IMANI ZINAVYOZUIA MAFANIKIO NA KUZIKA NDOTO ZA WATU WENGI DUNIANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

IMANI ZINAVYOZUIA MAFANIKIO NA KUZIKA NDOTO ZA WATU WENGI DUNIANI

Mtu mwenye imani

Tangu Kampeni ya maudhui ya kuku imeanza juzi hapa kwenye blog ya jifunzeujasiriamali, tumekuwa na masomo 2 na yote yalikuwa yakizungumzia matatizo makubwa 3 ambayo sekta ya ufugaji kuku wa kisasa na chotara Tanzania na hata Duniani kwa ujumla imekuwa ikikumbana nayo.

Matatizo hayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na IMANI POTOFU juu ya mambo mbalimbali yanayohusiana na kuku hawa wanaokua upesi na kutaga mayai mengi tofauti na kuku tuliozoea wa asili (kuku wa kienyeji).

Kwenye makala hizo mbili tulithibitisha kwa kutoa ushahidi wa upotofu wa dhana hizo 3 nitakazozitaja hapo chini. Watu wanaamini vitu hivi 3 kuhusiana na kuku wa kisasa;

                 1.      Kuku wa kisasa na chotara ni matokeo ya Wanasayansi na wataalamu wa vinasaba kubadilisha kuku wa kienyeji maabara (GMO)

                 2.      Chanzo cha kuku wa kisasa na chotara kukua upesi au kutaga mayai mengi ni matokeo ya kudungwa sindano au kulishwa dawa zenye homoni za kukuza maumbile.

                 3.      Nyama ya Kuku wa kisasa na mayai yake husababisha ugonjwa wa kansa na watoto wadogo kuota matiti kabla ya wakati wao sahihi (Wana balehe na kuvunja ungo mapema)

Lengo la somo hili la leo ni kueleza chanzo cha Imani hizi, kwanini watu huzing’ang’ania kiasi hicho, jinsi zinavyoiathiri sekta ya ufugaji wa kuku na uchumi wa watu kwa ujumla na pia ni kitu gani kifanyike ili jamii iondokane na imani hizi potofu.

Imani potofu juu ya kuku wa kisasa hazina tofauti na imani potofu nyingine juu ya masuala mbalimbali katika jamii.

Tuchukulie mfano imani za kishirikina, ni juzi tu Watanzania tumetoka kusikia kwa masikitiko makubwa kisa cha Mtoto albino kule Kagera aliyekatishwa uhai wake kisa Imani potofu za kishirikina. Imani siyo jambo baya kama tutakavyoenda kuona leo isipokuwa tu huwa mbaya pale zinapotumika katika mlengo hasi (Kiupotofu) kama hizi.

Kuna Imani za dini na madhehebu mbalimbali pia na zinapotumika katika njia iliyokuwa chanya zina matokeo mazuri ajabu lakini kinyume chake ndiyo tunasikia yale ya akina Kibwetere wa Uganda, Mchungaji Makenzio wa Shakahola kule Mombasa na hata kina Joseph Konyi wa Lords Resistance army, Bokoharam, Taliban na Dola la kiislamu kule Syria na Iraq.

Hebu jaribu ku ‘imagine’ ni roho ngapi za watu ambao mafanikio yao yalizuiwa na ndoto zao kuzikwa moja kwa moja shauri tu ya imani hizi potofu zilizochochewa na ‘wendawazimu’ wachache walioshindwa kuitumia vizuri kanuni mashuhuri tutakayokwenda kuisoma hivi punde.

Wakati tukifanya utafiti wa soko na biashara ya kuku chotara wa nyama tuligundua mambo ya kustaajabisha sana ambayo watu wanayo vichwani mwao juu ya kuku hawa, nitaeleza mambo hayo baadae kidogo hebu kwanza tuone Imani inachangia vipi matatizo hayo.

Katika somo letu hili nakuomba ndugu msomaji nikatumie maelezo katika Kitabu cha Napoleo Hill kiitwacho FIKIRI NA UTAJIRIKE kwa Kiswahili. Kitabu hiki katika lugha ya kiingereza kinaitwa THINK & GROW RICH. Maelezo hayo yapo ukurasa wa 75 - 106 katika Sura ya 3 (IMANI) ya kitabu toleo la Kiswahili ila toleo ‘version’ ya kiingereza nadhani ukurasa na sura vitakuwa tofauti.

Kwa mujibu wa kitabu hicho ukurasa wa 76;

IMANI ni hali ya akili ambayo inaweza ikaambukizwa au kutengenezwa kupitia kukiri au maelezo yanayojirudiarudia kwenye akili ya ndani kwa kutumia kanuni ya Kujishauri binafsi

Au katika

Uk. Wa 77

IMANI ni hali ya akili ambayo unaweza ukaijenga mwenyewe kupitia kurudiarudia kuiambia kwa dhati akili yako ya ndani. Ndiyo njia pekee inayojulikana ya kujenga hisia kubwa za IMANI kwa hiyari.

 

Imani hujengwa vipi?

Kanuni ya Kujishauri binafsi (Autosuggestion)

Kwenye kitabu mwandishi amezungumzia kanuni mashuhuri iitwayo Kujishauri binafsi ama Autosuggestion kwamba ndiyo inayotumika pale mtu anapotaka kujenga IMANI ya jambo lolote akilini mwake.

Kwa urahisi tu ni kwamba jinsi kanuni hii inavyofanya kazi hakuna tofauti na vile mtoto mdogo anavyojifunza mambo mbalimbali kutoka jamii inayomzunguka tangia utoto wake.

Mambo mbalimbali anayosikia na kuona mara kwa mara ndiyo baadae huja kuamini kwamba ndio ukweli wenyewe wa maisha hata kama kiuhalisia siyo kweli, na mfano mzuri sana ni haya maswala tunayojadili leo ya Imani potofu kuhusu kuku wa kisasa.

Kwa muda mrefu jamii imekaa katikati ya minongono hii bila ya mtu yeyote kukanusha wala kukataa jambo lililosababisha jamii kweli kuamini imani hizo ni za kweli.

Haishangazi kumkuta hata mwenye digrii ya udaktari akiamini dhana hizi, lakini ukimkuta kwenye shughuli kama ya harusi kwa mfano, udenda unamtoka anapokaribia kuchota kipaja cha kuku au kidari meza kuu ya chakula. Hakumbuki tena kama sherehe kubwa kama ya harusi yenye watu zaidi ya 500 isingeliwezekana kupata kuku wa kienyeji wote kwa gharama inayolipika.

Hata Manabii na Mitume wa siku hizi wengi huitumia sana tekiniki hii ya Autossugestion kuwajengea waumini wao Imani thabiti, utasikia wakisema; “Pokea...., Pokea, wewe.....”, Pokea gari, Pokea nyumba......” nk. Kurudiwarudiwa huko kwa maneno yaleyale kuna athari kubwa sana katika kumjengea muumini Imani akilini kwamba kweli ipo siku atamiliki gari ama nyumba.

Na muumini kweli ikiwa atakuwa na Imani thabiti jambo hilo inakuwa si vigumu kulitekeleza kwasababu kanuni inasema akili yake ya ndani itafanya kila linalowezekana mhusika apate njia za kutimiza hilo jambo/lengo.

Kupitia kanuni hii, Mtu unaweza kuwa mhalifu kwa kuishi miongoni mwa uhalifu.

Katika ukurasa wa 77 mwandishi ameandika maelezo yafuatayo aliyonukuu kutoka kwa mtaalamu mmoja wa uhalifu;

“Mara ya kwamza watu wanapokuwa karibu na maswala ya uhalifu huwa wanachukizwa nao, Ikiwa wataendelea kwa muda kuwa nao karibu, huuzowea na kuuvumilia. Ikiwa wataendelea kuushuhudia kwa kipindi kirefu zaidi, mwishowe huukumbatia kwa moyo na kushawishika nao.”

Mihemko / vichocheo vya akili

Katika kitabu cha THINK & GROW RICH pia tunajifunza jambo hili;

“Maelekezo yeyote akili itakayopewa yakiwa katika hali ya Imani au Itikadi, maelekezo hayo yatatekelezwa”  Uk. wa 79:

Imani, Upendo na Mapenzi (kujamiiana) ni vichocheo vya akili vyenye nguvu zaidi ya kushawishi akili ya mtu ya ndani na unapochanganya vichocheo hivi na jambo lolote lile akili yako ya ndani hulifikisha jambo hilo moja kwa moja mpaka kwa Nguvu Kuu Isiyokuwa na mipaka (MUNGU) sawa na ilivyokuwa suala la sala.

Hivyo kinachosababisha watu kung’ang’ania imani hizi kiasi hicho ni sababu kwamba tayari wameshajenga imani akilini kwamba hawa kuku wana athari katika afya zao, tayari tena hapo kuna kichocheo kingine cha suala la afya japo ni kidogo.

Tukichukua mfano wa Imani za kishirikina watu wana imani kwamba viungo vya binadamu vinaweza kuleta utajiri, tayari hapo licha ya kichocheo cha Imani lakini pia kuna kichocheo kingine cha pesa/utajiri ndio maana inakuwa vigumu kiasi hicho watu kuachana na hizi Imani potofu

Athari za Imani Potofu kwenye Sekta ya Kuku na Uchumi kwa ujumla

Pale mwanzoni kuna mahali niliahidi kwamba nitaelezea mambo ya ajabu niliyokutana nayo wakati nikifanya utafiti wa biashara na soko la kuku chotara aina ya Kuroiler.

Kusema ukweli ingawa imani hizi zimeshika mizizi sana lakini jambo la kutia moyo sana ni kwamba kadiri muda unavyozidi kwenda idadi ya wale wanaoamini mambo hayo inazidi kupungua.

Uthibitisho ni ongezeko kwa mara ya kwanza la idadi ya kuku wa kisasa Tanzania kuzidi idadi ya kuku wa kienyeji. Hotuba ya Waziri wa Kilimo 2021/2022 kati ya kuku jumla milioni 87.7, kuku  wa kisasa walikuwa milioni 47.34 wakati wale wa kienyeji ni milioni 40.36

Si hivyo tu mwamko wa ufugaji kuku wa kisasa na chotara unaendelea kuwa mkubwa mijini na vijijini huku walaji nao wakizidi kupuuza imani hizi. Pamoja na hayo hata hivyo kuna idadi ya watu ambao bado wameshikilia imani hizi kwa nguvu zote kiasi kwamba bado wanasababisha athari kubwa kijamii na kiuchumi.

Wakati wa utafiti wangu maeneo ya Moshi Kilimanjaro nilibaini kuwa asilimia kubwa ya wakaazi wake hawapendi wala kula kabisa mayai ya kuku chotara kutokana na Imani hizi kiasi kwamba ukitaka kufuga kuku chotara wa mayai basi usikubali mtu yeyote agundue kama kuku wako ni chotara.

Sikujua mara moja sababu ya wao kukataa mayai ya chotara ili-hali yale ya kuku wa kisasa wa kawaida hawana shida nayo. Maduka ya rejareja na wauza chipsi wakigundua unauza mayai ya chotara pia huonyesha upinzani fulani kuyakubali

Lakini chakutia moyo pia ni kwamba mayai ya chotara na yale ya kisasa hayana tofauti kubwa kimuoekano na mfugaji unaweza kudanganya ni ya kisasa na wasijue wakayanunua tu kama kawaida. Ni lazima kutakuwa na imani potofu fulani hapo iliyoenezwa juu ya mayai hayo ya kuku chotara.

Watu wanapenda sana biashara ya ufugaji wa kuku na wanavutiwa nayo mno kutokana na urahisi wake na muda mfupi wa kurudisha mtaji lakini Imani hizi zimekuwa kikwazo kikubwa kwa watu wengi kuweza kutimiza ndoto zao. Mtu anaanza kufuga lakini anakuambia, “mimi nafuga tu kuku wa kienyeji bwana siwezi kulisha watu madawa.”

Au “Nikifuga wa kisasa au chotara familia yangu haitaweza kuwala”. Wakati huohuo mtu huyo utakuta anakula chipsi mayai ya kisasa kama kawaida na akienda banda la chipsi jioni utamsikia akiulizia firigisi na kidari kama vipo utadhani wanauza kuku wa kienyeji.   

Ni nini kifanyie Basi?

Sekta nzima ya kuku inatakiwa kuamka, kila mdau kwenye sekta hii ajitahidi kutoa elimu kwa walaji juu ya kuachana na Imani hizi potofu. Sijawahi hata siku moja kusikia mdau yeyote akitoa elimu katika vyombo vya habari kukanusha imani hizi, hata na serikali pia inapaswa kusaidia juhudi hizo ili watu waachane nazo.

Mwisho kabisa ni sekta na jamii kwa ujumla kutumia mbinu zilezile za kujishauri binafsi (Autosuggestion) zilizotumika kujenga imani hizi miaka na miaka sasa kuzikomesha. Walaji wa kuku na Jamii kwa ujumla watakapokuwa wakipata ujumbe wa kukanusha imani hizo tena na tena kama ilivyokuwa kukanusha zile imani za kutajirika kwa viungo vya binadamu na mauaji ya vikongwe, itafika mahali akili za watu zitazoea na kuondokana kabisa na IMANI hizi mbaya au kupungua kwa kiasi kikubwa.

 

.....................................

DONDOO MUHIMU

·      MSIMU wa kuku unaendelea na hii ni makala yetu ya 3, fuatilia makala nyingine katika blog yako ya Jifunzeujasiriamali

·      SEMINA YA JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA KUKU CHOTARA KUROILER 300 leo tunaanza Darasa la awamu ya 3 usiku saa 2. Karibu ujiunge upate na OFFA ya vitu 9 kama uonavyo pale chini

·      Kujiunga na Semina Lipia Kitabu na Mchanganuo kwa ajili ya rejea, shilingi 10,000/= kupitia namba 0712202244 au 0765553030 Peter Augustino Tarimo. Kisha ujumbe; NATAKA SEMINA YA KUROILER NA OFFA YA VITU 6 Pamoja na OFFA zako nakutumia muda huohuo

·      Kupata kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE (THINK & GROW RICH) kwa lugha ya Kiswahili fungua hapa kwenye mtandao wa GETVALUE Kupitia link hiyo.

 

 

OFFA YA VITU 9 NI HII HAPA CHINI;

1.    Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)

2.    Mchanganuo Mpya: Biashara ya ufugaji wa kuku chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)

3.    Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-kiingereza

4.    Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili

5.    Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili

6.    Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili

7.    Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant)-kiingereza

8.    Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant) –kiswahili

9.    Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)

 

RATIBA YA SEMINA DARASA LA AWAMU YA 3

1. SEHEMU YA KWANZA 23/06/2024:

(Maandalizi)

2. SEHEMU YA PILI 24/06/2024

 (Muhtasari, Bidhaa & Biashara)

 

3. SEHEMU YA TATU 25/06/2024

(Soko, Mikakati & Utekelezaji)

 

4. SEHEMU YA NNE 26/06/2024

(Uendeshaji, Uongozi na Wafanyakazi)

 

5. SEHEMU YA TANO 27/06/2024

(Fedha & Viambatanisho)

 

Mtaalamu wa Michanganuo na Mjasiriamali;

Peter Augustino Tarimo

0712202244 / 0765553030

 

 

 

 

SOMA NA HIZI HAPA:

                 1.      Hivi unajua hatua za kuachana na umasikini zinafanana na zile za kuacha unga?

                 2.      Jinsi ya kutambua na kuacha fikra hasi ulizonazo juu ya pesa zinazokurudisha nyuma usifanikiwe.

                 3.      Maono yako ndiyo chanzo cha mabadiliko yako (your fantasies are the source of your changes)

                 4.      Jipatie vitabu-pdf, semina, masomo ya kipekee na michanganuo maarufu ya kuku aina zote

                 5.      Jinsi ya kuchora na kutumia chati & grafu kwenye mchanganuo wa biashara

0 Response to "IMANI ZINAVYOZUIA MAFANIKIO NA KUZIKA NDOTO ZA WATU WENGI DUNIANI"

Post a Comment