HATARI YA KUKU WA KISASA KUSABABISHA KANSA NA WATOTO KUOTA MATITI KABLA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HATARI YA KUKU WA KISASA KUSABABISHA KANSA NA WATOTO KUOTA MATITI KABLA

Seli hatari za ugonjwa wa kansa

Minongono kwamba ulaji wa kuku wa kisasa kama vile broilers, chotara, layers na mayai yake kuna uhusiano mkubwa na ugonjwa wa kansa na tatizo la watoto wadogo kuota matiti (maziwa) kabla ya wakati wao imesikika kwa muda mrefu sasa.

Ni aina zote za ugonjwa wa kansa zinazohusishwa na kwa upande wa uotaji wa matiti inasemekana ni kwa jinsia zote mbili, hata watoto wa kiume nao pia wanatajwa kuonekana kuanza kuota matiti isivyo kawaida yao tena kabla hata ya balehe. Watoto wa kike huota matiti kabla ya kuvunja ungo wengine hata wakiwa chini ya miaka 8.

Baadhi ya Wanasayansi waliofanya uchunguzi kuhusiana na tatizo hili waligundua kwamba ni kweli nyama na mazao mengine ya nyama yana mchango mkubwa karika kusababisha ugonjwa wa kansa lakini wakadai siyo nyama ya kuku peke yake bali ni nyama aina zote kutoka na kwa wanyama wengineo wakiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe

Sababu kubwa ni kwanini ulaji wa nyama uhusike ni kwamba wanasayansi wanasema kichocheo kikubwa cha kansa ni ongezeko au limbikizo la aina fulani za homoni zinazopatikana kwa asili kutoka katika miili ya wanyama wote hai.

Homoni hizo zinatajwa kuwa ni Estrogen, Progesteron na Testosteron. Homoni ni vichocheo vinavyozalishwa na matezi ya mwili wa mnyama/binadamu ambavyo huhusika na ufanyajikazi mbalimbali wa tishu za mwili. Wataalamu pia wanaweza kuunda vichocheo hivyo maabara kwa ajili ya kazi mbalimbali kama vile za kimatibabu nk.

Pamoja na kwamba mwili wa binadamu nao kwa asili pia huzalisha homoni hizi lakini binadamu huyohuyo anapolimbikiza aina hizo za homoni hasa kutoka nje ya mwili wake kupitia vyakula anavyokula, dawa, au maji basi hapo ndipo tatizo linapoanzia.

Siyo nyama tu peke yake bali pia maziwa hasa yale yanayotokana na ng’ombe wenye mimba yalionekana kuwa na kiasi kikubwa cha Estrogen. Wamesema kwamba matumizi makubwa ya vyakula vilivyojaa estrogen hupelekea estrogen hiyo kwenda kujilimbkiza mwilini tofauti na ile yakwake ya asili na hatimaye kuwa kisababishi cha kansa.

Kwahiyo huwezi ukahitimisha moja kwa moja kwamba eti ulaji wa kuku wa kisasa unachochea ugonjwa wa kansa na watoto kuota matiti kwani hizi homoni zinazotuhumiwa hazipo tu kwenye nyama na mazao ya kuku peke yake bali na hata kwa aina nyingine za wanyama.

Isitoshe kutokana na ongezeko kubwa la watu na wanyama duniani sasa hivi mazingira yamejaa hizo homoni zilizotajwa hapo juu kiasi kwamba karibu kila chakula tunachokula tunakutana nazo, mpaka kwenye mazao ya mimea wanasema homoni hizi zipo.

Homoni hizi pia zimekuwa zikiingia kwenye mazingira na miili yetu kutokana na ongezeko la matibabu na dawa zenye asili ya homoni hizo mfano baadhi ya dawa za mpango wa uzazi nk.

Homoni hatari zaidi siyo zile zinazozalishwa kwa asili na miili ya wanyama na binadamu bali ni zile za kutengenezwa viwandani, lakini kwakuwa kuku hawapewi kabisa homoni za viwandani hakuna ushahidi kwamba kuku ndiyo chanzo cha ongezeko la kansa na watoto kuota matiti kabla ya wakati ingawa wanaweza kuwa wanachangia matatizo hayo kama ilivyokuwa kwa wanyama wengineo na sababu nyingine zilizotajwa pale juu.

...................................

Mpenzi msomaji, Huu ni MSIMU WA KUKU na makala hii ya leo ni ya pili katika mfululizo wetu, makala ya kwanza ilikuwa siku ya jana na ilisema hivi;

KWANINI KUKU WA KISASA & CHOTARA HUDUNGWA SINDANO ZA HOMONI NA DAWA ILI WAKUE HARAKA NA KUTAGA MAYAI MENGI?

Ndani ya Msimu pia tuna Darasa la semina inayohusu Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa Biashara ya kuku chotara 300 aina ya Kuroiler. Darasa la tatu linaanza siku ya Jumapili tarehe 23/06/2024 saa 2 jioni

Kujiunga na semina hii unatakiwa kulipia Kitabu cha rejea na mchanganuo huo kamili sh, elfu 10 kisha nakutumia na OFFA ya Michanganuo mingine mbalimbali 6. Ukipenda pia nakuunganisha na group letu (MASTERMIND GROUP) kwa ajili ya mentorship mwaka mzima.

Kulipia tumia namba, 0712202244 au 0765553030 Jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe usemao; “NATAKA SEMINA YA KUROILER NA OFFA YA VITU 9”

Nitakutumia kila kitu papo hapo na kukuunganisha na group la semina uanze masomo rasmi Jumapili.

OFFA ya vitu 9 ni hii hapa;

 

1.    Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)

2.    Mchanganuo Mpya: Biashara ya ufugaji wa kuku chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)

3.    Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-kiingereza

4.    Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili

5.    Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili

6.    Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili

7.    Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant)-kiingereza

8.    Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant) –kiswahili

9.    Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)

 

RATIBA YA SEMINA DARASA LA AWAMU YA 3

1. SEHEMU YA KWANZA 23/06/2024:

(Maandalizi)

2. SEHEMU YA PILI 24/06/2024

 (Muhtasari, Bidhaa & Biashara)

 

3. SEHEMU YA TATU 25/06/2024

(Soko, Mikakati & Utekelezaji)

 

4. SEHEMU YA NNE 26/06/2024

(Uendeshaji, Uongozi na Wafanyakazi)

 

5. SEHEMU YA TANO 27/06/2024

(Fedha & Viambatanisho)

 

Mtaalamu wa Michanganuo na Mjasiriamali;

Peter Augustino Tarimo

0712202244 / 0765553030

 

 

 


SOMA NA HIZI HAPA:

1.   Shilingi milioni 5 itatosha kufuga kuku wangapi wa mayai? naomba mchanganuo

2.   Sababu 4 kwanini kipengele cha fedha ni moyo wa mpango wa biashara (the heart of a business plan)

3.   Jinsi ya kutengeneza mvuto wa ajabu na kupendwa haraka na kila mtu, wapenzi, wateja, ndugu na hata jamaa

4.   Wanaofanikiwa maishani wengi husema ‘no’(hapana) kwa vitu hivi 3

5.   Mchanganuo wa biashara ya car wash, kuosha magari, mtaji na vifaa vinavyohitajika

0 Response to "HATARI YA KUKU WA KISASA KUSABABISHA KANSA NA WATOTO KUOTA MATITI KABLA"

Post a Comment