Wakati asilimia kubwa ya wanawake nchini Tanzania
wakisitasiata kuanzisha miradi ya ufugaji wa kuku hasa wale chotara wa
kuroiler, wanawake wenzao nchini India na Uganda wanatajirika kwa ufugaji wa
kuku hao na kutoa mchangao mkubwa kwa pato la familia zao na Taifa kwa ujumla.
Ni
kwa vipi wanawake hao wa India na Uganda wanatajirika na ufugaji wa kuku
chotara aina ya kroiler?
Kabla hatujaenda kujua hasa ni jinsi gani wanawake hao
wanavyotajirika kupitia ufugaji wa kuku chotara wa kuroiler ni vizuri kwanza
tukaufahamu Mfumo wa Kiubunifu (Innovative
Mode) uliobuniwa na kampuni ya Keggfarms, waanzilishi wa kuku wa kuroiler,
na ni jinsi gani unavyofanya kazi mpaka Umoja wa Mataifa kuutunukia tuzo.
Mfumo bunifu wa kampuni ya Keggfarms ni tofauti na wa
kipekee ukilinganisha na mifumo mingine sokoni kutokana na sababu kubwa kwamba,
kwanza umetengenezwa kwa kuzingatia shughuli na mazingira ya mwanamke.
Kwa mfano kuku wa kuroiler wenyewe wanaweza kuishi kwa
kutegemea mabaki ya vyakula kutoka jikoni na shambani, yote hayo yakiwa ni
mazingira yanayomhusu mwanamke moja kwa moja.
Kwa kuzingatia vigezo vingi vinavyowahusu wanawake
wamewawezesha siyo tu wanawake wa mijini bali na hata wale wa vijijini.
Kitu kingine cha kipekee kwenye mfumo huu ni mnyororo
wake wa thamani ambao nao pia huutofautisha na mifumo mingine kwa kuhakikisha
wadau wote katika mnyororo kila mmoja anapata faida yake jambo linaloufanya
mfumo kuwa endelevu na wenye kutanuka kwa urahisi.
Mfumo
Bunifu wa ufugaji kuku wa Kuroiler
Kampuni ya Keggfarms ilianza tokea mwaka 1967 nchini
India ikijihusisha na ufugaji wa kuku kwa ujumla kama vile kuku wa nyama
Broilers na kuku wa mayai layers.
Lakini kutokana na ushindani mkubwa toka kwa makampuni ya
nje ikiwa ni pamoja na India kufungua soko lake (uchumi wa soko huria) kampuni
hatimaye iliamua kubadilisha mbinu kwa kubuni bidhaa yake yenyewe mpya sokoni ambayo
ingelikuwa ya kipekee zaidi. Bidhaa hiyo ndiyo hawa kuku wa Kuroiler
tunaoshuhudia leo.
Keggfarms waliunda mfumo huu ufuatao katika mnyororo wao wa
thamani;
1. SHAMBA LA KUKU:
Kampuni ndiyo huhusika na uzalishaji wa mayai na vifaranga na kisha huvipeleka
vifaranga hivyo kwa “Vituo Mama” vilivyotapakaa kote nchini.
2. VITUO MAMA
(Mother Units): Vituo hivi vinajitegemea kwenye faida na humilikiwa na
wajasiriamali binafsi. Kazi yake kubwa ni kutunza vifaranga kwa wiku 2 mpaka 4
na kuwapatia chanjo zote ili kupunguza vifo vya mapema. Kila kituo hutunza
vifaranga kati ya 50 – 2,000 kwa mara moja kisha kuwauza kwa Wasambazaji.
3. WASAMBAZAJI:
Hawa ni wasambazaji wadogowadogo wa vifaranga wajulikanao kama Pheriwallas ambao kazi yao ni kusambaza vifaranga kwa
wafugaji.
4. WAFUGAJI:
Hawa ni wafugaji mmoja mmoja wanaofuga kuku wa kuroiler mpaka muda wa kuuza kwa
walaji.
5. KAYA NA SOKO LA
KUROILER: Hawa ndio walaji wa mwisho katika mnyororo wa thamani.
Wadau wote kuanzia kampuni ya Keggfarms, Vituo Mama,
Wasambazaji na Wafugaji kila mmoja hupata faida yake.
Mfumo huu wa kampuni ya Keggfarms uliwahi kupewa tuzo
mbalimbali ikiwemo ile ya Business India Innovation Awards ukizingatiwa
uendelevu wake na uwezo wa kuongezeka.
Matokeo
ya Mfumo Huu.
Ufugaji wa wa kuku chotara wa kuroiler kwa kutumia mfumo
huu umewahamasisha sana Wanawake nchini India kupitia kuwapa uelewa mkubwa wa
masoko na mbinu mbalimbali za ujasiriamali.
Sasa hivi wanaweza kulipia gharama mbalimbali za maisha
kama vile ada za watoto shule, matibabu na chakula.
Kutokana na sababu hizo wanawake wanaofuga kuku wa
kuroiler kipato chao kimeongezeka kwa asilimia 60% mpaka 70% ukilinganisha na
wafugaji wa kuku wa asili asilimia 20% mpaka asilimia 30%
Wanawake wanahamasika zaidi kufuga kutokana na mfumo
kurahisisha mikopo ya chakula cha kuku, vifaranga na chanjo.
Ni mbadala wa rasilimali za asili kama misitu: Wanawake wameachana na matumizi ya
rasilimali adimu za misitu kama njia ya kuwapatia vipato na badala yake idara
ya misitu inawasaida katika uundaji wa vikundi kuanzisha miradi endelevu ya
ufugaji wa kuroiler
Umeharibu mnyororo wa Umasikini, Kuroile wamewawezesha
wanawake wazee, wajane na kina mama wasio na waume kuwa na vyanzo imara vya
mapato kutokana na mradi wa kuku kuroiler kutohitaji mtaji mkubwa wa kuanzia.
Mwisho Wanawake wameweza kuunda vikundi kwa lengo la kukutana
na kujadili mambo yao mbalimbali kuhusu miradi yao na hivyo kujiongezea zaidi
maarifa na uwezo. Wapo hata walioweza kuachana kabisa na biashara hatarishi
kama biashara ya usokotaji wa tumbaku na nyinginezo zilizokuwa zikidhuru afya
zao.
Kwa ujumla ufugaji wa kuku kuroiler umewawezesha Wanawake
wengi wa India kiasi cha wengine hata kuwa na uwezo wa kumiliki magari, nyumba
na biashara kubwakubwa.
UGANDA
Mfumo bunifu wa ufugaji wa kuku aina ya Kuroiler baada ya
kutambuliwa rasmi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula FAO, Uganda
miongoni mwa nchi nyingine kadhaa iliamua kuuchukua mfumo huu kwa ajili ya
majaribio. Kauli ya FAO ilisema hivi; “Kwa wastani kaya inayofuga Kuroiler
hupata mapato mara 5 zaidi ya zile kaya zisizofuga kuroiler”
Wanawake wa Uganda kama ilivyokuwa kwa wenzao wa India
hawakukubali kubaki nyuma katika kuchangamkia fursa hii kubwa ya kipato. Sasa
hivi pia makampuni ya kuku na wafugaji kutoka nchi za Kenya na Tanzania nao
wameanza kuichukua tekinolojia hii kutokea nchini Uganda na kuanza kuitumia
katika nchi zao.
Chuo kikuu cha Arizona Marekani katika utafiti wake
ilioufanya waligundua kuwa kuku wa kuroiler huzalisha nyama asilimia 132% zaidi
kuliko kuku wa kienyeji, mayai asilimia 462% zaidi, na asilimia 341% zaidi ya
kipato kuliko kuku wa kienyeji.
................................................
Ndugu msomaji wa makala hii, Katika MSIMU WETU WA KUKU,
hii ni makala ya 4 katika mfululizo wa maudhui yanayohusiana na kuku. Unaweza
kujisomea makala nyingine 3 chini ya makala hii.
Leo pia ni siku ya pili ya Semia ya kuandika Mchanganuo
wa kuku Kuroiler wa nyama likiwa ni Darasa la 3. Katika siku hii tunakwenda
kujifunza vipengele vya; MUHTASARI, BIASHARA & BIDHAA
Unaweza kujiunga na semina hata ikiwa umechelewa kwani
tuna utaratibu wa kuwafundisha wale wote waliochelewa kabla ya muda rasmi wa
darasa. Darasa huanza rasmi saa 3 kamili usiku
Kujiunga na Semina hii, lipia shilingi 10,000/= kupitia
namba zetu 0712202244 au 0765553030 Peter Augustino Tarimo, kwa ajili ya kupata
Kitabu na Mchanganuo kamili wa kuku 300 wa kuroiler. Vitu hivi ni muhimu kwa
ajili ya kufanya rejea.
Ukishalipa tuma ujumbe; “NATAKA SEMINA YA KUROILER NA OFFA
YA VITU 9”
Baada ya hapo nakutumia papo hapo Kitabu, mchanganuo wako
wa kuroiler pamoja na OFFA michanganuo mingine 6 jumla vinakuwa vitu 9
OFFA
HIYO NI HII HAPA CHINI;
1.
Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA
NA UJASIRIAMALI (Page 430)
2. Mchanganuo Mpya: Biashara ya ufugaji wa kuku
chotara wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)
3. Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-kiingereza
4.
Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili
5.
Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili
6.
Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili
7.
Mchanganuo wa Mgahawa wa
chakula (Jane Restaurant)-kiingereza
8.
Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula
(Jane Restaurant) –kiswahili
9.
Kuujiunga Mastermind group (Option/hiyari)
SOMA
NA HIZI HAPA:
1.
Biashara hii watu wengi huidharau
lakini ina faida kubwa na nzuri,mtaji laki 1
2.
Kilichokuwa nyuma ya pazia, ufugaji
kuku wa kienyeji(kuku wa asili).
3.
Kuku wa nyama broilers: kwanini faida
na gharama za ufugaji zinavunja moyo?
4. Biashara ndogo zilizosahaulika: bustani
ndogo ya miwa jijini dar es salaam
5.
Kama una biashara ndogo ya mtaji mdogo,
hizi hapa njia 11 za kuibusti
0 Response to "WANAWAKE WA INDIA NA UGANDA WANAVYOTAJIRIKA NA UFUGAJI WA KUKU CHOTARA WA KUROILER"
Post a Comment