ETI KUKU WA KIENYEJI UKIWAPA CHANJO NYAMA YAKE HUPOTEZA LADHA TAMU YA ASILI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

ETI KUKU WA KIENYEJI UKIWAPA CHANJO NYAMA YAKE HUPOTEZA LADHA TAMU YA ASILI?

Chanjo ya kuku

Michael aishiye Kiluvya Mkoa wa Pwani aliamua kufuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya mayai na nyama. Alijenga banda zuri na imara kwa ajili ya malazi ya kuku pamoja na viota vya kutagia mayai. Michael alichagua kutumia mfumo huria wa ufugaji wa kuku ambapo kuku wangezurura mchana kutwa wakijitafutia wenyewe chakula na kurudi bandani jioni kulala.

Alianza kutafuta matetea kwanza  kwa kuulizia ulizia kwa wafugaji wengine lakini ilikuwa vigumu sana kupata idadi ya kuku aliyokusudia kuanza nao. Yeye alihitaji kuanza na matetea 12 na majogoo 2 lakini alipata matetea watano peke yake.

Rafiki yake wa karibu ambaye pia ni jirani na mfugaji mzuri wa kuku alimshauri kwa kumwambia, “Michael kwanini usizunguke masoko ya kuku wa kienyeji ukachunguza wauzaji wenye matetea walio na umri mdogo ukaja kuwatenga kwa muda?

Michael aliafikiana na wazo la jirani yake huyo akachukua hatua ya kuzunguka masoko mbalimbali wanakouza kuku wa kienyeji, haikumchukua muda mrefu akawa ametimiza lengo lake la kuwa na matetea 12 na majogoo 2

Kitu cha kwanza kufanya aliwatenga kuku wote alionunua katika mazingira asiyokuwa na uhakika nayo kwani wauzaji wengine wa kuku huuza kuku wao pale tu waonapo kuna dalili za mlipuko wa magonjwa ya kuku mfano kideri nk. Hivyo kitendo cha kuwatenga kwa siku kadhaa au hata wiki kinasaida kubaini ikiwa kama walikuwa na maambukizi ya ugonjwa wowote na pia kuwalinda wale aliokuwa nao kabla wasiambukizwe.

Jirani aliendelea kumpa ushauri kwamba ingelikuwa jambo la busara pia ikiwa angewanunulia kuku wake chanjo muhimu za magojwa yasiyotibika mfano ugonjwa hatari wa kideri cha kuku, gumboro na hata dawa za minyoo kwa kuwa kuku walikwisha fikisha miezi zaidi ya 3.

Wazo la chanjo kwa kuku Michael hakulifurahia hata kidogo kwani alikuwa amewahi kusikia mara nyingi kwamba kuwapatia kuku wa kienyeji madawa na chanjo si jambo zuri kwani hufanya nyama yake baada ya kuchinjwa kupoteza kabisa ladha yake ya asili kama kuku wa kienyeji. Badala yake aliamua kuwafuga tu hivyohivyo bila ya kuwapatia chanjo wala dawa ya aina yeyote.

Kuku wa Michael waliendelea tu vizuri  licha ya kukataa ushauri wa rafiki yake ambaye alikuwa na uzoefu na kazi hii kwa muda mrefu. Miezi miwili baadae matetea walianza kutaga huku yale majogoo nayo yakawa yameshaanza kuwika kwani yalikuwa na umri mkubwa kidogo kuliko matetea. Michael alitumia mfumo huria wa ufugaji wa kuku ambapo kuku walizurura mchana kutwa wakijitafutia wenyewe chakula na kuingia bandani jioni.

Aliwawekea viota vya kutagia hivyo nyakati za mchana kuku matetea waliingia wenyewe katika viota na kutaga mayai kisha walitoka na kuendelea kuchakuara kwenye ardhi ya maeneo ya karibu na banda lao.

Alichowawekea jirani na banda ni vyombo kwa ajili ya maji tu kwani hakukuwa na chanzo cha maji karibu kuku wangeweza kunywa, lakini chakula hawakuwa na shida kabisa kwani walirudi jioni firigisi zao zikiwa zimejaa tele.

Kuku hatimaye walianza kuatamia na kila mmoja kwa wakati wake alitotoa vifaranga si chini ya kumi 10, na jumla walikuwa vifaranga 110. Rafiki yake kama kawaida yake hakuchoka kumpa ushauri na safari hii akampa mbinu ya kuwaweka vifaranga wote ndani ya banda baada ya kuota manyoya kisha walishwe mle mpaka watakapoweza kujitafutia chakula wenyewe na hatari ya kuliwa na wanyama au ndege kupungua.

Michael alifanya hivyo na kweli wakapona kuku 100 alioendelea nao mpaka walipofikisha umri wa kutaga na kuwika miezi 6. Wakati huohuo wale mama zao walikuwa wakiendelea kutaga ila safari hii hakuwaruhusu tena kutamia kutokana na jukumu zito la kuwatunza vifaranga wa mwanzo 100. Kwahiyo jumla alikuwa sasa na kuku 112 mchanganyiko wa matetea na majogoo humohumo.

Malengo ya Michael yalikuwa ni kufikisha kuku 500 kisha aanze kuwauza na kubakisha wachache kwa ajii ya kuendeleza uzao. Kuku wakiwa bado wanaendelea kutaga, sasa walikuwa wakitaga wote mama na watoto. Ghafla Michael alianza kuona dalili zisizokuwa za kawaida, baadhi ya kuku walianza kusinzia na kupoteza nguvu. Hakukurupuka kwenda kumwambia rafiki yake akajisemea tu, “Ah! Ni hali tu ya kawaida, hawa ni kuku wa kienyeji bwana watapona tu wenyewe ”

Kuku walioanza kuugua hali ilizidi kuwa mbaya, siku 3 mpaka wiki moja baadae walianza kufa mmoja mmoja ndipo sasa ikamlazimu aombe ushauri kwa jirani yake. Jirani alimwambia ule ulikuwa ni msimu wa mlipuko wa ugonjwa wa kideri na hakuna namna angeweza fanya zaidi ya kuwapatia vitamin na antibiotics kupunguza magojwa nyemelezi lakini siyo kuwatibu kabisa na hii ingesaidia tu kupunguza wingi wa vifo vya kuku.

Mpaka wimbi la ugojwa linatulia, Michael alikuwa amebakiwa na matetea  12 tu, jogoo wote walikufa na hata hawa matetea 12 wengi wao bado walionekana hawakuwa na nguvu mpaka wiki kadhaa baadae.

Kwa kifupi Bwana Michael alikuwa ndio kwanza anaanza tena ufugaji na idadi ileile kama aliyoanza nayo mwanzo isipokuwa sasa ilimbidi aingie tena mfukoni kwenda kutafuta majogoo 2. Ilimuuma sana kuona kuu wake wakiteketea huku wa jirani yake japo walikuwa wakicheza na kuchakura wote pamoja na wake shambani lakini hawakufa hata mmoja kwasababu aliwahi kuwapatia chanjo.

Isingelikuwa tahadhari jirani huyu aliyompatia Michael kipindi kile anaanza ufugaji, basi sasa hivi Michael angelikuwa akimshika uchawi na pengine wasingekuwa wanaongea tena kwa kudhania labda amemlogea kuku wake wakafa huku wakwake wakiendelea ‘kudunda’ kamakawaida.

Je, kuna ukweli kiasi gani wa kuku kupoteza ladha yake ya asili kisa kuwapatia chanjo?

Dhana hii kwa upande mmoja ina ukweli lakini kuna namna unaweza kuepukana na tatizo hilo. Wataalamu wa mifugo na siyo kuku tu peke yake wanashauri kwamba pindi unapompa mnyama dawa ya aina yeyote basi usimchinje kipindi kifupi.

Dawa ama chochote kiingiacho ndani ya mwili wa mnyama kina uwezekano wa kubadilisha ladha yake lakini ni kwa muda tu, baada ya kipindi fulani kupita hali hiyo hutoweka na nyama hurudia ladha yake ileile.  

Ukiwapatia kuku wako chanjo zingatia sana muda unaoshauriwa na wataalamu wa mifugo kuwachinja tangu siku umewapa chanjo.

Umuhimu wa chanjo kwa kuku wa kienyeji

Wengi tunadhani labda chanjo ni kwa ajili ya kuku wa kisasa ama chotara tu peke yake lakini hii siyo sahihi.Sababu kwamba kuku wa kienyeji ni wavumilivu sana kwa magonjwa haimaanishi kwamba hawaugui hapana, Magonjwa yote yanayowasumbua kuku wa kisasa yanaweza pia kuwapata wa kienyeji na wakafa au kupata madhara sema tu tofauti ipo kwenye kiwango cha madhara kwani wa kienyeji madhara ni asilimia kidogo zaidi ya wenzao wa kisasa.

Kwa mfano tuseme labda una kuku 100 wa kienyeji ukilipuka ugonjwa wanaweza kufa 20 au 30 lakini ikiwa ni wakisasa watakufa pengine 70 mpaka 90

Ufugaji wa kuku wa asili huria una faida kubwa sana lakini wafugaji wengi hushindwa kuipata kutokana na hatari zitokanazo na magojwa, wanyama na ndege walao kuku mfano vicheche, paka, kunguru na hata mbwa.Kuna njia madhubuti za kuzuia hatari hizi zote  mfugaji akiamua na tutazijadili siku nyingine.

Kwa mtu anayepambana kupata mtaji wa biashara ufugaji wa kuku wa kienyeji ni njia nzuri sana na rahisi ya kukuza mtaji kwa ajili ya kufanyia biashara nyingine. Ukiweka malengo na kuyapambania kuku wa kienyeji wanaweza wakakutoa. Kuku wako anatotoa vifaranga 10, kwanini mwshowe wapone wawili tu au mmoja? Hawapaswi kufa hata mmoja labda tu iwe bahati mbaya mmoja au wawili.

 

.............................................

 

MSIMU WA KUKU bado unaendelea na jana 27/06/2024 ndio ilikuwa siku ya mwisho ya Semina yetu ya Mchanganuo wa kuku kuroiler wa nyama Darasa la awamu ya 3.

Siku hii tulimalizia na Mpango wa fedha ambayo ilikuwa sura ndefu kuliko nyingine zote na tulijitahidi sana kuhakikisha washiriki wanafahamu vyema namna ya kukisia ripoti zote kama ile ya faida na hasara, cash flow, Mizania ya biashara na Sehemu za biashara (ratio) kwa mwaka lakini miaka 3

Madarasa ya semina hii yanaendelea na Siku ya Jumatatu tarehe 01/07/2024 tutaanza Darasa la awamu ya 4. Hivyo ikiwa unahitaji lipia kitabu na Mchanganuo wako kwa ajili ya rejea kupitia namba 0712202244 au 0765553030 kisha meseji, “NATAKA SEMINA YA KUROILER NA OFFA YA MICHANGANUO 6”

Ukishalipia nakutumia muda huohuo kila kitu na kukuunganisha na group la semina

Semina hii lengo lake kuu ni kumfanya mjasiriamali awe na uwezo wa kufanya mchanganuo wa biashara yeyote ile kwani imetengenezwa maalumu kwa ajili hiyo, vilevile kumpa uelewa mpana wa miradi ya ufugaji kuku kibiashara zaidi.

Washiriki wakimaliza semina huunganishwa group la Mentorship kwa mwaka mzima wakiendelea kujifunza, kushare mambo mbalimbali na kuuliza maswali yeyote yahusuyo ujasiriamali na biashara kwa ujumla.

Tumedhamiria kutengeneza wataalamu (experts) wa mipango ya biashara.

 

 

OFFA YA VITU HIVYO 9 NI HII HAPA CHINI;

 

1.    Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)

2.    Mchanganuo Mpya: Biashara ya ufugaji wa kuku chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)

3.    Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-kiingereza

4.    Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili

5.    Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili

6.    Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili

7.    Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant)-kiingereza

8.    Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant) –kiswahili

9.    Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)

 

 

 

SOMA NA HIZI HAPA:

1.   Kilichokuwa nyuma ya pazia, ufugaji kuku wa kienyeji (kuku wa asili)

2.   Banda la kuku 100 wa kienyeji, vipimo, ramani, picha na jinsi ya kulijenga kwa ubora

3.   Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado-1

4.   Kuku ni utajiri: angalia mchanganuo jinsi kuku wa mayai wanavyoweza kukutajirisha haraka

5.   Biashara ndogo rahisi kwa wajasiriamali zinazoenda na wakati tulio nao

6.   kkjk

0 Response to "ETI KUKU WA KIENYEJI UKIWAPA CHANJO NYAMA YAKE HUPOTEZA LADHA TAMU YA ASILI?"

Post a Comment