Binadamu kutokana na
kujaliwa uwezo wa ubunifu na akili siku zote tokea zile zama za kale za mawe
amekuwa akijitahidi kutafuta njia za kurahisisha na kuyaboresha maisha yake
ikiwemo biashara kwa kutumia mbinu mbalimbali na katika kila hatua amekuwa
akienda viwango vingine.
Ukisoma histroria ya
maendeleo yake utaona binadamu amepitia zama tofautitofauti zikiwemo zama za
kale za mawe, zama za chuma, zama za utumwa na ukabaila mpaka sasa hivi zama za
mapinduzi ya viwanda ambayo nayo yamegawanyika katika hatua kuu 4
Mapinduzi ya kwanza ya
viwanda yaliyoanza mwaka 1765 (karne ya 18) huko ulaya na Marekani yalihusisha
mashine zilizoendeshwa kwa mvuke wa makaa ya mawe.
Mapinduzi ya pili mwaka 1870
yalishuhudia umeme na gesi vikitumika katika uzalishaji kwa wingi viwandani (mass production) huku wanasayansi na
wajasiriamali wakiendelea kufanya ubunifu wa vitu mbalimbali
Na mapinduzi ya tatu yaliyotokea
kuanzia mwaka 1969 ambapo elektroniki na nyuklia ndiyo vilitawala na kuwa
mwanzo wa matumizi ya kompyuta za kisasa za kidigitali na teknolojia ya habari
na mawasiliano (ICT) wakati huohuo dhana ya ubunifu ikiendelea kushika kasi
Sasa hivi tupo katika hatua
ya 4 ya mapinduzi ya kiviwanda yaliyoanza tangu miaka ya 2000 ambapo akili
mnemba a.k.a akili bandia (Artificial
Intelligence au AI) ndiyo habari ya mjini. Compyuta na mashine za
kidigitali zilizotumika katika mapinduzi ya tatu hapo juu sasa hivi vinapewa
uwezo wa akili unaofanana na ule wa binadamu kutenda mambo kwa kufikiria na
wakati mwingine kujifunza na kufanya maamuzi bila usaidizi wa mtu.
Kwani
Akili bandia –Artificial Intelligence (AI) ni nini hasa?
Wengi huwa tunajiuliza akili
mnemba ni nini?. Akili bandia/akili mnemba ni matumizi ya mashine/kompyuta
kufanya vitu ambavyo kimsingi hapo zamani vilikuwa vinahitaji akili ya
binadamu. Ni sayansi inayozifanya mashine zifikirie sawasawa na binadamu anavyofikiria
na kutenda mambo kwa akili.
Akili bandia imeleta fursa
kubwa kwa binadamu kutokana na kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu magumu
ambayo yangelimgharimu muda mwingi na fedha. Hivyo wafanyabiashara na
wajasiriamali wanapaswa kulijua hili na kujaribu kuzichangamkia fursa hizo pale
inapowezekana wakitilia maanani ukweli kwamba ujasiriamali na ubunifu ni kama
watoto mapacha hawatengani.
Akili bandia imeleta
mapinduzi katika karibu kila nyanja uijuayo kuhusiana na maisha ya watu ya
kawaida kuanzia afya, usafirishaji, mitandao ya kijamii, lugha &
mawasiliano, biashara, benki na nyinginezo nyingi, nitatoa mifano michache hapa
chini;
1.Lugha
& mawasiliano:
Siku hizi kutafsiri lugha
yeyote kwenda nyingine duniani imekuwa rahisi mno, ujio wa programu mpya ya ChatGPT
yenye uwezo wa kuulizwa swali la aina yeyote ile na kujibu kwa usahihi kama
binadamu, imefikia hata hatua ya kuanza kuzua waiwasi juu ya akili bandia
kuleta maafa makubwa ya kimaadili na kibinadamu isipodhibitiwa mapema, mfano
imegundulika kuwa hata programu hii inao uwezo wa kujibu mtihani wowote unaohusisha
lugha kwa ufasaha kuzidi binadamu.
Unaweza kuandika taarifa
yeyote zikiwemo, makala, barua, ripoti na proposal mbalimbali kwa kuitumia hii
application bila kutoa jasho lolote. Tena isitoshe unaweza ukaiagiza ikushoree
picha yeyote ile na ikafanya hivyo kwa usahihi mkubwa.
Auto-correct,
wakati unapotype kitu kwenye kompyuta mfano barua au maandishi yeyote utaona
unapokosea spelling kompyuta inakuwekea alama nyekundu na unapoweka mouse yako
pale inakupa mapendekezo ya spelling sahihi za neno ulilokosea.
2.Tasnia
ya uanahabari:
Waandishi wa habari akili
mnemba imekuja kama muokozi wao kwani sasa hivi inaweza kutumika kuokoa muda na
kuwahisha habari zao katika vyumba vya habari kwa wakati kupitia matumizi ya
zana na application mbalimbali zinazoendeshwa kwa akili bandia mfano matumizi
ya ChatGPT na hata google lens kwa ajili ya uhakiki wa habari na picha kabla
havijafika kwa mhariri
3.Afya:
Akili bandia inatumika
kwenye vifaa vya kufanya uchunguzi wa afya kama vile sampuli za tishu kwa
usahihi mkubwa na kutoa majibu na aina ya matibabu yanayofaa. Akili bandia
inatumiwa katika utafiti na uundaji wa dawa za kutibu magonjwa hatari mfano
ebola na covid 19 kwa muda mfupi isivyo kawaida.
4.Usafiri
na usafirishaji:
Magari na ndege
zinazojiendesha zenyewe pasipo kuhitaji dereva ni matokeo ya AI. Gari hukwepa
hatari zote barabarani wakiwemo wapita kwa miguu na magari mengine bila ya
kuwagonga au kusababisha ajali. Kwenye
ramani za google mtu naweza kwenda popote pale akitumia usafiri kama wa Uber
huku ikitabiri foleni au kikwazo chochote kile kinachoweza kuchelewesha safari
na hivyo dereva kubadilisha njia.
5.Sekta
ya Fedha
Unakumbuka ni lini umekwenda
kupanga foleni benki? Kama wewe ni wa zamani kidogo vipi miaka ya 90 na
mwanzoni mwa 2000 ulikuwa ukienda benki mara ngapi kwa juma? Shida zote hizi
zimekuja kuondolewa na teknolojia ya akili bandia. Akili bandia imefanya iwe
rahisi mabenki kuthibiti wizi na udanganyifu kwa mfano haiwezekani mtu kuiba
password kwani watu hutumia utambulisho wa sauti, fingerprint, ama sura kama
neno siri kitu ambacho mwizi kamwe hawezi kuiga, na akili bandia kutokana na
kuwa na taarifa zote za mteja hushituka na kuchukua hatua mara moja inapoona
dalili za kitendo kisichofanana na cha mteja husika kikiendelea kwenye akaunti
yake. Hufunga mara moja au kuitisha mteja kuweka upya taarifa zake za msingi.
6.Mitandao ya kijamii
Mitando ya kijamii kwa
kutumia akili bandia inaweza kubaini ni kitu gani unachotafuta na kutoa
mapendekezo kwa bidhaa, maneno au chochote kile unachotafuta mtandaoni. Wakati
mwingine hata unaweza kushangaa kwani inajuaje? Kumbe ni kazi ya akili bandia
inayochunguza muda wote uwapo mtandaoni kujua mienendo na tabia zako zikoje.
Taarifa hizi ndizo huzitumia
katika kuonyesha matangazo watu wanayoweka. Wamiliki wa hii mitandao pia
hutumia akili bandia kuisimamia kwani ingelikuwa vigumu sana kuajiri maelfu ya
watu kama watoa huduma kwa mamilioni ya wateja wanaojiunga kila siku.
Mfano mzuri ni facebook,
ukiona akaunti yako facebook imefungiwa ghafla kutokana na kuvunja miiko yao
usidhani ni mtu wa kawaida kaifunga hapana, ni hiyohiyo akili bandia (bot) na
utafanya kazi ya ziada kuweza kuwasiliana na mtu halisi/mfanyakazi wa facebook
akufungulie.
Sachi injini mfano google na
nyinginezo kama yahoo, Bing nk. inatumia akili bandia kuwezesha watumiaji wake
kutafuta vitu mbalimbali mtandaoni.
Kwenye matangazo ya kulipia,
facebook ads na hata Instagram ni akili bandia hufanya kazi kwa kutumia taarifa
na tabia za watumiaji wa mitandao hiyo kuamua wanapaswa kuona tangazo lipi.
7.Kwenye
Biashara za Rejareja
Lengo la makala yangu hii ya
leo lilikuwa ni kipengele hiki hapa kutokana na maboresho tuliyoyafanya katika
toleo jipya la kitabu chetu cha MAFANIKIO
YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA lakini pia kampeni yetu kwa ujumla ya mwaka
huu isemayo, UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBUSTI BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO
VINGINE
Ili kwenda sambamba na kauli
mbiu hii tumefanya maboresho makubwa kwenye hili kitabu na kuongeza sura moja
nzima inayoelezea na kuonyesha jinsi akili bandia na ubunifu vinavyoweza
kusaidia katika kuboost biashara ndogo isiyokuwa na mtaji wa uhakika hatimaye
ikapata mtaji ndani ya muda mfupi ikapanda viwango vya juu. Kuiboost biashara
maana yake ni kuichangamsha ama kuipa nguvu zaidi.
Kitabu hiki kwa ujumla wake
kinalenga kumfanya mjasiriamali wa rejareja kukua haraka kwa kutumia nyenzo
mbalimbali kwa mfano kuna sura tulizungumzia nyenzo muhimu sana 2, mifumo
mbalimbali ya kawaida na ya kidigitali katika kusimamia mapato ya biashara ya
rejareja yasipotee au kuhujumiwa na wasaidizi/wafanyakazi.
Lakini tumeona kuna umuhimu
wa kuingiza sura hii inayozungumzia teknolojia ya akili bandia japo najua wengine
wanadhani ni kwa ajili ya maduka ya mtandaoni tu (e-commerce) lakini ukisoma sura hiyo vizuri utagundua ni kwa namna
gani hata mwenye kioski alivyokwishaanza kutumia teknolojia ya akili bandia bila
kujijua na ni kipindi kifupi tu kijacho kila mwenye biashara ya rejareja atahitaji
kuitumia teknolojia hii vingnevyo apitwe na washindani wake.
Hivi umewahi siku moja
kutafuta bidhaa fulani kwenye mtandao wa intaneti ukaikosa lakini siku nyingine
tu ukiwa unaperuzi mtandaoni wala huna tena wazo na ile bidhaa, ghafla kwenye
ukurasa huo ukashangaa inaibuka picha (ina-pop)
ya bidhaa ileile uliyokuwa ukiitafuta siku ile ukaikosa?
Hii ndiyo moja ya kazi za teknolojia
ya akili bandia. Mfumo tata wa kompyuta unaofuatalilia nyendo za watumiaji siku
zote ulishabaini kitu ulichokuwa ukikihitaji na hivyo siku ulipokikuta ukaamua
kukuonyesha ukijua una mapenzi nacho na unaweza kukinunua bila shaka.
Kwahiyo akili bandia/mnemba
kwenye biashara ya rejareja inaweza kuleta mapinduzi makubwa ikitumiwa
ipasavyo. Kuna njia nyingi mfanyabiashara anaweza akanufaika nayo na
zimeainishwa katika toleo jipya la kitabu hiki la mwaka 2024. Mwaka huu Jifunzeujasiriamali
blog tumejipanga kutoa suluhisho la ugumu wa biashara
kupitia ubunifu na njia mbalimbali za kurahisisha na kubusti biashara ikiwemo
teknolojia ya akili bandia (AI) ndio maana tukaja na kaulimbiu ya; UBUNIFU
NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBOOST BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE
Kabla hata ya kuja kwa
teknolojia hii ya Akili bandia kitabu hiki kimekuwa msaada mkubwa kwa
wafanyabiashara wengi wa rejareja hususani maduka na kila mwaka huwa tunaongeza
maudhui kulingana na mabadiliko ya teknolojia na mwelekeo wa sekta ya rejareja
kwa ujumla.
Unaweza kukipata kitabu hiki kwa kutumia moja kati ya njia hizi tatu (3) zifuatazo;
1.
Kupitia
simu au kompyuta yako (Nakala laini),
Bei ni Tsh. 6,000/= unatumiwa muda huohuo unapolipia. Namba za malipo ni 0712202244 au 0765553030 Peter Augustino Tarimo
2.
Kuletewa
Ulipo (Nakala ngumu) Ukiwa Dar es
salaam ni Tsh. 16,000/= na Ukiwa mkoa mwingine wowote ni sh. 26,000/= kwa njia
ya basi.
3.
Unaweza
pia kukipata kupitia application hii hapa iitwayo GETVALUE, bofya hiyo link, kwa Tsh. 10,000/=
unalipia kwa mitandao ya simu za mkononi, Tigopesa, Mpesa au Airtel Money.
SOMA
NA HIZI HAPA PIA;
1. Njia mpya za kufanya mambo: dunia, biashara, ajira vinabadilika
kwa kasi ya ajabu
2. Maana kamili ya ujasiriamali: ulikotoka, ulipo na unakoelekea
duniani
3. Mawazo ya biashara zitakazovuma miaka ijayo 2018 na kuendelea
mpaka 2030
4. Ujasiriamali: ubunifu ndiyo msingi wake mkuu na injini ya
uchumi katika soko huria.
5. Kanuni ya siri ya coca cola, birika la ajabu na wazo la dola
milioni 1
6. Kama una biashara ndogo ya mtaji mdogo, hizi hapa njia 11 za
kuibusti
7. Mamilionea vijana 10 wakisimulia siri za utajiri wao
walivyofanikiwa
0 Response to "UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBOOST BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE"
Post a Comment