Tangu Kampeni ya maudhui ya kuku imeanza juzi hapa kwenye
blog ya jifunzeujasiriamali, tumekuwa na masomo 2 na yote yalikuwa
yakizungumzia matatizo makubwa 3 ambayo sekta ya ufugaji kuku wa kisasa na
chotara Tanzania na hata Duniani kwa ujumla imekuwa ikikumbana nayo.
Matatizo hayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na IMANI POTOFU juu ya mambo mbalimbali
yanayohusiana na kuku hawa wanaokua upesi na kutaga mayai mengi tofauti na kuku
tuliozoea wa asili (kuku wa kienyeji).
Kwenye makala hizo mbili tulithibitisha kwa kutoa
ushahidi wa upotofu wa dhana hizo 3 nitakazozitaja hapo chini. Watu wanaamini
vitu hivi 3 kuhusiana na kuku wa kisasa;
1.
Kuku wa kisasa na chotara ni matokeo ya
Wanasayansi na wataalamu wa vinasaba kubadilisha kuku wa kienyeji maabara (GMO)
2.
Chanzo cha kuku wa kisasa na chotara kukua
upesi au kutaga mayai mengi ni matokeo ya kudungwa sindano au kulishwa dawa
zenye homoni za kukuza maumbile.
3.
Nyama ya Kuku wa kisasa na mayai yake
husababisha ugonjwa wa kansa na watoto wadogo kuota matiti kabla ya wakati wao
sahihi (Wana balehe na kuvunja ungo mapema)
Lengo la somo hili la leo ni kueleza chanzo cha Imani
hizi, kwanini watu huzing’ang’ania kiasi hicho, jinsi zinavyoiathiri sekta ya
ufugaji wa kuku na uchumi wa watu kwa ujumla na pia ni kitu gani kifanyike ili
jamii iondokane na imani hizi potofu.
Imani potofu juu ya kuku wa kisasa hazina tofauti na
imani potofu nyingine juu ya masuala mbalimbali katika jamii.
Tuchukulie mfano imani za kishirikina, ni juzi tu
Watanzania tumetoka kusikia kwa masikitiko makubwa kisa cha Mtoto albino kule
Kagera aliyekatishwa uhai wake kisa Imani potofu za kishirikina. Imani siyo
jambo baya kama tutakavyoenda kuona leo isipokuwa tu huwa mbaya pale
zinapotumika katika mlengo hasi (Kiupotofu) kama hizi.
Kuna Imani za dini na madhehebu mbalimbali pia na
zinapotumika katika njia iliyokuwa chanya zina matokeo mazuri ajabu lakini
kinyume chake ndiyo tunasikia yale ya akina Kibwetere wa Uganda, Mchungaji
Makenzio wa Shakahola kule Mombasa na hata kina Joseph Konyi wa Lords
Resistance army, Bokoharam, Taliban na Dola la kiislamu kule Syria na Iraq.
Hebu jaribu ku ‘imagine’ ni roho ngapi za watu ambao
mafanikio yao yalizuiwa na ndoto zao kuzikwa moja kwa moja shauri tu ya imani
hizi potofu zilizochochewa na ‘wendawazimu’ wachache walioshindwa kuitumia
vizuri kanuni mashuhuri tutakayokwenda kuisoma hivi punde.
Wakati tukifanya utafiti wa soko na biashara ya kuku
chotara wa nyama tuligundua mambo ya kustaajabisha sana ambayo watu wanayo
vichwani mwao juu ya kuku hawa, nitaeleza mambo hayo baadae kidogo hebu kwanza
tuone Imani inachangia vipi matatizo hayo.
Katika somo letu hili nakuomba ndugu msomaji nikatumie
maelezo katika Kitabu cha Napoleo Hill kiitwacho FIKIRI NA UTAJIRIKE kwa
Kiswahili. Kitabu hiki katika lugha ya kiingereza kinaitwa THINK & GROW
RICH. Maelezo hayo yapo ukurasa wa 75 - 106 katika Sura ya 3 (IMANI) ya kitabu toleo
la Kiswahili ila toleo ‘version’ ya kiingereza nadhani ukurasa na sura vitakuwa
tofauti.
Kwa mujibu wa kitabu hicho ukurasa wa 76;
IMANI
ni hali ya akili
ambayo inaweza ikaambukizwa au kutengenezwa kupitia kukiri au maelezo
yanayojirudiarudia kwenye akili ya ndani kwa kutumia kanuni ya Kujishauri binafsi
Au katika
Uk. Wa 77
IMANI ni hali ya akili ambayo unaweza ukaijenga mwenyewe
kupitia kurudiarudia kuiambia kwa dhati akili yako ya ndani. Ndiyo njia pekee
inayojulikana ya kujenga hisia kubwa za IMANI kwa hiyari.
Imani
hujengwa vipi?
Kanuni
ya Kujishauri binafsi (Autosuggestion)
Kwenye kitabu mwandishi amezungumzia kanuni mashuhuri
iitwayo Kujishauri binafsi ama Autosuggestion kwamba ndiyo inayotumika
pale mtu anapotaka kujenga IMANI ya jambo lolote akilini mwake.
Kwa urahisi tu ni kwamba jinsi kanuni hii inavyofanya
kazi hakuna tofauti na vile mtoto mdogo anavyojifunza mambo mbalimbali kutoka
jamii inayomzunguka tangia utoto wake.
Mambo mbalimbali anayosikia na kuona mara kwa mara ndiyo
baadae huja kuamini kwamba ndio ukweli wenyewe wa maisha hata kama kiuhalisia
siyo kweli, na mfano mzuri sana ni haya maswala tunayojadili leo ya Imani potofu
kuhusu kuku wa kisasa.
Kwa muda mrefu jamii imekaa katikati ya minongono hii
bila ya mtu yeyote kukanusha wala kukataa jambo lililosababisha jamii kweli
kuamini imani hizo ni za kweli.
Haishangazi kumkuta hata mwenye digrii ya udaktari
akiamini dhana hizi, lakini ukimkuta kwenye shughuli kama ya harusi kwa mfano,
udenda unamtoka anapokaribia kuchota kipaja cha kuku au kidari meza kuu ya
chakula. Hakumbuki tena kama sherehe kubwa kama ya harusi yenye watu zaidi ya
500 isingeliwezekana kupata kuku wa kienyeji wote kwa gharama inayolipika.
Hata Manabii na Mitume wa siku hizi wengi huitumia sana
tekiniki hii ya Autossugestion kuwajengea waumini wao Imani thabiti, utasikia
wakisema; “Pokea...., Pokea, wewe.....”,
Pokea gari, Pokea nyumba......” nk.
Kurudiwarudiwa huko kwa maneno yaleyale kuna athari kubwa sana katika kumjengea
muumini Imani akilini kwamba kweli ipo siku atamiliki gari ama nyumba.
Na muumini kweli ikiwa atakuwa na Imani thabiti jambo
hilo inakuwa si vigumu kulitekeleza kwasababu kanuni inasema akili yake ya
ndani itafanya kila linalowezekana mhusika apate njia za kutimiza hilo jambo/lengo.
Kupitia
kanuni hii, Mtu unaweza kuwa mhalifu kwa kuishi miongoni mwa uhalifu.
Katika ukurasa wa 77 mwandishi ameandika maelezo
yafuatayo aliyonukuu kutoka kwa mtaalamu mmoja wa uhalifu;
“Mara ya kwamza watu wanapokuwa karibu
na maswala ya uhalifu huwa wanachukizwa nao, Ikiwa wataendelea kwa muda kuwa
nao karibu, huuzowea na kuuvumilia. Ikiwa wataendelea kuushuhudia kwa kipindi
kirefu zaidi, mwishowe huukumbatia kwa moyo na kushawishika nao.”
Mihemko / vichocheo vya akili
Katika kitabu cha THINK & GROW RICH pia tunajifunza
jambo hili;
“Maelekezo yeyote akili itakayopewa yakiwa katika
hali ya Imani au Itikadi, maelekezo hayo yatatekelezwa” Uk.
wa 79:
Imani,
Upendo na Mapenzi (kujamiiana) ni vichocheo vya akili
vyenye nguvu zaidi ya kushawishi akili ya mtu ya ndani na unapochanganya
vichocheo hivi na jambo lolote lile akili yako ya ndani hulifikisha jambo hilo
moja kwa moja mpaka kwa Nguvu Kuu Isiyokuwa na mipaka (MUNGU) sawa na ilivyokuwa suala la sala.
Hivyo kinachosababisha watu kung’ang’ania imani hizi
kiasi hicho ni sababu kwamba tayari wameshajenga imani akilini kwamba hawa kuku
wana athari katika afya zao, tayari tena hapo kuna kichocheo kingine cha suala
la afya japo ni kidogo.
Tukichukua mfano wa Imani za kishirikina watu wana imani
kwamba viungo vya binadamu vinaweza kuleta utajiri, tayari hapo licha ya
kichocheo cha Imani lakini pia kuna kichocheo kingine cha pesa/utajiri ndio
maana inakuwa vigumu kiasi hicho watu kuachana na hizi Imani potofu
Athari
za Imani Potofu kwenye Sekta ya Kuku na Uchumi kwa ujumla
Pale mwanzoni kuna mahali niliahidi kwamba nitaelezea
mambo ya ajabu niliyokutana nayo wakati nikifanya utafiti wa biashara na soko
la kuku chotara aina ya Kuroiler.
Kusema ukweli ingawa imani hizi zimeshika mizizi sana
lakini jambo la kutia moyo sana ni kwamba kadiri muda unavyozidi kwenda idadi
ya wale wanaoamini mambo hayo inazidi kupungua.
Uthibitisho ni ongezeko kwa
mara ya kwanza la idadi ya kuku wa kisasa Tanzania kuzidi idadi ya kuku wa
kienyeji. Hotuba ya Waziri wa Kilimo 2021/2022 kati ya kuku jumla milioni 87.7,
kuku wa kisasa walikuwa milioni 47.34
wakati wale wa kienyeji ni milioni 40.36
Si hivyo tu mwamko wa
ufugaji kuku wa kisasa na chotara unaendelea kuwa mkubwa mijini na vijijini
huku walaji nao wakizidi kupuuza imani hizi. Pamoja na hayo hata hivyo kuna
idadi ya watu ambao bado wameshikilia imani hizi kwa nguvu zote kiasi kwamba
bado wanasababisha athari kubwa kijamii na kiuchumi.
Wakati wa utafiti wangu
maeneo ya Moshi Kilimanjaro nilibaini kuwa asilimia kubwa ya wakaazi wake
hawapendi wala kula kabisa mayai ya kuku chotara kutokana na Imani hizi kiasi
kwamba ukitaka kufuga kuku chotara wa mayai basi usikubali mtu yeyote agundue
kama kuku wako ni chotara.
Sikujua mara moja sababu ya
wao kukataa mayai ya chotara ili-hali yale ya kuku wa kisasa wa kawaida hawana
shida nayo. Maduka ya rejareja na wauza chipsi wakigundua unauza mayai ya
chotara pia huonyesha upinzani fulani kuyakubali
Lakini chakutia moyo pia ni
kwamba mayai ya chotara na yale ya kisasa hayana tofauti kubwa kimuoekano na
mfugaji unaweza kudanganya ni ya kisasa na wasijue wakayanunua tu kama kawaida.
Ni lazima kutakuwa na imani potofu fulani hapo iliyoenezwa juu ya mayai hayo ya
kuku chotara.
Watu wanapenda sana biashara
ya ufugaji wa kuku na wanavutiwa nayo mno kutokana na urahisi wake na muda
mfupi wa kurudisha mtaji lakini Imani hizi zimekuwa kikwazo kikubwa kwa watu
wengi kuweza kutimiza ndoto zao. Mtu anaanza kufuga lakini anakuambia, “mimi nafuga tu kuku wa kienyeji bwana siwezi
kulisha watu madawa.”
Au “Nikifuga wa kisasa au chotara familia yangu haitaweza kuwala”.
Wakati huohuo mtu huyo utakuta anakula chipsi mayai ya kisasa kama kawaida na
akienda banda la chipsi jioni utamsikia akiulizia firigisi na kidari kama vipo
utadhani wanauza kuku wa kienyeji.
Ni
nini kifanyie Basi?
Sekta nzima ya kuku inatakiwa kuamka, kila mdau kwenye
sekta hii ajitahidi kutoa elimu kwa walaji juu ya kuachana na Imani hizi potofu.
Sijawahi hata siku moja kusikia mdau yeyote akitoa elimu katika vyombo vya
habari kukanusha imani hizi, hata na serikali pia inapaswa kusaidia juhudi hizo
ili watu waachane nazo.
Mwisho kabisa ni sekta na jamii kwa ujumla kutumia mbinu
zilezile za kujishauri binafsi (Autosuggestion) zilizotumika kujenga imani hizi
miaka na miaka sasa kuzikomesha. Walaji wa kuku na Jamii kwa ujumla
watakapokuwa wakipata ujumbe wa kukanusha imani hizo tena na tena kama
ilivyokuwa kukanusha zile imani za kutajirika kwa viungo vya binadamu na mauaji
ya vikongwe, itafika mahali akili za watu zitazoea na kuondokana kabisa na
IMANI hizi mbaya au kupungua kwa kiasi kikubwa.
.....................................
DONDOO
MUHIMU
· MSIMU wa kuku
unaendelea na hii ni makala yetu ya 3, fuatilia makala nyingine katika blog
yako ya Jifunzeujasiriamali
· SEMINA YA JINSI YA
KUANDIKA MCHANGANUO WA KUKU CHOTARA KUROILER 300 leo tunaanza Darasa la awamu
ya 3 usiku saa 2. Karibu ujiunge upate na OFFA ya vitu 9 kama uonavyo pale
chini
· Kujiunga na Semina
Lipia Kitabu na Mchanganuo kwa ajili ya rejea, shilingi 10,000/= kupitia namba
0712202244 au 0765553030 Peter Augustino Tarimo. Kisha ujumbe; “NATAKA
SEMINA YA KUROILER NA OFFA YA VITU 6” Pamoja na OFFA zako nakutumia
muda huohuo
· Kupata kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE (THINK &
GROW RICH) kwa lugha ya Kiswahili fungua hapa kwenye mtandao wa GETVALUE Kupitia link hiyo.
OFFA
YA VITU 9 NI HII HAPA CHINI;
1. Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)
2.
Mchanganuo Mpya:
Biashara ya ufugaji wa kuku chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)
3.
Mchanganuo wa kuku wa
nyama (Tumaini
Broilers)-kiingereza
4. Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili
5. Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora
Project)-kiswahili
6. Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada
watermelon)-kiswahili
7. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant)-kiingereza
8. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant) –kiswahili
9. Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)
RATIBA YA SEMINA DARASA LA
AWAMU YA 3
1.
SEHEMU YA KWANZA 23/06/2024:
(Maandalizi)
2.
SEHEMU YA PILI 24/06/2024
(Muhtasari, Bidhaa & Biashara)
3.
SEHEMU YA TATU 25/06/2024
(Soko, Mikakati &
Utekelezaji)
4.
SEHEMU YA NNE 26/06/2024
(Uendeshaji, Uongozi na
Wafanyakazi)
5.
SEHEMU YA TANO 27/06/2024
(Fedha & Viambatanisho)
Mtaalamu
wa Michanganuo na Mjasiriamali;
Peter
Augustino Tarimo
0712202244
/ 0765553030
SOMA
NA HIZI HAPA:
1.
Hivi unajua hatua za kuachana na umasikini
zinafanana na zile za kuacha unga?
2.
Jinsi ya kutambua na kuacha fikra hasi
ulizonazo juu ya pesa zinazokurudisha nyuma usifanikiwe.
3.
Maono yako ndiyo chanzo cha mabadiliko yako
(your fantasies are the source of your changes)
4.
Jipatie vitabu-pdf, semina, masomo ya kipekee
na michanganuo maarufu ya kuku aina zote
5.
Jinsi ya kuchora na kutumia chati & grafu
kwenye mchanganuo wa biashara
0 Response to "IMANI ZINAVYOZUIA MAFANIKIO NA KUZIKA NDOTO ZA WATU WENGI DUNIANI"
Post a Comment