Upo wasiwasi mkubwa unaosambaa miongoni mwa watu kote
duniani juu ya kuku hawa wa kisasa kwa upande wa nyama (Broilers), kuku wa
mayai (Layers) na hata kuku chotata (Hybrid) mfano kuroiler na sasso.
Kwamba ukuaji wake wa haraka na utagaji wa mayai mengi
kuliko kuku wa kienyeji waliozoeleka ni matokeo ya wanasayansi na wahandisi wa
vinasaba (Genetic engineers) kutengeneza homoni na virutubishi ambavyo kuku hao
hudungwa au kuwekewa kwenye chakula na maji ya kunywa.
Unajua siyo kila mtu anayekula mazao ya kuku amewahi
kufuga kuku au hata tu kujua ‘ABC’ za kuku, wanakula kitu gani, wanafugwa vipi
au ni mchakato upi wafugaji hupitia mpaka kuku anachinjwa au yai linafika
mezani.
Hivyo ni rahisi sana wasiwasi kama huo kuwepo na kusambaa
Dunia nzima hata na zile nchi zilizoendelea kama Marekani, Uingereza na China.
Mfano utafiti mmoja uliofanyika kule nchini Marekani ulionyesha kwamba asilimia
77% ya Wamarekani wa kawaida wana imani hii kwamba wafugaji wa kuku hutumia
dawa au homoni za kukuza kuku haraka.
Swali kubwa ni kwamba, Je hawa kuku ni kwanini wakue
haraka kiasi hiki au kutaga mayai mengi vile tofauti na ilivyo kwa kuku wa
asili (kuku wa kienyeji)? Kuna tekiniki gani imetumika wataalamu wanaweza kututhibitishia
haina madhara kwa afya na mustakabali wetu kinasaba?
Kwa mfano kuku wa kisasa miaka ya 70s alikuwa na uzito
karibu nusu ya kuku wa kisasa wa miaka hii ya 2000 na kwa kadri miaka inavyozidi
kwenda wataalamu hao wanazidi kubuni kuku wenye maumbie makubwa zaidi,wanaokua
kwa muda mfupi zaidi, wanaotaga mayai mengi zaidi, wasiougua kabisa baadhi ya
magojwa na hata wasiokuwa na manyoya kabisa
Je,
Ni kweli kuku hudungwa sindao za homoni au kupewa dawa za kusaidia wakue haraka?
Siyo kweli kwamba kuku wa kisasa au hata wale chotara
hupewa dawa na homoni zozote za kuwafanya wakue haraka ndani ya muda mfupi,
bali kinachosababisha hawa kuku kuwa na tabia tofauti na kuku wa kienyeji kama
kukua upesi na kutaga sana mayai ni uchaguzi wa muda mrefu wa mbegu bora ya
kuku wazazi walio na tabia hizo nzuri.
Mbegu bora inayotoa matokeo mazuri ukichanganya na sababu
nyinginezo kama vile ulishaji chakula chenye virutubisho sahihi pamoja na
kupatiwa mazingira muafaka mfano joto na hali ya hewa inayofaa vimewezesha kuku
kukua nusu ya muda wake wa asili na utagaji mayai kufikia karibu mara 5 zaidi
ya utagaji wa kuku wa asili (kienyeji).
Kimsingi Dunia nzima imepiga marufuku kabisa matumizi ya
dawa za homoni zinazohusika na ukuaji wa wanyama haraka hasa kwa upande wa kuku.
Na hata kusingelikuwa na marufuku hiyo kuzitumia kusingeliwezekana kwa sababu
za kiuchumi kwani homoni ni gharama kubwa mno kuliko faida kifedha ambayo mfugaji
angeipata.
Kwanza ni lazima zichomwe kupitia njia ya sindano kila
siku kama uonavyo wenye tatizo la sukari wanavyochoma insulini, maana kutumia
homoni kwa njia ya mdomo haiwezi kufanya kazi kwani ikifika tumboni huyeyushwa
na kupoteza maana yake kabisa, isingeliweza kufanya kazi iliyokusudiwa.
Sasa hebu fikiria ikiwa utaamua kuwachoma homoni kuku
wako kila siku ili wakue harakaharaka na una kuku tuseme labda 300 tu, niambie
ni shughuli pevu kiasi gani ungelikuwa nayo sembuse kwa wenye mashamba ya kuku
2,000 huko mpaka 10,000? hivyo ni jambo lisilowezekana hata kidogo kutumia
homoni za kukuza kuku upesi.
Kuna
ukweli Kuku wa Kisasa wametengenezwa Maabara kijenetiki?
Hili jambo nalo limesababisha mkanganyiko mkubwa dunia
nzima. Kuna dhana kwamba Wataalamu kwa kutumia uhandisi wa vinasaba (Genetic engineering) wamehusika katika kutengeneza
mbegu ya kuku wa kisasa na chotara maabara.
Huu nao ni upotofu mkubwa na hakuna kitu kama hicho
kilichofanyika bali ni uchaguzi wa kizazi cha kuku waliokuwa na sifa
zinazohitajika, kuku hao majogoo kwa matetea wanapoachwa wapandane hutotoa
vifaranga ambao watakuwa na sifa mchanganyio za wazazi wao na kwa kuwa wazazi
wote 2 walikuwa na sifa mfano ya kukua haraka basi uzao wao wa kwanza watakua
haraka mara dufu ya wazazi.
Wataalamu kwa kuchanganya mbegu za aina mbalimbali (kucross breed) zilizo na sifa wanazozihitaji
hatimaye hukuta wamepata aina fulani ya wazazi ambao uzao wao wa kwanza unakuwa
na sifa za hali ya juu waliyoihitaji mfano kutaga mayai mengi nk. Kwa jina
jingine huitwa Selective Breeding
Hivyo watatunza kizazi hicho bila ya kukichanganya na
kingine tena kwa ajili ya kupata mayai tu ya kutotolesha vifaranga wenye hiyo
sifa teule. Na wanakuwa na mpaka hakimiliki ya ugunduzi wao kwasababu hapo
kabla hakukuwa na mtu mwingine aliyejua wala kuchanganya aina hizo za kuku
kupata hiyo aina teule waliyoipata wao. Hivyo huwezi ukasema eti kuchagua mbegu
bora ya mnyama au mmeai basi mazao yake yanaweza yakaleta madhara kwa binadamu,
si kweli.
Selective
Breeding hii hata sisi binadamu huwa tunafanya japo wengi hatujui,
pale mtu anapotaka kuoa/kuolewa utasikia wazazi au jamaa wakimhimiza achunguze
kwanza ukoo anakochukua ‘jiko’ asijekuta
wana historia ya magonjwa ya kurithi akaja kuzaa watoto wenye matatizo hayo
baadae.
Kwa ujumla huwezi ukasema eti kuchagua mbegu bora ya
kiumbe hai kiasili bila kupita maabara basi mazao yake yanaweza yakaleta
madhara kwa binadamu hapana.
Na
chanjo za kuku Je, zina madhara yeyote yale kwa binadamu?
Chanjo za kuku kama zilivyo za binadamu ni vigumu ukasema
zina madhara kwa binadamu kwani zimetengenezwa kufanya kazi maalumu tu kwenye
miili ya kuku. Isitoshe chanjo nyingi zimetengenezwa kwa vimelea vya magojwa
yaleyale zinazoyakinga, na kwa magojwa mengi ya kuku/ndege huwa ni vigumu
binadamu kuambukizwa.
Hatari
za wazi na matatizo ya kweli ya kuku wa kisasa na chotara binadamu tunapaswa
kuhofia
1. Antibiotics
- Dawa za kutibu magojwa ya Bakteria:
Matumizi holela ya dawa za kutibu magojwa ya kuku hasa
yale yanayosababishwa na bacteria (antibiotics) yameonyesha kusababisha hatari
kubwa kutokana na dawa kutengeneza usugu wa vimelea hao kupitia binadamu
anapokula nyama ya kuku aliyetumia dawa hizo pasipo kufuata utaratibu unaofaa
na hili ndio kila mtu anapaswa kuwa makini nalo.
2. Haki za wanyama
Kwa kuwafanya kuku wakue haraka au kutaga mayai mengi
sana kinyume na walivyoumbwa, hii ni kama binadamu hatuwatendei haki. Kwa
Wanaharakati wa haki za wanyama haya siyo maadili.
Kwa mfano kuku wa nyama broiler hupata matatizo mengi
sana kuanzia uzito uliokithiri unaosababisha wakati mwingine washindwe hata
kusimama, matatizo ya moyo na hata kuku wa mayai kuishiwa madini ya Kalsium
kwenye mifupa yao shauri ya utagaji uliokithiri.
Kuna nchi zimeanza kupiga marufuku baadhi ya tabia
tunazowatendea kuku mfano hata kuwalundika kwenye vizimba vidogo (cages) idadi
kubwa ya kuku, wanadai hii siyo haki ya wanyama na kupiga marufuku uzalishaji
kuku kwa njia hizi za kisasa ambao wafugaji mara zote hulenga tu kupata faida
kubwa.
.....................................
Ndugu
msomaji wangu hii ni makala yetu ya kwanza katika “MSIMU WA KUKU” tunaolenga kukupa habari na taarifa nyingi ulizokuwa
huzijui kuhusiana na ufugaji wa kuku.
Msimu
huo unakwenda sambamba na semina za kuandika Michanganuo ya biashara za ufugaji
wa kuku aina zote na Semina inayoendelea sasa hivi ni ile ya Kuku chotara wa
nyama aina ya Kuroiler
SEMINA
yetu ina matoleo (Version) 2, toleo la Bure na toleo la malipo ambalo unalipia sh. elfu 10 kwa ajili ya kupata vitabu na
michanganuo ya rejea wakati ukijifunza
Kupata
toleo la malipo ambapo unapata full semina kwa siku 5 mfululizo ndani ya group
maalumu na wenzako unalipia sh. elfu 10 kupitia namba zetu 0712202244 au
0765553030 Peter Augustino Tarimo, Tuma na neno, “NATAKA SEMINA YA KUROILER” kisha nakutumia OFFA ya vitu 8
vifuatavyo papo hapo pamoja na kukuunganisha na group la Mentorship mwaka
mzima;.
1. Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)
2.
Mchanganuo Mpya:
Biashara ya ufugaji wa kuku chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)
3.
Mchanganuo wa kuku wa
nyama (Tumaini
Broilers)-kiingereza
4. Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili
5. Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora
Project)-kiswahili
6. Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada
watermelon)-kiswahili
7. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant)-kiingereza
8. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant) –kiswahili
9. Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)
Darasa la tatu la malipo litaanza siku ya Jumapili tarehe
23/06/2024 mpaka tarehe 27/06/2024 hivyo wahi mapema kwani tutabadilisha
mchanganuo muda wowote kabla ya msimu kuisha rasmi, Pia msimu ukiisha semina
hizi hamna namna tena unaweza kuzipata.
Kupata
toleo la bure ambalo kuna baadhi ya vitu havijakamilika unaweza sasa hivi kubonyeza
maandishi haya;- JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA KUKU 300 WA NYAMA KUROILER,
na kuanza kufuatilia semina yako kwenye blog ya jifunzeujasiriamali
RATIBA YA SEMINA DARASA LA
AWAMU YA 3
1.
SEHEMU YA KWANZA 23/06/2024:
(Maandalizi)
2.
SEHEMU YA PILI 24/06/2024
(Muhtasari, Bidhaa & Biashara)
3.
SEHEMU YA TATU 25/06/2024
(Soko, Mikakati &
Utekelezaji)
4.
SEHEMU YA NNE 26/06/2024
(Uendeshaji, Uongozi na
Wafanyakazi)
5.
SEHEMU YA TANO 27/06/2024
(Fedha & Viambatanisho)
Mtaalamu
wa Michanganuo na Mjasiriamali;
Peter
Augustino Tarimo
0712202244 /
0765553030
SOMA
NA HIZI HAPA:
1. Shilingi milioni 5 itatosha kufuga kuku wangapi wa mayai?
naomba mchanganuo
2.
Ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai vs kuku wa nyama ni biashara
ipi inayolipa faida zaidi?
3.
Ile chanjo ya kwanza ya malaria sasa imekamilika
4.
Utajuaje kama biashara yako ya ufugaji wa kuku itakupa faida?
5. Biashara ndogondogo zenye faida ya haraka Tanzania ni hizi
hapa, zipo nne (4)
0 Response to "KWANINI KUKU WA KISASA & CHOTARA HUDUNGWA SINDANO ZA HOMONI NA DAWA ILI WAKUE HARAKA NA KUTAGA MAYAI MENGI? "
Post a Comment