Kaulimbiu hii ya ‘Make
yourself Great Again’ siyo mara yangu ya kwanza kuitumia hapa, nimewahi
huko nyuma kipindi kama hiki cha kampeni za urais wa Marekani 2017, Donald
Trump alipokuwa akichuana tena na Mwanamama mwingine Hillary Clinton.
Mimi siyo mshabiki sana wa siasa za Marekani wala mfuasi kisiasa
wa Donald Trump, akishinda yeyote kwangu mimi ni poa tu, iwe Trump ama Harris,
isipokuwa tu navutiwa na kuzihusudu sana harakati na mikakati ya Bwana Trump
kwenye suala zima la biashara na uchumi.
Huyu mwamba ananikosha pale linapokuja suala la kutokata tamaa
hata akabiliwe na magumu kiasi gani na msimamo thabiti usioyumbishwa kiurahisi.
Haijalishi atashinda uraisi au ataanguka lakini mimi kwenye hili nitabakia kuwa
mfuasi wake daima.
Slogan ya “Kujirudishia tena Ukuu wako uliopotea hapa
imetumika kuhamasisha suala zima la kujikomboa kiuchumi kwa mara nyingine tena
baada ya kuanguka au kufeli mara ya kwanza.
Bila shaka binadamu kuna nyakati fulani katika maisha unaweza kuwa bora sana kwenye eneo fulani iwe ni kiuchumi, kiafya, kiimani, kimahusiano, kielimu, kijamii au katika nyanja nyingine yeyote ile walakini ikafika kipindi ukashuka kiwango kile ulichokuwa umefikia awali na sasa unatamani urudi tena katika viwango vile vya juu.
Blogu yako hii pamoja na majukwaa yetu mengine mbalimbali
kwa mwaka mpya ujao wa 2025 tumeanzisha kampeni kubwa ya kujirudishia tena kile
kilichopotea (Make yourself great again) kupitia njia za makala, semina na
programu mbalimbali. Siyo lazima uwe ni mtu uuliyewahi kufanikiwa ukaja
kuanguka na sasa unataka kuurudia tena ukuu wako hapana, bali kampeni hii inawafaa
pia hata wale watu wanaotamani kuujenga ukuu wao sasa ili hapo baadae waje
waweze kuwa watu wakubwa wanaosikilizwa katika jamii.
Kumbuka wale walio na mafanikio makubwa husikilizwa zaidi
kwenye jamii zetu kushinda watu wa kawaida tu wasiokuwa na mafanikio makubwa. Na
kufanikiwa mara nyingi watu huangalia zaidi pesa ingawa kuna mafanikio ya aina
nyingine pia.
Sisi tutakwenda kujikita kwenye mafanikio ya kifedha kwa
maana ya matumizi ya mbinu mbalimbali za kibiashara zinazotoa matokeo chanya
kwa haraka zaidi. Tutajifunza jinsi ya kuandaa mipango madhubuti ya biashara kwani
ndiyo kitu kila mtu anayetaka kuanzisha biashara huwa nacho kichwani
Mpango wa biashara / Business plan pia hubeba vipengele
vingine vyote vinavyounda biashara kuanzia Maono(vision), Malengo, Biashara
yenyewe, Bidhaa/Huduma, Masoko, Mikakati, Rasilimaliwatu, Uendeshaji na Fedha
kwa biashara unayoifanya. Hii ni kusema kwamba unapojifunza kutayarisha mpango
wa biashara yako ni sawa na umejifunza kila kitu kuihusu biashara yako kabla
hata hujaianza.
Katika programu yetu 2025 mbali na mipango ya biashara,
tutajifunza pia suala zima la Ubunifu katika biashara mbalimbali, jinsi ya
kupata mitaji kwa njia nyepesi na matumizi ya teknolojia za kisasa kufanya
biashara.
Unaweza ukaamua tu kufuatilia blogu yetu ya Jifunzeujasiriamali
pamoja na makala tunazotuma kwa email bure kabisa bila malipo yeyote, lakini
pia ukipenda kujifunza zaidi unalipia kiasi kidogo tu cha fedha kwa mwaka mzima
shilingi, 10,000/= na kujiunga na Mastermind-Group letu la MICHANGANUO-ONLINE 2025 ambalo utapata Semina kamili ya kujifunza
jinsi ya kuandiaka mchanganuo mrefu wa biashara yeyote ile, kisha kila siku
masomo ya fedha, ubunifu na michanganuo mifupimifupi ya biashara zenye fursa
kubwa ya kuleta faida haraka kwa mwaka mzima wa 2025
Semina yetu ya kwanza kabisa ya kuandika hatua kwa hatua
mchanganuo mrefu wa biashara itafanyika mnamo tarehe 15/11/2024 na tutajifunza
jinsi ya kuandika mchanganuo kamili wa biashara tukitumia biashara ya
usagishaji mahindi (Unga wa Sembe na Dona).
Kupitia mchanganuo huo mshiriki atapewa mbinu zote
zinazohitajika kuandaa mchanganuo wa biashara nyingine yeyote ile hata kama
siyo ya usagishaji mahindi.
OFFA
/ZAWADI KWA WATU 10 WA MWANZO WATAKAOWAHI KUJIANDIKISHA
Nitatoa zawadi maalumu ya vitabu na michanganuo ya
biashara, jumla ni vitu 11 kwa watu 10 tu wa mwanzo kujiandikisha kabla ya
tarehe 14/11/2024 saa 6 usiku. Navyo ni;-
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na
Ujasiriamali
2.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri
wasiyopenda kuitoa
3.
KITABU: Toleo jipya la Elimu ya pesa na Mafanikio
4.
KITABU: Sayansi & Sanaa ya Upishi wa chapatti
laini.
5.
MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji unga
wa Dona (USADO Milling)
6.
MCHANGANUO: Ufugaji kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-Kiswahili &kiingereza
7.
MCHANGANUO: Ufugaji kuku chotara
Kuroiler-nyama
8.
MCHANGANUO: Kilimo cha tikiti maji (Kibada watermelon)
9.
MCHANGANUO: Uboreshaji Mashamba ya zabibu
Dodoma (Makupila Real Estate)
10. MCHANGANUO:
Biashara ya kuuza chipsi
11. MCHANGANUO:
Biashara ya mgahawa (Jane Restaurant) –Kiswahili & Kiingereza
JINSI YA KULIPIA
Namba za malipo ni; 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha ujumbe sms au watsap usemao “NATAKA OFFA YA MWISHO KWA 2024 NA OFFA YA VITU 11” Mara moja nitakutumia zawadi zako zote 10 pamoja na kukuunganisha na MASTERMIND-GROUP letu la mwaka 2025
AU
Unaweza kuingia kwenye duka letu hili la mtandaoni, Selar.co/augustinopeter na
kulipia moja kwa moja sh. elfu 10 pasipo kuwasiliana na sisi ukitumia mtandao
wowote unaotumia halafu utapewa kifurushi cha ZIP utakachodownload zawadi. Unzip
kifurushi na kutoa zawadi zako zote 10. Kisha nitakuunga kwenye MASTERMIND
GROUP
NB:
Unaweza kunikumbusha kwa meseji nikuunganishe endapo nitachelewa kucheki mfumo.
0 Response to "2025 MAKE YOUR SELF GREAT AGAIN (NI MWAKA WA KUJIRUDISHIA TENA KILE ULICHOPOTEZA)"
Post a Comment