SEMINA SEHEMU YA 4: MCHANGANUO WA BIASHARA YA UFUGAJI KUKU CHOTARA WA NYAMA KROILER – (UENDESHAJI, UONGOZI & WAFANYAKAZI) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA SEHEMU YA 4: MCHANGANUO WA BIASHARA YA UFUGAJI KUKU CHOTARA WA NYAMA KROILER – (UENDESHAJI, UONGOZI & WAFANYAKAZI)

Uendeshaji na Usimamizi biashara ya kuku wa kuroiler 

SEMINA KUKU  WA NYAMA KUROILER

(SEHEMU YA NNE)

(Uendeshaji, Uongozi & Wafanyakazi)

 

6.0 Mpango wa Uendeshaji

Uendeshaji, sura hii huelezea jinsi michakato mbalimbali kwenye biashara itakavyofanyika kila siku kusudi kufikia malengo yaliyokusudiwa

Sura hii huwa na vipengele vingi vidogovidogo kulingana na ukubwa na aina ya biashara. Kuna biashara nyingine hazina kabisa kipengele hiki au zina vipengele vichache hasa zile zisizokuwa na michakato ya uzalishaji.

Kabla ya kuendelea nitavitaja vipengele vidogo mbalimbali ambavyo mara nyingi huwekwa katika sura hii ya Uendeshaji ingawa mimi kwenye mchanganuo wetu huu wa kuku chotara aina ya kuroiler nimetumia vipengele vichache tu kwa kadiri ya mahitaji ya biashara yenyewe;

                            ·        Mchakato wa Uzalishaji

                            ·        Eneo

                            ·        Teknolojia

                            ·        Vifaa na mashine

                            ·        Malighafi

                            ·        Wasambazaji

                            ·        Gharama za mradi

                            ·        Masuala ya kisheria

                            ·        Sera ya mkopo

                            ·        Vihatarishi vya mradi

Hapa unaweza ukaelezea shughuli yeyote ile ya kiuendeshaji inayofanyika katika biashara yako kila siku.

Kwenye mchanganuo huu wa CPPC tumechagua baadhi ya vipengele hivyo na unaweza ukasoma maelezo yake moja kwa moja katika mchanganuo wetu huo.

Tuchukue kwa mfano kipengele cha Eneo, katika uendeshaji unaeleza kwa undani jinsi eneo hilo lilivyo, vipimo vyake, rasilimali zilizomo hapo na jiografia yake kwa ujumla, sawa tu na nilivyofanya kwenye mchanganuo huu

Kipengele kingine cha Gharama za mradi kwa mfano nimeorodhesha na kufafanua kwa undani kabisa gharama zote zitakavyotumika nikianza na zile za kudumu kama..................... ............................................................................................ kisha nikafuatia na Gharama zinazobadilika za.................................... .....................................................................................................

Mfano mzuri kwenye gharama ni chakula, nimechora mpaka jedwali linaloonyesha ratiba ya ulaji wa kuku, kila siku kuku mmoja anakula chakula kiasi gani na kwa gharama ipi.

Sasa ukishafahamu kuku mmoja kwa mfano anakula kilo 3 za chakula kwa miezi 2 basi kwa kuku 300 unazidisha tu mara kilo 3 kupata kiasi watakachokula kuku wako wote 300 ndani ya miezi hiyo 2

Katika sura hii mtu ukisoma kwenye kipengele cha (2a) gharama za chakula ndipo unaweza kuona na kujifunza Ubunifu uliotumika kwenye biashara hii kuhakikisha gharama zinakuwa chini kusudi faida nayo iweze kuwa kubwa, gharama hizo zimegawanyishwa katika makundi....................................... wawili.......................................................................................................................................................................................

 

Mwisho wa Sura 6 (Utekelezaji) karibu Sura ya 7

 

7.0 Uongozi & Wafanyakazi

Sura inayohusu Uongozi na Wafanyakazi hubeba vipengele vifuatavyo;

7.1 Muundo wa Uongozi

7.2 Timu ya Uongozi

7.3 Pengo la Uongozi

7.4 Mpango wa Mishahara

Nimeanza na aya ya muhtasari mdogo unaobeba pointi zote muhimu za kwenye vipengele vingine vidogo lakini niliandika baada ya kumaliza kuviandika kwanza vipengele vyenyewe

7.1 Muundo wa Uongozi

Kwakuwa biashara mwanzoni haitakuwa na wafanyakazi wengi, siwezi nikachora chati inayoonyesha muundo wa utawala ulivyo na badala yake maelezo machache tu yanatosha. Soma maelezo katika mchanganuo wa kuku kuroiler 300 wa nyama

7.2 Timu ya Uongozi     

Hapa nawataja wale watu muhimu wanaounda uongozi wa biashara, majukumu yao pamoja na historia yao kwa kifupi. Maelezo kwa kirefu ya historia zao (CV) huwa yanawekwa kwenye vielelezo kama viambatanisho.

Nimemtaja Bibi Amina Abdallah kama mmiliki na msimamizi mkuu wa biashara, nikaeleza pia elimu yake na uzoefu aliokuwa nao kwenye biashara hii ya kuku. Nimemtaja pia mfanyakazi, majukumu yake na sifa anazotakiwa kuwa nazo muombaji wa nafasi hii................................................................ ...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................

7.3 Mpango wa Mishahara

Katika mpango wetu wa biashara wa CPPC mwanzoni ni mfanyakazi mmoja tu atakayekuwa akilipwa mshahara hivyo sikuwa na haja ya kuchora jedwali la mishahara badala yake nimetaja tu kiasi atakacholipwa kwa mwezi shilingi laki moja au laki 3 katika mzunguko mmoja wa wiki 12 (miezi 3).

 

 

Mpaka kufikia hapo tumemaliza Sehemu hii ya 4 iliyobeba Sura 2 za; Uendeshaji na Uongozi & Wafanyakazi. Karibu tena Sehemu ya 5 na ya mwisho


 

SEMINA SEHEMU YA 3                SEMINA SEHEMU YA 5

 

 

 

 SOMA NA HIZI HAPA;

1.   Semina: mchanganuo wa kuomba mkopo biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama 2000

2.   Orodha ya biashara za vijijini unazoweza kuanza na mtaji wa sh. laki 3 (300,000/=)

3.   Mchanganuo wa biashara ya kuuza chipsi, je, unajua gharama ya sahani moja mpaka inafika mezani ni sh. ngapi?

4.   Semina: mchanganuo wa biashara ya kusaga na kuuza unga safi wa dona (usado milling)-1

5.   Biashara 7 nzuri mwaka huu: chagua 1 uingize faida na kipato cha ziada kwa urahisi

0 Response to "SEMINA SEHEMU YA 4: MCHANGANUO WA BIASHARA YA UFUGAJI KUKU CHOTARA WA NYAMA KROILER – (UENDESHAJI, UONGOZI & WAFANYAKAZI)"

Post a Comment