TUMIA SIRI HIZI 4 ZA USHINDI WA TRUMP BIASHARA YAKO IFANIKIWE 2025 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

TUMIA SIRI HIZI 4 ZA USHINDI WA TRUMP BIASHARA YAKO IFANIKIWE 2025

 

Mabilionea Donald Trump, Elon Musk na Robert Kiyosaki
Habari za muda huu ndugu msomaji wa blog ya jifunzeujasiriamali;

Karibu kwa makala nyingine tena tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka 2024 na kuanza mwaka mpya wa 2025. Kama kaulimbiu yetu ya mwaka inavyosema; “MAKE YOURSELF GREAT AGAIN” tunaendelea na makala na masomo yanayoamsha ndani yetu ari ya kupambana kurudisha ukuu uliopotea ama kujenga ukuu utakaotusaidia kwenye maisha yetu yajayo hasa kiuchumi.

Kabla ya Donald Trump kushinda kura ya Urais Marekani niliandika makala iliyosema, KUJIRUDISHIA TENA UKUU WAKO ULIOPOTEA au MAKE YOURSELF GREAT AGAIN, nikasema kwamba mwaka 2025 hiyo ndiyo itakayokuwa kaulimbiu yetu kuu Blog ya jifunzeujasiriamali, tukilenga kujifunza na kuhamasishana mbinu mbalimbali za mafanikio kwenye biashara bila kujali uliwahi kufanikiwa ukaja kufeli au ndio kwanza unaanza safari yako ya utafutaji pesa.

Nilisema kutumia kaulimbiu hii ya Trump simaanishi kwamba mimi ni shabiki kindakindaki wa siasa za Trump au chama cha Republican nchini Marekani hapana, bali niseme tu ukweli mimi ni shabiki mkubwa wa mikakati ya kibiashara ya Bwana Trump ambayo bila shaka mikakati hiyo pia ameweza kuitumia kwenye siasa na ikampatia mafanikio makubwa.

SOMA: Jinsi ya kuanzisha biashara ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo hata kama huna mia mfukoni

Sasa leo hii nitazumngumzia vitu vikubwa vine (4) ambavyo bila shaka Donald Trump Bilionea wa biashara ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo (Real Estate) alivitumia kikamilifu hatimaye akaweza kuibuka kidedea kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi licha ya kura za maoni mpaka dakika za majeruhi kuonyesha Bibi Harris alikuwa akienda kumbwaga vibaya Trump. Mikakati hiyo ni hii hapa chini;

1. Usijaribu kuligundua tairi upya (You can’t Reinvent the Wheel)

Hakuna tatizo jipya chini ya jua, karibu kila kitu unachojaribu kuwaza kuna mtu mwingine alishawahi kufanya hivyo na wengine kupata suluhisho kabisa, kwa hiyo wewe jambo la msingi ni kutumia masuluhisho yao kutatua tatizo lako uokoe muda wa kuanza kuhangaika kugundua suluhisho lako jipya mwenyewe.

SOMA: Jinsi ya kutumia maajabu yaliyopunguza corona tanzania kubusti uchumi wako unaosambaratika

Trump kwa mfano alifahamu fika ya kwamba mtandao maarufu wa Twitter (sasa X) ulikuwa ni Game changer kwake, lakini angelifanya nini wakati tayari mmiliki wake wa mwanzo Jack Dorsey akishirikiana na maadui zake kisiasa walikwisha mpiga marufuku kuutumia na hata kudelete kabisa account yake?

Ni nani ajuaye ikiwa swahiba yake Trump Bilionea namba moja Duniani Elon Musk ulikuwa ni mkakati maalumu waliokuwa wameupanga na Trump kuinunua Twitter mwaka 2021 ili baadae ije kuwapiga tafu?  

SOMA: Kamwe, kamwe, usikate tamaa(never, never give up)

Pamoja na Trump kuhangaika kuanzisha jukwaa lake jipya mwenyewe liitwalo TRUTH lakini ukweli ni kwamba lisingeweza katika kipindi kifupi namna ile kuvutia idadi kubwa ya watu ambao Twitter ilikuwa imevutia, hivyo hapa utaona kwamba Trump mara moja kwa  kulitambua hilo hakukubali kirahisirahisi kufanya kampeni zake nje ya jukwaa la X au Twitter. Trump nje ya Twitter ni sawa na samaki nje ya maji

Somo kuu tunalojifunza hapa ni kwamba angalia kile kinachofanya kazi uwekeze nguvu zako kwake, tuseme kwa mfano kila siku kwenye mitaa unayoishi unaona kabisa watu wengi wanakazana kuuza nyanya katika magenge yao kwa kuwa zinatoka haraka, sasa wewe na mtaji wako kidogo usianze kubahatisha kuweka gengeni kwako vitu hata hujawahi kuona mtu akiuza mtaani vitakudodea bure, labda tu iwe mtaji wako siyo wa wasiwasi basi unaweza kubahatisha vitu namna hiyo.

SOMA:  Njia wajanja wanayoitumia kupata matokeo bora zaidi kwa kila wanachokifanya maishani

Sihamasishi kuiga biashara za watu wengine hapana bali ninachosisitiza hapa tu ni kwamba, soma kwanza mazingira kuona ni kipi kinawezekana kwa rasilimali chache ulizokuwa nazo, angalia pia muda ulio nao nk. Kisha ongeza ubunifu kwa kile unachoiga.

SOMA: Hotuba ya kwanza kabisa ya Rais Donald J. Trump baada ya kuapishwa kuingia ikulu White house

Trump angeliweza kung’ang’ana tu na jukwaa lake la TRUTH lakini siamini ikiwa angetoboa ndani ya miezi ile michache iliyokuwa imebakia uchaguzi ufanyike. Na si hivyo tu, wapinzani wake pia wangeliweza kulitumia jukwaa hili lenye nguvu la X kumshinda kiurahisi mno.

2. Pesa ni Ulinzi, pesa ni karibia kila kitu kasoro uhai tu!

Pamoja na kasoro zote za Donald Trump katika Ikulu ya White House mhula wake wa kwanza, lakini kwa kweli pesa iliweza kumsafishia njia akarudi tena. Binafsi siamini kabisa ikiwa Trump angekuwa mtu wa kawaida tu kama marais wengine waliopita angeliweza kurudi tena Ikulu.

SOMA:  Je, pesa inaweza kutatua kila tatizo duniani au ndio chanzo cha matatizo yote?

Tumeshuhudia pesa ikitumika vizuri utaratibu wa kisheria unaweza ukacheleweshwa hata kama ikiwa hautasitishwa kabisa na ndivyo tulivyoona kwa kesi za Trump, tunaambiwa tu hazijaamuliwa bado na zinaweza kucheleweshwa mpaka baada ya kipindi chake kumalizika. Hivi angekuwa mtu hohehahe asiyeweza kuwalipa wanasheria nguli unadhani angeponyoka kweli?

Siyo siri Elon Musk alitumia pesa “kuwahonga” wapiga kura kukichagua chama cha Republican ingawa kisheria hakuvunja sheria na hakuna mtu wa kuhoji ni kwanini atumie pesa zake kwenye kampeni

Sasa ni somo gani tunapata hapa kwenye pesa? Ikiwa serikali na taasisi kubwa kubwa hutegemea kupata pesa toka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha mipango yake mikubwa, hivi wewe na mimi na biashara zetu hizi ndogondogo au hata za kati si ndiyo kabisa tungehitaji pesa kwa udi na uvumba?

SOMA:  Ili ufanikiwe kuwa tajiri mkubwa jiepushe kabisa na kauli hizi 4

Kuanzia sasa hebu amini kwamba ili utoke pale ulipo unahitaji namna fulani ya uwezeshaji zaidi ya fedha unazopata mwenyewe kila siku kufanya mambo makubwa zaidi, unahitaji mmoja kati ya watu wafuatao au wote, wabia, benki, washirika, masponsa au vyovyote vile utakavyowaita wewe ilimradi tu unawakaribisha walete mtaji kwako ili uweze kufanya zaidi ya vile unavyoweza kufanya binafsi kwa mtaji kidogo ulio nao.

Ni mambo mangapi umekuwa ukitamani kuyafanya lakini kikwazo kikubwa kikawa ni PESA? Sisemi ukipata pesa ndiyo muarobaini wa kila kitu hapana, bali mipango yeyote ile mwisho wa siku inahitaji bajeti ya pesa kuitekeleza huku pesa hiyo ukiisimamia kikamilifu itumike kulingana na mipango uliyoweka.

3. Kufanya utafiti (Research) na kuheshimu matokeo yake

Kabla ya kufanya mradi wa aina yeyote ule uwe ni wa kibiashara au wa kisiasa ni muhimu sana kufanya kwanza utafiti wa kina na kuzingatia matokeo yake ili kuepuka makosa yatakayosababisha anguko la mradi husika. Kosa kubwa lililowagharimu ushindi chama cha Democrats ni kuidharau kanuni hii. Utafiti siyo wa kura za maoni tu peke yake bali hata matukio ya nyuma unaweza kuyatumia kwenye utafiti.

SOMA: Kama unatafuta mafanikio kuna somo kubwa la kujifunza kwa ushindi wa talibani afghanistan na rais hichilema wa zambia

Hawakuhitaji maprofesa wa utafiti kubaini Wamarekani hawajafikia hatua ya kumkubali Mwanamke kuwa Raisi wa Taifa lao, ule uchaguzi wa Bibi Hilary Clinton na Trump ulitosha kuwapa alama ya tahadhari. Safari hii wakidanganywa na udhaifu wa Biden na historia ya fujo ya Trump wakadhania Wamarekani ingekuwa rahisi kuachana na kasumba yao ya ubaguzi wa kijinsia. Bibi Harris asingepita kirahisi kama angeshindanishwa na wanaume wa chama chake.

Tunapata somo kubwa hapa kwamba, chochote utakachokifanya kwenye biashara yako ukitaka ufanikiwe basi heshimu matakwa ya wateja wako na siyo yakwako binafsi.

Usifikirie kwa kuwa wewe unapenda sana juisi ya mapera basi na dukani kwako ukajaze juisi  kibao za pera ukidhani kila mtu anapendelea kile unachopenda wewe, chunguza kwanza wateja wa eneo unalofungua biashara yako wanapenda vitu gani ndipo uviagize vitu hivyo kwa wingi na siyo kuagiza vile unavyojisikia kuvipenda wewe na familia yako vitakudodea.

SOMA:

Nimetumia mfano huu wa juisi ya pera kwani unanikumbusha wakati naandika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI katika sura ya pili inayohusu somo la kufanya utafiti au upembuzi yakinifu kwenye biashara nilitumia mfano wa mfanyabiashara aliyekuwa akitafiti soko la juisi za embe na juisi ya pera. Ni moja kati ya masomo muhimu sana kwenye kitabu hiki wasomaji wengi hunipa mrejesho mara kwa mara.

4. Kuwa na Washirika sahihi

Umuhimu wa kuwa na Washirika sahihi tunauona kwa Bwana Trump, timu yake nzima ya kampeni mpaka mgombea mwenza wake. Kuna watu walihoji chaguo la Trump kwa atakayeshika nafasi ya umakamu wa Rais kuwa ni mtu asiyekuwa na jina kubwa lakini yeye ndiye mtu sahihi aliyeona atamfaa. Kitendo cha kushirikiana na watu kama kina Elon Musk, R.F Kennedy Junior na wengineo ulikuwa ni mkakati wake mkubwa wa ushindi.

SOMA: Kwanini kundi la kushauriana (master mind group) ni muhimu kwa kila anayetafuta mafanikio?

Trump ni muumini mkubwa wa kuunda ushirika sahihi na ukitaka kulithibitisha hili nenda kasome kitabu chake alichoandika akishirikiana na nguli mwingine mkubwa wa biashara Bwana Robert Kiyosaki kiitwacho, WHY WE WANT YOU TO BE RICH

Kitabu why we want you to be rich
Somo tunalolipata hapa ni kuwa kwenye biashara tunapaswa kuwa na washirika mbalimbali tunaoweza kunufaika kutoka kwao lakini pia na wao kunufaika kutoka kwetu. Usifikirie tu ni nini utapata kutoka kwa mshirika bali pia ufikirie ni nini utatoa kwa mshirika wako muhimu. Unaweza ukajenga ushirika kupitia magroup ya watsap kama lile la kwetu (MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP 2025) ama hata kuwa na washirika wengine nje ya mitandao.

SOMA: Kitabu baba tajiri na baba masikini (rich dad, poor dad) cha robert kiyosaki

Naamini katika siri au pointi hizi 4 Donald Trump alizotumia kupata ushindi na wewe pia zinaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine kufanikisha biashara yako mwaka 2025.

Ikiwa basi utapenda kujiunga na Washirika wengine ndani ya Mastermind group letu la Michanganuo online 2025 kujifunza zaidi masomo ya ubunifu kwenye biashara  karibu nafasi bado zipo chache. Chakufanya ni kulipia Semina na OFFA ya vitu 12 hapo chini shilingi 10,000/= kisha ujumbe usemao “NATAKA SEMINA NA OFFA YA MWISHO MWAKA HUU”  

Vitabu na michanganuo hii vitakusaidia kama rejea kwenye masomo yetu kwa mwaka mzima. OFFA hii ina thamani ya shilingi laki moja lakini unaipata kwa sh. elfu 10 tu!

Semina ya Kuandika mchanganuo wa biashara ya usagishaji unga wa Sembe na Dona inafanyika kila siku kabla ya mwaka huu 2024 kumalizika. 

Semina hii inamwezesha mshiriki kuandaa mpango wa biashara nyingine yeyote ile hata kama siyo ya usagishaji kwani tunafundisha kwanza misingi ya uandishi wa michanganuo.

Unapojiunga tunakutumia OFFA zako 12 kisha unaanza masomo ya semina siku hiyohiyo kwa siku 7. Baada ya semina unaendelea kuwa mwanachama wa kundi letu kwa mwaka mzima.

SOMA: Semina: mchanganuo wa biashara ya kusaga na kuuza unga safi wa dona (usado milling)-1

Group letu 2025 tutajifunza Michanganuo ya biashara na masomo ya fedha lakini katika mlengo tofauti kabisa na ilivyozoeleka. Tunazingatia ubunifu na mbinu za kipekee zinazomwezesha mjasiriamali kukuza haraka mtaji wake hata ikiwa biashara ni ndogo. Tumeandaa Biashara za mfano (Mashamba darasa) kwa ajili ya mafunzo hayo

 

OFFA INAYOKARIBIA MWISHO WAKE 2024 NI HII HAPA CHINI;

 

                           1.      KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali

                           2.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa

                           3.      KITABU: Toleo jipya la Elimu ya  pesa na Mafanikio

                           4.      KITABU: Sayansi & Sanaa ya Upishi wa chapatti laini.

                           5.      MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji unga wa Dona (USADO Milling)

                           6.      MCHANGANUO: Ufugaji kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-Kiswahili &kiingereza

                           7.      MCHANGANUO: Ufugaji kuku chotara Kuroiler-nyama

                           8.      MCHANGANUO: Kilimo cha tikiti maji (Kibada watermelon)

                           9.      MCHANGANUO: Uboreshaji Mashamba ya zabibu Dodoma (Makupila Real Estate)

                        10.    MCHANGANUO: Biashara ya kuuza chipsi

                        11.    MCHANGANUO: Biashara ya mgahawa (Jane Restaurant) Kiswahili & Kiingereza

                        12.    KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara

                    

   JINSI YA KULIPIA

Namba za malipo ni; 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe wa sms au watsap usemao “NATAKA OFFA YA MWISHO KWA 2024” Mara moja nitakutumia zawadi zako zote 11 pamoja na kukuunganisha na MASTERMIND-GROUP LA MICHANGANUO la mwaka 2025

 

AU

Unaweza kuingia kwenye Duka letu hili la vitabu mtandaoni, Selar.co, na kulipia moja kwa moja sh. elfu 10 pasipo kuwasiliana na sisi ukitumia mtandao wowote unaotumia halafu utapewa kifurushi cha ZIP utakachodownload zawadi. Unzip kifurushi na kutoa zawadi zako zote 11. Kisha nitakuunga kwenye MASTERMIND GROUP muda huohuo 

NB: Unaweza kunikumbusha kwa meseji nikuunganishe endapo nitachelewa kucheki mfumo.

0 Response to "TUMIA SIRI HIZI 4 ZA USHINDI WA TRUMP BIASHARA YAKO IFANIKIWE 2025"

Post a Comment