Kawenye mfululizo wa makala za MSIMU WA KUKU leo tutajibu
swali la msomaji wetu mmoja aliyeuliza hivi;
Habari
mtaalam, Naitwa Amos...nipo Njombe.
Nimesoma
makala zenu za msimu wa kuku zimenivutia, lakini kuna kitu bado kinanichanganya
sijakielewa vizuri.
Mnadai
kuku huwa hawapewi kabisa madawa ya kuwakuza haraka wala kuwafanya watage mayai
mengi, lakini nimewahi kusoma sehemu nyingi nikaona kuku hupewa dawa na vitu
vingi sana mbali na chakula na antibiotics za kutibu magojwa, miongoni mwa hivyo
vitu nitavitaja hapa;
(1) Premix
(2) Egg
Booster
(3) Coccidiostat
(4) Vitalyt
(5) DCP
(6) Threonine
(7) Lysine
(8) Methionine
(9) Mycotoxin
binder
Naomba
unifafanulie vizuri ikiwa kama hizo zote siyo madawa yenyewe na Homoni za
kuboost kuku wakue upesi ni kitu gani?
Amos
MAJIBU:
Asante sana ndugu Amosi kwa swali lako;
Ni kweli katika tasnia ya ufugaji wa kuku hasa kuku wale
wa kisasa wakiwemo, kuku wa nyama broile, kuku wa mayai layers na hata kuku
chotara kama kuroiler, Sasso na wengineo kuna dawa na virutubishi mbalimbali (Additives)
vinavyoongezwa katika chakula chao ili waweze kuwa na afya njema.
Vitu hivyo ama Additives
ni tofauti kabisa na homoni za ukuaji (growth hormones) zinazopigiwa kelele sana na watu kote
duniani, vimeidhinishwa na mashirika mbalimbali yanayoshugulika na afya duniani
yakiwemo yale ya Umoja wa Mataifa yenyewe.
Vitu vyote ulivyovitaja hapo juu na vingine ambavyo
hukuvitaja lakini vinatumiwa na wafugaji wa kuku tunaweza kuviweka katika
makundi makuu 4 kama ifuatavyo;
(1) Vitamini
(2) Madini
(3) Amino
acids (Protini)
(4) Dawa
na Chanjo
Vitu hivi havina sthari
yeyote ile mbaya kwa kuku wenyewe wala kwa binadamu wanaokula kuku ikiwa tu
vitatumika kama ilivyopendekezwa na wataalamu wa mifugo. Hata ikiwa hautawapa
kabisa kuku wako vitu hivi, kuku hao watavipata kwenyo mlo wa kawaida wanaokula
kila siku na endapo watavikosa basi matokeo yake hudumaa au kupatwa na magonjwa
mbalimbali.
Kwahiyo vyote ni virutubisho
vinavyopatikana kwenye udongo au kwenye mimea wakati kuku akijitafutia chakula
chake kiasili kwa kuchakurachakura mchangani. Wataalamu wamevitengeneza
makusudi kutokana na kuku wa kisasa kuwa hawana uwezo wa kujitafutia vyakula
wenyewe na hata wangeweza haiwezekani kutokana na kuku hao kufugwa idadi kubwa
mno ya kuku kibiashara
Hapa chini nitaelezea kimoja
kimoja baada ya kuvipanga kwenye makundi yake kwenye jdwali;
VITAMINI |
Premix,
Egg Booster, Vitalyt, nk. |
MADINI |
DCP,
Chokaa nk, |
PROTINI |
Threonine, Lysine, Methionine,
Tryptophan nk.
|
DAWA & CHANJO |
Mycotoxin binder,
Antibiotics, Coccidiostat nk.
|
Premix,
Hili ni neno na lina
maanisha kitu kinachoongezewa baada ya kingine. Ni mchanganyiko wa Vitamini za
aina mbalimbali na madini kwa ajili ya kuongeza kwenye chakula cha kuku. Zipo
za aina tofauti kulingana na umri wa kuku au kundi mfano wanaotaga, vifaranga,
wa nyama nk.
Egg
Booster
Kama ilivyokuwa kwa premix
hapo juu hii nayo ni mchanganyiko wa vitamin mbalimbali na madini kwa ajili ya
kuku wanaotaga, Neno Booster lisikutishe, madini na vitamin husaidia mwili
kutengeneza protini za kukuza mwili
Vitalyt
Pia nayo ni mchanganyiko wa
Vitamini kwa ajili ya mifugo
DCP
Kirefu chake ni Dicalcium Phosphate: Huu ni mchanganyiko
wa madini ya Calciun na Phosphate kwa ajili ya kuimarisha mifupa ya kuku
Chokaa
Nayo pia ni madini na
hupatikana hata kwenye mifupa ya wanyama, viumbe wa bahari, konokono nk.
Threonine,
Lysine, Methionine, Tryptophan
Hizi ni amino acids au Protini ambazo hupatikana kwenye
vyakula mbalimbali na hata binadamu pia tunazihitaji sana kwa ajili ya ufanyaji
kazi mzuri wa tishu na seli za mwili. Hazina madhara yeyote kwani hata
usipowawekea kuku kwenye chakula watazipata wenyewe kwenye kile watakachokula,
wakikosa kabisa watadhoofika na kuugua.
Coccidiostat,
Mycotoxin binder, Antibiotics nk.
Hili ni kundi la dawa, ka mfano hii Coccidiostat
huongezwa kwenye chakula cha kuku kuzuia ugonjwa wa coccidiosis unaosababishwa
na protozoa.
Mycotoxin
binder ni kiua sumu pia kinachozuia sumusumu zinazotokana na
chakula
Kwenye vyakula vya kuku zinaweza zikaongezwa additives nyingine zozote zile ilimradi
tu zimeidhinishwa na mamlaka zinazosimamia mifugo au serikali.
Antbiotics: Kwa
upande wa antibiotiki au madawa ya kutibu magojwa ya bacteria ndio penye tatizo
kubwa kushinda hata dhana nyingine zote watu wanazohofia.
Matumizi ya dawa hizi hayakatazwi kwa kuku wanaoumwa
lakini tatizo kubwa lipo kwa wafugaji hasa wale wakubwa na hata wadogo,
wanapoamua kuzitumia dawa hizi kama kinga ya magonjwa hayo au kuzitumia
kiholela pasipo kuzingatia kwamba dawa hizihizi zina asili moja na zile
tunazotumia wenyewe binadamu.
Matokeo ya matumizi hayo holela husababisha usugu mkubwa
wa dawa hizo kwa walaji wa kuku waliozoeshwa hayo madawa. Hili ni tatizo kubwa
linalosumbua siyo Tanzania tu bali dunia nzima.
...............................................
Mpenzi msomaji wa makala hii, Katika MSIMU WETU WA KUKU,
hii ni makala ya 5 katika mfululizo wa maudhui yanayohusiana na kuku. Unaweza
kujisomea makala nyingine 4 chini ya makala hii.
Leo pia ni siku ya 3 ya Semia ya kuandika Mchanganuo wa
kuku Kuroiler wa nyama likiwa ni Darasa la awamu ya 3. Katika siku hii
tunakwenda kujifunza vipengele vya; SOKO, MIKAKATI & UTEKELEZAJI
Unaweza kujiunga na semina hata ikiwa umechelewa kwani
tuna utaratibu wa kuwafundisha wale wote waliochelewa kabla ya muda rasmi wa
darasa. Darasa huanza rasmi saa 3 kamili usiku
Kujiunga na Semina hii, lipia shilingi 10,000/= kupitia
namba zetu 0712202244 au 0765553030 Peter Augustino Tarimo, kwa ajili ya kupata
Kitabu na Mchanganuo kamili wa kuku 300 wa kuroiler. Vitu hivi ni muhimu kwa
ajili ya kufanya rejea.
Ukishalipia tuma ujumbe; “NATAKA SEMINA YA KUROILER NA OFFA
YA VITU 9”
Baada ya hapo nakutumia papo hapo Kitabu, mchanganuo wako
wa kuroiler pamoja na OFFA ya michanganuo mingine 6 jumla vinakuwa vitu 9
OFFA
HIYO NI HII HAPA CHINI;
1.
Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA
NA UJASIRIAMALI (Page 430)
2. Mchanganuo Mpya: Biashara ya ufugaji wa kuku
chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)
3. Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-kiingereza
4.
Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili
5.
Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili
6.
Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili
7.
Mchanganuo wa Mgahawa wa
chakula (Jane Restaurant)-kiingereza
8.
Mchanganuo wa Mgahawa wa
chakula (Jane Restaurant) –kiswahili
9.
Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)
SOMA
NA HIZI HAPA:
2.
Njia mpya za kufanya mambo: dunia,
biashara, ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu
5.
Muongozo kamili wa jinsi ya kufuga kuku wa nyama (broilers)
kitaalamu - semina siku-3
0 Response to "KWANI HIZI SIYO DAWA ZA KUKUZA KUKU HARAKA? PREMIX, LYSEN, BOOSTER, COCCIDIOSTAT NA DCP"
Post a Comment