Minongono kwamba ulaji wa kuku wa kisasa kama vile
broilers, chotara, layers na mayai yake kuna uhusiano mkubwa na ugonjwa wa
kansa na tatizo la watoto wadogo kuota matiti (maziwa) kabla ya wakati wao
imesikika kwa muda mrefu sasa.
Ni aina zote za ugonjwa wa kansa zinazohusishwa na kwa
upande wa uotaji wa matiti inasemekana ni kwa jinsia zote mbili, hata watoto wa
kiume nao pia wanatajwa kuonekana kuanza kuota matiti isivyo kawaida yao tena
kabla hata ya balehe. Watoto wa kike huota matiti kabla ya kuvunja ungo wengine
hata wakiwa chini ya miaka 8.
Baadhi ya Wanasayansi waliofanya uchunguzi kuhusiana na tatizo
hili waligundua kwamba ni kweli nyama na mazao mengine ya nyama yana mchango
mkubwa karika kusababisha ugonjwa wa kansa lakini wakadai siyo nyama ya kuku
peke yake bali ni nyama aina zote kutoka na kwa wanyama wengineo wakiwemo ng’ombe,
mbuzi, kondoo na nguruwe
Sababu kubwa ni kwanini ulaji wa nyama uhusike ni kwamba
wanasayansi wanasema kichocheo kikubwa cha kansa ni ongezeko au limbikizo la
aina fulani za homoni zinazopatikana kwa asili kutoka katika miili ya wanyama
wote hai.
Homoni hizo zinatajwa kuwa ni Estrogen, Progesteron na
Testosteron. Homoni ni vichocheo vinavyozalishwa na matezi ya mwili wa
mnyama/binadamu ambavyo huhusika na ufanyajikazi mbalimbali wa tishu za mwili.
Wataalamu pia wanaweza kuunda vichocheo hivyo maabara kwa ajili ya kazi
mbalimbali kama vile za kimatibabu nk.
Pamoja na kwamba mwili wa binadamu nao kwa asili pia
huzalisha homoni hizi lakini binadamu huyohuyo anapolimbikiza aina hizo za
homoni hasa kutoka nje ya mwili wake kupitia vyakula anavyokula, dawa, au maji
basi hapo ndipo tatizo linapoanzia.
Siyo nyama tu peke yake bali pia maziwa hasa yale yanayotokana
na ng’ombe wenye mimba yalionekana kuwa na kiasi kikubwa cha Estrogen. Wamesema
kwamba matumizi makubwa ya vyakula vilivyojaa estrogen hupelekea estrogen hiyo
kwenda kujilimbkiza mwilini tofauti na ile yakwake ya asili na hatimaye kuwa
kisababishi cha kansa.
Kwahiyo huwezi ukahitimisha moja kwa moja kwamba eti
ulaji wa kuku wa kisasa unachochea ugonjwa wa kansa na watoto kuota matiti
kwani hizi homoni zinazotuhumiwa hazipo tu kwenye nyama na mazao ya kuku peke
yake bali na hata kwa aina nyingine za wanyama.
Isitoshe kutokana na ongezeko kubwa la watu na wanyama duniani
sasa hivi mazingira yamejaa hizo homoni zilizotajwa hapo juu kiasi kwamba karibu
kila chakula tunachokula tunakutana nazo, mpaka kwenye mazao ya mimea wanasema
homoni hizi zipo.
Homoni hizi pia zimekuwa zikiingia kwenye mazingira na
miili yetu kutokana na ongezeko la matibabu na dawa zenye asili ya homoni hizo
mfano baadhi ya dawa za mpango wa uzazi nk.
Homoni hatari zaidi siyo zile zinazozalishwa kwa asili na
miili ya wanyama na binadamu bali ni zile za kutengenezwa viwandani, lakini
kwakuwa kuku hawapewi kabisa homoni za viwandani hakuna ushahidi kwamba
kuku ndiyo chanzo cha ongezeko la kansa na watoto kuota matiti kabla ya wakati
ingawa wanaweza kuwa wanachangia matatizo hayo kama ilivyokuwa kwa wanyama
wengineo na sababu nyingine zilizotajwa pale juu.
...................................
Mpenzi msomaji, Huu ni MSIMU WA KUKU na makala hii ya leo ni ya pili katika mfululizo wetu,
makala ya kwanza ilikuwa siku ya jana na ilisema hivi;
Ndani ya Msimu pia tuna Darasa la semina inayohusu Jinsi
ya kuandika Mchanganuo wa Biashara ya kuku chotara 300 aina ya Kuroiler. Darasa
la tatu linaanza siku ya Jumapili tarehe 23/06/2024 saa 2 jioni
Kujiunga na semina hii unatakiwa kulipia Kitabu cha rejea
na mchanganuo huo kamili sh, elfu 10 kisha nakutumia na OFFA ya Michanganuo
mingine mbalimbali 6. Ukipenda pia nakuunganisha na group letu (MASTERMIND GROUP) kwa ajili ya
mentorship mwaka mzima.
Kulipia tumia namba, 0712202244 au 0765553030 Jina ni
Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe usemao; “NATAKA SEMINA YA KUROILER NA
OFFA YA VITU 9”
Nitakutumia kila kitu papo hapo na kukuunganisha na group
la semina uanze masomo rasmi Jumapili.
OFFA ya vitu 9 ni hii hapa;
1. Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)
2.
Mchanganuo Mpya:
Biashara ya ufugaji wa kuku chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)
3.
Mchanganuo wa kuku wa
nyama (Tumaini
Broilers)-kiingereza
4. Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili
5. Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora
Project)-kiswahili
6. Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada
watermelon)-kiswahili
7. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant)-kiingereza
8. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant) –kiswahili
9. Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)
RATIBA YA SEMINA DARASA LA
AWAMU YA 3
1.
SEHEMU YA KWANZA 23/06/2024:
(Maandalizi)
2.
SEHEMU YA PILI 24/06/2024
(Muhtasari, Bidhaa & Biashara)
3.
SEHEMU YA TATU 25/06/2024
(Soko, Mikakati &
Utekelezaji)
4.
SEHEMU YA NNE 26/06/2024
(Uendeshaji, Uongozi na
Wafanyakazi)
5.
SEHEMU YA TANO 27/06/2024
(Fedha & Viambatanisho)
Mtaalamu
wa Michanganuo na Mjasiriamali;
Peter
Augustino Tarimo
0712202244
/ 0765553030
SOMA
NA HIZI HAPA:
1.
Shilingi milioni 5 itatosha kufuga kuku wangapi wa mayai?
naomba mchanganuo
2.
Sababu 4 kwanini kipengele cha fedha ni moyo wa mpango wa
biashara (the heart of a business plan)
4.
Wanaofanikiwa maishani wengi husema ‘no’(hapana) kwa vitu hivi
3
5.
Mchanganuo wa biashara ya car wash, kuosha magari, mtaji na
vifaa vinavyohitajika
0 Response to "HATARI YA KUKU WA KISASA KUSABABISHA KANSA NA WATOTO KUOTA MATITI KABLA"
Post a Comment