KWANINI KUKU WA KISASA & CHOTARA HUDUNGWA SINDANO ZA HOMONI NA DAWA ILI WAKUE HARAKA NA KUTAGA MAYAI MENGI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KWANINI KUKU WA KISASA & CHOTARA HUDUNGWA SINDANO ZA HOMONI NA DAWA ILI WAKUE HARAKA NA KUTAGA MAYAI MENGI?

Kuku akichomwa sindano ya chanjo na mtaalamu wa mifugo
Ndugu Msomaji wetu karibu sana MSIMU WETU WA KUKU, kupata makala na taarifa za kina kuhusiana na biashara ya ufugaji wa kuku kibiashara. Makala ya leo ni miongoni mwa nyingi tutakazokuletea; Karibu tusome hadi mwisho

Upo wasiwasi mkubwa unaosambaa miongoni mwa watu kote duniani juu ya kuku hawa wa kisasa kwa upande wa nyama (Broilers), kuku wa mayai (Layers) na hata kuku chotata (Hybrid) mfano kuroiler na sasso.

Kwamba ukuaji wake wa haraka na utagaji wa mayai mengi kuliko kuku wa kienyeji waliozoeleka ni matokeo ya wanasayansi na wahandisi wa vinasaba (Genetic engineers) kutengeneza homoni na virutubishi ambavyo kuku hao hudungwa au kuwekewa kwenye chakula na maji ya kunywa.

Unajua siyo kila mtu anayekula mazao ya kuku amewahi kufuga kuku au hata tu kujua ‘ABC’ za kuku, wanakula kitu gani, wanafugwa vipi au ni mchakato upi wafugaji hupitia mpaka kuku anachinjwa au yai linafika mezani.

Hivyo ni rahisi sana wasiwasi kama huo kuwepo na kusambaa Dunia nzima hata na zile nchi zilizoendelea kama Marekani, Uingereza na China. Mfano utafiti mmoja uliofanyika kule nchini Marekani ulionyesha kwamba asilimia 77% ya Wamarekani wa kawaida wana imani hii kwamba wafugaji wa kuku hutumia dawa au homoni za kukuza kuku haraka.

Swali kubwa ni kwamba, Je hawa kuku ni kwanini wakue haraka kiasi hiki au kutaga mayai mengi vile tofauti na ilivyo kwa kuku wa asili (kuku wa kienyeji)? Kuna tekiniki gani imetumika wataalamu wanaweza kututhibitishia haina madhara kwa afya na mustakabali wetu kinasaba?

Kwa mfano kuku wa kisasa miaka ya 70s alikuwa na uzito karibu nusu ya kuku wa kisasa wa miaka hii ya 2000 na kwa kadri miaka inavyozidi kwenda wataalamu hao wanazidi kubuni kuku wenye maumbie makubwa zaidi,wanaokua kwa muda mfupi zaidi, wanaotaga mayai mengi zaidi, wasiougua kabisa baadhi ya magojwa na hata wasiokuwa na manyoya kabisa

Je, Ni kweli kuku hudungwa sindao za homoni au kupewa dawa za kusaidia wakue haraka?

Siyo kweli kwamba kuku wa kisasa au hata wale chotara hupewa dawa na homoni zozote za kuwafanya wakue haraka ndani ya muda mfupi, bali kinachosababisha hawa kuku kuwa na tabia tofauti na kuku wa kienyeji kama kukua upesi na kutaga sana mayai ni uchaguzi wa muda mrefu wa mbegu bora ya kuku wazazi walio na tabia hizo nzuri.

Mbegu bora inayotoa matokeo mazuri ukichanganya na sababu nyinginezo kama vile ulishaji chakula chenye virutubisho sahihi pamoja na kupatiwa mazingira muafaka mfano joto na hali ya hewa inayofaa vimewezesha kuku kukua nusu ya muda wake wa asili na utagaji mayai kufikia karibu mara 5 zaidi ya utagaji wa kuku wa asili (kienyeji).

Kimsingi Dunia nzima imepiga marufuku kabisa matumizi ya dawa za homoni zinazohusika na ukuaji wa wanyama haraka hasa kwa upande wa kuku. Na hata kusingelikuwa na marufuku hiyo kuzitumia kusingeliwezekana kwa sababu za kiuchumi kwani homoni ni gharama kubwa mno kuliko faida kifedha ambayo mfugaji angeipata.

Kwanza ni lazima zichomwe kupitia njia ya sindano kila siku kama uonavyo wenye tatizo la sukari wanavyochoma insulini, maana kutumia homoni kwa njia ya mdomo haiwezi kufanya kazi kwani ikifika tumboni huyeyushwa na kupoteza maana yake kabisa, isingeliweza kufanya kazi iliyokusudiwa.

Sasa hebu fikiria ikiwa utaamua kuwachoma homoni kuku wako kila siku ili wakue harakaharaka na una kuku tuseme labda 300 tu, niambie ni shughuli pevu kiasi gani ungelikuwa nayo sembuse kwa wenye mashamba ya kuku 2,000 huko mpaka 10,000? hivyo ni jambo lisilowezekana hata kidogo kutumia homoni za kukuza kuku upesi.

Kuna ukweli Kuku wa Kisasa wametengenezwa Maabara kijenetiki?

Hili jambo nalo limesababisha mkanganyiko mkubwa dunia nzima. Kuna dhana kwamba Wataalamu kwa kutumia uhandisi wa vinasaba (Genetic engineering) wamehusika katika kutengeneza mbegu ya kuku wa kisasa na chotara maabara.

Huu nao ni upotofu mkubwa na hakuna kitu kama hicho kilichofanyika bali ni uchaguzi wa kizazi cha kuku waliokuwa na sifa zinazohitajika, kuku hao majogoo kwa matetea wanapoachwa wapandane hutotoa vifaranga ambao watakuwa na sifa mchanganyio za wazazi wao na kwa kuwa wazazi wote 2 walikuwa na sifa mfano ya kukua haraka basi uzao wao wa kwanza watakua haraka mara dufu ya wazazi.

Wataalamu kwa kuchanganya mbegu za aina mbalimbali (kucross breed) zilizo na sifa wanazozihitaji hatimaye hukuta wamepata aina fulani ya wazazi ambao uzao wao wa kwanza unakuwa na sifa za hali ya juu waliyoihitaji mfano kutaga mayai mengi nk. Kwa jina jingine huitwa Selective Breeding

Hivyo watatunza kizazi hicho bila ya kukichanganya na kingine tena kwa ajili ya kupata mayai tu ya kutotolesha vifaranga wenye hiyo sifa teule. Na wanakuwa na mpaka hakimiliki ya ugunduzi wao kwasababu hapo kabla hakukuwa na mtu mwingine aliyejua wala kuchanganya aina hizo za kuku kupata hiyo aina teule waliyoipata wao. Hivyo huwezi ukasema eti kuchagua mbegu bora ya mnyama au mmeai basi mazao yake yanaweza yakaleta madhara kwa binadamu, si kweli.

 

Selective Breeding hii hata sisi binadamu huwa tunafanya japo wengi hatujui, pale mtu anapotaka kuoa/kuolewa utasikia wazazi au jamaa wakimhimiza achunguze kwanza ukoo anakochukua ‘jiko’ asijekuta wana historia ya magonjwa ya kurithi akaja kuzaa watoto wenye matatizo hayo baadae.

Kwa ujumla huwezi ukasema eti kuchagua mbegu bora ya kiumbe hai kiasili bila kupita maabara basi mazao yake yanaweza yakaleta madhara kwa binadamu hapana.

 

Na chanjo za kuku Je, zina madhara yeyote yale kwa binadamu?

Chanjo za kuku kama zilivyo za binadamu ni vigumu ukasema zina madhara kwa binadamu kwani zimetengenezwa kufanya kazi maalumu tu kwenye miili ya kuku. Isitoshe chanjo nyingi zimetengenezwa kwa vimelea vya magojwa yaleyale zinazoyakinga, na kwa magojwa mengi ya kuku/ndege huwa ni vigumu binadamu kuambukizwa.

Hatari za wazi na matatizo ya kweli ya kuku wa kisasa na chotara binadamu tunapaswa kuhofia

1. Antibiotics - Dawa za kutibu magojwa ya Bakteria:

Matumizi holela ya dawa za kutibu magojwa ya kuku hasa yale yanayosababishwa na bacteria (antibiotics) yameonyesha kusababisha hatari kubwa kutokana na dawa kutengeneza usugu wa vimelea hao kupitia binadamu anapokula nyama ya kuku aliyetumia dawa hizo pasipo kufuata utaratibu unaofaa na hili ndio kila mtu anapaswa kuwa makini nalo.

 2. Haki za wanyama

Kwa kuwafanya kuku wakue haraka au kutaga mayai mengi sana kinyume na walivyoumbwa, hii ni kama binadamu hatuwatendei haki. Kwa Wanaharakati wa haki za wanyama haya siyo maadili.

Kwa mfano kuku wa nyama broiler hupata matatizo mengi sana kuanzia uzito uliokithiri unaosababisha wakati mwingine washindwe hata kusimama, matatizo ya moyo na hata kuku wa mayai kuishiwa madini ya Kalsium kwenye mifupa yao shauri ya utagaji uliokithiri.

Kuna nchi zimeanza kupiga marufuku baadhi ya tabia tunazowatendea kuku mfano hata kuwalundika kwenye vizimba vidogo (cages) idadi kubwa ya kuku, wanadai hii siyo haki ya wanyama na kupiga marufuku uzalishaji kuku kwa njia hizi za kisasa ambao wafugaji mara zote hulenga tu kupata faida kubwa.

.....................................

 

Ndugu msomaji wangu hii ni makala yetu ya kwanza katika “MSIMU WA KUKU” tunaolenga kukupa habari na taarifa nyingi ulizokuwa huzijui kuhusiana na ufugaji wa kuku.

Msimu huo unakwenda sambamba na semina za kuandika Michanganuo ya biashara za ufugaji wa kuku aina zote na Semina inayoendelea sasa hivi ni ile ya Kuku chotara wa nyama aina ya Kuroiler

SEMINA yetu ina matoleo (Version) 2, toleo la Bure na toleo la malipo ambalo unalipia  sh. elfu 10 kwa ajili ya kupata vitabu na michanganuo ya rejea wakati ukijifunza

Kupata toleo la malipo ambapo unapata full semina kwa siku 5 mfululizo ndani ya group maalumu na wenzako unalipia sh. elfu 10 kupitia namba zetu 0712202244 au 0765553030 Peter Augustino Tarimo, Tuma na neno, “NATAKA SEMINA YA KUROILER” kisha nakutumia OFFA ya vitu 8 vifuatavyo papo hapo pamoja na kukuunganisha na group la Mentorship mwaka mzima;.

 

1.    Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)

2.    Mchanganuo Mpya: Biashara ya ufugaji wa kuku chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)

3.    Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-kiingereza

4.    Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili

5.    Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili

6.    Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili

7.    Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant)-kiingereza

8.    Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant) –kiswahili

9.    Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)

 

Darasa la tatu la malipo litaanza siku ya Jumapili tarehe 23/06/2024 mpaka tarehe 27/06/2024 hivyo wahi mapema kwani tutabadilisha mchanganuo muda wowote kabla ya msimu kuisha rasmi, Pia msimu ukiisha semina hizi hamna namna tena unaweza kuzipata.

Kupata toleo la bure ambalo kuna baadhi ya vitu havijakamilika unaweza sasa hivi kubonyeza maandishi haya;- JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA KUKU 300 WA NYAMA KUROILER, na kuanza kufuatilia semina yako kwenye blog ya jifunzeujasiriamali

 

RATIBA YA SEMINA DARASA LA AWAMU YA 3

1. SEHEMU YA KWANZA 23/06/2024:

(Maandalizi)

2. SEHEMU YA PILI 24/06/2024

 (Muhtasari, Bidhaa & Biashara)

 

3. SEHEMU YA TATU 25/06/2024

(Soko, Mikakati & Utekelezaji)

 

4. SEHEMU YA NNE 26/06/2024

(Uendeshaji, Uongozi na Wafanyakazi)

 

5. SEHEMU YA TANO 27/06/2024

(Fedha & Viambatanisho)

 

Mtaalamu wa Michanganuo na Mjasiriamali;

Peter Augustino Tarimo

0712202244  /  0765553030

 

 

 

SOMA NA HIZI HAPA:

1.    Shilingi milioni 5 itatosha kufuga kuku wangapi wa mayai? naomba mchanganuo

2.    Ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai vs kuku wa nyama ni biashara ipi inayolipa faida zaidi?

3.    Ile chanjo ya kwanza ya malaria sasa imekamilika

4.    Utajuaje kama biashara yako ya ufugaji wa kuku itakupa faida?

5.    Biashara ndogondogo zenye faida ya haraka Tanzania ni hizi hapa, zipo nne (4)

0 Response to "KWANINI KUKU WA KISASA & CHOTARA HUDUNGWA SINDANO ZA HOMONI NA DAWA ILI WAKUE HARAKA NA KUTAGA MAYAI MENGI? "

Post a Comment