Hili ni somo la leo la fedha katika Mastermind group la Michanganuo-online na nitajibu swali la mdau wetu mmoja alilouliza kama ifuatavyo;
Habari
Peter, Mimi nimeolewa naishi na mume
wangu na kila mmoja kati yetu anapopata pesa nyingi kuliko kiasi kile
tulichokizoea kupata huwa tunaweka malengo mbalimbali ikiwemo kujiwekea akiba
kwa ajili ya kujenga nyumba yetu wenyewe, kununua usafiri nk.
Lakini
jambo la kustaajabisha ni kwamba mara tu tupatapo fedha hizo, hujitokeza matumizi
ya ajabuajabu ambayo hayakuwepo kabisa kabla ya kuzipata.
Huibuka
magonjwa, faini zisizokuwa na kichwa wala miguu ilimradi tu fedha kwa ajili ya
mipango yetu zimetumika kinyume na malengo tuliyojiwekea. Mpaka imefikia mahali
sasa tunapopata pesa nyingi tunaogopa kuweka malengo yeyote. Nataka nifahamu
kama hii ni hali tu ya kawaida au kuna mapepo na majini ndani yake?
MAJIBU:
Kila mtu huwa ana kiwango chake cha kushika pesa na ni
vigumu sana mtu kuingiza pesa zaidi kuvuka kiwango hicho lakini kuna njia za
mtu kuweza kufanya hatimaye kuondokana na kizingiti hiki na hata kuongeza
kiwango chako cha upataji wa fedha.
Nakushauri
hebu fanya jaribio lifuatalo;
Chukua kidumu chenye maji lita 5 na kisha uyajaze maji hayo
ndani ya chombo kingine lakini cha ujazo wa lita 1. Ni dhahiri kabisa kwamba
maji hayo yataingia mle kiasi cha lita moja tu huku mengine yakimwagika chini
na kulowanisha sakafu au meza unayofanyia jaribio hili. Ni wazi pia wala
hautahangaika kwenda kufanya jaribio hili kama nilivyokuelekeza kwani natambua kimantiki
wala haliwezi kuleta maana yeyote ile.
Katika ulimwengu wa pesa kwa kila mtu hali pia inashabihiana
sana na hii. Kuna kiwango fulani tu cha pesa kila mtu anachoweza kuingiza katika
maisha yake kama ilivyokuwa kwa dumu la maji la lita moja. Uwezo huo wa mtu wa
kupata pesa hauwezi kumruhusu aingize fedha zaidi ya kile kiwango chake
alichozoea. Na hata mtu huyu anaweza kulazimisha na kusema afanye kazi kwa
juhudi zote na maarifa ili kuongeza kipato hicho lakini kila senti
itakayoongezeka juu ya kiwango kile itapotea katika mazingira ya ajabu.
Jinsi
ya kutambua kiwango cha uwezo wako wa kumiliki pesa na namna ya kukizidisha
Ni rahisi kutambua kiwango chako cha fedha, Kokotoa
wastani wa kipato chako cha mwezi kwa miezi 6 iliyopita na jibu hilo ndiyo
uwezo wako wa kuingiza pesa kwa mwezi. Kiasi hiki huwa ndio sawa na ukanda wako
wa faraja (comfort zone) na hukuwekea mipaka kwenye kiwango chako cha
mapato, matumizi, madeni na matokeo ya biashara yako kwa ujumla kiasi kwamba
ukipata pesa zaidi tu, akili yako ya ndani (Subconconscious mind)
hukuzuia usipate.
Kila kiasi cha pesa kinachoongezeka zaidi ya kiwango
hicho mtu hujikuta akikipoteza, kukiweka katika miradi isiyo na tija, kukopesha
watu wengine hovyo au hata kutatafuta njia yeyote ile, ilimradi tu ameitumia
ikaisha (mfano wa maji kwenye lita 5
yanapozidi kwenye lita 1 na kumwagika sakafuni). Kuna nguvu ya ajabu huja
na kuchukua kiasi kilichozidi kupitia matumizi yasiyotarajiwa.
Tatizo hili halisababishwi na nguvu za giza kama
unavyodhania bali lina mizizi yake ndani kabisa ya ufahamu wetu (subconscious
mind), na kuibadilisha hali hii ni lazima kwanza mtu kuingia moja kwa moja
katika mawazo hayo ya ndani na kubadilisha programu tulizoziruhusu wenyewe
kuota mizizi pale miaka na miaka.
Programu hizo hubeba woga, uwongo na kila aina ya
mitazamo hasi inayochangia viwango vya uwezo wetu wa kujiingizia pesa
visiongezeke. Usipobadilisha mitazamo hiyo daima utaendelea kubakia na uwezo
uleule wa kiwango cha fedha uliokua nao katika maisha yako yote mpaka unaingia
kaburini. Kuna baadhi ya mbinu za
kuongeza kiwango cha uwezo wako wa kumiliki fedha nazo ni hizi zifuatazo;
1.
Tambua tabia yako ya fedha:
Wakati unapokuwa na shida ya fedha, utafanya kila njia
kuzipata, utafanya kazi muda wa ziada, utajinyima kila kitu ilimradi tu umepata
pesa lakini mara tu unapozipata hivi, unaona sasa hamna tena haja ya kujituma
zaidi. Programu yote hii hufanya kazi ndani ya akili zetu za ndani pasipo
wenyewe kujua, hivyo usishangae kuona unapoingiza pesa nyingi zinayeyukia
kusikojulikana. Ukifahamu namna akili yako ya ndani inavyofanya kazi juu ya
hili ni njia mojawapo ya kuondokana na tatizo hili moja kwa moja.
2.
Badilisha mfumo wako wa maisha
Tambua mpangilio wako wa kawaida wa pesa ukoje. Usizuie shauku yako ya kupata kile kitu usichoweza kukinunua. Uwezo wako wa kuwa na pesa zaidi utaongezeka iwapo utairuhusu nafsi yako kuhitaji kile unachokitamani kwani utajijengea nguvu zaidi ya kukitafuta na siyo kutumia ulicho nacho kukinunua. Jinyime lakini usizuie nafsi yako kutamani kuwa nacho.....................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Ndugu
msomaji wa somo hili, bado somo halijamalizika na unaweza kupata somo zima
kwenye channel yetu ukijiunga na group la masomo ya kila siku ya fedha na
michanganuo mifupimifupi ya biashara. Masomo yaliyopita utayapata yote
Kujiunga
lipia kiingilio cha mwaka sh. 10,000/= ambapo unapata pia fursa ya kushiriki
katika Semia kubwa ya kujifunza jinsi ya kuandika mchanganuo kamili wa biashara
Semina
iliyo karibu ni ya tarehe 15/11/2024 na tutachambua biashara ya usagishaji
mahindi (Sembe na Dona)
Namba
za malipo ni 0765553030 au 0712202244 Peter Augustino,
Ukishalipia
tuma ujumbe wa “nataka kujiunga Mastermind Group 2025 na offa ya vitu 11”.
Offa hii ni kwa watu 20 watakaowahi kabla ya tarehe 14/11/20224
0 Response to "HIVI NINA PEPO AU JINI?, KILA NIPATAPO FEDHA ZA ZIADA HUTUMIKA AU KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA AJABU!"
Post a Comment