MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUUZA NDIZI MZUZU KUTOKA MOROGORO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUUZA NDIZI MZUZU KUTOKA MOROGORO

Mkukungu wa ndizi mzuzu

Biashara ya ndizi mzuzu kutoka Mkoani Morogoro hasa katika maeneo ya mijini kama Dar es salaam ni biashara yenye faida nzuri na endelevu kutokana na sababu kubwa kwamba ndizi ni chakula kinacholiwa na kila mtu.Unaweza kuuza ndizi mbichi au hata ukauza ndizi mbivu ni chaguo lako mwenyewe.

Leo tarehe  katika darasa letu la Michanganuo mifupi ya biashara tutakuwa na mchanganuo mfupi wa biashara ya kuuza ndizi mzuzu kutoka Morogoro. Darasa hili la bure ni la mwaka mzima kwa wale wote wanaolipia darasa la siku 7 liitwalo MASTER CLASS linalofundisha jinsi ya kuandika mchanganuo kamili/ mrefu wa biashara (a comlete business plan course)

Michanganuo hii mifupi sifa yake kuu ni UBUNIFU. Tunajitahidi kubuni mambo ambayo yataitofautisha biashara yako ndogo na biashara nyingine wateja wapate sababu ya kuja kununua kwako na si kwa washindani wako.

Soko la wateja wa ndizi mzuzu mijini

Ndizi mzuzu huhitajika sana hasa na makundi yafuatayo ya wateja;

               (1)     Watu wote wanaofanya biashara ya kuuza mishikaki na ndizi

               (2)     Wanaofanya biashara ya kuuza ndizi kwenye magenge ya mitaani

               (3)     Wanaofanya biashara ya ndizi za kukaanga kwenye mabanda ya chipsi, mabaa na katika vituo vya mabasi stendi mbalimbali

               (4)     Wakaanga crisp za ndizi

               (5)     Wateja wa kawaida wanaokwenda kupika au kukaanga majumbani mwao

Ikiwa unatafuta wazo la biashara ya kufanya chapchap na bado hujalipata unaweza ukajiunga na darasa letu hili ambapo unaweza kupata wazo zuri la biashara miongoni mwa mawazo ya biashara nyingi tunazochanganua kila siku. 

ndizi mzuzu za kukaanga

Uzuri wa mawazo ya biashara zetu ni kwamba unapata faida ya ubunifu ambao pengine wewe mwenyewe usingeliweza kufikiria kuufanya. Unapata wazo la biashara unayokwenda kuianza mara moja na siyo kwenda kuanza tena kulifanyia upembuzi yakinifu kujua kama linafaa au halifai.

 

Bei na faida ya ndizi mzuzu sokoni

Ukienda sokoni au gengeni ndizi moja watakuuzia kuanzia shilingi 200 mpaka 300. Sasa ikiwa utaamua kuanzisha biashara hii, tumekutafutia kabisa bei za mkungu mmoja wa ndizi kule Morogoro na bei ya ndizi mzuzu Dar es salaam au mkoa mwingine wowote ulipo.

Kwa wauzaji wa mwisho kwenye maeneo ya kuuza vyakula mfao Bar, mabanda ya chipsi, mahotelini, migahawani na kwa mamalishe/babalishe bei ya ndizi moja iliyokwisha pikwa,kuchomwa au kukaangwa huanzia shilingi 500 mpaka 1000 kwa ndizi moja. Mkungu mmoja wa ndizi mzuzu unaweza kuuza hadi mara 2 ya bei ya manunuzi ukiweka mpaka gharama za usafirishaji, faida inakaribia nusu kwa usu

Mchanganuo wetu huu wa biashara ya kuuza ndizi mzuzu kutoka Morogoro tutalenga zaidi wafanyabiashara wanaouza ndizi kwa jumla, wananunua ndizi kutoka Mkoani Morogoro kwa mkulima na kuja kuuza ndizi hizo kwa wafanyabiashara wa mwisho rejareja.

Jinsi ya kujiunga na Darasa hili

Ili kupata tiketi ya kujifunza course ya siku 7 ya jinsi ya kuandaa mchanganuo kamili wa biashara yeyote ile unalipia shilingi elfu 10 kisha unapatiwa papo hapo OFFA ya vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali wakati ukisubiri Darasa la siku 7 lianze. Course ya siku saba huhusisha mafunzo ya jumla juu ya uandishi wa michanganuo lakini pia uchanganuzi wa biashara moja maalumu inayoweza kuwa biashara yeyote ile mfano ufugaji wa kuku, biashara ya chakula, biashara ya saluni nk.

Baada ya hapo ukipeda unaweza kuendelea kubaki katika group letu la whatsap la masomo (MENTORSHIP CLASS) kwa muda wa mwaka mzima. 

Namba za kulipia ni; 0712202244 au 0765553030 kisha tuma ujumbe usemao,

“NIUNGE MASTERCLASS NA OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO"

 

HUDUMA ZETU NYINGINE NI HIZI HAPA;

1.   Duka jipya la vitabu na Michanganuo ya Biashara mtandaoni; kutembelea bofya hapa>>DUKA LA VITABU NA MICHANGANUO YA BIASHARA MTANDAONI

2.   Kuandikiwa mchanganuo/mpango wa biashara yako kwa ajili ya malengo mbalimbali mfano kuombea fedha, kutafutia wabia au kwa ajili tu ya kuendeshea biashara yako kwa ufanisi. Gharama zetu ni kidogo, asilimia 1% tu ya mtaji au chini ya hapo. Unaweza kucheki baadhi ya kampuni na watu tuliowahi kufanya nao kazi hapa >>OUR PORTFOLIO

3.   Kupata nakala ya kitabu kizima cha Think & Grow Rich kwa lugha ya Kiswahili bofya jina la kitabu hapa>> FIKIRI NA UTAJIRIKE




SOMA NA HIZI HAPA PIA;

                 1.      Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado-1

                 2.       Biashara ndogo ya mtaji wa 80,000/= niuze nini kupata faida ya haraka?

                 3.       Biashara ya mtaji mdogo yenye faida kubwa zaidi tanzania ilivyoshangaza darasa la michanganuo ya biashara

                 4.      Biashara hii watu wengi huidharau lakini ina faida kubwa na nzuri,mtaji laki 1

                 5.      Ujasiriamali: ubunifu ndiyo msingi wake mkuu na injini ya uchumi katika soko huria.

 

0 Response to "MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUUZA NDIZI MZUZU KUTOKA MOROGORO"

Post a Comment