Biashara
ya ndizi mzuzu kutoka Mkoani Morogoro hasa katika maeneo ya mijini kama Dar es
salaam ni biashara yenye faida nzuri na endelevu kutokana na sababu kubwa
kwamba ndizi ni chakula kinacholiwa na kila mtu.Unaweza kuuza ndizi mbichi au
hata ukauza ndizi mbivu ni chaguo lako mwenyewe.
Leo
tarehe katika darasa letu la Michanganuo mifupi ya biashara tutakuwa na
mchanganuo mfupi wa biashara ya kuuza ndizi mzuzu kutoka Morogoro. Darasa hili
la bure ni la mwaka mzima kwa wale wote wanaolipia darasa la siku 7
liitwalo MASTER CLASS linalofundisha
jinsi ya kuandika mchanganuo kamili/ mrefu wa biashara (a comlete business plan course)
Michanganuo
hii mifupi sifa yake kuu ni UBUNIFU.
Tunajitahidi kubuni mambo ambayo yataitofautisha biashara yako ndogo na
biashara nyingine wateja wapate sababu ya kuja kununua kwako na si kwa
washindani wako.
Soko la wateja wa ndizi mzuzu mijini
Ndizi
mzuzu huhitajika sana hasa na makundi yafuatayo ya wateja;
(1) Watu
wote wanaofanya biashara ya kuuza mishikaki na ndizi
(2) Wanaofanya
biashara ya kuuza ndizi kwenye magenge ya mitaani
(3) Wanaofanya
biashara ya ndizi za kukaanga kwenye mabanda ya chipsi, mabaa na katika vituo
vya mabasi stendi mbalimbali
(4) Wakaanga
crisp za ndizi
(5) Wateja
wa kawaida wanaokwenda kupika au kukaanga majumbani mwao
Ikiwa unatafuta wazo la biashara ya kufanya chapchap na bado hujalipata unaweza ukajiunga na darasa letu hili ambapo unaweza kupata wazo zuri la biashara miongoni mwa mawazo ya biashara nyingi tunazochanganua kila siku.
Uzuri wa
mawazo ya biashara zetu ni kwamba unapata faida ya ubunifu ambao pengine wewe
mwenyewe usingeliweza kufikiria kuufanya. Unapata wazo la biashara unayokwenda
kuianza mara moja na siyo kwenda kuanza tena kulifanyia upembuzi yakinifu kujua
kama linafaa au halifai.
Bei
na faida ya ndizi mzuzu sokoni
Ukienda sokoni au gengeni ndizi moja watakuuzia kuanzia
shilingi 200 mpaka 300. Sasa ikiwa utaamua kuanzisha biashara hii,
tumekutafutia kabisa bei za mkungu mmoja wa ndizi kule Morogoro na bei ya ndizi
mzuzu Dar es salaam au mkoa mwingine wowote ulipo.
Kwa wauzaji wa mwisho kwenye maeneo ya kuuza vyakula mfao
Bar, mabanda ya chipsi, mahotelini, migahawani na kwa mamalishe/babalishe bei
ya ndizi moja iliyokwisha pikwa,kuchomwa au kukaangwa huanzia shilingi 500
mpaka 1000 kwa ndizi moja. Mkungu mmoja wa ndizi mzuzu unaweza kuuza hadi mara
2 ya bei ya manunuzi ukiweka mpaka gharama za usafirishaji, faida inakaribia
nusu kwa usu
Mchanganuo wetu huu wa biashara ya kuuza ndizi mzuzu
kutoka Morogoro tutalenga zaidi wafanyabiashara wanaouza ndizi kwa jumla,
wananunua ndizi kutoka Mkoani Morogoro kwa mkulima na kuja kuuza ndizi hizo kwa
wafanyabiashara wa mwisho rejareja.
Jinsi
ya kujiunga na Darasa hili
Ili kupata tiketi ya kujifunza course ya siku 7 ya jinsi ya kuandaa mchanganuo kamili wa biashara yeyote ile unalipia shilingi elfu 10 kisha unapatiwa papo hapo OFFA ya vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali wakati ukisubiri Darasa la siku 7 lianze. Course ya siku saba huhusisha mafunzo ya jumla juu ya uandishi wa michanganuo lakini pia uchanganuzi wa biashara moja maalumu inayoweza kuwa biashara yeyote ile mfano ufugaji wa kuku, biashara ya chakula, biashara ya saluni nk.
Baada ya hapo ukipeda unaweza kuendelea kubaki katika group letu la whatsap la masomo (MENTORSHIP CLASS) kwa muda wa mwaka mzima.
Namba za kulipia ni; 0712202244 au 0765553030 kisha tuma
ujumbe usemao,
“NIUNGE MASTERCLASS NA OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO"
HUDUMA ZETU NYINGINE NI HIZI HAPA;
1.
Duka jipya la vitabu na Michanganuo ya
Biashara mtandaoni; kutembelea bofya hapa>>DUKA LA VITABU NA MICHANGANUO YA BIASHARA MTANDAONI
2.
Kuandikiwa mchanganuo/mpango wa biashara
yako kwa ajili ya malengo mbalimbali mfano kuombea fedha, kutafutia wabia au
kwa ajili tu ya kuendeshea biashara yako kwa ufanisi. Gharama zetu ni kidogo,
asilimia 1% tu ya mtaji au chini ya hapo. Unaweza kucheki baadhi ya kampuni na
watu tuliowahi kufanya nao kazi hapa >>OUR PORTFOLIO
3. Kupata nakala ya kitabu kizima cha Think & Grow Rich kwa lugha ya Kiswahili bofya jina la kitabu hapa>> FIKIRI NA UTAJIRIKE
SOMA
NA HIZI HAPA PIA;
1.
Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado-1
2. Biashara ndogo ya mtaji wa 80,000/= niuze nini kupata faida ya haraka?
4.
Biashara hii watu wengi huidharau lakini ina faida kubwa na
nzuri,mtaji laki 1
5.
Ujasiriamali:
ubunifu ndiyo msingi wake mkuu na injini ya uchumi katika soko huria.
0 Response to "MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUUZA NDIZI MZUZU KUTOKA MOROGORO"
Post a Comment