KUFANIKIWA BIASHARA USITAZAME KITU KIMOJA, CHANGANUA SOKO, BIDHAA, MAUZO, UTAWALA, FEDHA & MIKAKATI YAKO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUFANIKIWA BIASHARA USITAZAME KITU KIMOJA, CHANGANUA SOKO, BIDHAA, MAUZO, UTAWALA, FEDHA & MIKAKATI YAKO

Biashara ni kama gari ina sehemu mbalimbali

Biashara ni sawa na mfumo wa gari ulivyo, lina sehemu nyingi mbalimbali zinazotegemeana na kila kimoja kina umuhimu wake ili kulifanya liweze kuwaka na kutembea barabarani. Kikikosekana kimoja au kuwa na hitilafu basi gari zima halitaweza kufanya kazi yake barabara kama ilivyokusudiwa

Katika tasnia ya biashara kitu pekee kinachoweza kukuonyesha sehemu ama ‘spea’ zinazounda biashara ni mchanganuo wa biashara peke yake. Ni kwenye mpango wa biashara unapoweza kupata maelezo ya kila kiungo kinachosababisha biashara iitwe biashara

Sawa na gari linavyoitwa gari kwa kuwa na engine, gear box, betri, bodi, chases nk. ndivyo hivyo hivyo biashara nayo ilivyokuwa na Bidhaa/huduma, mtaji, soko/wateja, mikakati, usimamizi, wafanyakazi, fedha, mawasiliano nk.

Hii ni kusema kwamba unapojifunza namna ya kuchanganua biashara yako moja kwa moja umejifunza kila kipengele ama sehemu inayounda biashara hiyo na mtu hawezi kukudanganya kitu kwenye hiyo biashara husika

Huhitaji kuwa na digrii ya biashara au CPA kujua kufanya mchanganuo wa biashara yako, midhali unajua kufanya biashara na kusoma basi inatosha.

Watu wengi wamewahi kufanikiwa kibiashara hata pasipo kuandka mipango ya biashara zao mahali zaidi ya kuishika tu kichwani. Kwahiyo ikiwa utasoma na kuiandika hiyo ni faida ya ziada kwako na unazidisha mara dufu uwezekano wa kufanikiwa.

Tumeandaa package nzima (kifurushi) kwa ajili ya mtu yeyote anayehitaji kujifunza kila kitu kuhusiana na michanganuo ya biashara kuanzia Semina, vitabu, templates,  na mentorship watsap ya mwaka mzima wa 2025

Kifurushi hiki ni OFFA ya kumaliza mwaka na inakaribia mno kumalizika muda wake.

Tuna semina ya siku 7 inayoendelea kila siku asubuhi na jioni kabla mwaka huu haujamalizika, lakini washiriki wanaojiunga wanapata fursa ya kuwa katika familia yetu kwa mwaka mzima 2025

Unapojifunza semina hii unakuwa na uwezo wa kuandika mchanganuo wa biashara nyingine yeyote ile ingawa tumetumia mfano wa biashara ya usagishaji unga wa sembe na Dona.

Kujiunga na kifurushi hiki ada ni shilingi elfu 10 tu kupitia namba 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha ujumbe watsap au sms usemao, NATAKA KIFURUSHI KINACHOKARIBIA KUISHA MUDA WAKE  2024.

AU

Unaweza kudownload kifurushi hicho kwenye duka letu la mtandaoni kwa kufanya malipo yas h. elfu 10 hapa>>Selar.co ukitumia mtandao wako wa simu. Baada ya malipo nitakuona katika mfumo huo na kukuunganisha na group kwa ajili ya semina na masomo, nikichelewa kucheki mfumo unaweza kunistua

 

IFUATAYO NI ORODHA YA VITU 14 VYA OFFA YA PAPO KWA HAPO;

 

                 1.      KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali

                 2.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa

                 3.      KITABU: Toleo jipya la Elimu ya  pesa na Mafanikio

                 4.      KITABU: Sayansi & Sanaa ya Upishi wa chapatti laini.

                 5.      MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji unga wa Dona (USADO Milling)

                 6.      MCHANGANUO: Ufugaji kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-Kiswahili &kiingereza

                 7.      MCHANGANUO: Ufugaji kuku chotara Kuroiler-nyama

                 8.      MCHANGANUO: Kilimo cha tikiti maji (Kibada watermelon)

                 9.      MCHANGANUO: Uboreshaji Mashamba ya zabibu Dodoma (Makupila Real Estate)

              10.    MCHANGANUO: Biashara ya kuuza chipsi

              11.    MCHANGANUO: Biashara ya mgahawa (Jane Restaurant) Kiswahili & Kiingereza

              12.    KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara yako

              13.    TEMPLATE: Kiingereza

              14.    TEMPLATE: Kiswahili

 

 

 

 

SOMA NA HIZI HAPA PIA;

 

1.   Biashara ya mtaji mdogo yenye faida kubwa zaidi tanzania ilivyoshangaza darasa la michanganuo ya biashara

2.   Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.

3.   Biashara hii watu wengi huidharau lakini ina faida kubwa na nzuri,mtaji laki 1

4.   Semina siku ya 6: mpango wa fedha mchanganuo wa biashara kiwanda cha dona (usado milling

5.   Kwanini kundi la kushauriana(master mind group) ni muhimu kwa kila anayetafuta mafanikio?

 

0 Response to "KUFANIKIWA BIASHARA USITAZAME KITU KIMOJA, CHANGANUA SOKO, BIDHAA, MAUZO, UTAWALA, FEDHA & MIKAKATI YAKO"

Post a Comment