Hivi umewahi kujiuliza ni kwanini watu wengi
huwa tunafahamu fika siri, njia, mbinu na mikakati yote ya mafanikio lakini
bado tu tumekuwa tukishindwa kuyafikia mafanikio tunayotamani tuwe nayo.
Kufuatia mapinduzi makubwa kwenye zama hizi za taarifa, siri kubwa
walizotumia waliofanikiwa karibu katika kila nyanja hapa duniani zinajulikana.
Katika makala hii tutakwenda kufahamu kile hasa
kinachotuzuia tusiitumie siri hiyo ingawa tayari tunaifahamu.
SOMA: Kumbe Nelson Mandela alikuwa mpenzi wa vitabu vya Mafanikio
Kuna watu wengi mashuhuri Duniani na hata hapahapa
Tanzania waliowahi kuitumia siri hii na ikafanya kazi vizuri sana kwao, mtu
kama Eric Shigongo ikiwa uliwahi kufuatilia makala zake utakubaliana nami kuwa
aligundua na kuitumia siri hiyo. Lakini pia kuna watu kama kina Ophrah Winfrey,
Muhammad Ally, Nelson Mandela, Kelvin Kiptum, Magic Johnson na wengineo wengi.
Yamkini kwa miaka mingi umekuwa ukijifunza njia nyingi za
mafanikio katika maisha, siri ya pesa, ujasiriamali na siri nyingine lukuki za
kufanikiwa kibiashara lakini cha kustaajabisha imekuwa vigumu mno kwako kuyatia
hayo kwenye vitendo kusudi uweze kupata matokeo tarajiwa
SOMA: Muhammad Ali, uvumilivu, nidhamu, ujasiri, msimamo vilimpa ubingwa Kinshasa Zaire
Katika blogu na makala zangu kwenye mitandao ya kijamii
nimekuwa nikifundisha wajasiriamali mbinu na mikakati bora kabisa ya kuzikuza
biashara zao zifike viwango vingine pamoja na njia za mafanikio katika maisha lakini bado
wapo wengine pamoja na kujifunza yoote hayo wanaendelea tu kuhaha huku na kule
wakisaka dawa ya mafanikio katika biashara zao. Shida ni nini hasa?
MTAZAMO
WA AKILI (MINDSET)
Hili ndilo jibu lake: Tunafahamu kila kitu cha kufanya
ili tufanikiwe lakini hatufanyi kwa sababu mitazamo ya akili zetu haiwezi
kuturuhusu tufanye hivyo, inatuvuta nyuma. Siri kubwa waliofanikiwa huitumia
wengine hatuijui ni kujenga Mtazamo
chanya wa akili (Positive mindset)
Kwani
mtazamo wa akili (Mindset) ni kitu gani hasa?
Mindset kwa maana rahisi kabisa ni jinsi mtu
anavyofikiri. Ni imani au maoni ya mtu aliyojengewa tokea utotoni juu yake
mwenyewe na vitu vingine mbalimbali vinavyomzunguka. Imani hii ndiyo huamua
kufanikiwa ama kufeli kwake. Huathiri namna anavyofikiri, anavyojihisi na tabia
yake kwa ujumla.
SOMA: Imani, mapenzi na ngono ndiyo vitu vyenye nguvu kuliko mihemko mingine yote mikubwa
Aina
2 za Mtazamo wa akili
Kuna aina mbili za mtazamo wa akili, Mtazamo chanya wa
akili(+) na Mtazamo hasi wa akili (-) Kwa walio na mtazamo chanya wa akii
wanaamini mambo mbalimbali yanawezekana wakati walio na mtazamo hasi huamini
karibu kila jambo ni mkosi haiwezekani kulifanya kirahisi.
Jinsi
ya kubadilisha mtazamo wako wa akili
Kwa bahati njema sana Mwenyezi Mungu ameweka njia ya
walio na mitazamo hasi ya akili kuwa na uwezo wa kurekebisha mitazamo yao na
kuwa na mitazamo chanya. Kuna njia mbalimbali unaweza ukazitumia kurekebisha
mtazamo wako wa akili lakini mimi hapa napendekeza njia zilizotajwa kwenye
kitabu kilichoandikwa na Napoleon Hill, Think & Grow Rich (FIKIRI & UTAJIRIKE)
SOMA: Vipaji, uwezo, akili ni vitu tunazaliwa navyo au kujifunza?
Kama jina la kitabu linavyosadifu, kitabu hiki kwa
asilimia kubwa kinazungumzia jinsi mtazamo wa akili wa mtu unavyoweza kumsaidia
kufanikiwa au kutokufanikiwa katika nyanja aitakayo maishani iwe ni katika
pesa, mahusiano, masomo, kiroho nk. Napoleon Hill anataja njia ya Kujishauri-binafsi (Autosuggestion) katika sura ya 4 kama
njia kuu ya kurekebisha mtazamo hasi wa akili kuwa mtazamo chanya wa akili kupitia
kitendo cha kukariri ama kurudiarudia
kujiambia maneno chanya yanayoweza hatimaye kuchukua pahala pa maneno hasi
uliyopandikiziwa tangia utotoni au siku za nyuma.
Mbinu hii hutumiwa pia hata na Wahubiri wa dini katika
imani mbalimbali siku hizi, sijui kama huipata kwenye vitabu vya imani zao ama
wanaichukua kutoka vitabu vya kawaida kama hiki cha Napoleon hill, lakini
inafanya kazi kwao pia.
Utamsikia kiongozi wa dini au madhehebu flani akiwahimiza
waumini wake kukariri maneno kwa mfano anaweza kurudiarudia maneno, “Pokea muujiza, pokea gari” mara nyingi kiasi kwamba muumini huamini kweli anamiliki
kitu mfano gari, pesa nk. mtazamo huu anaojengewa muumini hatima yake
unatengeneza njia na mipango itakayomwezesha kweli kumiliki gari au kitu
alichoaminishwa kukipata.
Soma vizuri sura zifuatazo kubadiliisha mindset yako;
Sura ya pili (SHAUKU)-“Hatua 6 za kubadilisha shauku yako kuwa
katika kipimo halisi cha fedha”,
Sura ya 4 (KUJISHAURIBINAFSI)-
“Hakuna mawazo yawe ni chanya ama hasi,
yanayoweza kuingia akili ya ndani bila msaada wa kanuni hii ya
kujishauri-binafsi”
Sura
ya 14 (MLANGOFAHAMU WA 6) –Kuitisha
mikutano ya kufikirika na kundi la washauri wasioonekana
Kwahiyo unapokuwa na mtizamo sahihi wa akili ni suala la
muda tu, hakuna kitakachokuzuia kutoboa kwani njia ya kufanikiwa kwako ni
nyeupe pee kama theluji.
................................
Makala yetu iliyopita
tulizindua kaulimbiu ya mwaka huu isemayo; UBUNIFU
NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBOOST BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE. Nikiwa
na maana kwamba 2024 tuta-focus zaidi kwenye vitu hivi 2 katika kuzifanya
biashara zetu kupiga hatua kubwa na kwa haraka zaidi.
Kwa mantiki hiyo tumeanza
pia kwenye MASTERMIND GROUP letu la watsap semina za kuandaa Michanganuo bunifu
ya biashara zinazolipa haraka. Siku ya Jumatatu ya tarehe 25 saa 3 usiku
tutaanza semina ya kuandika Mchanganuo bunifu wa Biashara ya ufugaji wa kuku
Chotara (300) aina ya Kuroiler
Kwa kuwa focus yetu kubwa ni
UBUNIFU, katika mchanganuo huu
tofauti na michanganuo mingi ya miradi ya ufugaji wa kuku uliyowahi kupitia,
huu tumeonyesha ubunifu wa kipekee kabisa ambapo mtu anatengeneza faida kubwa
ndani ya kipindi kifupi sana.
Ufugaji wa kuku ni miradi
inayopendwa sana na watu wengi nchini kutokana na urahisi wake lakini pamoja na
hivyo watu hujikuta wakivunjika mioyo baada ya kukuta kumbe siyo rahisi kivile
kupata faida ya uhakika kama inavyodhaniwa. Kuna changamoto kubwa ambazo kama
mtu hujawa mbunifu utaiona biashara ya kufuga kuku kama ni bishara ya faida
kidogo sana au kwaajili tu ya kitoweo cha Idi na Krismasi
Tafadhali fuatilia makala
zetu siku hizi 2 kujua yatakayokuwemo katika semina hiyo, ratiba na muda wa
kumalizika.
JINSI
YA KUJIUNGA NA SEMINA HII
Tiketi ya kushiriki semina
unapaswa kuwa na mchanganuo kamili wa kuku wa nyama aina ya kuroiler ambao
tayari tumekwishauandaa pamoja na Kitabu chetu cha Michanganuo ya Biashara na
Ujasiriamali. Ili kupata vitu hivi unalipia shilingi elfu 10 tu badala ya sh.
Elfu 20
Mchanganuo wa kuku chotara
wa nyama utakuwezesha kufuatilia semina yetu kwani tutauandika upya hatua kwa
hatua. Kitabu ni kwa ajili ya marejeo ya kanuni mbalimbali za uandishi wa
Michanganuo ya Biashara za aina mbalimbali.
BONUS
Mbali na michanganuo 10
iliyoko ndani ya kitabu lakini pia utapata papo hapo bure michanganuo ifuatayo
isiyo ndani ya kitabu na yenye thamani ya sh. elfu 60;
1.
Mchanganuo wa kuku wa nyama( Tumaini Broilers)-kiingereza
2.
Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili
3.
Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora
Project)-swahili
4.
Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada
watermelon)-kiswahili
5.
Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant)-kiingereza
6.
Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant) -kiswahili
Kujiunga lipia sh. 10,000/= kwa namba 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe
usemao; “NIUNGE SEMINA BUNIFU YA
KUROILER”
Utatumiwa kila kitu muda huohuo na kuunganishwa Mastermind group la MICHANGANUO-ONLINE
UPEKEE
WA GROUP LA MWAKA HUU
Ukishamaliza semina una hiyari ya kuendelea kubakia
katika MASTERMIND GROUP letu kwa
ajili ya masomo ya kila siku ya fedha na Michanganuo pamoja na mentorship
Tofauti na magroup ya miaka iliyopita hili tumetumia
mtindo uliopendekezwa na Napoleon Hill katika kitabu cha Think and Grow Rich, Sura ya 10 (NGUVU YA USHIRIKA) au The Power of
Mastermind -“ushirikiano wa maarifa na juhudi katika roho ya masikilizano kati ya
watu wawili au zaidi kwa ajili ya kufikia lengo kamili”
VITABU
ZAIDI NA HUDUMA TUNAZOZITOA
·
Ukitaka kitabu cha Think & Grow Rich
nakala ya Kiswahili tembelea mtandao huu hapa>>GETVALUE na
ukifuata taratibu zote utakipakua kwenye simu janja yako.
·
Kwa vitabu vyetu vingine vyote ukilipia tu tunakutumia
kupitia simu au kompyuta yako muda huohuo, Cheki ushuhuda kwa mteja wa kitabu
cha SIRI YA MAFANIKIO
YA DUKA LA REJAREJA HAPA alvyonunua nakala yake na kutumiwa muda uleule.
·
Tunatoa pia huduma ya kuandika Mchanganuo wa
biashara yeyote ile kwa gharama rafiki. Wasiliana nasi tuweze kufanya kazi pamoja: call/watsap: 0712202244 au
0765553030
0 Response to "NI SIRI KUBWA WALIOFANIKIWA HUITUMIA LAKINI WENGI BADO HATUIJUI"
Post a Comment