SEHEMU YA TANO
Mpango
wa Fedha na Viambatanisho
8.0
Mpango wa Fedha
Katika Sura hii ya Fedha kunakuwa na muhtasari mdogo wa
yale mambo muhimu yanayopatikana ndani ya Sura nzima kisha baada ya hapo
hufuata vipengele vidogo ambavyo ni hivi;
8.1 Dhana/Makisio muhimu
8.2 Tathmini ya mauzo
yakurudisha gharama (Break Even Analysis)
8.3 Makisio ya Faida na
Hasara
8.4 Makisio ya Mtiririko wa
Fedha Taslimu
8.5 Makisio ya Mizania ya
Biashara
8.6 Sehemu muhimu za
biashara
8.1
Dhana/Makisio muhimu
Hapa nimeorodhesha Dhana au makisio niliyotumia kukisia
ripoti za mahesabu yangu, dhana hizo ni kama vile; idadi ya kuku katika
mzunguko mmoja, uchakavu, bei za vyakula, bei ya kifaranga mmoja nk.
8.2 Tathmini ya mauzo ya kurudisha gharama
zote (Break even Analysis)
Haya ni mauzo au idadi ya bidhaa mradi utakazozalisha na
kuuza katika kipindi fulani tuseme, mzunguko mmoja, mwaka au kipindi kingine
chochote kile ambayo yatalingana na gharama zilizotumika. Au kwa manemo mengine
unaweza ukasema; utatakiwa uuze kiasi gani kwa kipindi husika kusudi uweze
kurudisha gharama zote zilizotumika katika kipindi hicho?
Ina maana kwamba ukiuza chini ya kiasi hicho unapata
hasara na ukiuza juu ya kiasi hicho unapata faida.
Kwakuwa biashara hii ya CPPC uzalishaji wake unafanyika
kwa mzunguko wa miezi 3, basi hatuna budi kufanya tathmini hii ya break even katika kipindi hicho cha
miezi 3 badala ya kutumia kipindi cha mwezi mmoja ambacho imezoeleka zaidi kwa
biashara za aina nyigine tofauti na kuku.
Katika tathmini hii huwa kuna vitu muhimu 3 ambavyo mtu
unapaswa kwanza kuwa navyo kabla ya kukokotoa, navyo ni;
(1) Mauzo
jumla = 3,037,200/=
(2) Gharama
za kudumu = 55,750/=
(3) Gharama
zinazojirudiaa (za mauzo) = 2,223,150/=
(4) Asilimia
ya faida ghafi katika mauzo (Cotribution margin ratio) = 26.8%
Taarifa hizi zote 3 tunaweza tukazipata kutoka katika
jedwali la faida na hasara la mzunguko mmoja wa miezi 3, tungeliweza kuzipata
pia hata kama tungeliamua kutumia vipindi vya mwezi mwaka nk. Tazama jedwali
hilo kwenye mchanganuo wako
Kupata Contribution
margin% unaweza ukatumia kanuni ifuatayo;
CM%
=Mauzo – Gharama zinazojirudia / Mauzo x 100
= 3,037,200/ 2,223,150 x 100 = 26.8%
Na kanuni ya kukokotoa mauzo ya kurudisha gharama Break
even sales nayo ni hii hapa;
B.E Sales = Gharama za kudumu / CM% = 55,750 /0.268
= 208,022
Jinsi
ya Kuchora chati ya mauzo ya kurudisha gharama (Break even chart)
Ili kuchora chati hii kwanza unahitaji kuzingatia kanuni
kuu ya Break even analysisi ifuatayo na ambayo ndiyo kanuni nyingine zote
zinazotumika kukokotoa tathmini hii huanzia
Faida
= Mauzo – Gharama zinazobadilika – Gharama za kudumu
Laini kumbuka Faida ni sifuri (0) mauzo ya kurudisha
ghara yanapofikiwa, na pia Gharama zinzobadilika tunaziweka katika sehemu ya
mauzo ambapo ni asilimia 73.2% x Mauzo au 0.732 ya mauzo
Kwa maana hiyo tutatengeneza jedwali la taarifa (data) za
chati yetu, MAUZO VS FAIDA tukitumia
kanuni hiyo huku kila penye gharama zinazobadilika tukiweka (0.732 ya Mauzo)
kama ifuatavyo;
Tukianza na Mauzo =sifuri (0) faida itakuwa hivi;
Faida = 0 – 0.732(0) – 55,750 = -55,750
Kwahiyo kukiwa hamna mauzo kabisa (0) faida ni hasi
-55,750 maana yake ni kuwa kuna gharama za kudumu peke yake bado hamna kazi
iliyofanyika
Tukiweka mauzo yetu ni sh. 50,000/= Faida itakuwa kama
ifuatavyo;
Faida = 50,000 – 0.732(50,000) – 55,750 = -42,350 Hapa
tunaona bado faida ni hasi
Tukiweka mauzo = 100,000/=
Faida = 100,000 – 0.732(100,000) – 55,750 = -28,950 Hapa
faida bado ni hasi lakini inazidi kuongezeka kuwa +.
Tuweke mauzo yetu ni sh. 150,000/=
Faida = 150,000 – 0.732(150,000) – 55,750 = -15,550
Tukiweka mauzo ni sh. 200,000
Faida = 200,000 – 0.732(200,000) – 55,750 = -2,150
Tuweke Mauzo ni sh. 250,000
Faida = 250,000 – 0.732(250,000) – 55,750 = 11,250 Hapa
sasa unaona mauzo yakiwa sh 250,000 faida inaanza kuwa chanya na kadiri mauzo yatakavyoongezeka
faida nayo itazidi kuongezeka lakini kuna mahali mauzo yatalingana na gharama
ambapo faida itakuwa ni 0 na utaweza kuona kwenye jedwali letu.
Heu sasa tuweke taarifa/data zetu za kutosha kwenye
jedwali hili ndipo tuchore chati yetu;
Jedwali:
Mauzo vs Faida
Mauzo |
Faida |
0 |
-54,250 |
50,000 |
-42,350 |
100,000 |
-28,950 |
150,000 |
-15,550 |
200,000 |
-2,150 |
250,000 |
11,250 |
300,000 |
24,650 |
350,000 |
38,050 |
400,000 |
51,450 |
450,000 |
64,850 |
500,000 |
78,250 |
550,000 |
91,650 |
Chati:
Tathmini ya Mauzo ya kurudisha gharama (Break even sales)
Kwa kutumia taarifa zetu hapo juu sasa tunaweza kuchora
chati yetu kwenye Microsoft word kama ifuatavyo.
Kituo faida inapokuwa ‘0’ ukisoma kwa umakini thamani ya mauzo pale chini mstari ulipopishana utaona ni sh. 208,022 sawa na jibu tulilopata kwa kutumia kanuni ya kukokotoa Break Even sales pale juu.
8.3
Makisio ya Faida na Hasara
Miradi ya kuku hasa wa nyama
ni tofauti kidogo na biashara nyingine kwenye kipindi cha makisio. Kwa kuwa
kuku wa nyama huwezi kuwauza mpaka muda wa kukua ufike huwezi kukisia hesabu ya
kila mwezi na badala yake utakisia hesabu ya mzunguko mzima wa kipindi chote
tangu vifaranga wa siku moja mpaka unawauza, kwa kesi yetu ni miezi 3(wiki 12).
Kisha hesabu za mzunguko mmoja ndiyo zinakuwa msingi wa hesabu za vipindi
vingine kama mwaka mmoja na miwili.
Kumbuka taarifa zote kuanzia mauzo mpaka gharama zote
tulikwisha zipata huko nyuma na hapa ni suala la kuzipachika tu kwenye jedwali
letu la faida na hasara la mzunguko mmoja tukianza na Mauzo pale juu kabisa
kisha tunatoa gharama zinazobadilika, tunatoa tena gharama za kudumu, toa kodi
na riba na mwishoni tunapata Faida halisi.(Tazama
mchanganuo wako)
Makisio
ya Faida na Hasara mwaka wa 1
Faida na hasara mwaka mmoja yanaundwa na makisio ya
vipindi tofauti na kwa mchanganuo wetu ni vipindi 4, kwahiyo vipindi hivyo 4
tukijumlisha taarifa zake katika kila safu iliyolala ndipo tunapata taarifa za
mwaka mzima kama ifuatavyo;
MAKISIO YA FAIDA NA HASARA |
|
||||
Mzunguko1 |
Mzunguko2 |
Mzunguko3 |
Mzunguko4 |
MWAKA 1 |
|
|
|||||
MAUZO |
3,037,200 |
3,037,200 |
3,037,200 |
3,037,200 |
12,148,900 |
Gharama zinazobadilika |
2,223,150 |
2,223150 |
2,223,150 |
2,223,150 |
8,892,600 |
Faida
ghafi |
814,050 |
814,050 |
814,050 |
814,050 |
3,256,200 |
%Faida ghafi |
26.8% |
26.8% |
26.8% |
26.8% |
26.8% |
|
|||||
Gharama
za kudumu |
|
||||
Uchakavu wa banda |
18,750 |
18,750 |
18,750 |
18,750 |
75,000 |
Uchakavu wa vifaa |
17,000 |
17,000 |
17,000 |
17,000 |
68,000 |
Umeme |
5,000 |
5,000 |
5,000 |
5,000 |
20,000 |
Matangazo na usafiri |
15,000 |
15,000 |
15,000 |
15,000 |
60,000 |
Jumla
gharama za kudumu |
55,750 |
55,750 |
55,750 |
55,750 |
223,000 |
|
|||||
Faida kabla ya kodi na Riba |
758,300 |
758,300 |
758,300 |
758,300 |
3,033,200 |
Kodi |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Riba |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Faida
Halisi |
758,300 |
758,300 |
758,300 |
758,300 |
3,033,200 |
%Faida Halisi |
25% |
25% |
25% |
25% |
25% |
Kupata jumla ya makisio ya kila mstari uliolala (rows)
ambayo yatakuwa ndiyo makisio yetu ya mwaka mzima unajumlisha kila namba ya
mzunguko kwa mizunguko yote 4 mfano mauzo mzunguko wa kwanza + mauzo mzunguko
wa 2 nk. hadi wa nne = 12,148,900/=
Hapa sasa unakuwa tayari umekwishakamilisha makisio yako
ya faida na hasara kwa mwaka wa kwanza kama uonavyo kwenye jedwali hapo chini
ukisubiri kupata makisio ya miaka 2 inayofuata;
Makisio ya Faida na
Hasara |
|||
|
Mw1 |
Mw2 |
Mw3 |
|
Sh. |
Sh. |
Sh. |
MAUZO |
12,148,800 |
|
|
Gharama zinazojirudia |
8,892,600 |
|
|
Faida Ghafi |
3,256,200 |
|
|
%Faida ghafi |
26.8% |
|
|
Gharama za kudumu
za uendeshaji |
|
|
|
Uchakavu wa banda
|
75,000 |
|
|
Uchakavu wa vifaa
|
68,000 |
|
|
Umeme |
20,000 |
|
|
Matangazo/usafiri |
60,000 |
|
|
Jumla ya Gharama za kudumu |
223,000 |
|
|
Faida kabla ya kodi
na riba |
3,033,200 |
|
|
Riba ya mkopo. |
0 |
|
|
Kodi ya mapato . |
0 |
|
|
Faida halisi. |
3,033,200 |
|
|
%Faida halisi / mauzo. |
25% |
|
|
Jinsi
ya kukisia faida na hasara kwa miaka 2 inayofuata;
1.
Mauzo;
Tunaanza na mauzo kwanza na
kumbuka tulipokuwa tukikisia mauzo huko nyuma tulikisia kwamba mwaka wa pili
mauzo yataongezeka kwa asilimia 50% na mwaka wa tatu asilimia 33.3%
Inamaana kwamba,
Mauzo
ya mwaka wa pili tutakokotoa hivi;
50% x 12,148,800 +
12,148,800 = 18,223,200
Mauzo
ya mwaka wa tatu;
33.3% x 18,223,200 + 18,223,200 = 24,297,600
2. Gharama
zinazobadilika (za mauzo)
Gharama
zinazobadilika tuliweka makisio ya asilimia 73.2% ya Mauzo,
hivyo kwa
Mwaka
wa pili tutafanya hivi;
73.2% x 18,223,200 = 13,339,384
Mwaka wa 3;
73,2% x 24,297,600
= 17,785,844
3.
Gharama za kudumu
Uchakavu:
Kumbuka kwamba
tulisema kila mwaka mabanda na vifaa vya chakula na maji vitaongezwa kulingana
pia na ongezeko la vifaranga; hivyo mwaka wa 2 kuku 150 wataongezeka na banda
pia itabidi liongezwe kwa nusu ya banda la mwaka wa kwanza ambapo gharama yake
ni nusu pia ya ile ya mwaka wa kwanza
Kwahiyo tutachukua
uchakavu wa mwaka wa kwanza sh. 75,000 + uchakavu wa banda lililoongezwa sh.
37,500 = 12,500 na kwa upande wa vifaa vya maji na chakula ni hivyohivyo.
Umeme na Matangazo:
Tutakisia ongezeko
kidogo la shilingi elfu 10 kwenya umeme na
shilingi elfu 40 kwenye matangazo kwani inategemewa kwamba ni lazima
gharama hizi zipande kidogo kulingana pia na ongezeko la shughuli za biashara,
kwa hiyo ni suala tu la kutumia uzoefu wako kuamua gharama hizo kwa makisio
zinaweza kuongezeka kwa kiasi gani.
Tukitoa gharama zote
kutoka kwa Mauzo tunapata faida kabla ya kodi na Riba na kwa kuwa biashara yetu
tumekisia hakutakuwa na kodi wala riba wakati inaanza basi faida halisi
itabakia kuwa hiyohiyo sawa na faida kabla ya kodi na riba ambayo ni
shilingi 4,536,316 mwaka wa pili na
shilingi 6,045,756 mwaka wa tatu
Mwisho kabisa jedwali
letu la Faida na hasara kwa miaka yote 3 litaonekana kama ifuatavyo;
Jeswali: Faida na Hasara miaka 3
Makisio ya Faida na
Hasara |
|||
|
Mw1 |
Mw2 |
Mw3 |
|
Sh. |
Sh. |
Sh. |
MAUZO |
12,148,800 |
18,223,200 |
24,297,600 |
Gharama zinazojirudia |
8,892,600 |
13,339,384 |
17,785,844 |
Faida Ghafi |
3,256,200 |
4,883,816 |
6,511,756 |
%Faida ghafi |
26.8% |
26.8% |
26.8% |
Gharama za kudumu
za uendeshaji |
|
|
|
Uchakavu wa banda
|
75,000 |
112,500 |
150,000 |
Uchakavu wa vifaa
|
68,000 |
105,000 |
136,000 |
Umeme |
20,000 |
30,000 |
30,000 |
Matangazo/usafiri |
60,000 |
100,000 |
150,000 |
Jumla ya Gharama za kudum |
223,000 |
347,500 |
466,000 |
Faida kabla ya kodi
na riba |
3,033,200 |
4,536,316 |
6,045,756 |
Riba ya mkopo. |
0 |
0 |
0 |
Kodi ya mapato . |
0 |
0 |
0 |
Faida halisi. |
3,033,200 |
4,536,316 |
6,045,756 |
%Faida halisi / mauzo. |
25% |
25% |
25% |
8.4 Makisio ya Mtiririko wa Fedha taslimu
Mtiririko wa fedha
taslimu tofauti na Faida na Hasara huwa unatakiwa kushughulika tu na fedha
taslimu zinazoingia na kutoka kwenye biashara, kwahiyo ikiwa kuna madeni,
malighafi au stoku ya bidhaa ambazo bado hazijauzwa hapa hatuwezi kuziweka
vinginevyo muundo wake unafanana.
Makisio ya Mtiririko wa
fedha yanaingiliana au kuhusiana na makisio ya faida na hasara na pia makisio
ya mizania ya biashara, kwahiyo kuna vitu tunapokuwa tukikokotoa kwenye
mtiririko wa fedha basi moja kwa moja tunakuwa tukikamilisha na baadhi ya vitu
katika jedwali la mizania ya biashara. Hivyo ni lazima ripoti zote 3 zihusike
Tunaanza kwa kutumia namba
zetu za jedwali la kwanza kabisa la kianzio au mizania ya biashara ya kuanzia
(cheki mchanganuo wako Sura ya 2 ya maelezo ya biashara kipengele cha Kianzio,
mizania ya biashara). Hapa ndipo tunapata kianzio chetu cha fedha taslimu
ambacho ni sh. 2,223,150
Ili kupata makisio ya
mtiririko wa fedha mwaka mzima wa 1 tutatafuta kwanza mtiririko wa fedha kwa
mizunguko yote 4 ya mwaka 1 na kisha tutakuja kujumlisha safu mlalo (rows) za
miezi yote 4 kupata makisio ya mwaka 1.
MAKISIO YA MTIRIRIKO WA FEDHA TASLIMU |
||||
Mzunguko1 |
Mzunguko2 |
Mzunguko3 |
Mzunguko4 |
|
FEDHA
INGIA |
TZS |
TZS |
TZS |
TZS |
Kianzio |
2,223,150 |
|||
Mauzo Taslimu |
3,037,200 |
3,037,200 |
3,037,200 |
3,037,200 |
Makusanyo ya deni |
0 |
0 |
0 |
0 |
Mkopo mpya |
0 |
0 |
0 |
0 |
Mauzo ya rasilimali |
0 |
0 |
0 |
0 |
Mtaji mpya |
0 |
0 |
0 |
0 |
Jumla
fedha Ingia |
3,037,200 |
3,037,200 |
3,037,200 |
3,037,200 |
FEDHA TOKA |
||||
Matumizi fedha taslimu |
2,520,000 |
2,320,000 |
2,220,000 |
2,220,000 |
Malipo ya bili |
0 |
0 |
0 |
0 |
Malipo deni la muda mrefu |
0 |
0 |
0 |
0 |
Ununuzi mali za muda mfupi |
0 |
0 |
0 |
0 |
Ununuzi mali za kudumu |
0 |
0 |
0 |
0 |
Utoaji gawio |
0 |
0 |
0 |
0 |
Jumla
ya fedha toka |
2,520,000 |
2,320,000 |
2,220,000 |
2,220,000 |
Mtiririko wa fedha taslimu |
517,200 |
717,200 |
817,200 |
817,200 |
SALIO
LA FEDHA TASLIMU |
2,740,350 |
3,457,550 |
4,274,750 |
5,091,950 |
Kuona majedwali yenye namba zilizokamilika
tafadhali jipatie Semina kamili, mchanganuo wako wa kuku chotara 300 aina ya
kuroiler, Kitabu pamoja na Offa ya michanganuo mingine ya aina mbalimbali.
FEDHA
INGIA
Nitaeleza kila mstari uliolala (rows) nikianza na Fedha
Ingia
1.
Kianzio: Kianzio tunakipata kutoka jedwali letu la mizania ya kuanzia
sh. 2,223,150
2.
Mauzo taslimu: Hizi ni fedha taslimu zinazoingia kwenye
biashara kupitia mauzo taslimu tu ikiwa kuna kiasi umekopesha hakihusiki hapa.
Katika mzunguko wetu wa 1 na hata mizunguko mingine inayofuata tumeona kwenye
jedwali la faida na hasara mauzo yetu ni fedha taslimu sh. 3,037,200 na
hayabadiliki kila mzunguko, hivyo tutaweka kiasi hicho katika kila chumba cha
mzunguko
3.
Makusanyo ya deni
Unakisia ikiwa kama utakopesha wateja watalipa kiasi gani
kila mzunguko. Lakini tumeona jedwali letu la faida na hasara hakutakuwa na
mauzo ya mkopo na hivyo hakutakuwa pia na makusanyo ya madeni toka kwa wateja,
hivyo nimeweka ‘0’ pale
4.
Mkopo mpya:
Hakuna mkopo mpya unaotarajiwa
5.
Mauzo ya rasilimali
Hakuna rasilimali zinazotarajiwa kuuzwa
6.
Mtaji mpya
Hakutarajiwi mtaji mpya
FEDHA
TOKA
Kwa upande wa fedha zinazotoka nitaanza na;
1.
Matumizi ya fedha taslimu; Hapa tunatazama jedwali letu la faida
na hasara ni matumizi gani yatakayohitaji kulipiwa fedha taslimu (yasiyo ya
mkopo)
Kwanza kabisa kuna gharama zote zinazobadilika, zile za
kudumu mfano umeme na matangazo isipokuwa uchakavu maana uchakavu hautoi fedha
taslimu (cash) mfukoni, lakini pia kuna kodi na riba. Hapa inabidi tujumlishe
gharama zote hizo katika kila mzunguko
Lakini kitu cha kukumbuka ni kwamba gharama zinazobadilika hutokana na malighafi ambazo nazo hununuliwa kwa fedha taslimu, kwa hiyo tunapaswa kwanza kukadiria kiasi cha malighafi zitakazokuwa zikinunuliwa kila mzunguko mmoja kwani haiwezekani ununue malighafi zinazotosheleza kiasi kamili cha gharama zinazobadilika tu; ni lazima ununue malighafi kiasi kikubwa zaidi ya gharama utakazozitumia, zikibaki unakwenda kuzitumia mzunguko unaofuata.
Jedwali
la kukokotoa kiasi cha malighafi ni hili hapa chini;
Kukadiria
Bidhaa/malighafi. |
Mzung
1 |
Mzung
2 |
Mzung
3 |
Mzung
4 |
|
SH. |
SH. |
SH. |
SH. |
Makadirioya muda wa kukaa na bidhaa
ni miezi 3 |
|
|
|
|
Bidhaa za kuanzia (kutoka kipindi
kilichopita) |
0 |
276,850 |
353,700 |
330,550 |
+Ununuzi bidhaa/malighafi. |
2,500,000 |
2,300,000 |
2,200,000 |
2,200,000 |
-Matumizi(gharama zinazobadilika) |
2,223,150 |
2,223,150 |
2,223,150 |
2,223,150 |
Salio la bidhaa mzunguko huu |
276,850 |
353,700 |
330,550 |
307,400 |
1.
Penye bidhaa za kuanzia mzunguko wa 1
unatazama mizania ya kuanzia utaona hatukuwa na kitu hivyo weka 0
2.
Ununuzi wa malighafi kwa fedha taslimu
mzunguko huohuo wa 1 tukadirie sasa tutanunua malighafi kiasi gani. Kwa kuwa
tumesema malighafi ni lazima zizidi kidogo gharama zinazobadilika hivyo
tutaweka pale kiasi kikubwa kuliko sh. 2,223,150 ambacho mimi nilikadiria sh.
2,500,000
3.
Matumizi au gharama zinazobadilika, hizi
zinajulikana za mizunguko yote 4 kwamba ni sh. 2,223,150 kila mzunguko kutokana
na jedwali letu la faida na hasara.
4.
Hivyo ili kupata salio la malighafi mwishoni
mwa mzunguko wa 1 tunachukua
Malighafi za kuanzia jumlisha + Ununuzi wa malighafi Toa
–Matumizi/ghara zinazobadilika
=0 + 2,500,000 – 2,223,150 = 276,850
Kwahiyo katika mzunguko wa 1 utaona kwamba fedha taslimu
zilizotumika ni hizi za kununulia malighafi sh. 2,500,000 lakini pia kuna sh.
5,000 za umeme na sh. 15,000 za matangazo jumla zote ni, 2,500,000 + 15,000 +
5000 = 2,520,000
Katika mzunguko wa pili wa tatu na wanne napo unachukua
matumizi yake ya fedha taslimu zitakazonunua malighafi kisha unajumlisha umeme
na matangazo ambazo ni sh. elfu 5 na elfu 20 unapata jumla ya fedha zote
zitakazotoka katika jedwali lako la mtiririko wa fedha taslimu.
Hili jedwali la kukisia
Malighafi linasaidia moja kwa moja kufahamu salio la malighafi katika kila
mzunguko ambacho ni kipengele kilicho kwenye jedwali la mizania ya biashara,
ndio maana nikasema awali kuwa unapokuwa ukikokotoa baadhi ya vipengele kwenye
jedwali la mtiririko wa fedha basi moja kwa moja unakuwa ukikamilisha na baadhi
ya vipengele kwenye Mizania ya biashara.
Mistari mingine inayofuata
katika Fedha toka ni,
2.
Malipo ya bili:
Hapa ningejaza kama biashara
ingekuwa inatazamia kulipa madeni ya wasambazaji kwa fedha taslimu lakini
katika biashara hii hatutakopa malighafi mahali
3.
Malipo ya deni la muda mrefu:
Hili nalo hakuna kwani
biashara haijaonyesha kama itakopa fedha mahali
4.
Ununuzi wa mali za muda mfupi
Pia hakuna
5.
Ununuzi wa mali za kudumu
Katika mwaka mzima wa 1
hakuna mali za kudumu zitakazonunuliwa zaidi ya zile za kuanzia ila kwa miaka 2
inayofuata wa 2 na wa 3 utaona ongezeko la mabanda na vifaa ambavyo vyote ni
mali za kudumu.
Mpaka hapo sasa unajumlisha
na kupata jumla ya fedha zote zinazotoka.
Kisha unachukua jumla ya
fedha Ingia na kutoa jumla ya fedha toka kupata Mtiririko wa fedha taslimu.
Baada ya hapo unachukua
kianzio na kujumlisha mtiririko wa fedha taslimu katika kila mzunguko ili
kupata salio la fedha taslimu mwishoni mwa kila mzunguko. Na hapo sasa ndio
unakuwa umemaliza jedwali lako la Mtiririko wa fedha taslimu kwa mizunguko yote
minne
Mzunguko
wa fedha taslimu kwa mwaka 1
Hapa tunafanya kama kwenye lile jedwali la faida na
hasara kwa kujumlisha safu zote zilizolala (rows) kupata safu iliyosimama
(column) itakayowakilisha Mzunguko wa fedha taslimu kwa mwaka wa 1.
Kuona jedwali hili kamili jipatie
semina na mchanganuo wako kamili. Unapata na offa ya vitu 6 (Michanganuo na
Kitabu) muda huohuo bila kuchelewa
Kabla ya kwenda kutazama
mwaka wa 2 na wa 3 hebu kwanza tukamilishe pia na makisio ya Mizania ya
biashara kwa mizunguko 4 na mwaka wa kwanza kwani tumesema unapokamilisha
mtiririko wa fedha moja kwa moja na mizania unakuwa pia umekamilisha.
8.5
Makisio ya Mizania ya Biashara
Unapokisia mizania ya
biashara katika miezi au mizunguko ya mwaka wa 1 unaanza na Mizania ya mwanzo
kutoka kule kwenye kianzio, unatumia pia jedwali la faida na hasara pamoja na
jedwali la Mtiririko wa fedha taslimu kwa kuongeza au kupunguza katika
vipengele vya jedwali hilo la mizania ya kuanzia.
Safu nilizoweka namba kwa rangi ya blue zote ni safu ambazo tayari namba zake unakuwa nazo ikiwa umeshamaliza kutengeneza ripoti za faida na hasara na mtiririko wa fedha katika mizunguko ya mwaka wa 1, kwa hiyo unazipachika tu kisha nyingine unazikokotoa
MAKISIO YA MIZANIA YA BIASHARA |
|||||
Kianzio |
Mzung.1 |
Mzun.2 |
Mzung.3 |
Mzung.4 |
|
TZS |
TZS |
TZS |
TZS |
TZS |
|
RASILIMALI |
|||||
Mali za muda mfupi |
|||||
Fedha
taslimu |
2,223,150 |
2,740,350 |
3,457,550 |
4,274,750 |
5,091,950 |
Wadaiwa |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Malighafi |
0 |
276,850 |
353,700 |
330,550 |
307,400 |
Mali
nyinginezo za muda mfupi |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Jumla mali za muda mfupi |
2,223,150 |
3,017,200 |
3,811,250 |
4,605,300 |
5,399,350 |
Mali za kudumu |
1,840,000 |
1,840,000 |
1,840,000 |
1,840,000 |
1,840,000 |
Uchakavu
uliolimbikizwa |
0 |
35,750 |
71,500 |
107,250 |
143,000 |
Jumla ya mali za kudumu |
1,840,000 |
1,804,250 |
1,768,500 |
1,732,750 |
1,697,000 |
JUMLA YA RASILIMALI ZOTE |
4,063,150 |
4,821,450 |
5,579,750 |
6,338,050 |
7,096,350 |
MTAJI NA DENI |
|||||
Wadai |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Mkopo
wa muda mfupi |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Mkopo
wa muda mrefu |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Jumla ya Deni lote |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Mtaji uliowekezwa |
4,063,150 |
4,063,150 |
4,063,150 |
4,063,150 |
4,063,150 |
Faida
iliyolimbikizwa |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
Faida |
0 |
758,300 |
1,516,600 |
2,274,900 |
3,033,200 |
Jumla
ya Mtaji |
4,063,150 |
4,821,450 |
5,579,750 |
6,338,050 |
7,196,350 |
JUMLA YA MTAJI NA DENI |
4,063,150 |
4,821,450 |
5,579,750 |
6,338,050 |
7,096,350 |
RASILIMALI
1. Fedha
Taslimu;
Katika safu hii ya mwanzo kabisa, namba zake unazitoa
kwenye lile jedwali la mtiririko wa fedha taslimu kwenye salio la fedha taslimu
pale chini kabisa, unakopi za mizunguko yote na kuweka hapa
2.
Wadaiwa:
Katika biashara hii hatuna wadaiwa wowote
3. Malighafi:
Tunaenda moja kwa moja kwenye jedwali letu tulilokadiria
malighafi tunachukua salio la malighafi katika kila mwisho wa mzunguko na kuja
kupachika hapa.
4. Mali
nyinginezo za muda mfupi:
Hatuna katika biashara hii
6.
Mali za kudumu
Unaangalia kwenye kianzio ni shilingi ngapi kisha unaweka
kiasi hicho kwenye kila mzunguko kwa mfano sisi hapa ilikuwa ni sh. 1,840,000
7.
Uchakavu uliolimbikizwa
Limbikizo la Uchakavu linapunguza thamani ya mali za
kudumu, uchakavu wa mzunguko huu ni limbikizo la uchakavu wa mzunguko uliopita
+ na wa mzunguko huu kutoka katika jedwali la faida na hasara ukianzia pale
kwenye kianzio
8.
Jumla ya Mali za kudumu
Hii ni baada ya kutoa uchakavu kwenye mali za kudumu
katika kila mzunguko.
9.
Jumla ya Rasilimali zote
Unajumlisha mali za muda
mfupi na zile za kudumu
DENI NA MTAJI
Deni:
1.
Wadaiwa
Upande wa pili tunaanza na
Wadaiwa lakini biashara hii haina wadaiwa
2.
Mkopo wa muda mfupi
Pia hatuna mkopo wa muda
mfupi
3.
Mkopo wa muda mrefu
Nao hatuna katika biashara
hii
4.
Jumla ya Deni
Hakuna
tunaweka 0
Mtaji:
5.
Mtaji uliowekezwa
Hapa tunaangalia kwenye kianzio na namba tunayoikuta pale
mfano sisi ni, 4,063,150 inawekwa
kwenye kila mzunguko
6.
Faida iliyolimbikizwa
Tunaangalia kwenye kianzio na kuweka namba zake katika
kila mzunguko, hii hubadilika mara moja tu kwa mwaka kwa kuongeza faida
iliyopatikana kwa mwaka.
7. Faida
Hii
tunaitoa moja kwa moja kutoka jedwali la faida na hasara, ni malimbikizo ya
faida inayopatikana katika kila mzunguko
8. Jumla ya Mtaji:
Unajumlisha
kuanzia pale namba 5 +6 +7 = jibu unapata la kila mzunguko
9. Jumla Deni na Mtaji:
Hapa
unajumlisha deni na mtaji ambapo thamani yake kimahesabu ikiwa upo sahihi ni
lazima ilingane na namba zilizoko kwenye Jumla
ya Rasilimali zote upande ule wa kwanza kule juu ya hili jedwali.
Makisio ya Mizania ya biashara mwaka wa
1
Tofauti
na ilivyokuwa kwenye jedwali la Faida na Haasara na lile la Fedha Taslimu, kwa
upande wa hili la Mizania, namba za kukamilisha mali na madeni ya mwaka wa
kwanza hatujumlishi namba za safu zilizolala kwenye mizunguko yote 4 hapana,
bali tunachokifanya ni kuchukua safu nzima iliyosimama/column ya mzunguko wa
mwisho(wa 4) na kuifanya ndiyo namba za mwaka wa 1
Makisio ya Mizania ya biashara Miaka 2
inayofuata
Kwenye
jedwali lifuatalo vyumba nilivyoweka namba kwa rangi
ya bluu maana yake tayari thamani yake inajulikana kutokana na majedwali
yaliyokwishakamilika aidha lile la faida na hasara, mizania ya kuanzia au
mtiririko wa fedha taslimu mwaka wa kwanza.
Rangi
ya kijani ni namba zinazohitaji kukokotolewa
lakini kwa kutumia kanuni iitwayo asilimia ya mauzo%.
Vyumba
nilivyowekwa rangi nyekundu ni namba
zinazohitaji kukokotolewa kutokana na namba zilizokwishawekwa kwenye hili
jedwali.
1. Namba za mwaka wa kwanza
(Safu iliyosimama) tayari tulishaipata kutokana na jedwali la mizania la
mizunguko 4
2. Mtaji uliowekezwa sh.
4,063,150 tunaupata toka kwenye jedwali la mizania ya kuanzia na huwekwa katika
safu nzima kwa miaka yote 3 pasipo kubadilika
3. Faida:
Hizi ni faida kutoka katika kila mwaka ambazo tayari tunazipata kwenye jedwali
la Faida na hasara la miaka 3.
4. Faida iliyolimbikizwa;
Faida iliyolimbikizwa mwaka huu ni malimbikizo ya faida ya miaka iliyopita
5. Deni:
Katika biashara hii hakuna deni lolote hivyo tunaweka 0 katika kila chumba cha
deni
6. Jumla ya Mtaji na Deni:
Tunajumlisha jumla ya mtaji na jumla ya deni vitu ambavyo tayari tunavyo ingawa
deni ni sifuri(0).
7. Jumla ya Rasilimali zote: Kwa
kuwa ipo kanuni isemayo Jumla ya
rasilimali zote = Jumla ya Deni na Mtaji basi tunahamisha safu ya jumla ya
Deni na Mtaji kama ilivyo mpaka kwenye safu ya Jumla ya Rasilimali zote.
8. Mali za kudumu
Zinajulikana
kutokana na jedwali la Mizania ya kuanzia na hubadilika tu pale unaponunua mali
nyingine au kuuza, sisi hapa mwaka wa 2 na wa 3 kuna mali za kudumu
ziliongezeka yakiwemo mabanda na vifaa.
9. Uchakavu ni limbikizo la uchakavu kila
mwaka ambapo mwaka wa pili unachukua uchakavu mwaka wa 1 kwenye faida na hasara
unajumlisha na uchakavu mwaka wa pili kwenye faida na hasara mwaka wa pili,
mwaka wa 3 ni hivyohivyo.
10. Jumla ya mali za kudumu:
Unachukua mali za kudumu unatoa limbikizo la uchakavu.
11. Jumla ya mali za muda mfupi:
Tunazipata kwa kuchukua jumla ya Rasilimali zote na kutoa jumla ya mali za muda
mrefu vitu ambavyo tayari vipo.
12. Fedha Taslimu mwaka wa 2 na wa 3,
Tutatumia kanuni ya asilimia ya mauzo% kwa kuchukua thamani ya fedha taslimu
mwaka wa 1 na kugawa kwa mauzo ya mwka wa kwanza kisha uwiano tunaopata
tunauzidisha mara mauzo mwaka wa pili. Na mwaka wa tatu ili kupata salio la
fedha taslimu katika miaka hiyo.
13. Malighafi; Tunachukua jumla ya mali za muda mfupi na kutoa kiasi cha fedha taslimu na hapo tunakuwa tayari tumekamilisha jedwali letu la Makisio ya mizania ya biashara kwa miaka yote 3
Makisio
ya mizania ya biashara |
|||
Mw1 |
Mw2 |
MW3 |
|
TZS |
TZS |
TZS |
|
RASILIMALI |
|||
Mali za muda mfupi |
|||
Fedha
taslimu |
5,091,950 |
7,637,925 |
10,183,900 |
Wadaiwa |
0 |
0 |
0 |
Malighafi |
307,400 |
1,580,241 |
4,461,022 |
Mali
nyinginezo za muda mfupi |
0 |
0 |
0 |
Jumla mali za muda mfupi |
5,399,350 |
9,218,166 |
14,644,922 |
Mali za kudumu |
1,840,000 |
2,775,000 |
3,680,000 |
Uchakavu |
143,000 |
360,500 |
646,500 |
Jumla ya mali za kudumu |
1,697,000 |
2,414,500 |
3,033,500 |
JUMLA YA RASILIMALI ZOTE |
7,096,350 |
11,632,666 |
17,678,422 |
MTAJI NA DENI |
|||
Wadai |
0 |
0 |
0 |
Mkopo
wa muda mfupi |
0 |
0 |
0 |
Mkopo
wa muda mrefu |
0 |
0 |
0 |
Jumla ya Deni lote |
0 |
0 |
0 |
Mtaji uliowekezwa |
4,063,150 |
4,063,150 |
4,063,150 |
Faida
iliyolimbikizwa |
0 |
3,033,200 |
7,569,516 |
Faida |
3,033,200 |
4,536,316 |
6,045,756 |
Jumla
ya Mtaji |
7,096,350 |
11,632,666 |
17,678,422 |
JUMLA YA MTAJI NA DENI |
7,096,350 |
11,632,666 |
17,678,422 |
Mzunguko wa fedha taslimu kwa miaka 2 inayofuata
Baada ya kukamilisha majedwali ya Mizania ya biashara na Faida
na Hasara miaka yote 3 sasa ni rahisi sana kukamilisha na hili la mzunguko wa
fedha kwani kama nilivyotangulia kusema ripoti hizi tatu pamoja na mizania ya
kuanzia zinaingiliana na kutegemeana.
Nitaanza kutaja vitu ambavyo tayari tunavyo kulingana na majedwali
hayo mengine matatu na hapo chini nimevitia rangi ya bluu;
1.
Mwaka wa 1 safu iliyosimama (column) tuliipata toka jedwali la
mtiririko wa fedha taslimu jumla ya mizunguko ile 4
2.
Kianzio tumekipata jedwali la mizania ya biashara la kianzio
3.
Mauzo taslimu, haya tunayapata kutoka jedwali la faida na
hasara la miaka 3
4.
Ununuzi wa mali za kudumu; Kutoka jedwali la Mizania ya biashara
mali za kudumu zililipiwa fedha taslimu (cash)
Kisha nitafuata vitu tutakavyokokotoa, nimeviwekea rangi ya
kijani;
5.
Jumla ya fedha Ingia: Tunachukua mauzo taslimu kama yalivyo kwani
ndiyo pesa taslimu pekee inayoingia kwenye biashara
6.
Mtiririko wa fedha taslimu: Kwa kutumia salio la fedha taslimu
mwishoni na kianzio cha fedha taslimu mwanzoni ambavyo tayari vyote tunavyo
tunaweza kukokotoa mtririrko wa fedha katika mwaka wa pili na watatu kama
ifuatavyo;
Mwaka wa pili: Salio la fedha taslimu mwaka wa1 +
Mtiririko wa fedha mwaka wa 2 = salio la fedha taslimu mwaka wa 2
=5,091,950 + y = 7,637,925
y =salio la fedha taslimu mwaka wa 1
y = 7,637,925 – 5,091,950
y =
2,545,975
Mwaka wa tatu: Salio la fedha taslimu mwaka wa 2 +
Mtiririko wa fedha mwaka wa 3 = salio la fedha taslimu mwaka wa 3
Y =Mtiririko wa fedha mwaka wa 3
7,637,925 + Y = 10,183,900
Y =
2,545,975
7. Jumla ya Fedha
Toka: Tutachukua Jumla ya Fedha Ingia –toa Mtiririko wa fedha kama
ifuatavyo;
Mwaka wa pili:
= 18,223,200 -
2,545,975 = 15,677,225
Mwaka wa tatu:
= 24,297,600 -
2,545,975 = 21,751,625
8.
Matumizi ya fedha taslimu: Jumla ya Fedha toka – toa ununuzi wa
mali za kudumu kama ifuatavyo;
Mwaka wa 2:
= 15,677,225 - 935,000 = 14,742,225
Mwaka wa 3:
= 21,751,625 - 905,000 = 20,846,625
Mpaka hapo tayari tumekamilisha jedwali letu la Makisio
ya Mtiririko wa fedha kwa miaka yote 3 kama linavyoonekana hapo chini;
NB:
Kumbuka tu kwamba, hapa maeneo mengi sijatumia kanuni maalumu bali nimekokotoa
tu baadhi ya safu kulingana na uwepo tayari wa namba katika safu nyinginezo
kutoka majedwali yaliyokwishakamilika huko nyuma.
Makisio ya Mtiririko wa fedha
taslimu |
|||
Mw1 |
Mw2 |
MW3 |
|
FEDHA
INGIA |
TZS |
TZS |
TZS |
Kianzio |
2,223,150 |
||
Mauzo Taslimu |
12,148,800 |
18,223,200 |
24,297,600 |
Makusanyo ya deni |
0 |
||
Mkopo mpya |
0 |
||
Mauzo ya rasilimali |
0 |
||
Mtaji mpya |
0 |
||
Jumla
fedha Ingia |
12,148,800 |
18,223,200 |
24,297,600 |
FEDHA
TOKA |
|||
Matumizi fedha taslimu |
9,280,000 |
14,742,225 |
20,846,625 |
Malipo ya bili |
0 |
||
Malipo deni la muda mrefu |
0 |
||
Ununuzi mali za muda mfupi |
0 |
||
Ununuzi mali za kudumu |
0 |
935,000 |
905,000 |
Utoaji gawio |
0 |
||
Jumla
ya fedha toka |
9,280,000 |
15,677,225 |
21,751,625 |
Mtiririko wa fedha taslimu |
2,868,800 |
2,545,975 |
2,545,975 |
SALIO
LA FEDHA TASLIMU |
5,091,950 |
7,637,925 |
10,183,900 |
8.6 Sehemu muhimu za biashara
Kipengele hiki kinahusu uwiano wa sehemu mbali mbali za
biashara kutoka katika makisio ya ripoti zetu tatu kwa miaka 3. Hapa kunakuwa
na jedwali ambalo unaweka uwiano wa zile sehemu muhimu. Kwa kawaida kuna uwiano
wa aina nyingi lakini siyo lazima uweke kila mmoja hapa.
Katika jedwali kwenye huu mchanganuo tuliweka baadhi tu
ya sehemu hizo. Unaweza kupata kanuni/formula za kukokotoa sehemu mbalimbali
kutoka katika kitabu chako cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI ukurasa
ule wa 129
Jedwali: Sehemu muhimu za biashara
Tathmini ya Sehemu za
biashara |
Mw1 |
Mw2 |
MW3 |
Ukuaji
wa mauzo |
n.a. |
50% |
33.3% |
|
|
|
|
Asilimia
ya mauzo |
|
|
|
Mauzo |
100% |
100% |
100% |
Faida ghafi (Gross margin) |
26.8% |
26.8% |
26.8% |
Jumla ya gharama za
uendeshaji |
1.84% |
1.90% |
1.91% |
Faida halisi (Net profit
margin) |
25% |
25% |
25% |
|
|
|
|
Asilimia
ya Mali zote |
100% |
100% |
100% |
Mauzo |
171% |
157% |
137% |
Wadaiwa |
n.a. |
n.a. |
n.a. |
Malighafi/Bidhaa |
4.3% |
13.5% |
25% |
Mali za muda mfupi |
76% |
79% |
83% |
Mali za kudumu. |
24% |
21% |
17% |
Mtaji |
100% |
100% |
100% |
|
|
|
|
Sehemu
nyinginezo. |
|
|
|
Uwiano sasa (current
ratio) |
n.a. |
n.a. |
n.a. |
Uwiano haraka (Quick
ratio) |
n.a. |
n.a. |
n.a. |
Faida/Mtaji (ROI) |
43% |
39% |
34% |
Faida/Rasilimali (ROA) |
43% |
39% |
34% |
Inventory Turnover |
58 |
14 |
6 |
Mtaji endeshi (Net Working
capital) |
5,399,350/= |
9,218,166/= |
14,644,922/= |
8.7
Muda wa mradi kurudisha mtaji (Pay Back Period)
Pay back period ni kukokotoa
muda unaotakiwa ili kurudisha mtaji wa awali uliowekezwa kwenye biashara/mradi.
Kanuni yake unachukua Mtaji uliowekezwa kisha unagawanya kwa faida (Faida
inayoingia kwenye biashara kwa mwaka) ikiwa faida hiyo inalingana kila mwaka
Lakini utakuta kwa mfano
biashara yetu hii faida inayoingia hutofautiana kila mwaka katika miaka 3 (Uneven profit) hivyo hatuwezi tu
tukasema pay back period = Mtaji/Faida halisi.
Tutatumia jedwali lifuatalo
kukokotoa pay back period yenye faida zinazopishana kila mwaka (uneven profit)
Mwaka |
Faida |
Faida inayolimbikizwa (cumulative
profit) |
0 |
(4,063,150) |
(4,063,150) |
1 |
3,033,200 |
(1,029,950) |
2 |
4,536,316 |
3,506,366 |
3 |
6,045,756 |
9,552,122 |
Mwaka ‘0’ hakuna faida
inayoingia isipokuwa kuna fedha inayowekezwa kwenye mradi sh. (4,063,150) ndio maana ikawekewa alama - hasi
ikimaanisha inadaiwa haijarudi bado
Kwenye faida iliyolimbikizwa
(Cumulative profit) mwaka ‘0’ pia ni
deni lilelile la mtaji uliowekezwa
Mwaka wa 1 kuna faida sh.
3,033,200 inaingia, kwenye faida limbikizi kiasi hicho kitakwenda kupunguza
deni la mtaji na mtaji utabaki ukidaiwa sh. (1,029,950)
Mwaka wa 2 kuna faida sh.
4,536,416 inaingia ambapo katika faida limbikizi itakwenda kufuta kabisa lile
deni la mtaji sh. (1,029,950) na kuendelea
kubakia limbikizo la faida chanya kiasi cha sh. 3,506,366
Sasa
kanuni ya kukokotoa pay back period inasema hivi;
= Namba ya miaka yenye
limbikizo la faida hasi + (Limbikizo la mwisho lenye alama hasi / Faida ya
mwaka unaofuata
Namba ya miaka yenye
limbikizo la faida hasi (A) = 1
Limbikizo la mwisho lenye
alama hasi (B) = 1,029,950
Faida ya mwaka unaofuata (C)
= 4,536,316
Pay back period
= A + B/C
= 1 +1,029,950/4,536,316
= 1 + 0.23
= miaka, 1.227
Sawa
na Mwaka 1 na miezi 3
Kwa hiyo mtaji wa biashara
hii au gharama zote za kuanzisha biashara zitarudi baada ya mwaka 1 na miezi 3
Na hapa ndiyo mwisho wa
kipengele cha Mpango wa fedha, karibu kipengele kingine na cha mwisho cha
Viambatanisho
9.0 Viambatanisho
Katika kipengele hiki cha Viambatanisho au vielelezo mimi
nimeweka tu Majedwali ya hesabu kwa undani kila mzunguko wa wiki 12, laini kuna
vitu vingi unaweza kuambatanisha ambavyo huwezi ukaviweka ndani ya mchanganuo
wako
Ningeliweza pia kuweka, mikataba ya biashara CPPC iliyofanya
na wadau wake mbalimbali, picha na ramani, kopi za matangazo, CV za viongozi,
nyaraka za dhamana za mikopo, nyaraka za utafiti uliofanyika nk.
SOMA NA HIZI HAPA;
1. Kuku ni utajiri: angalia mchanganuo jinsi kuku wa mayai
wanavyoweza kukutajirisha haraka
2. Ufugaji bora wa kuku wa mayai: mchanganuo wa biashara, kuku 1000
3. Soko la sungura tanzania linakua kwa kasi kuliko uzalishaji
wenyewe
4. Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya
biashara yako
5. Ujenzi wa mabanda ya kuku isiwe kikwazo cha wewe kuanzisha
biashara ya ufugaji wa kuku
6.
Utajuaje kama biashara yako ya ufugaji wa kuku itakupa faida?
0 Response to "SEMINA SEHEMU YA 5: MCHANGANUO, UFUGAJI WA KUKU CHOTARA WA NYAMA KIBIASHARA – (MPANGO WA FEDHA NA VIAMBATANISHO)"
Post a Comment