(SOKO,
MIKAKATI & UTEKELEZAJI)
4.0
Tathmini ya Soko:
Tathmini ya Soko ni sura katika mpango wa biashara
inayohitaji taarifa kutoka nje ya biashara husika kuliko sura nyinginezo zote.
Taarifa hizo zinahusu hasa wateja watarajiwa, Sekta biashara inapoangukia na
Ushindani.
Hii ni kusema kwamba sura hii utatumia sana taarifa
ulizozipata wakati wa kufanya utafiti wa soko lako na biashara kwa ujumla.
Kama tulivyokwishaona, utafiti au upembuzi yakinifu
kulingana na KITABU CA MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI unaweza kuufanya
kwa njia rahisi kupitia kwenda moja kwa moja kwa wateja wa bidhaa/huduma
tarajiwa na kuwauliza maswali mbalimbali yanayolenga kupata taarifa zao na
bidhaa wanazonunua. Kitabu hicho kimeeleza njia zote mbili, rahisi na ile ya
kitaalamu zaidi ya kutafiti soko la biashara yeyote ile
Utafiti pia unaweza kuufanya kwa njia ya kusoma
machapisho au majarida na vyombo vya habari vyenye taarifa kutoka taasisi
mbalimbali kama vile Wizara za serikali, Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Serikali za
mitaa, vyama vya wafanyabiashara na wataalamu wengineo.
Katika mchanganuo wetu huu wa kuku chotara kuroiler tutazingatia baadhi ya vipengele vinavyounda sura hii ingawa siyo lazima tuvitumie vyote kulingana na mahitaji ya biashara yenyewe. Navyo ni;
4.1 Mgawanyo wa soko
4.2 Soko lengwa
4.2.1 Mahitaji ya soko
4.2.2 Mwelekeo wa soko
4.2.3 Ukuaji wa soko
4.3 Tathmini ya Sekta
4.3.1 Washiriki katika sekta
4.3.2 Usambazaji
4.3.3 Ushindani
4.3.4 Washindani wako wakuu
Kama kawaida wakati nikianza kuandika Sura hii sina budi
kuacha nafasi ya kuja kuandika muhtasari wa sura nzima baadae kwa kuchagua
baadhi ya mistari au pointi zile muhimu.
4.1
Mgawanyo wa soko
Katika kipengele hiki kidogo nataja ni makundi gani ya
soko tutakayoyalenga na nitayataja makundi matatu ambayo ni;
(1) .........................................................
(2) ..........................................................
(3) ..........................................................
Kuligawa soko lako fikiria kwanza ni vigezo vipi
vinavyosababisha makundi hayo yatofautiane kwenye kununua mfano umri, kipato,
elimu, eneo, ufikiwaji na vyombo vya habari ama kigezo kingine chochote kile.
Ikiwa wateja wako ni taasisi au biashara basi unaweza kutumia vigezo kama idadi
ya wateja, kiasi cha mtaji, ukubwa wa biashara nk.
Mimi kwa mfano katika makundi haya matatu nimetaja sifa
za kila kundi na katika kuligawanya soko hili nimezingatia zaidi idadi ya kuku
wanaonunua pamoja na kiasi cha mtaji walichokuwa nacho kama kitofautishi cha
makundi hayo.
4.2
Mkakati wa soko lengwa
Hiki ni kipengele kingine kidogo kwenye sura hii ambacho
ni kama vile tunazidi kuchambua kile kipengele kilichopita kusudi tupate
kipande cha soko tutakachokilenga zaidi ya vingine na kuelezea ni mkakati upi
uliotufanya tuchague kulenga zaidi kipande hicho na wala siyo vipande vingine
2.......................
.................Mpenzi
msomaji wangu Jipatie mchanganuo kamili wa kuku chotara 300 wa nyama aina ya
Kroiler pamoja na Semina yake ya siku 5 uweze kujua undani wa kipengele hiki na
vingine ndani ya mpango huu bunifu wa biashara yenye faida kubwa katika kipindi
kifupi..............
4.2.1
Mahitaji na Mwelekeo wa soko
Hapa nimeunganisha vipengele vidogo viwili ambavyo ni
“mahitaji ya soko” na “Mwelekeo wa soko”, vilipaswa kujitegemea kila kimoja
lakini kutokana na ufupi wake nikaona ni vyema niviunganishe pamoja.
Katika kila kipande cha soko unachokilenga unaelezea
mahitaji ya wateja katika kipande husika yanayowafanya wanunue bidhaa/huduma
zako huku ukilenga zaidi faida aipatayo mteja na wala siyo faida unayoipata
wewe.
Kwa mfano sisi hapa hatulengi tu kuwauzia wateja wetu
kuku bali tunahakikisha tumekidhi mahitaji ya wateja wetu ya kutaka kitoweo cha
kuku kilicho na ladha tamu kwa bei inayohimilika na mtu wa kipato chochote,
vilevile ni kukidhi hitaji la wateja la kula nyama nyeupe inayosisitizwa sana
na wataalamu wa afya likiwemo Shirika la chakula Duniani FAO
Kwenye Mweleko wa soko unataja kigezo kinachoonekana
kubadilisha hali ya soko siku za usoni, kwa mfano sisi hapa katika mchanganuo
wetu huu mwelekeo wa soko la kuku jijini Dar es salaam unaonyesha
wateja..............................................
..........................................................................................................................................................................................................
4.2.2
Ukuaji wa Soko
Kulingana na utafiti wako wa soko ulioufanya, hapa
unatakiwa kutoa nukuu kulingana na taarifa mbalimbali za kitaalamu ulizozipata
kuonyesha ni jinsi gani soko lako lina uwezekano wa kukua.
Kwa mfano kwenye mchanganuo wetu huu nilionyesha soko
kukua kwa kutumia takwimu za Sensa ya watu na makazi, kwamba kila mwaka idadi
ya wateja jijinI Dar es salaam wanaohitaji kitoweo cha kuku huongezeka kwa
sababu idadi ya watu nayo inaonyesha kukua....................................................
Ningeliweza pia kwa mfano kutumia taarifa za wataalamu
wengine kwenye sekta hii ya kuku zinazoonyesha ukuaji wa soko hili mwaka hadi
mwaka kama vile mauzo ya kuku katika soko moja moja, idadi ya kuku wanaochinjwa
kwa mwezi, idadi ya machinjio zinavyoongezeka kila mwaka nk.
4.3
Sekta ya Ufugaji wa kuku (Ndege)
Katika tathmini ya sekta uliyopo, kwanza unataja ni sekta
gani hiyo, kwa mfano sisi hapa tumetaja ni sekta ya ufugaji wa kuku/ndege,
unaweza ukataja ndege au kuku vyote ni sawa. Kama ilivyokuwa kwa taarifa za
soko, Sekta nayo taarifa zake hutokana na utafiti ulioufanya hasa kutokana na
machapisho mbalimbali yanayohusiana na sekta ya kuku.
Taarifa hizo mbali na zile zinazohusisha kampuni/biashara
yako moja kwa moja lakini pia unatakiwa kuwa na taarifa zinazohusu mazingira
mazima yanayoizunguka biashara hiyo
Unaweza kuzungumzia jambo lolote lile kwenye sekta
linaloshika chati (kutrend) kwa
wakati huo huku ukitoa takwimu mbalimbali ulizonukuu kutoka katika utafiti
wako. Kwa mfano kwenye mchanganuo wetu huu wa kuku wa Kuroiler kwa ajili ya
nyama kwenye sekta nimezungumzia.........................................
...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Vilevile nilieleza jinsi sekta hiyo ilivyogawanyika makundi
makundi pamoja na washiriki wake mbalimbali wanaounda sekta nzima.
4.3.1
Ushindani
Hiki ni kipengele kidogo ndani ya Sekta. Unaweza ukaona
kwamba sijaweka katika mchanganuo huu vipengele vidogo vyote kama vilivyotajwa
kwenye mlolongo wa vipengele kamili kwani siyo lazima mtu kufanya hivyo. Mfano
sijaweka, “Washiriki katika sekta” na
“Mfumo wa usambazaji”
Hivyo niliingia moja kwa moja kwenye kpengele kidogo cha
Ushindani nikaelezea hali ya ushindani ilivyo, kwamba ushindani katika biashara
ya kuroiler siyo mkubwa sana katika eneo la Kimara ingawa wapo washindani
wasiokuwa wa moja kwa moja. Nilielezea na aina mbili za ushindani, ule wa moja
kwa moja na usiokuwa wa moja kwa moja.
Ningleliweza pia kuelezea na kigezo kinachotumika wateja
kuchagua ni kwa mshindani yupi wanunue kutoka kwake mfano wanaweza kutumia
kigezo cha bei, ubora wa huduma, jina (brand) ama kigezo kingine chochote
kile.
Kipengele hiki pia nilikiunganisha na kipengele kingine
cha “Washindani wako wakubwa” ambacho
kilipaswa kuwa kinajitegemea baada ya hiki.
Kwa kila mshindani niliyemtaja nimeelezea sifa zake,
nguvu na udhaifu aliokuwa nao katika vigezo/maeneo mbalimbali mfano bei, hali
ya kifedha, teknolojia, jina, usambazaji nk.
Mazingira
ya Biashara
Nilisema haipaswi kukariri mlolongo wa vipengele kama
ulivyotajwa bali unautumia tu kama muongozo. Ndio maana unaweza kuona kipengele
hiki hakipo kwenye mlomlongo rasmi nilioweka pale juu lakini nimekiweka kwenye
mchanganuo na inategemewa mtu unaweza ukaweka kipengele kingine chochote ilimradi
kihusiane na soko.
Mfano hapa niliweka vipengele vidogo vya “Mazingira ya nje ya biashara (PESTLE)”
na “NUFUVI”, kwa kirefu (Nguvu Udhaifu,
Fursa na Vikwazo)
Tathmini hizi 2 kwa ujumla zinaelezea mazingira ya
biashara au nguvu mbalimbali kutokea nje na ndani ya biashara yenyewe
zinazoweza kuiathiri biashara yako katika mlengo chanya au hasi. Faida zake ni
kwamba zinakuwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa urahisi zaidi na
kuzitumia fursa zilizopo kikamilifu.
4.4 Mazingira
ya nje ya Biashara (PESTLE)
Kirefu cha PESTLE kwa kiingereza ni Political, Economoc,
Social, Technological, Legal and Enviromental. Ikimanisha, mazingira ya
Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii, Kiteknolojia, Kisheria na Kimazingira. Vyote
nimevielezea vizuri kabisa kwenye mpango wa biashara hii ya ufugaji wa kuku
chotara wa nyama kroiler.
4.5
Nguvu, Udhaifu, Fursa na Vikwazo (NUFUVI au SWOT analysis kwa kiingereza)
Kama ilivyokuwa kwa mazingira ya nje ya biashara hapo
juu, hii nayo ni tathmini lakini yenyewe imebeba mazingira ya ndani ya biashara
na mazingira ya nje ya biashara kwa pamoja.
Nguvu
na Udhaifu ni mazingira chanya na hasi ya
ndani ya biashara wakati Fursa na Vikwazo ni mazingira ya nje ya biashara
chanya na hasi. Chanya namaanisha mazingira wezeshi na hasi ni mazingira yale
yanayodhoofisha biashara au kukwamisha biashara isishamiri.
Mwisho wa kipengele cha
Soko, karibu kipengele cha Mikakati na Utekelezaji
5.0 Mikakati
na utekelezaji
Mikakati ni malengo au vipaumbele vya biashara
ulivyochagua miongoni mwa vitu vingine ili kuifanya iweze kuwa juu kuliko za
washindani wako.
Tuseme
labda umelenga kuwa na mauzo ya shilingi milioni 10 kwa mwezi katika biashara
yako, ni lazima ukae chini na kupanga utaitangaza vipi biashara yako, utauza
namna gani na hata usambazaji utakuwa vipi ikiwa ni bidhaa nk.
Ili
kuielewa vizuri sura hii na nyinginezo ni vyema ukawa nacho kitabu chako cha
Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali pamoja na mchanganuo kamili wa Biashara
hii ya kuku wa nyama Kuroiler.
Kabla ya kufanya chochote kwenye Sura hii hebu kwanza
tuweke mezani vipengele vidogo vinavyounda sura hii nzima kama dira
itakayotuongoza;
5.1 Nguvu za kiushindani
5.2 Mkakati wa Soko
5.2.1 Kaulimbiu ya kujipanga
katika soko
5.2.2 Mkakati wa Bei
5.2.3 Matangazo na
Promosheni
5.2.4 Programu za masoko
5.3 Mkakati wa Mauzo
5.3.1 Makisio ya mauzo
5.3.2 Programu za mauzo
5.4 Mkakati wa ushirkiano
5.5 Vitendo na Utekelezaji
Mwanzoni kabisa nimeweka ufupisho wa vipengele vya sura
hii nzima ambao niliandika mwishoni baada ya kukamilisha sura nzima
5.1
Faida za kiushindani
Hivi ni vitu biashara/kampuni inavyofanya vizuri kuzidi
washindani wake na hivyo kujitofautisha nao, na hapa nimevitaja vitu 3 visome
kwenye mchanganuo wako wa kuku kuroiler wa nyama
5.2
Mkakati wa Soko
Mkakati wa soko chini yake umebeba vipengele vidogo
kadhaa ambavyo ni bidhaa, Bei, Matangazo & Promosheni na Usambazaji,
kwahiyo hapa tunaweka muhtasari tu wa vipengele hivyo kisha tunaendelea na
vipengele vyenyewe
5.2.1
Bidhaa
Hapa nimeelezea mkakati wetu wa bidhaa jinsi CPPC
tutakavyozalisha..........................................................................
.....................................................................................................
5.2.2
Matangazo & Promosheni
Ni mkakati wa kuhakikisha wateja wetu watarajiwa wanapata
taarifa za uwepo wa bidhaa zetu na kuvutiwa nazo, na nimeelezea katika
mchanganuo wetu ni mambo gani tutakayoyafanya kutimiza hilo
5.2.3
Bei
Nimeelezea pia ni mkakati upi kwenye suala la upangaji wa
bei tutakaoutumia tofauti na washindani wetu ili kuweza kuibuka kidedea sokoni.
Fungua mchanganuo wako wa ufugaji wa kuku chotara wa Kroiler usome mkakati huo
mpaka mwisho
5.3 Usambazaji
Mkakati wa usambazaji
nimetaja njia zitakazotumika kuwafikishia wateja kuku
nikataja................................................ ..........................................................................................................................................................................................................
5.3
Mkakati wa Mauzo
Mauzo ni mkakati tofauti na ile ya Soko tuliyoiona hapo
juu na chini yake umebeba pia mikakati mingine midogomidogo kama Makisio ya
mauzo na Programu za mauzo. Nimeweka maelezo ya ni kipi kitakachofanyika
kuhakikisha mauzo yanakuwa makubwa na kwa ufanisi zaidi
5.3.1
Makiso ya mauzo
Hapa nimekisia mauzo kwa kila bidhaa yatakuwa shilingi
ngapi kwenye mzunguko mmoja wa wiki 12 kisha mwaka 1 na miaka 2 inayofuata
unaweza kucheki kwenye mchanganuo kamili wa kuku chotara wa nyama kuroiler
5.4
Utekelezaji
Baada ya kuweka mikakati mbalimbali hapa ndipo
unapoonyesha mikakati hiyo utakavyoitekeleza. Nimechora jedwali
linaloonyesha..................................................................
..........................................................................................................................................................................................................
Mpaka hapo tumemaliza Sehemu
yetu ya tatu ambapo tulichanganua Sura mbili za Soko na Mikakati &
Utekelezaji. Karibu Sehemu ya nne
SEMINA SEHEMU YA 2 SEMINA SEHEMU YA 4
SOMA
NA HIZI HAPA;
2. Kupata faida kwenye ufugaji wa kuku
wa kienyeji au wa kisasa mfugaji mjanja hutumia mbinu hizi.
3. Ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai
vs kuku wa nyama ni biashara ipi inayolipa faida zaidi?
4. Njia mpya za kufanya mambo: dunia, biashara, ajira
vinabadilika kwa kasi ya ajabu
5. Gharama za ujenzi wa banda la kuku
100 chotara au kienyeji ni shilingi ngapi?
6. Mwaka wa ubunifu zaidi kwenye biashara kukabiliana na majanga
0 Response to "SEMINA SEHEMU YA 3: MPANGO WA BIASHARA, UFUGAJI KUKU WA NYAMA KUROILER – (SOKO, MIKAKATI & UTEKELEZAJI)"
Post a Comment