FEDHA ZA KUWEKA AKIBA UTAZIPATA WAPI WAKATI HUNA KAZI WALA BIASHARA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

FEDHA ZA KUWEKA AKIBA UTAZIPATA WAPI WAKATI HUNA KAZI WALA BIASHARA?

uwekaji wa akiba

Kama ilivyokuwa kwangu mimi ndugu msomaji, bila shaka yeyote najua na kwako pia kwa muda mrefu umekuwa ukipata msisitizo mkubwa kuhusiana na dhana nzima ya kuweka akiba sehemu fulani ya fedha unazopata kila siku. Uwekaji akiba hakuna mtu anayeweza kupinga kuwa ndiyo msingi mkuu wa mtu kuja siku moja kuufikia uhuru wake wa kifedha. 

Lakini watu wengi sana wanajikuta kwenye mtanziko mkubwa pale wanapokuwa wakijiuliza swali hili mara kwa mara, Je, nitaweza vipi kuweka akiba wakati sina chanzo chochote kile cha fedha kama kazi/ajira wala biashara?

Akiba ndiyo fedha unayoweza kuja kuitumia katika uwekezaji kwenye miradi ya kibiashara iliyo na uwezo wa kuingiza faida, kwa maneno mengine badala ya kuendelea kuiweka akiba hiyo unaamua sasa kuifanya izae na kuongezeka mithili ya mmea, unapopanda mazao shambani mbegu hazijai hata kwenye kisado lakini zikikua zinakuja kuzaa magunia kwa magunia ya mazao.

Fedha za kuweka akiba utazipata wapi sasa?

Ukiuliza fedha za kuweka akiba unazipata wapi ni sawa na mtu anayeuliza mtoto mdogo anapozaliwa atapata wapi chakula wakati amezaliwa bila ya chochote. Tuachane kwanza na mtu ambaye keshamaliza zake shule au chuo ama ni mtu mzima zaidi ya hata miaka 18 yupo zake mtaani na anajiuliza swali hili. Kimsingi kabisa binadamu tunapaswa mara tu tunapozaliwa hivi tukiwa watoto wachanga tuanze kujiwekea akiba ya fedha kidogokidogo na hili linawezekana.

Hebu fikiria kwa mfano tokea siku wewe umezaliwa ingelikuwa unaweka akiba hata ya shilingi moja kila siku mpaka sasa hivi ungelikuwa na shilingi ngapi?. Unaweza ukaniuliza swali jingine, “Sasa itawezekanaje mtoto wa siku moja kujiwekea akiba wakati anasaidiwa kila kitu na wazazi wake?

Jibu ni kwamba matumizi yaleyale mtoto anayotumia, mzazi afanye juu chini kumega hapo kiasi kidogo na kumwekea akiba mpaka atakapokuja kujitambua mwenyewe. Badala ya kumnunulia beseni la elfu 50 nunu la elfu 30 ishirini mdumbukizie kwenye kibubu, akaunti maalumu au ‘whatever’ ulichoamua kumuwekea akiba zake humo akikua atazikuta.

Unajua ukishazaliwa tu hivi unaanza kuingiza kipato hata ikiwa siyo kwa njia ya moja kwa moja. Kipato cha pesa siyo lazima kitokane tu na ajira au biashara, kuna ruzuku, zawadi, misaada, hii yote ni aina za vipato mtu anapata katika nyakati mbalimbali za maisha yake ukiachilia mbali kazi na biashara.

Nimetolea mfano wa mtoto aliyezaliwa leo lakini kuna wanafunzi wanapata ruzuku za aina mbalimbali ikiwemo ‘pocket money’. Mwanafunzi mjanja anaweza kumega kiasi fulani kutoka katika fedha anazogaiwa na wazazi/walezi wake au boom kwa wale wanavyuo, akajibana kidogo na kujiwekea akiba ambayo baadae itakuja kuwa msaada mkubwa kwake.

Sababu kubwa inayotufanya watu tuone suala la uwekaji akiba ni jambo gumu sana ni ile hali ya kutokuwa na NIDHAMU. Kujenga tabia ya nidhamu ndiyo kiini cha wale wote wanaofanikiwa katika jukumu hili zito.

Lakini pia pamoja na hayo yote ikiwa mtu umeshafika mahali fulani huna kazi wala biashara, tayari ulishakosa kujijengea nidhamu hiyo tokea unazaliwa, wazazi wako hawakujisumbua kukufungulia junior accounts na maisha yako mengine yote hukujisumbua kuweka akiba sasa utafanyaje ili kuondoka hapo ulipo?

Hauna kazi yeyote wala mtaji wa kufungulia biashara hata ile ndogondogo

Na mara nyingi tunakuwa navyo lakini tunadhani kipato tunachoingiza ni kidogo mno kuweza kujiwekea akiba. Kwanza ieleweke tu kwamba kauli ya kutokuwa na kazi wala mtaji wa kuanzisha biashara ni kauli ya kimtazamo zaidi kuliko uhalisia wenyewe (Mentality)

Hivi unataka kuniambia una nguvu na afya njema ukiweka aibu pembeni ukatoka na kutafuta kibarua cha kufanya kwa siku hata ikiwa ni kuosha vyombo migahawani au kwa mama lishe kweli jioni unaweza kukosa elfu mbili au tatu? Au umeamua kuweka aibu pembeni ukaamua kuzunguka mitaani kuokota vitu chakavu na plastiki za maji kwa siku utakosa hata buku tano kweli?

Suluhisho la kweli ni Ubunifu na matumizi ya teknolojia

Hayo yote niliyoeleza hapo juu yanawezekana kivitendo japo unatakiwa utashi na kujitolea kikamilifu kwani kuna watu hata pamoja na kumiliki biashara au kuwa na ajira bado ‘wanastruggle’,  wanahangaika kuweka akiba kutokana na ukweli kwamba kipato wanachokipata ukilinganisha na mahitaji yao makubwa inakuwa ni kama haiwezekani kabisa kujiwekea akiba na ukiangalia huko nyuma walishakosea kujiwekea akiba tangu zamani.

Ubunifu na matumizi ya teknolojia hata zile rahisi kabisa vina uwezo mkubwa wa kuboost haraka biashara hata iwe ndogo vipi na kuyafanya mapato yake yaweze kuendana na kasi ya mahitaji ya mmiliki wa biashara yenyewe. Aliyeajiriwa naye pia anaweza akatumia dhana hizihizi kwa kuanzisha biashara yeyote ile hata iwe ndogo vipi nje ya ajira yake ambayo anaweza hapo baadae akatumia uzoefu na taarifa mbalimbali atakazokuwa amekusanya kuja kuifanya biashara hiyo full time akaachana hata na kazi baada ya kugundua inamlipa kipato kikubwa kuliko ajira/kazi yenyewe.

Kwa kulitambua hilo, jifunzeujasiriamali blog tumeanzisha masomo ya ubunifu katika biashara kila siku kwenye MENTORSHIP GROUP letu la Michanganuo-online ambapo tunakuwa na michanganuo mifupi ya biashara lakini yenye mtazamo wa kiubunifu zaidi. Biashara tunazozijadili humo mtu yeyote anaweza akatumia ubunifu tunaoupendekeza na ukamletea mafanikio makubwa haraka kuliko kufanya tu biashara hivihivi kimazoea.

Michanganuo hii mifupimifupi itaenda sambamba na darasa letu jingine la wiki la semina za kujifunza uandishi wa Michanganuo mirefu ya biashara (Complete business plan courses) darasa hili linaitwa One week Business plan Master Class

Wanafunzi wote kwenye Mentorship Class ni lazima wapite kwanza kwenye One Week Master Class na kujiunga na darasa hili unalipa kiingilio sh. 10,000/= tu, kisha unapata offa ya kujiunga bure Mentorship class kwa mwaka mzima(miezi 12), pamoja na offa nyingine mpya ya vitabu na michanganuo ya biashara (vitu 12) yenye thamani ya sh. 120,000/=

**OFFA hizi zote 2 siyo za kudumu ingawa madarasa yatadumu, kwa hiyo wajanja mara zote huwa hawalazi damu Offa kubwa namna hii zinapotokea kuepusha kuja kujutia zinapoondolewa au kubadilishwa.  

Lipia sasa hivi kupitia namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo nikutumie offa zako zote muda huohuo huku ukisubiri darasa la ubunifu (Mentorship class) kila siku jioni na Masterclass tarehe 25/08/2024. Master class ya safari hii tutajifunza uandishi wa michanganuo kwa ujumla(General), kisha mchanganuo kamili mpya wa kuku Chotara Kuroiler wa Mayai hatua kwa hatua. Kumbuka iliyopita tuliandika Kuroiler wa nyama.

 

OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO (VITU 13)

                           1.       Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (Page 430)

                           2.       Mchanganuo Mpya: Biashara ya ufugaji kuku chotara kuroiler wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)-swahili

                           3.       Kitabu Kipya: Semina nzima ya kuandika mchanganuo wa kuku chotara kuroiler wa nyama 300 hatua kwa hatua-kiswahili

                           4.       Mchanganuo wa biashara kiwanda cha usagishaji unga wa Dona (USADO Milling Co.) -kiswahili

                           5.       Mchanganuo wa biashara, kiwanda cha mvinyo na juice ya Rosella (Choya Investment Co.)-kiswahili

                           6.       Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-kiingereza

                           7.       Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili

                           8.       Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili

                           9.       Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili

                         10.     Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant)-kiingereza

                         11.     Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant) –kiswahili

                         12.     Mchanganuo wa Biashara ya Kuongeza thamani mashamba ya zabibu (Makupila Real Estate Agency) –kiswahili

                         13.     Kujiunga Mentorship Class

 

Bado tunaendelea kutumia mtindo uleule aliotumia NAPOLEON HILL kwenye madarasa na Semina zake katika Mastermind Group na Mikutano yake na washauri wasioonekaka kwenye kitabu cha Think & Grow Rich.

Wakufunzi huwa tunawahi darasani masaa 2 mpaka 3 kabla ya muda halisi kusudi kusuluhisha changamoto mbalimbali za wanafunzi wakiwemo wale waliochelewa kujiunga na semina au ambao hawakuelewa barabara somo lililopita.

Tunakuwa tayari masaa yote hata nje ya darasa kusikiliza na kujibu maswali ya wanafunzi wetu.

 

 

 



SOMA NA HIZI HAPA;

                                     1.       Njia mpya za kufanya mambo: dunia, biashara, ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu

                                     2.       Kama una biashara ndogo ya mtaji mdogo, hizi hapa njia 11 za kuibusti

                                     3.       Ujasiriamali: ubunifu ndiyo msingi wake mkuu na injini ya uchumi katika soko huria.

                                     4.       Semina: mchanganuo wa biashara ya kusaga na kuuza unga safi wa dona (usado milling)-1

                                     5.       Faida duka la mahitaji ya nyumbani: niweke akiba kiasi gani cha mapato ya siku?

                                     6.       Wazo la biashara ipi yenye hatari kidogo naweza kufanya kwa mtaji wa milioni 5?: mwajiriwa serikalini

0 Response to "FEDHA ZA KUWEKA AKIBA UTAZIPATA WAPI WAKATI HUNA KAZI WALA BIASHARA?"

Post a Comment