DUKA LA REJAREJA UKITUMIA SILAHA (NYENZO) HIZI 2 UMETOBOA KWA URAHISI SANA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

DUKA LA REJAREJA UKITUMIA SILAHA (NYENZO) HIZI 2 UMETOBOA KWA URAHISI SANA

nyenzo ya kubiringisha jiwe

Binadamu tangu kuumbwa kwa Dunia hii amekuwa ni kiumbe anayetafuta kila njia yenye uwezekano wa kurahisisha maisha yake. Katika kusaka urahisi huo ama tuseme mbinu hizo ndipo akajikuta akibuni nyenzo mbalimbali zilizosababisha hatimaye kuja kugundulika mashine na mifumo ya aina kwa aina katika kila nyanja za kimaisha.

Baadhi ya mifano ya nyenzo rahisi binadamu alizoweza kubuni zama hizo za mawe ni kama vile kusugua vijiti viwili mpaka vikasababisha moto kutokea, kubiringisha kitu mfano jiwe kubwa kwa kutumia mti au koleo, kupandisha maji kisimani,  kutumia mawe kama kisu, jembe la kulimia nk. Miaka zaidi ya 5000 kabla ya kuja Kristo inasemekana Wamisri wa kale tayari walikuwa wakitumia aina mbalibali za nyenzo na inasadikiwa hata Mapiramidi ya kale kule Giza kuna aina fulani hivi ya nyenzo iliyotumika kupandisha juu majabali yenye uzito zaidi ya tani 2 na nusu

Mpaka kufikia karne za hivi karibuni binadamu aliweza kufanya mapinduzi makubwa kwenye zile nyenzo rahisi alizobuni hatimaye akaanza kuunda mashine tata zilizokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kurahisisha kazi kwa viwango vya kustaajabisha. Tukashuhudia sasa nyenzo tata kama magari, ndege na mitambo ya kila aina mingine inayojiendesha yenyewe.

Kifupi tu ni kwamba nyenzo ni kitu chochote kinachosaidia kukuza ama kuongeza nguvu inayoingia (Input force) na kutengeneza au kufanya nguvu kubwa zaidi inayotoka (Output force). Hata kwenye biashara tunatumia nyenzo kutengeneza faida kubwa zaidi kutokana na mtaji na nguvu kidogo tunazoweka katika biashara hizo na mfano mzuri sana ni biashara ya duka la rejareja. Katika kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA ukurasa wa 63 kimezungumzia nyenzo muhimu sana mbili (2) ambazo hakuna mtu yeyote aliyeweza kutoboa kirahisi kwa biashara ya duka pasipo kuzitumia.

Nazungumzia kutoboa kwa maana ya kutajirika na si kujikimu kimaisha. Maduka mengi ya rejareja wamiliki wamekuwa wakiyatumia tu kama chanzo cha fedha ndogondogo za kuendeshea familia huku wakiwa na vyanzo vyao vingine vikubwa zaidi vya fedha(mapato) lakini kuna wachache wanaoamua kuyafanya maduka ya rejareja “seriously” ambapo maduka hayo unakuta yanawafanyia pia mambo makubwa sana mfano unakuta mtu anajenga, anamiliki usafiri wa maana na kufanya mambo chungu nzima sawa tu na mtu anayemiliki kampuni kubwa lakini kumbe ni duka tu la rejareja moja au zaidi ya moja.

Sasa unangoja nini usitumie nyenzo hizi mbili? Acha kuhangaika na biashara yako ya rejareja na kulialia kila siku chuma ulete wengi, mara oo..... sijui wachawi......., duka lina faida kidogo sana.......na visingizio tele. Sikatai kweli kuna baadhi ya changamoto na kila moja ina suluhisho lake kama utasoma kitabu hiki vyema, lakini hili la nyenzo wala huna haja ya kumtafuta mchawi kwani mchawi ni wewe mwenyewe hutaki kuzitumia nyenzo hizo 2.

Ikiwa mababu zetu wa zama hizo ambao hata shule hawakwenda waliweza kufikiria na kubuni nyenzo mbalimbali wenyewe kurahisisha maisha yao, leo hii wewe uliesoma kabisa umuhimu wa nyenzo ukiwa darasa la tatu na mifano mwalimu akakuchorea ubaoni unasubiri malaika waje wakukumbushe?

Ikiwa bado huna nakala yako ya kitabu cha Mafanikio ya Duka la rejareja, tuwasiliane sasa hivi kwa namba 0765553030 au 0712202244 na bei ya kitabu ni sh. 6,000/= unapata kitabu ndani ya simu au kompyuta yako. Ukihitaji nakala ngumu ya karatasi unaletewa mpaka ulipo Dar es salaam kwa sh. 16,000/= Mkoa mwingine wowote ni sh. 26,000/= kwa njia ya basi.

Unaweza pia kukinunua kwa kutumia mtandao wako wa simu, bofya hapa kukinunua sasa hivi.

 

 

SOMA NA HIZI HAPA:

1.   Biashara ya Duka inavyoweza kukutoa ukiwa mjanja

2.   Mtaji wa biashara ya duka la rejareja; nianze na shilingi ngapi ili nifanikiwe?

3.   Faida duka la mahitaji ya nyumbani: niweke akiba kiasi gani cha mapato ya siku?

4.   Je, wajua binadamu ni lazima afanye biashara angalao mara moja maishani?

5.   Mbinu hizi 2 za uendeshaji duka la rejareja kwa mafanikio hazipo mahali pengine popote

 

0 Response to "DUKA LA REJAREJA UKITUMIA SILAHA (NYENZO) HIZI 2 UMETOBOA KWA URAHISI SANA"

Post a Comment