka kwa kutumia nyenzo mbalimbali kwa mfano kuna sura tulizungumzia nyenzo muhimu sana 2, mifumo mbalimbali ya kawaida na ya kidigitali katika kusimamia mapato ya biashara ya rejareja yasipotee au kuhujumiwa na wasaidizi/wafanyakazi.

Lakini tumeona kuna umuhimu wa kuingiza sura hii inayozungumzia teknolojia ya akili bandia japo najua wengine wanadhani ni kwa ajili ya maduka ya mtandaoni tu (e-commerce) lakini ukisoma sura hiyo vizuri utagundua ni kwa namna gani hata mwenye kioski alivyokwishaanza kutumia teknolojia ya akili bandia bila kujijua na ni kipindi kifupi tu kijacho kila mwenye biashara ya rejareja atahitaji kuitumia teknolojia hii vingnevyo apitwe na washindani wake.

Hivi umewahi siku moja kutafuta bidhaa fulani kwenye mtandao wa intaneti ukaikosa lakini siku nyingine tu ukiwa unaperuzi mtandaoni wala huna tena wazo na ile bidhaa, ghafla kwenye ukurasa huo ukashangaa inaibuka picha (ina-pop) ya bidhaa ileile uliyokuwa ukiitafuta siku ile ukaikosa?

Hii ndiyo moja ya kazi za teknolojia ya akili bandia. Mfumo tata wa kompyuta unaofuatalilia nyendo za watumiaji siku zote ulishabaini kitu ulichokuwa ukikihitaji na hivyo siku ulipokikuta ukaamua kukuonyesha ukijua una mapenzi nacho na unaweza kukinunua bila shaka.

Kwahiyo akili bandia/mnemba kwenye biashara ya rejareja inaweza kuleta mapinduzi makubwa ikitumiwa ipasavyo. Kuna njia nyingi mfanyabiashara anaweza akanufaika nayo na zimeainishwa katika toleo jipya la kitabu hiki la mwaka 2024. Mwaka huu Jifunzeujasiriamali blog tumejipanga kutoa suluhisho la ugumu wa biashara kupitia ubunifu na njia mbalimbali za kurahisisha na kubusti biashara ikiwemo teknolojia ya akili bandia (AI) ndio maana tukaja na kaulimbiu ya;  UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBOOST BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE

Kabla hata ya kuja kwa teknolojia hii ya Akili bandia kitabu hiki kimekuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wengi wa rejareja hususani maduka na kila mwaka huwa tunaongeza maudhui kulingana na mabadiliko ya teknolojia na mwelekeo wa sekta ya rejareja kwa ujumla.

Unaweza kukipata kitabu hiki kwa kutumia moja kati ya njia hizi tatu (3) zifuatazo; 

 

1.   Kupitia simu au kompyuta yako (Nakala laini), Bei ni Tsh. 6,000/= unatumiwa muda huohuo unapolipia. Namba za malipo ni 0712202244 au 0765553030 Peter Augustino Tarimo

2.   Kuletewa Ulipo (Nakala ngumu) Ukiwa Dar es salaam ni Tsh. 16,000/= na Ukiwa mkoa mwingine wowote ni sh. 26,000/= kwa njia ya basi.

3.   Unaweza pia kukipata kupitia application hii hapa iitwayo GETVALUE, bofya hiyo link, kwa Tsh. 10,000/= unalipia kwa mitandao ya simu za mkononi, Tigopesa, Mpesa au Airtel Money. 

 

 

SOMA NA HIZI HAPA PIA;

1. Njia mpya za kufanya mambo: dunia, biashara, ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu

2. Maana kamili ya ujasiriamali: ulikotoka, ulipo na unakoelekea duniani

3. Mawazo ya biashara zitakazovuma miaka ijayo 2018 na kuendelea mpaka 2030

4. Ujasiriamali: ubunifu ndiyo msingi wake mkuu na injini ya uchumi katika soko huria.

5. Kanuni ya siri ya coca cola, birika la ajabu na wazo la dola milioni 1

6. Kama una biashara ndogo ya mtaji mdogo, hizi hapa njia 11 za kuibusti

7. Mamilionea vijana 10 wakisimulia siri za utajiri wao walivyofanikiwa

0 Response to "UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBOOST BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE"

Post a Comment