Michael aishiye Kiluvya Mkoa
wa Pwani aliamua kufuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya mayai na nyama. Alijenga
banda zuri na imara kwa ajili ya malazi ya kuku pamoja na viota vya kutagia
mayai. Michael alichagua kutumia mfumo huria wa ufugaji wa kuku ambapo kuku
wangezurura mchana kutwa wakijitafutia wenyewe chakula na kurudi bandani jioni
kulala.
Alianza kutafuta matetea kwanza kwa kuulizia ulizia kwa wafugaji wengine
lakini ilikuwa vigumu sana kupata idadi ya kuku aliyokusudia kuanza nao. Yeye
alihitaji kuanza na matetea 12 na majogoo 2 lakini alipata matetea watano peke
yake.
Rafiki yake wa karibu ambaye
pia ni jirani na mfugaji mzuri wa kuku alimshauri kwa kumwambia, “Michael kwanini usizunguke masoko ya kuku wa
kienyeji ukachunguza wauzaji wenye matetea walio na umri mdogo ukaja kuwatenga
kwa muda?”
Michael aliafikiana na wazo
la jirani yake huyo akachukua hatua ya kuzunguka masoko mbalimbali wanakouza
kuku wa kienyeji, haikumchukua muda mrefu akawa ametimiza lengo lake la kuwa na
matetea 12 na majogoo 2
Kitu cha kwanza kufanya
aliwatenga kuku wote alionunua katika mazingira asiyokuwa na uhakika nayo kwani
wauzaji wengine wa kuku huuza kuku wao pale tu waonapo kuna dalili za mlipuko
wa magonjwa ya kuku mfano kideri nk. Hivyo kitendo cha kuwatenga kwa siku
kadhaa au hata wiki kinasaida kubaini ikiwa kama walikuwa na maambukizi ya
ugonjwa wowote na pia kuwalinda wale aliokuwa nao kabla wasiambukizwe.
Jirani aliendelea kumpa
ushauri kwamba ingelikuwa jambo la busara pia ikiwa angewanunulia kuku wake
chanjo muhimu za magojwa yasiyotibika mfano ugonjwa hatari wa kideri cha kuku,
gumboro na hata dawa za minyoo kwa kuwa kuku walikwisha fikisha miezi zaidi ya
3.
Wazo la chanjo kwa kuku
Michael hakulifurahia hata kidogo kwani alikuwa amewahi kusikia mara nyingi
kwamba kuwapatia kuku wa kienyeji madawa na chanjo si jambo zuri kwani hufanya
nyama yake baada ya kuchinjwa kupoteza kabisa ladha yake ya asili kama kuku wa
kienyeji. Badala yake aliamua kuwafuga tu hivyohivyo bila ya kuwapatia chanjo
wala dawa ya aina yeyote.
Kuku wa Michael waliendelea
tu vizuri licha ya kukataa ushauri wa
rafiki yake ambaye alikuwa na uzoefu na kazi hii kwa muda mrefu. Miezi miwili
baadae matetea walianza kutaga huku yale majogoo nayo yakawa yameshaanza kuwika
kwani yalikuwa na umri mkubwa kidogo kuliko matetea. Michael alitumia mfumo
huria wa ufugaji wa kuku ambapo kuku walizurura mchana kutwa wakijitafutia
wenyewe chakula na kuingia bandani jioni.
Aliwawekea viota vya kutagia
hivyo nyakati za mchana kuku matetea waliingia wenyewe katika viota na kutaga
mayai kisha walitoka na kuendelea kuchakuara kwenye ardhi ya maeneo ya karibu
na banda lao.
Alichowawekea jirani na
banda ni vyombo kwa ajili ya maji tu kwani hakukuwa na chanzo cha maji karibu
kuku wangeweza kunywa, lakini chakula hawakuwa na shida kabisa kwani walirudi
jioni firigisi zao zikiwa zimejaa tele.
Kuku hatimaye walianza
kuatamia na kila mmoja kwa wakati wake alitotoa vifaranga si chini ya kumi 10,
na jumla walikuwa vifaranga 110. Rafiki yake kama kawaida yake hakuchoka kumpa
ushauri na safari hii akampa mbinu ya kuwaweka vifaranga wote ndani ya banda
baada ya kuota manyoya kisha walishwe mle mpaka watakapoweza kujitafutia
chakula wenyewe na hatari ya kuliwa na wanyama au ndege kupungua.
Michael alifanya hivyo na
kweli wakapona kuku 100 alioendelea nao mpaka walipofikisha umri wa kutaga na
kuwika miezi 6. Wakati huohuo wale mama zao walikuwa wakiendelea kutaga ila safari
hii hakuwaruhusu tena kutamia kutokana na jukumu zito la kuwatunza vifaranga wa
mwanzo 100. Kwahiyo jumla alikuwa sasa na kuku 112 mchanganyiko wa matetea na
majogoo humohumo.
Malengo ya Michael yalikuwa
ni kufikisha kuku 500 kisha aanze kuwauza na kubakisha wachache kwa ajii ya
kuendeleza uzao. Kuku wakiwa bado wanaendelea kutaga, sasa walikuwa wakitaga
wote mama na watoto. Ghafla Michael alianza kuona dalili zisizokuwa za kawaida,
baadhi ya kuku walianza kusinzia na kupoteza nguvu. Hakukurupuka kwenda
kumwambia rafiki yake akajisemea tu, “Ah!
Ni hali tu ya kawaida, hawa ni kuku wa kienyeji bwana watapona tu wenyewe ”
Kuku walioanza kuugua hali
ilizidi kuwa mbaya, siku 3 mpaka wiki moja baadae walianza kufa mmoja mmoja
ndipo sasa ikamlazimu aombe ushauri kwa jirani yake. Jirani alimwambia ule ulikuwa
ni msimu wa mlipuko wa ugonjwa wa kideri na hakuna namna angeweza fanya zaidi
ya kuwapatia vitamin na antibiotics kupunguza magojwa nyemelezi lakini siyo
kuwatibu kabisa na hii ingesaidia tu kupunguza wingi wa vifo vya kuku.
Mpaka wimbi la ugojwa linatulia,
Michael alikuwa amebakiwa na matetea 12
tu, jogoo wote walikufa na hata hawa matetea 12 wengi wao bado walionekana
hawakuwa na nguvu mpaka wiki kadhaa baadae.
Kwa kifupi Bwana Michael
alikuwa ndio kwanza anaanza tena ufugaji na idadi ileile kama aliyoanza nayo
mwanzo isipokuwa sasa ilimbidi aingie tena mfukoni kwenda kutafuta majogoo 2.
Ilimuuma sana kuona kuu wake wakiteketea huku wa jirani yake japo walikuwa
wakicheza na kuchakura wote pamoja na wake shambani lakini hawakufa hata mmoja
kwasababu aliwahi kuwapatia chanjo.
Isingelikuwa tahadhari jirani
huyu aliyompatia Michael kipindi kile anaanza ufugaji, basi sasa hivi Michael angelikuwa
akimshika uchawi na pengine wasingekuwa wanaongea tena kwa kudhania labda
amemlogea kuku wake wakafa huku wakwake wakiendelea ‘kudunda’ kamakawaida.
Je,
kuna ukweli kiasi gani wa kuku kupoteza ladha yake ya asili kisa kuwapatia
chanjo?
Dhana hii kwa upande mmoja
ina ukweli lakini kuna namna unaweza kuepukana na tatizo hilo. Wataalamu wa
mifugo na siyo kuku tu peke yake wanashauri kwamba pindi unapompa mnyama dawa
ya aina yeyote basi usimchinje kipindi kifupi.
Dawa ama chochote kiingiacho
ndani ya mwili wa mnyama kina uwezekano wa kubadilisha ladha yake lakini ni kwa
muda tu, baada ya kipindi fulani kupita hali hiyo hutoweka na nyama hurudia
ladha yake ileile.
Ukiwapatia kuku wako chanjo
zingatia sana muda unaoshauriwa na wataalamu wa mifugo kuwachinja tangu siku
umewapa chanjo.
Umuhimu
wa chanjo kwa kuku wa kienyeji
Wengi tunadhani labda chanjo
ni kwa ajili ya kuku wa kisasa ama chotara tu peke yake lakini hii siyo sahihi.Sababu
kwamba kuku wa kienyeji ni wavumilivu sana kwa magonjwa haimaanishi kwamba
hawaugui hapana, Magonjwa yote yanayowasumbua kuku wa kisasa yanaweza pia
kuwapata wa kienyeji na wakafa au kupata madhara sema tu tofauti ipo kwenye
kiwango cha madhara kwani wa kienyeji madhara ni asilimia kidogo zaidi ya wenzao
wa kisasa.
Kwa mfano tuseme labda una
kuku 100 wa kienyeji ukilipuka ugonjwa wanaweza kufa 20 au 30 lakini ikiwa ni
wakisasa watakufa pengine 70 mpaka 90
Ufugaji wa kuku wa asili
huria una faida kubwa sana lakini wafugaji wengi hushindwa kuipata kutokana na
hatari zitokanazo na magojwa, wanyama na ndege walao kuku mfano vicheche, paka,
kunguru na hata mbwa.Kuna njia madhubuti za kuzuia hatari hizi zote mfugaji akiamua na tutazijadili siku
nyingine.
Kwa mtu anayepambana kupata
mtaji wa biashara ufugaji wa kuku wa kienyeji ni njia nzuri sana na rahisi ya
kukuza mtaji kwa ajili ya kufanyia biashara nyingine. Ukiweka malengo na
kuyapambania kuku wa kienyeji wanaweza wakakutoa. Kuku wako anatotoa vifaranga
10, kwanini mwshowe wapone wawili tu au mmoja? Hawapaswi kufa hata mmoja labda
tu iwe bahati mbaya mmoja au wawili.
.............................................
MSIMU
WA KUKU bado unaendelea na jana 27/06/2024 ndio ilikuwa siku ya mwisho ya
Semina yetu ya Mchanganuo wa kuku kuroiler wa nyama Darasa la awamu ya 3.
Siku
hii tulimalizia na Mpango wa fedha ambayo ilikuwa sura ndefu kuliko nyingine
zote na tulijitahidi sana kuhakikisha washiriki wanafahamu vyema namna ya
kukisia ripoti zote kama ile ya faida na hasara, cash flow, Mizania ya biashara
na Sehemu za biashara (ratio) kwa mwaka lakini miaka 3
Madarasa
ya semina hii yanaendelea na Siku ya Jumatatu tarehe 01/07/2024 tutaanza Darasa
la awamu ya 4. Hivyo ikiwa unahitaji lipia kitabu na Mchanganuo wako kwa ajili
ya rejea kupitia namba 0712202244 au 0765553030 kisha meseji, “NATAKA SEMINA YA KUROILER NA OFFA YA
MICHANGANUO 6”
Ukishalipia
nakutumia muda huohuo kila kitu na kukuunganisha na group la semina
Semina
hii lengo lake kuu ni kumfanya mjasiriamali awe na uwezo wa kufanya mchanganuo
wa biashara yeyote ile kwani imetengenezwa maalumu kwa ajili hiyo, vilevile
kumpa uelewa mpana wa miradi ya ufugaji kuku kibiashara zaidi.
Washiriki
wakimaliza semina huunganishwa group la Mentorship kwa mwaka mzima wakiendelea
kujifunza, kushare mambo mbalimbali na kuuliza maswali yeyote yahusuyo
ujasiriamali na biashara kwa ujumla.
Tumedhamiria
kutengeneza wataalamu (experts) wa mipango ya biashara.
OFFA YA VITU HIVYO 9 NI HII
HAPA CHINI;
1. Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)
2.
Mchanganuo Mpya:
Biashara ya ufugaji wa kuku chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)
3.
Mchanganuo wa kuku wa
nyama (Tumaini
Broilers)-kiingereza
4. Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili
5. Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora
Project)-kiswahili
6. Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada
watermelon)-kiswahili
7. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant)-kiingereza
8. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant) –kiswahili
9. Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)
SOMA
NA HIZI HAPA:
1.
Kilichokuwa nyuma ya pazia, ufugaji kuku wa kienyeji (kuku wa
asili)
2.
Banda la kuku 100 wa kienyeji, vipimo, ramani, picha na jinsi
ya kulijenga kwa ubora
3. Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado-1
4. Kuku ni utajiri: angalia
mchanganuo jinsi kuku wa mayai wanavyoweza kukutajirisha haraka
5. Biashara ndogo rahisi kwa wajasiriamali zinazoenda na wakati
tulio nao
6. kkjk
0 Response to "ETI KUKU WA KIENYEJI UKIWAPA CHANJO NYAMA YAKE HUPOTEZA LADHA TAMU YA ASILI?"
Post a Comment