HIVI NINA PEPO AU JINI?, KILA NIPATAPO FEDHA ZA ZIADA HUTUMIKA AU KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA AJABU! | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HIVI NINA PEPO AU JINI?, KILA NIPATAPO FEDHA ZA ZIADA HUTUMIKA AU KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA AJABU!

Hili ni somo la leo la fedha katika Mastermind group la Michanganuo-online na nitajibu swali la mdau wetu mmoja alilouliza kama ifuatavyo;

 

Habari Peter,  Mimi nimeolewa naishi na mume wangu na kila mmoja kati yetu anapopata pesa nyingi kuliko kiasi kile tulichokizoea kupata huwa tunaweka malengo mbalimbali ikiwemo kujiwekea akiba kwa ajili ya kujenga nyumba yetu wenyewe, kununua usafiri nk.

Lakini jambo la kustaajabisha ni kwamba mara tu tupatapo fedha hizo, hujitokeza matumizi ya ajabuajabu ambayo hayakuwepo kabisa kabla ya kuzipata.

Huibuka magonjwa, faini zisizokuwa na kichwa wala miguu ilimradi tu fedha kwa ajili ya mipango yetu zimetumika kinyume na malengo tuliyojiwekea. Mpaka imefikia mahali sasa tunapopata pesa nyingi tunaogopa kuweka malengo yeyote. Nataka nifahamu kama hii ni hali tu ya kawaida au kuna mapepo na majini ndani yake?   

 

MAJIBU:

Kila mtu huwa ana kiwango chake cha kushika pesa na ni vigumu sana mtu kuingiza pesa zaidi kuvuka kiwango hicho lakini kuna njia za mtu kuweza kufanya hatimaye kuondokana na kizingiti hiki na hata kuongeza kiwango chako cha upataji wa fedha.

Nakushauri hebu fanya jaribio lifuatalo;

Chukua kidumu chenye maji lita 5 na kisha uyajaze maji hayo ndani ya chombo kingine lakini cha ujazo wa lita 1. Ni dhahiri kabisa kwamba maji hayo yataingia mle kiasi cha lita moja tu huku mengine yakimwagika chini na kulowanisha sakafu au meza unayofanyia jaribio hili. Ni wazi pia wala hautahangaika kwenda kufanya jaribio hili kama nilivyokuelekeza kwani natambua kimantiki wala haliwezi kuleta maana yeyote ile.

Katika ulimwengu wa pesa kwa kila mtu hali pia inashabihiana sana na hii. Kuna kiwango fulani tu cha pesa kila mtu anachoweza kuingiza katika maisha yake kama ilivyokuwa kwa dumu la maji la lita moja. Uwezo huo wa mtu wa kupata pesa hauwezi kumruhusu aingize fedha zaidi ya kile kiwango chake alichozoea. Na hata mtu huyu anaweza kulazimisha na kusema afanye kazi kwa juhudi zote na maarifa ili kuongeza kipato hicho lakini kila senti itakayoongezeka juu ya kiwango kile itapotea katika mazingira ya ajabu.

Jinsi ya kutambua kiwango cha uwezo wako wa kumiliki pesa na namna ya kukizidisha

Ni rahisi kutambua kiwango chako cha fedha, Kokotoa wastani wa kipato chako cha mwezi kwa miezi 6 iliyopita na jibu hilo ndiyo uwezo wako wa kuingiza pesa kwa mwezi. Kiasi hiki huwa ndio sawa na ukanda wako wa faraja (comfort zone) na hukuwekea mipaka kwenye kiwango chako cha mapato, matumizi, madeni na matokeo ya biashara yako kwa ujumla kiasi kwamba ukipata pesa zaidi tu, akili yako ya ndani (Subconconscious mind) hukuzuia usipate. 

Kila kiasi cha pesa kinachoongezeka zaidi ya kiwango hicho mtu hujikuta akikipoteza, kukiweka katika miradi isiyo na tija, kukopesha watu wengine hovyo au hata kutatafuta njia yeyote ile, ilimradi tu ameitumia ikaisha (mfano wa maji kwenye lita 5 yanapozidi kwenye lita 1 na kumwagika sakafuni). Kuna nguvu ya ajabu huja na kuchukua kiasi kilichozidi kupitia matumizi yasiyotarajiwa.

Tatizo hili halisababishwi na nguvu za giza kama unavyodhania bali lina mizizi yake ndani kabisa ya ufahamu wetu (subconscious mind), na kuibadilisha hali hii ni lazima kwanza mtu kuingia moja kwa moja katika mawazo hayo ya ndani na kubadilisha programu tulizoziruhusu wenyewe kuota mizizi pale miaka na miaka. 

Programu hizo hubeba woga, uwongo na kila aina ya mitazamo hasi inayochangia viwango vya uwezo wetu wa kujiingizia pesa visiongezeke. Usipobadilisha mitazamo hiyo daima utaendelea kubakia na uwezo uleule wa kiwango cha fedha uliokua nao katika maisha yako yote mpaka unaingia kaburini. Kuna  baadhi ya mbinu za kuongeza kiwango cha uwezo wako wa kumiliki fedha nazo ni hizi zifuatazo;

1. Tambua tabia yako ya fedha:

Wakati unapokuwa na shida ya fedha, utafanya kila njia kuzipata, utafanya kazi muda wa ziada, utajinyima kila kitu ilimradi tu umepata pesa lakini mara tu unapozipata hivi, unaona sasa hamna tena haja ya kujituma zaidi. Programu yote hii hufanya kazi ndani ya akili zetu za ndani pasipo wenyewe kujua, hivyo usishangae kuona unapoingiza pesa nyingi zinayeyukia kusikojulikana. Ukifahamu namna akili yako ya ndani inavyofanya kazi juu ya hili ni njia mojawapo ya kuondokana na tatizo hili moja kwa moja.

 

2. Badilisha mfumo wako wa maisha

Tambua mpangilio wako wa kawaida wa pesa ukoje. Usizuie shauku yako ya kupata kile kitu usichoweza kukinunua. Uwezo wako wa kuwa na pesa zaidi utaongezeka iwapo utairuhusu nafsi yako kuhitaji kile unachokitamani kwani utajijengea nguvu zaidi ya kukitafuta na siyo kutumia ulicho nacho kukinunua. Jinyime lakini usizuie nafsi yako kutamani kuwa nacho.....................................................................................................................................................................................................................................................................................................

Ndugu msomaji wa somo hili, bado somo halijamalizika na unaweza kupata somo zima kwenye channel yetu ukijiunga na group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mifupimifupi ya biashara. Masomo yaliyopita utayapata yote

Kujiunga lipia kiingilio cha mwaka sh. 10,000/= ambapo unapata pia fursa ya kushiriki katika Semia kubwa ya kujifunza jinsi ya kuandika mchanganuo kamili wa biashara

Semina iliyo karibu ni ya tarehe 15/11/2024 na tutachambua biashara ya usagishaji mahindi (Sembe na Dona)

Namba za malipo ni 0765553030 au 0712202244 Peter Augustino,

Ukishalipia tuma ujumbe wa “nataka kujiunga Mastermind Group 2025 na offa ya vitu 11”.

Offa hii ni kwa watu 20 watakaowahi kabla ya tarehe 14/11/20224 


0 Response to "HIVI NINA PEPO AU JINI?, KILA NIPATAPO FEDHA ZA ZIADA HUTUMIKA AU KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA AJABU!"

Post a Comment