Binadamu tangu kuumbwa kwa Dunia hii amekuwa ni kiumbe anayetafuta kila njia yenye uwezekano wa kurahisisha maisha yake. Katika kusaka urahisi huo ama tuseme mbinu hizo ndipo akajikuta akibuni nyenzo mbalimbali zilizosababisha hatimaye kuja kugundulika mashine na mifumo ya aina kwa aina katika kila nyanja za kimaisha.
Baadhi ya mifano ya nyenzo rahisi binadamu alizoweza
kubuni zama hizo za mawe ni kama vile kusugua vijiti viwili mpaka vikasababisha
moto kutokea, kubiringisha kitu mfano jiwe kubwa kwa kutumia mti au koleo,
kupandisha maji kisimani, kutumia mawe
kama kisu, jembe la kulimia nk. Miaka zaidi ya 5000 kabla ya kuja Kristo inasemekana
Wamisri wa kale tayari walikuwa wakitumia aina mbalibali za nyenzo na
inasadikiwa hata Mapiramidi ya kale kule Giza kuna aina fulani hivi ya nyenzo
iliyotumika kupandisha juu majabali yenye uzito zaidi ya tani 2 na nusu
Mpaka kufikia karne za hivi karibuni binadamu aliweza
kufanya mapinduzi makubwa kwenye zile nyenzo rahisi alizobuni hatimaye akaanza
kuunda mashine tata zilizokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kurahisisha kazi kwa
viwango vya kustaajabisha. Tukashuhudia sasa nyenzo tata kama magari, ndege na
mitambo ya kila aina mingine inayojiendesha yenyewe.
Kifupi tu ni kwamba nyenzo ni kitu chochote kinachosaidia
kukuza ama kuongeza nguvu inayoingia (Input
force) na kutengeneza au kufanya nguvu kubwa zaidi inayotoka (Output force). Hata kwenye biashara
tunatumia nyenzo kutengeneza faida kubwa zaidi kutokana na mtaji na nguvu
kidogo tunazoweka katika biashara hizo na mfano mzuri sana ni biashara ya duka
la rejareja. Katika kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
ukurasa wa 63 kimezungumzia nyenzo muhimu sana mbili (2) ambazo hakuna mtu
yeyote aliyeweza kutoboa kirahisi kwa biashara ya duka pasipo kuzitumia.
Nazungumzia kutoboa kwa maana ya kutajirika na si
kujikimu kimaisha. Maduka mengi ya rejareja wamiliki wamekuwa wakiyatumia tu
kama chanzo cha fedha ndogondogo za kuendeshea familia huku wakiwa na vyanzo vyao
vingine vikubwa zaidi vya fedha(mapato) lakini kuna wachache wanaoamua
kuyafanya maduka ya rejareja “seriously” ambapo
maduka hayo unakuta yanawafanyia pia mambo makubwa sana mfano unakuta mtu
anajenga, anamiliki usafiri wa maana na kufanya mambo chungu nzima sawa tu na
mtu anayemiliki kampuni kubwa lakini kumbe ni duka tu la rejareja moja au zaidi
ya moja.
Sasa unangoja nini usitumie nyenzo hizi mbili? Acha
kuhangaika na biashara yako ya rejareja na kulialia kila siku chuma ulete
wengi, mara oo..... sijui wachawi......., duka lina faida kidogo sana.......na
visingizio tele. Sikatai kweli kuna baadhi ya changamoto na kila moja ina
suluhisho lake kama utasoma kitabu hiki vyema, lakini hili la nyenzo wala huna
haja ya kumtafuta mchawi kwani mchawi ni wewe mwenyewe hutaki kuzitumia nyenzo
hizo 2.
Ikiwa mababu zetu wa zama hizo ambao hata shule
hawakwenda waliweza kufikiria na kubuni nyenzo mbalimbali wenyewe kurahisisha
maisha yao, leo hii wewe uliesoma kabisa umuhimu wa nyenzo ukiwa darasa la tatu
na mifano mwalimu akakuchorea ubaoni unasubiri malaika waje wakukumbushe?
Ikiwa bado huna nakala yako ya kitabu cha Mafanikio ya Duka la rejareja,
tuwasiliane sasa hivi kwa namba 0765553030 au 0712202244 na bei ya kitabu ni
sh. 6,000/= unapata kitabu ndani ya simu au kompyuta yako. Ukihitaji nakala
ngumu ya karatasi unaletewa mpaka ulipo Dar es salaam kwa sh. 16,000/= Mkoa
mwingine wowote ni sh. 26,000/= kwa njia ya basi.
Unaweza pia kukinunua kwa kutumia mtandao wako wa simu, bofya hapa kukinunua
sasa hivi.
SOMA
NA HIZI HAPA:
1.
Biashara ya Duka inavyoweza kukutoa ukiwa mjanja
2. Mtaji wa biashara ya duka la rejareja; nianze na shilingi ngapi ili nifanikiwe?
3. Faida duka la mahitaji ya nyumbani: niweke akiba kiasi gani cha
mapato ya siku?
4. Je, wajua binadamu ni lazima afanye biashara angalao mara moja
maishani?
5. Mbinu hizi 2 za uendeshaji duka la rejareja kwa mafanikio
hazipo mahali pengine popote
0 Response to "DUKA LA REJAREJA UKITUMIA SILAHA (NYENZO) HIZI 2 UMETOBOA KWA URAHISI SANA"
Post a Comment