Kama ilivyokuwa kwangu mimi ndugu msomaji, bila shaka yeyote najua na kwako pia kwa muda mrefu umekuwa ukipata msisitizo mkubwa kuhusiana na dhana nzima ya kuweka akiba sehemu fulani ya fedha unazopata kila siku. Uwekaji akiba hakuna mtu anayeweza kupinga kuwa ndiyo msingi mkuu wa mtu kuja siku moja kuufikia uhuru wake wa kifedha.
Lakini watu wengi sana wanajikuta kwenye mtanziko mkubwa
pale wanapokuwa wakijiuliza swali hili mara kwa mara, Je, nitaweza vipi
kuweka akiba wakati sina chanzo chochote kile cha fedha kama kazi/ajira wala biashara?
Akiba ndiyo fedha unayoweza kuja kuitumia katika
uwekezaji kwenye miradi ya kibiashara iliyo na uwezo wa kuingiza faida, kwa
maneno mengine badala ya kuendelea kuiweka akiba hiyo unaamua sasa kuifanya
izae na kuongezeka mithili ya mmea, unapopanda mazao shambani mbegu hazijai
hata kwenye kisado lakini zikikua zinakuja kuzaa magunia kwa magunia ya mazao.
Fedha
za kuweka akiba utazipata wapi sasa?
Ukiuliza fedha za kuweka akiba unazipata wapi ni sawa na
mtu anayeuliza mtoto mdogo anapozaliwa atapata wapi chakula wakati amezaliwa
bila ya chochote. Tuachane kwanza na mtu ambaye keshamaliza zake shule au chuo
ama ni mtu mzima zaidi ya hata miaka 18 yupo zake mtaani na anajiuliza swali
hili. Kimsingi kabisa binadamu tunapaswa mara tu tunapozaliwa hivi tukiwa
watoto wachanga tuanze kujiwekea akiba ya fedha kidogokidogo na hili
linawezekana.
Hebu fikiria kwa mfano tokea siku wewe umezaliwa
ingelikuwa unaweka akiba hata ya shilingi moja kila siku mpaka sasa hivi
ungelikuwa na shilingi ngapi?. Unaweza ukaniuliza swali jingine, “Sasa itawezekanaje
mtoto wa siku moja kujiwekea akiba wakati anasaidiwa kila kitu na wazazi wake?
Jibu ni kwamba matumizi yaleyale mtoto anayotumia, mzazi
afanye juu chini kumega hapo kiasi kidogo na kumwekea akiba mpaka atakapokuja
kujitambua mwenyewe. Badala ya kumnunulia beseni la elfu 50 nunu la elfu 30
ishirini mdumbukizie kwenye kibubu, akaunti maalumu au ‘whatever’ ulichoamua kumuwekea akiba zake humo akikua atazikuta.
Unajua ukishazaliwa tu hivi unaanza kuingiza kipato hata
ikiwa siyo kwa njia ya moja kwa moja. Kipato cha pesa siyo lazima kitokane tu
na ajira au biashara, kuna ruzuku, zawadi, misaada, hii yote ni aina za vipato
mtu anapata katika nyakati mbalimbali za maisha yake ukiachilia mbali kazi na
biashara.
Nimetolea mfano wa mtoto aliyezaliwa leo lakini kuna
wanafunzi wanapata ruzuku za aina mbalimbali ikiwemo ‘pocket money’. Mwanafunzi mjanja anaweza kumega kiasi fulani kutoka
katika fedha anazogaiwa na wazazi/walezi wake au boom kwa wale wanavyuo,
akajibana kidogo na kujiwekea akiba ambayo baadae itakuja kuwa msaada mkubwa
kwake.
Sababu kubwa inayotufanya watu tuone suala la uwekaji
akiba ni jambo gumu sana ni ile hali ya kutokuwa na NIDHAMU. Kujenga tabia ya nidhamu ndiyo kiini cha wale wote
wanaofanikiwa katika jukumu hili zito.
Lakini pia pamoja na hayo yote ikiwa mtu umeshafika
mahali fulani huna kazi wala biashara, tayari ulishakosa kujijengea nidhamu
hiyo tokea unazaliwa, wazazi wako hawakujisumbua kukufungulia junior accounts na maisha yako mengine
yote hukujisumbua kuweka akiba sasa utafanyaje ili kuondoka hapo ulipo?
Hauna
kazi yeyote wala mtaji wa kufungulia biashara hata ile ndogondogo
Na mara nyingi tunakuwa navyo lakini tunadhani kipato
tunachoingiza ni kidogo mno kuweza kujiwekea akiba. Kwanza ieleweke tu kwamba
kauli ya kutokuwa na kazi wala mtaji wa kuanzisha biashara ni kauli ya
kimtazamo zaidi kuliko uhalisia wenyewe (Mentality)
Hivi unataka kuniambia una nguvu na afya njema ukiweka
aibu pembeni ukatoka na kutafuta kibarua cha kufanya kwa siku hata ikiwa ni
kuosha vyombo migahawani au kwa mama lishe kweli jioni unaweza kukosa elfu
mbili au tatu? Au umeamua kuweka aibu pembeni ukaamua kuzunguka mitaani kuokota
vitu chakavu na plastiki za maji kwa siku utakosa hata buku tano kweli?
Suluhisho
la kweli ni Ubunifu na matumizi ya teknolojia
Hayo yote niliyoeleza hapo juu yanawezekana kivitendo
japo unatakiwa utashi na kujitolea kikamilifu kwani kuna watu hata pamoja na
kumiliki biashara au kuwa na ajira bado ‘wanastruggle’,
wanahangaika kuweka akiba kutokana na
ukweli kwamba kipato wanachokipata ukilinganisha na mahitaji yao makubwa
inakuwa ni kama haiwezekani kabisa kujiwekea akiba na ukiangalia huko nyuma
walishakosea kujiwekea akiba tangu zamani.
Ubunifu na matumizi ya teknolojia hata zile rahisi kabisa
vina uwezo mkubwa wa kuboost haraka
biashara hata iwe ndogo vipi na kuyafanya mapato yake yaweze kuendana na kasi
ya mahitaji ya mmiliki wa biashara yenyewe. Aliyeajiriwa naye pia anaweza
akatumia dhana hizihizi kwa kuanzisha biashara yeyote ile hata iwe ndogo vipi
nje ya ajira yake ambayo anaweza hapo baadae akatumia uzoefu na taarifa
mbalimbali atakazokuwa amekusanya kuja kuifanya biashara hiyo full time akaachana hata na kazi baada
ya kugundua inamlipa kipato kikubwa kuliko ajira/kazi yenyewe.
Kwa kulitambua hilo, jifunzeujasiriamali
blog tumeanzisha masomo ya ubunifu katika biashara kila siku kwenye MENTORSHIP
GROUP letu la Michanganuo-online ambapo tunakuwa na michanganuo mifupi ya
biashara lakini yenye mtazamo wa kiubunifu zaidi. Biashara tunazozijadili humo
mtu yeyote anaweza akatumia ubunifu tunaoupendekeza na ukamletea mafanikio
makubwa haraka kuliko kufanya tu biashara hivihivi kimazoea.
Michanganuo hii mifupimifupi itaenda sambamba na darasa
letu jingine la wiki la semina za kujifunza uandishi wa Michanganuo mirefu ya
biashara (Complete business plan courses)
darasa hili linaitwa One week Business plan Master Class
Wanafunzi wote kwenye Mentorship Class ni lazima wapite kwanza
kwenye One Week Master Class na kujiunga na darasa hili unalipa kiingilio sh.
10,000/= tu, kisha unapata offa ya kujiunga bure Mentorship class kwa mwaka
mzima(miezi 12), pamoja na offa nyingine mpya ya vitabu na michanganuo ya
biashara (vitu 12) yenye thamani ya sh. 120,000/=
**OFFA hizi zote 2 siyo za kudumu ingawa madarasa
yatadumu, kwa hiyo wajanja mara zote huwa hawalazi damu Offa kubwa namna hii
zinapotokea kuepusha kuja kujutia zinapoondolewa au kubadilishwa.
Lipia sasa hivi kupitia namba zetu, 0712202244 au
0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo nikutumie offa zako zote muda huohuo
huku ukisubiri darasa la ubunifu (Mentorship class) kila siku jioni na
Masterclass tarehe 25/08/2024. Master class ya safari hii tutajifunza uandishi
wa michanganuo kwa ujumla(General), kisha mchanganuo kamili mpya wa kuku Chotara
Kuroiler wa Mayai hatua kwa hatua. Kumbuka iliyopita tuliandika Kuroiler wa
nyama.
OFFA
YA VITABU NA MICHANGANUO (VITU 13)
1.
Kitabu: MICHANGANUO YA BIASHARA
NA UJASIRIAMALI (Page 430)
2.
Mchanganuo Mpya: Biashara ya ufugaji kuku
chotara kuroiler wa nyama 300 (Chotara Poultry Production Co.)-swahili
3.
Kitabu Kipya: Semina nzima ya
kuandika mchanganuo wa kuku chotara kuroiler wa nyama 300 hatua kwa hatua-kiswahili
4.
Mchanganuo wa biashara kiwanda
cha usagishaji unga wa Dona (USADO Milling Co.) -kiswahili
5.
Mchanganuo wa biashara, kiwanda
cha mvinyo na juice ya Rosella (Choya Investment Co.)-kiswahili
6.
Mchanganuo wa kuku wa
nyama (Tumaini
Broilers)-kiingereza
7.
Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili
8.
Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili
9.
Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili
10. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant)-kiingereza
11. Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane
Restaurant) –kiswahili
12. Mchanganuo wa Biashara ya Kuongeza thamani mashamba ya zabibu (Makupila Real Estate Agency) –kiswahili
13. Kujiunga Mentorship Class
Bado
tunaendelea kutumia mtindo uleule aliotumia NAPOLEON HILL kwenye madarasa na Semina zake katika Mastermind
Group na Mikutano yake na washauri wasioonekaka kwenye kitabu cha Think & Grow Rich.
Wakufunzi
huwa tunawahi darasani masaa 2 mpaka 3 kabla ya muda halisi kusudi kusuluhisha
changamoto mbalimbali za wanafunzi wakiwemo wale waliochelewa kujiunga na
semina au ambao hawakuelewa barabara somo lililopita.
Tunakuwa
tayari masaa yote hata nje ya darasa kusikiliza na kujibu maswali ya wanafunzi
wetu.
SOMA NA HIZI HAPA;
1.
Njia mpya za kufanya mambo: dunia,
biashara, ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu
2.
Kama una biashara ndogo ya mtaji
mdogo, hizi hapa njia 11 za kuibusti
3.
Ujasiriamali:
ubunifu ndiyo msingi wake mkuu na injini ya uchumi katika soko huria.
4.
Semina: mchanganuo wa biashara ya kusaga na kuuza unga
safi wa dona (usado milling)-1
5.
Faida duka la mahitaji ya nyumbani: niweke akiba kiasi gani cha
mapato ya siku?
0 Response to "FEDHA ZA KUWEKA AKIBA UTAZIPATA WAPI WAKATI HUNA KAZI WALA BIASHARA?"
Post a Comment